Friday, July 1, 2016

Mkuu wa Mkoa aunga Mkono mradi wa PHC Kuimarisha Afya za wanarukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameonana na watu wa mradi wa Priamry Health Care (PHC) unaojishughulisha na kuboresha vituo vya afya katika vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika ili kusikiliza mipango na mapendekezo yao ya kuboresha mazingira ya kiafya katika mkoa wa Rukwa.

Eneo la Mradi wa PHC

Mradi wa PHC ulianza kufanya kazi mwaka 2006 katika vijiji 35 vilivyopo katika mwambao wa ziwa Tanganyika, ambapo makao makuu ya mradi huo ni katika kijiji cha Kipili, Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa.

Mradi huo unafadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Kanisa la Monravian linalotoa nyumba za kuishi wahudumu, serikali ya Denmark inayotoa fedha za kuendesha na mardi na serikali ya Tanzania inayotoa wahudumu wa kufanya shughuli hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwasikiliza kwa makini watu wa Mradi wa PHC

Mradi unajishughulisha na kuwafundisha Wahudumu wa Afya ya Jamii (WAJA) kuzuia magonjwa mbalimbali ikiwemo kuwaelimisha wananchi kutumia maji safi, kutumia vyoo na usafi wa nyumba wa kila siku.

Katika kufanikisha shughuli hizi watu wa mradi wa PHC wanashirikiaa na Kamati za Afya za vijiji zinazojumuisha Wahudumu wa Afya, viongozi wa dini, mwalimu, wakunga wa jadi, waganga wa kienyeji, mwenyekiti wa kijiji, Wahudumu wa Afya ya Jamii wawili wa kike na wakiume.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwasikiliza kwa makini watu wa Mradi wa PHC

Kila kijiji kina wahudumu wa Afya ya Jamii wawili na kufanya kuwa na wahudumu 70 na miongoni mwa kazi wanazofanya wahumu hao ni pamoja na kuwasaidia kuwatibu wananchi wenye magonjwa yanayoweza kutibika bila ya kufika hospitali na kuwapa wananchi elimu ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kuzuilika na hatimae kuimarisha afya zao.

Kutokana na vimiji hivyo kuwa na tabu ya maji Mwezi June mwaka 2016 mradi umeanza kutafiti uwezekano wa kuanzisha miradi ya kuweka pampu za maji katika vijiji 10 kama jaribio la kwanza wakishirikiana na wananchi ili kupunguza tatizo la maji katika vijiji hivyo.

Mradi unaona kuna umuhimu wa wanakijiji kuchangia kwa kiasi kidogo ili waone miradi hiyo ni ya kwao ili kuweza kuitunza na kuilinda, na kufanya hiyo ni kuunga mkono sera ya Afya na Maji Taifa.

 

 Kutoka Kushoto kwenda kulia, Bw.Bert Muizebelt na Bi.Marjo Ten kate Washauri wa Mradi, pamoja na  msimamizi wa mradi Ndg. Respice Mbalu

No comments:

Post a Comment