Wednesday, July 6, 2016

Miradi iliyotembelewa na Mwenge Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

mmoja wa viongozi wa Mbio za Mwnge Alex Kayuni akiwaongoza wenziwe katika kuukimbiza Mwenge.
Viongozi mbalimbali wa Mbio za Mwenge Kitaifa na viongozi wa Serikali na wa wananchi wakikagua Hosteli zilizozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa George Mbijima katika shule ya Sondari Uchile, kijiji cha Laela, wilayani Sumbawanga.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule akipanda Mti katika Shule ya sekondari Uchile kuweka kumbukum ya kupita kwa mwenge katika shule hiyo.

mmoja wa kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa Munira Saidi Abbas akiwapitishia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uchile katika Kijiji cha Laela Wilayani Sumbawanga

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akiwasha moja ya pikipiki walizopewa watendaji wa kata 27 za Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwajili ya kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akiwa amekaa pamoja na mwalimu na wanafunzi wake baada ya kukabidhiwa madawati 40 kwa shule ya msingi Laela "A"

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akielekezwa na afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Msea Juma juu ya kazi mbalimbali za vifaa vya kurinia Asali katika kijiji cha Laela

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi vifaa vya kurinia asali na mizinga kwa kikundi cha Mnokola Kilichopo katika kijiji cha Laela Wilayani Sumbawanga. Mavazi ya kurininia asali ni Shilingi 300,000/= na Vifaa vya kurinia ni shilingi 700,000/=

Bango la Kuukaribisha Mwenge 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi madawati 40 kwa Shule ya Sekondari Lusaka iliyopo katika kijiji cha Lusaka Wilayani Sumbawanga.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akimkabidhi kadi ya Bima ya Afya mmoja wa wazee 240 waliopatiwa kadi za Bima ya Afya kupitia  mradi wa Mwenge. katika kijiji cha Mpui, Wilayani Sumbawanga 

Baadhi ya wazee 240 waliopatiwa kadi za Bima ya Afya kupitia mradi wa Mwenge katika kijiji cha Mpui, Wilayani Sumbawanga 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi Hundi ya shilingi Milioni 2.5 kwa Palesiano Philemon mwakilshi wa kikundi cha Upendo Tunko, kikundi inachojishughulisha na kukopeshana kulea yatima na sanaa. Kiongozi huyo aligawa Hundi kwa vikundi Saba zenye Thamani ya Shilingi Milioni 23.5 kwa vikundi vya ujasiliamali. Katika Kata ya Mpui Wilayani Sumbawanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi Hundi ya shilingi Milion 4 kwa kikundi cha wanawake Nsangu kutoka Msandamuungano. Hapa Kiongozi wa Mbio za Mwenge alitoa Hundi mbili zenye Thamani ya Shilingi Milioni 8 kwa vikundi viwili vya wanawake wajasiriamali katika Kijiji cha Kaengesa, Wilayani Sumbawanga.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi chandarua kwa Mama Janeth Pelisius, mmoja wa kinamama waliopatiwa Vyandarua kwaajili ya kutokomeza Malaria kupitia Mradi wa Mwenge katika Kijiji cha Kaengesa, Wilayani Sumbawanga 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi vyandarua kwa wazee kwaajili ya kutokomeza Malaria kupitia Mradi wa Mwenge katika Kijiji cha Kaengesa, Wilayani Sumbawanga 

Wananfunzi wakiwa wamekaa juu ya madawati 40 yaliyokabidhiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima kwa shule ya Msingi Mpui katika Kijiji cha Mpui, Wilayani SumbawangaKiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi Hundi ya shilingi Milion 4 kwa kikundi cha wanawake Mchakamchaka kutoka kijiji cha kaengesa Wilayani Sumbawanga.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi moja ya seti 8 za kurinia asalikwa kikundi cha katonto na Lula katika Kijiji cha Kaengesa Wilayani Sumbawanga lakini pia hapohapo aligawa mizinga 60 ya Nyuki

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akikabidhi madawati 40 kwa shule ya msingi Kaengesa, katika kijiji cha kaengesa Wilayani Sumbawanga 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akimtwisha ndoo mama aliyechota maji katika uzinduzi wa maji mserereko katika kijiji cha Lusaka, Wilayani Sumbawanga 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akiweka Jiwe la msingi Katika zahanati ya Kizumbi katika Kijiji cha Kizumbi, wilayani Sumbawanga 

Jiwe la Msingi la Zahanati ya Kizumbi

Mwenge Ukitoka katika eneo la maji Mserereko katika Kijiji cha Lusaka, Wilayani Sumbawanga 

Baadhi ya wananchi waliohudhuria kuushuhudia Mwenye katika kijiji cha Kizumbi, Wilayani Sumbawanga, (mbele ni skout kwaajili ya kuimarisha ulinzi)

Baadhi ya Wananfunzi wa Shule ya Msingi Kizumbi waliokuwa wamehudhuri kuushuhudia Mwenye katika Kijiji cha Kizumbi wilayani Sumbawanga

No comments:

Post a Comment