Friday, July 8, 2016

Mwenge Ulivyoingia Wilaya ya Kalambo

Maandalizi ya Kuukabidhi Mwenge Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.


Mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa Lucia Vitalis Kamafa akimuaga Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk Halfan Haule aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, wakati wakijiandaa kuingia Wilaya ya Kalambo. 


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Janckson Mbijima akimuaga Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk Halfan Haule aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, wakati wakijiandaa kuingia Wilaya ya Kalambo. 


Mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa akivishwa Skafu mpya na kuvuliwa ya zamani ikiwa ni Ishara ya kutoka Wilaya Moja kwenda nyingine kuendelea kuukimbiza Mwenge ambao utapita katika Wilaya zote Nchini.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Janckson Mbijima akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, wakati wakiukaribisha Mwenge katika Wilaya ya Kalambo. 


Timu ya wakimbiza Mwenge kitaifa ( wanne waliovaa mashati ya Ugoro) pamoja na Viongozi mbalimbali wa Wilaya na  Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo wakisubiri kukabidhiwa Mwenge Ili kuendelea na mbio hizo.


Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk Halfan Haule akimkabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura ili aweze kuendelea na mbio hizo katika Wilaya yake.


Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akiupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk Halfan Haule ili aweze kuendelea na mbio hizo katika Wilaya yake


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo James Makwinye akiupokea Mwenge wa Uhuru.


Wakinamama na wananchi wa Wilaya  ya Kalambo waliohudhuri katika kiwanja cha makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru wakiimba kwa furaha.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Janckson Mbijima akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura kuliani kwake wakisubiri kuendelea na Safari ya Mwenge katika Wilaya ya Kalambo.

No comments:

Post a Comment