Saturday, July 2, 2016

Mkuu wa Mkoa awafuturisha Waislamu

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaalika waislamu na viongozi wao katika futari ya pamoja nae nyumbani kwake leo katika swaumu ya 26 ya kumi la Mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kamishna mstaafu katika kuonwaunganisha viongozi wa dini pamoja pia aliwaita viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo kushiki pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu katika futari hiyo.

Mkuu wa Mkoa katika Futari hiyo alisisitiza kudumisha umoja na mshikamano kwa waumini wa dini zote nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa kofia nyeupe,kanzu na koti) akiwa katika Foleni ya futari pamoja na baadhi ya viongozi wa dini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoka kwenye foleni ya kuchukua futari kenda kukaa.
Baadhi ya Viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu walioshiriki kwenya futari ya pamoja 
Baadhi ya Viongozi wa dini Kiislamu walioshiriki katika futari
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa neno la Shurani kwa waumini wa kiislamu,viongozi wao pamoja na viongozi wa madhehebu ya Kikristo waliohudhuria katika Futari
Baadhi ya Waumini na Viongozi wa dini Kiislamu walioshiriki katika futari 
Baadhi ya Waumini na Viongozi wa dini Kiislamu walioshiriki katika futari
Baadhi ya Waumini na Viongozi wa dini Kiislamu walioshiriki katika futari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu  Zelote Stephen wakati alipokuwa akitoa nasaha ya Kudumisha umoja na mshikamano kwa waumini wa Dini zote nchini. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu  Zelote Stephen wakati alipokuwa akitoa nasaha ya Kudumisha umoja na mshikamano kwa waumini wa Dini zote nchini.
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Shekh Rashid Akilimali akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen kwa kuwafuturisha katika siku iliyomo katika Kumi la mwisho la Mwezi wa Ramadhani
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu  Zelote Stephen wakati alipokuwa akitoa nasaha ya Kudumisha umoja na mshikamano kwa waumini wa Dini zote nchini.
Baadhi ya Viongozi wa dini ya Kikristo  walioshiriki kwenya futari, pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawe (wa pili kutoka kulia)
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu  Zelote Stephen wakati alipokuwa akiagana na baadhi ya waumini waliohudhuria katika Futari hiyo
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu  Zelote Stephen (katikati) akiteta na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawe (kushoto) pamoja na Kaimu RAS Mkoa wa Rukwa Ndg. Kilonzo (Kulia)

No comments:

Post a Comment