Monday, July 4, 2016

Mkuu wa Mkoa aagiza mambo sita ya kufanyiwa kazi na Wakuu wapya wa Wilaya

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Nkembanyi Binyura akila kiapo mble ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo, pamoja na Katibu wa Mkuu wa Mkoa Frank Mateni pamoja na Makamu Katibu tawala Mkoa Aboubakar Kunenge.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Dk. Halfan Boniface Haule akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani).

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda (kulia) akikabidhiwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama kukabidhiwa majukmu na mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ametaja mambo nane na kuwaonyesha njia ya kufuata wakuu wapya wa Wilaya tatu za Mkoa wa Rukwa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kutimiza kauli ya “Hapa kazi Tu” ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Aliyataja mambo hayo wakati alipokuwa akitoa nasaha muda mfupi baada ya kiapo cha wakuu wa wilaya hao tukio lililofanyika katika Ikulu ndogo ya Mkoa wa Rukwa Mjini Sumbawanga.

Kamishna Mstaafu Zelote Stephen alianza kwa kuwakumbusha juu ya utawala bora na kuwaomba wakuu hao wapya wa wilaya kusimamia maendeleo ya wananchi bila upendeleo wa aina yoyote na kusisitiza kuwa wawe na sura moja tu tena ya kazi

“Nitawaomba sana msimamie maendeleo ya wananchi tena bila ya upendeleo haki itendeke na katika kulifanya hili msiwe na sura mbili, sura iwe ni moja tu ya kazi, hatutegemei kuwa na Ndumi la kuwili, mhakikishe ilani ya CCM mnaisimamia na kuifanyia kazi ili ilete maendeleo kwa wananchi,” Mkuu wa Mkoa alisema.

Kutokana na kufikia ukomo wa agizo la Rais D. John Pombe Magufuli juu ya madawati, Mkuu wa Mkoa hakusita kuwakumbusha na kuwasisitizia wakuu hawa wapya wa wilaya juu ya umaliziaji wa usimamizi wa madawati ili kuhakikisha wananfunzi hawakai chini tena.

“Mtapewa taarifa ya madawati ambayo itawaonyesha takwimu lakini msiridhike na takwimu mtakazoziona, muzifuatilie ili kujiridhisha na taarifa hizo,” Mkuu wa Mkoa aliongeza.

N katika kuhakikisha Mkoa wa Rkwa na Halmashauri zake zinakuwa safi Mkuu wa Mkoa Kamishna Mstaaafu Zelote Stephen hakuacha kugusia suala zima la usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na kuwasihi kuwahimiza wananchi kufanya usafi kila wiki na kilele chake kuwa Jumamosi ya mwisho wa kila mwezi.

Na katika kulisimamia hilo kwa uangalifu na umakini aliwasihi ikibidi washirikiane na mabaraza ya madiwani ili kuweka sheria ndogondogo na kuhakikisha wananchi wanazitii ili Mkoa wa Rukwa uwe msafi na msamiati wa uchafu uftike katika vichwa vya wanarukwa.
Mkuu wa Mkoa alisema, “Mshirikiane na mabaraza ya madiwani kutunga sheria ndogondogo zitakazokomesha suala la Uchafu katika Mkoa wetu.”

Katika kukazia suala la usafi Mkuu wa Mkoa hakusahau kuwaeleza wakuu hao wapya wa Wilaya umuhimu wa wananchi wa Rukwa kuwa na afya nzuri, na wao kuwahamasisha wananchi kujiunga na CHF, jambo ambalo ni la msingi katika kujenga taifa imara.

Suala la mazingira lilionekana kuchukua nafasi yake katika nasaha zake pale alposema, “Uharibifu wa Mazingira ni Mkubwa na hili naliweka mabegani mwenu,” na hivyo kuwasisitiza wakuu hao wapya wa Wilaya kuwahamasisha wananchi kuweza kupanda miti na kuwasihi wafuate ushauri wa wataalamu waliomo kweye halmashauri za Mkoa ili kuweza kutunza vyanzo vya maji na kuonya kuwa hatakubali kusikia miti inayonyonya maji ndio inayopandwa kwa wingi.

