Monday, June 27, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aweka Jiwe la msingi Ofisi ya Kata Kizwite.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameweka jiwe la msingi katika ofisi ya kata ya kizwite katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga katika Ziara aliyoifanya kwenye Kata hiyo alipokuwa akitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Manispaa.Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephenakifunua kitambaa kilichoficha jiwe la msingi katika ofisi mpya ya kata ya Kizwite
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
akisema " Napenda kusimamia Haki, lazima wote tusimamie haki, Rushwa sipendi, sipendi kuona mambo yanafanyika halafu hakuna uwazi, hayo sitakubaliana nayo, lazima kila nguvu ya kila mmoja isemwe na penye kasoro msisite kuja kwenye ofisi zetu Mkoani na Wilayani, tusiposimamia haki hakuna maendeleo"
Jiwe la Msingi Katika Ofisi ya Kata ya Kizwite

Kata ya Kizwite ni miongoni mwa kata 19 zinazounda Manispaa ya Sumbawanga, kata hiyo ina jumla ya mitaa 15 na jumla ya Wakazi 17,187 kutokana na sensa yam mwaka 2012, na wakazi hao wanajishughulisha na ufugaji, biashara ndogondogo na ukulima.


Katika kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo kata ya kizwite ilipata fedah zake kutoka kwa wananchi, wahisani pamoja na Mkurugenzi wa manispaa na kufanya jumla ya fedha kuwa milioni 8.


Mwanafunzi wa Darasa la Sita wa Shule ya Msingi Ndua iliyopo kata ya Kizwite Debora, akisoma kwa sauti jiwe la Msingi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akionesha wananchi ilani anayoifuata katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yanayokusudiwa kwa faida ya kizazi cha leo na cha kesho katika mkutano wa hadhara alioufanya alipokwenda kuweka jiwe la Msingi katika ofisi ya kata ya Kizwite. kuliani kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawe


Ofisi ya ata iliyowekewa jiwe la Msingi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika kata ya Kiwite 

No comments:

Post a Comment