Monday, July 4, 2016

"Nawahakikishia wanarukwa kuwa hakuna shida ya Sukari" - Mkuu wa Mkoa

Katika Kuhakikisha wananchi wanaondokewa na kero ya upungufu na ulanguzi wa sukari katika mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amefanya ziara yakushtukiza katika ghala la Mfanyabiashara maarufu katika Mji wa Sumbawanga Mselem Nassor.

Ziara hiyo aliifanya mara tu baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya tatu za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa Mkoa alilivalia njuga suala hilo baada ya kusikia wananchi wengi wakilalamika kuwa wanauziwa sukari kwa bei isiyoelekezi ya serikali jambo ambalo lilimsikitisha Mkuu wa Mkoa na kuamua kufuatilia ili kujua mbivu na mbichi.

Kabla ya kufika katika ghala hilo Mkuu wa Mkoa alishafanya ziara katika ghala kubwa lililopo Mbeya linalomilikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji mwenye kampuni ya  Mo Enterprises ambapo alikuta Sukari ya kutosha jambo linalomshangaza kusikia wananchi wakilalamika upungufu wa sukari.

"Mimi mwenyewe nanunua sukari 3000," alisikika mmoja wa wanchi akisema wakati Mkuu wa Mkoa akiendelea kuhojiana na mmiliki wa ghala,Mselem Nassor ambapo kwenye ghala lake kulikuwa na Tani 70 za Sukari wakati Mkuu wa Mkoa alipofika hapo.

Mkoa wa Rukwa umepewa sukari Tani 200 na Serikali ili kupunguza shida ya bidhaa hiyo katika Mkoa huu, na katika Mkoa huu kuna maakala watatu ambao walitakiwa kupata Tani, 60,66 na 74 ili kutimiza tani 200 kwa Mkoa wa Rukwa.

"Nisisikie suari hii imekwenda nchi za nje, imefichwa au kulanguliwa, sukari hii imeletwa kwaajili ya wanarukwa na nawahakikishia warukwa kuwa hakuna shida ya Sukari na wananchi wasilanguliwe, yeyote atakaelanguliwa aje kushitaki, tutwawashughulikia," Mkuu wa Mkoa alisema kwa Msisitizo. 

Mwisho alimsifu mfanyabiashara Mselem Nassor kwa juhudi zak za kuleta Sukari kutoka Mbeya na Kuiuza Mkoani Rukwa. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisubiri ghala lifunguliwe aone Sukari iliyomo ndani

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiendelea kuhoji usambazaji wa Sukari hiyo katika Wilaya za Mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyeshika rununu na miwani) akisisitiza jambo mbele ya wakuu wapya wa wilaya aliyotoa kuwaapisha siku hiyo. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani) akisubiri kwenda kwenye ghala. (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Dk Halfan Haule, (kulia) ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiongoza Msafara wa kwenda kwenye ghala

Mselem Nassor akihojiwa na waandishi wa habari juu ya upatikanaji wa Sukari Moa wa Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitilia mkazo sukari isitoke na kuuzwa nje ya nchi


No comments:

Post a Comment