Wednesday, July 6, 2016

Mwenge Waingia Rukwa kuzindua miradi ya thamani ya Bilioni 11.6


 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiupokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chifu Galawa.


Timu ya Mkoa wa Songwe ikijiandaa kuukabihi Mweye wa Taifa kwa Mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stepehen akimpongeza mmoja wa viongozi wa wakimbiza Mwenge Lucia Kamafa walipokuwa wakitaka kuupokea mwenge kutoka Mkoa wa Songwe katika viwanja vya Shule ya Msingi Tunko.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stepehen akimpongeza kiongozi wa wakimbiza Mwenge George Mbijima walipokuwa wakitaka kuupokea mwenge kutoka Mkoa wa Songwe katika viwanja vya Shule ya Msingi Tunko.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stepehen (wa tatu kutoka kulia) pamoja na Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Rukwa DAvid Kilonzo wakiusubiria Mwenge.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chifu Galawa (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen  wakisalimiana kabla ya Mwenge Kukabidhiwa Rasmi kwa Mkoa wa Rukwa.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisoma taarifa ya Mkoa Kuhusu Mwenge mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima(kuliwa) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chifu Galawa. (hayupo pichani) pamoja na wananchi na watumishi wengine wakiserikali.
Walinzi wa Mwenge wa Uhuru wakiwa makini kulinda mwenge.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mohamed Ntanda alipopewa Mwenge na mmoja wa viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo  Mh. Julieth Nkembanyi Binyura alipopewa Mwenge na mmoja wa viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen  akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Mh. Halfan Haule ili kuanza safari ya kuzungukia miradi mbalimbali iliyomo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Mh. Halfan Haule aikabidhiwa  Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen  ili kuanza safari ya kuzungukia miradi mbalimbali iliyomo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Mwenyekii wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Kalolo Ntila alipoushika Mwege wa Uhuru kabala ya Kuanza kwa mbio zake katika Halmashauri .

No comments:

Post a Comment