Saturday, June 25, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Awaonya wale wasiofanya Usafi Jumamosi ya mwisho wa mwezi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maelekezo wa watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga juu ya Umuhimu wa Kutumia sheria kwa yeyote kmwenye kukaidi kufuata maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Pombe Magufuli katika suala la Usafi wa Kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amesikitishwa na kitendo cha Wananchi kushindwa kushiriki katika Usafi wa kila Mwisho wa mwezi na kusema kuwa sheria itabidi zitumike ili watu wazoee kufanya usafi kwenye maeneo yao ya Biashara kila Wiki na Kilele kiwe siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Aliyasema hayo katika majumuisho aliyoyafanya na watumishi Halmashauri ya manispaa baada ya kuzunguka kwa Muda wa dakika 45 akikagua usafi uliofanywa na watumishi hao wakishirikiana na baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye maeneo yanayozunguka Uwanja wa Nelson Mandela pamoja na Soko la Mandela hapa mjini Sumbawanga.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa alisema uwa suala la usafi linatakiwa kuanzia ngazi ya chini katika mitaa hadi ngazi ya juu na watu wote washiriki bila ya shuruti na kama watashindwa kufanya hivyo basi sheria ichukue mkondo wake ili watu waweze kuona umuhimu wa kutekeleza agizo la Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli.

"Nimeteuliwa na Rais John Pombe Magufuli niwe mwakilishi wake katika Mkoa huu, nami sitafumbia macho wale wote ambao wanazembea katika kutekeleza agizo la Rais John Pombe Magufuli na katika Suala hili la usafi nitaanza kuwashughulikia watendaji wa mitaa, maana pamoja na majukumu yao mengine na hili la usafi pia limo, hivyo sitapenda kuona watu wa mtaa fulani hawafanyi usafi na mtendaji wa mtaa yupo na hafanyi lolote, mimi nitakula nae sahani moja, maana wananchi wakifanya usafi kwenye mitaa yao kazi unakuwa ndog" mkuu wa mkoa alisema.

Katika ukamilisha zoezi hili kuna watu  52 walikaidi na  kukamatwa na kila mmoja kulipishwa faini ya Shilingi 50,000/= na kupatikana shilingi Milioni 2.4 na wanne kati yao hawakulipa Fain taratibu za kuwafikisha mahakamani siku ya Jumatatu zishachukuliwa.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisimamia Usafi katika eneo la Uwanja wa Mandela katika kutekeleza Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya Usafi kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akishiriki kwenye usafi katika eneo la Uwanja wa Mandela katika kutekeleza Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya Usafi kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akishiriki kwenye usafi katika eneo la Uwanja wa Mandela katika kutekeleza Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufanya Usafi kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.

Mtumishi wa Manispaa ya Sumbawanga akiendelea na USafi katika eneo la uwanja wa mandela Mjini Sumbawanga.

Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Sumbawanga waishirikiana na wananchi kuzoa taka baada ya kufagia eneo linalozunguka Uwanja wa Mandela Mjini Sumbawanga.

Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Sumbawanga waishirikiana na wananchi wakifagia eneo linalozunguka Uwanja wa Mandela Mjini Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (mwenye kofia nyeupe) pamoja na RPC George Kyanda (mwenye kofia nyeusi) Afisa Mazingira wa Manispaa ya Sumbawanga Hamidu Masare pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga George Lupilya (mwenye koti la bluu). Mkuu wa Mkoa akiwaonesha tope linalotakiwa lisafishwe.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen  (mwenye kofia nyeupe) akijibu baadhi ya kero za wananchi katika Soko la Mandela wakati alipokuwa akikagua usafi ulivyofanyika katika Soko hilo

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (mwenye kofia nyeupe) akijaribu kufungua bomba la maji (halionekani pichani) ili kuopna kama maji yanatoka na hatimae hayakutoka na kuatoa masaa Manne hayo maji yawe yanatoka.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (mwenye kofia nyeupe) akitoa agizo la kuhakikisha maji yanatoka baada ya masaa manne katika soko hilo kwa Afisa Mazingira wa manispaa ya Sumbawanga Hamidu Masare 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (mwenye kofia nyeupe) akitoa agizo la kuhakikisha madimbwi yenye matope yanasafishwa kwa Afisa Mazingira wa manispaa ya Sumbawanga Hamidu Masare 

Baadhi ya wanafanyabiasha wa Soko la Mandela wakishangilia maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa kamishana Mstaafu Zelote Stephen alipokuwa akikagua usafi katika Soko la mandela mjini Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (mwenye kofia nyeupe) akiongozana na wagam,bo, maafisa usalama pamoja watumishi wasimamizi wa usafi kutoka Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha kila kona Inasafishwa na asiyetekelza agizo hilo achukuliwe hatua zinazostahili. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (mwenye kofia nyeupe) akitembelea vibanda vya wauza mitumba katika soko la mandela kuhakikisha usafi umefanyika, kushotoni kwakwe ni Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Rukwa  George Kyanda na kuliani kwake   Afisa Mazingira wa manispaa ya Sumbawanga Hamidu Masare 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (mwenye kofia nyeupe) akitoa magizo  lkwa Watumishi wa Manispaa ya Sumbawanga ili kuhakikisha mapungufu yaliyojitokeza jumamosi hii hayajitokezi tena. 
No comments:

Post a Comment