Monday, June 20, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa awatahadharisha wafugaji kulinda Afya zao kujiunga na NHIF.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen  akiwatambulisha watumishi wa Shirika la Bima la Taifa NHIF Pendoeva Kapola (wa kulia) na Godwin Samweli katika Mkutano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilaya ya Nkasi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewatahadharisha Umoja wa wafugaji wa Wilaya ya Nkasi kulinda afya zao kwa kujiunga na Shirika la Bima la Taifa NHIF katika Mkutano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilaya ya Nkasi.

"Taifa bila ya wananchi kuwa na afya njema haliwezi kuwa na maendeleo, na kujiunga na NHIF ni gharama ndogo sana, ndio maana niliposikia kuwa mna mkutano nikawaagiza hawa (akiwaonesha mbele yake) waje ili muwatumie" Mkuu wa Mkoa 
Mkuu wa Wilaya Mstaafu Kanali Antonio Mzurikwao akitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen kwa niaba ya Umoja wa wafugaji wa Wilaya ya Nkasi.

Mkuu wa Wilaya Mstaafu Kanali Antonio Mzurikwao akiendesha Zoezi la uchangiaji wa madawati kwa kila aliyehudhuria kwenye mkutano huo kutoa alichonacho ili kutekeleza agizo la Rais wa Nchi yetu Dk. John Pombe Magufuli la kuhakikisha hadi 30 June,2016 hakuna mwanafunzi atakaekaa chini.

Mchango huo uliendeshwa ghafla kama zawadi ya Mkuu wa Wilaya Mstaafu Kanali Antonio Mzurikwao kwa Wilaya ya Nkasi katika kusaidia zoezila uchangiaji wa madawati, hadi kufikia mwisho wa mchango huo Shilingi 264,000/= zilipatikana.

Nae Mbunge Mstaafu Dkt. Chrisant Mzindakaya nae pia alitumia nafasi hiyo kuchangia Shilingi 500,000/= 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwaaga na kuondoka katika ukumbi ulipofanyikia mkutano wa umoja wa wafugaji wa Wilaya ya NkasiNo comments:

Post a Comment