Wednesday, June 15, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven awaasa wakandarasi kumaliza mradi wa maji mapema na kwa ufanisi ili kumaliza tatizo hilo Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven Zelote akitoa maelekezo katika mkutano wa dharura  aliouitisha alipotembelea ofisi za mkandarasi wa mradi wa maji wa 7TUUP (7 Towns Urban Upgrading Program) kampuni ya TECHNOFAB iliyopo Majengo, Sumbawanga.

Mradi huo ambao upo chini ya Mamlaka ya Maji safi Sumbawanga (SUWASA)  
unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) pamoja na Benki ya Ujerumani KFW  una lengo la kuboresha upatikanaji wa maji katika Mji wa Sumbawanga,Mji ambao wananchi wake huwa na tabu ya maji wakati wa kiangazi kuanzia mwezi September hadi November

"Mradi huu utakapomalizika utatupa ahueni ya shida ya maji katika mji wetu wa Sumbawanga" alisema Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa aliwasihi wakandarasi hao kutosita kumfuata ofisini kwake pindi wanapokwama kwa jambo lolote na kuongeza kuwa mradi huo hauwezi kufanyika kwa ufanisi kama hakuna ushirikiano.

"Kama mtapata shida yeyote msiogope kuja ofisini kwangu ili tuweze kutatua kwa pamoja, kwani tukishirikiana kwa umoja ndio mradi utafanikiwa" Mkuu wa Mkoa alimalizia.

Mradi huo wa 7TUUP ulianza March,2013 na unatarajiwa kuisha September,2016, mradi huo utachimba visima 17 vyenye kuzalisha lita za ujazo 7500 kwa siku,kwa sasa Mamlaka ya Maji safi Sumbawanga (SUWASA) ina uwezo wa kuzalisha lita za ujazo 6000 na wakati wa kiangazi hupungua na kufikia 3500 kwa siku.

Mradi huo utakapomalizika unatarajiwa kuhudumia wananchi 134,000 kwa kutoa jumla ya lita za ujazo 13500 kwa siku, ambapo mpaka sasa visima vyote 17 vishachimbwa na visima vinne vinatarajiwa kufunga Pampu hivi karibuni ili kuweza kuanza kutoa huduma kwa wananchi

Visima hivyo vitakuwa vikiendeshwa kwa mitambo ya kisasa kutoka katika kituo cha kusafishia maji (water treatment plant) kilichopo Majengo, Sumbawanga.

Kutokana na hayo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliwataka SUWASA kuongeza wataalamu watakaosimamia na kuendesha mitambo hiyo pindi mkandarasi atakapokabidhi, na si kumtegemea mtaalam mmoja ambae atakapopata matatizo na wananchi watakosa huduma.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven Zelote akitoa maelekezo
 Msimamizi wa Mradi wa 7TUUP  Eng. Colman Ngaenayo (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya mradi na hatua walizofikia mbele ya timu ya Mkuu wa Mkoa iliyomtembelea katika ofisi yake.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akioneshwa ramani ya visima 17 vya mradi huo na Eng. Colman Ngaenayo wakati walipotoka nje ya ofisi baada ya kumaliza kikao.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akimsikiliza kwa makini mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi SUWASA, Zakaria Ngunda mbele ya Tanki la kuhifadhia maji lililopo eneo la Kilimani, Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akisikiliza maelezo kwa makini kutoka kwa Msimamizi wa mradi wa 7TUUP Eng.Colman Ngaenayo (aliyevaa vest ya njano) nje ya ofisi ya mkandarasi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akijikinga jua kuangalia madimbwi ya kuhifadhia uchafu unaotokana na kusafishwa kwa maji (hayapo kwenye picha) katika Water treatment plant huku akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa mradi wa 7TUUP Eng.Colman Ngaenayo (aliyevaa vest ya njano)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akiuliza swali la kutaka ufahamu juu ya utendaji kazi wa vichujio vya maji katika kituo cha kusafishia maji (Water treatment plant)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven pamoja na timu aliyoongozana nayo wakiangalia vichujio vya maji katika kituo cha kusafishia maji (Water treatment plant) kilichopo Majengo, Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akiongozwa na Msimamizi wa mradi wa 7TUUP Eng.Colman Ngaenayo (aliyevaa vest ya njano) kwenda kuona Madimbwi ya kuhifadhia uchafu baada ya maji kusafishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akichangiana mawazo na Msimamizi wa mradi wa 7TUUP Eng.Colman Ngaenayo (aliyevaa vest ya njano) nje ya ofisi ya mkandarasi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven na timu yake wakiangalia  Madimbwi ya kuhifadhia uchafu baada ya maji kusafishwa 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven na timu yake wakiangalia  mabomba yanayopita maji yalisafishwa kutoka katika vichujio kwenye kituo cha kusafishia maji(Water treatment plant)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Steven akiagana na wafanyakazi wa kituo cha kusafishia maji (Water treatment plant)

Ujenzi wa Madimbwi ya kuhifadhia uchafu unaotokana na kusafishwa kwa maji baada ya kutoka kwenye vichujio, katika Water treatment plant


No comments:

Post a Comment