Pia Mkuu wa Mkoa aligusia suala la wakulima na wafugaji na uwaomba wakuu hao wapya wa wilaya kuweza kuhakikisha wakulima na wafihgaji hawavunji Amani katika maeneo wanayoingiliana. Na kusema, “Ondoeni wavamizi, angalieni wakulima na wafugaji waishi kwa Amani.”

Mkuu wa Mkoa alisisitiza Wakulima na Wafugaji wasaidiwe wasifanywe kuwa vhanzo vha watu kutajiika kupitia migongo yao. Na katika kulikazi hilo mkuu wa Mkoa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen aliongelea suala la usambazaji wa pembejeo na mbegu feki kwa wakulima na wafugaji.
“Tunategemea nini pale ambapo mbegu ni feki, mbolea feki halafu tuna maafisa kilimo, serikali ipo, mimi kwa hayo sitakuwa Tayari naamini nanyi hamko tayari, mtaniunga mkono na tutamuunga mkono Mh. Rais.” Mkuu wa Mkoa alionya.

Ili halmashauri ziweze kujiendesha zinahitaji kukusanya mapato ya kutosha hivyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliwataka wakuu hao wapya wa Wilaya kuhakikisha taarifa wanazopewa na wataalamu wanazifuatilia kwa umakini na uweledi mkubwa na ikibidi waweke utaratibu wa kupewa taarifa za kila siku za utendaji kazi wa Halmashauri wanazozisimiamia.

“Taarifa mnazopewa zisiwe za kubumba, ziwe halisi, maana mimi naweza kuzka muda wowote na nikute taarifa za kweli, na madiwani wapo kwaajili ya kuwatumikia wananchi mshirikiane nao kaka kuleta maendeleo, na kupata taarifa za kila siku ni Muhimu sana.” Mkuu wa Mkoa alisema.

Mkuuwa Mkoa aliwasisitizia Wakuu hao wapya wa Wilaya kuangalia miradi ya maji, barabara, na miundo mbinu mingine ambayo haiendani na fedha na kutaja baadhi ya miradi ya benki ya Dunia ambayo ipo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ambayo inaendelea kutekelezwa.

“Jitengenezeeni utaratibu wenu wa kufuatilia mambo, hasa yale madogo madogo ndio muyafuatilie kweli, muwe Flexible, approachable na mfute ule utendaji kazi wa kimazoea, jitahidini kurejesha nidhamu.” Mkuu wa Mkoa alimalizia.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo, pamoja na Katibu wa Mkuu wa Mkoa Frank Mateni pamoja na Makamu Katibu tawala Mkoa Aboubakar Kunenge. wakati wa wimbo wa Taifa.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Dk. Halfan Boniface Haule 

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Nkembanyi Binyura 

(kuanzia kulia) Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Nkembanyi Binyura, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Mtanda na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Dk. Halfan Boniface Haule 

Safu ya mbele kabisa ni Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na wenyeviti wa madiwani na Mstahiki Meya wa manispaa ya sumbawanga na Nyuma yao ni wafanyakazi wa Sekretarieti ya mkoa wa Rukwa 

Baadhi ya Viongozi wa Dini pamoja na maafisa wa Uasalama wa Raia waliohudhuria.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisisitiza Utawala bora na wa haki kwa wananchi bila ya Upendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisisitiza ukusanyaji wa mapato kwa halmashauri zote ili ziweze kujiendesha na kuendeleza Mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisisitiza upandaji wa miti kutunza mazingira na kuupendezesha Mkoa.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Ngazi ya Mkoa waliohudhuria.

Picha ya pamoja ya Mkuuwa Mkoa, Wakuu wa wilaya na viongozi wa Vyama nyuma yao

Picha ya pamoja ya Mkuuwa Mkoa, Wakuu wa wilaya na Kaimu Katibu Tawala Mkoa (wa kwanza kushoto)

Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa.

Picha ya pamoja ya Mkuuwa Mkoa, Wakuu wa wilaya na Makatibu tawala wa Wilaya Tatu za Mkoa wa Rukwa

Picha ya pamoja ya Mkuuwa Mkoa, Wakuu wa wilaya na wafanyakazi wa sekretarieti ya Mkoa

Picha ya pamoja ya Mkuuwa Mkoa, Wakuu wa wilaya na Viongozi wa dini waliohudhuria.


No comments:

Post a Comment