Monday, July 11, 2016

Mwenge Ulipoondoka Rukwa Kuingia Katavi

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati akiupokea Mwenge huo kutoka Mkoa wa Rukwa.
Wakimbiza Mwenge wa Mkoa wa Rukwa na Wilaya zake pamoja na Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakikimbiza Mwenge kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda kuwapa timu ya Mkoa wa Katavi.

Mkuu wa wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akimuaga mmoja wa wakimbiza Mwenge kitaifa Nahoda Makame Nahoda wakati mwenge uo ulipokabidhiwa kutoka Wilaya ya Nkasi kwenda kwa Ofisi ya Mkuu wa Rukwa kabla ya kukabidhiwa kwa Mkoa wa Katavi. 

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa George Jackson Mbijima akisalimiana na timu ya Mwenge kimkoa akitokea kukimbiza Mwenge katika Wilaya ya Nkasi.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa David Kilonzo 

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa David Kilonzo akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda 


Waanafunzi wa Shule za Msingi pamoja na wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Katavi wakiusubiri Mwenge wa Uhuru kwa Hamu katika Kijiji cha Mpimbwe.

Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda, Mkuu  Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nkasi Festus Chonya baada ya kuaga Mwenge wa Uhuru ulioelekea Mkoa wa Katavi

Watumishi wa Mkoa wa Rukwa wakijitayarisha kuuaga mwenge wa uhuru kutoka Mkoa wa Rukwa Kwenda Mkoa wa Katavi.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Nkasi waliohudhuri akatika Kuuaga Mwenge wa Uhuru Ukielekea Mkoa wa Katavi.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo akimuaga mmoja wa Mkimbiza Mwenge Kitaifa Alex Kayuni na kuwakabidhi wakimbiza Mwenge hao kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga

Baadhi ya Wakimbiza Mbio za Mwenge Kitaifa wakipa wamejipanga kubadilishiwa Skafu ishara ya kutoka katika Mkoa wa Rukwa kuingia katika Mkoa wa Katavi.  

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akimkaribisha Mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa Lucia Makafa katika Mkoa wa Katavi.

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa George Jackson Mbijima akiagana na Makamu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Aboubakar Kunenge kutoka kwa wakimbiza Mwenge wa Mkoa wa Rukwa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa George Jackson Mbijima akibadilishiwa Skafu na Skaut Ishara ya Kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda Mkoa wa Katavi.Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Paul Chagonja akipokea mwege kutoka kwa Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa (hayupo pichani)

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wake Paul Chagonja (hayupo pichani)

Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa George Jackson Mbijima pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakiusubiri Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akiupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza Mwenge kitaifa Alex Kayuni, baada ya kuwasili kutoka Mkoa wa Rukwa.

No comments:

Post a Comment