Thursday, September 15, 2016

Mkuu wa Mkoa aanza kushughulikia upatikanaji wa madawa katika zahanati za Mkoa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen amesikitishwa na hali mbaya ya ukosefu wa madawa katika vituo vya afya na zahanati nyingi zilizopo katika mkoa wake na kuahidi kulishughulikia suala hilo.

Aliyasema hayo baada ya kukutana na waganga wakuu wa Halmashauri ya Wilaya na Manispaa ya Sumbawanga pamoja na wakurugenzi wake, akiwemo mgamga mkuu wa mkoa katika kikao alichokifanya ofisini kwake.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na meneja wa MSD kanda ya nyanda za juu kusini Daudi Msasi ambae alipewa nafasi ya kuelezea namna upatikanaji na utoaji wa dawa kutoka bohari ya dawa hadi kufika katika vituo vya afya na Zahanati.

Ndugu Msasi alisema kuwa ucheleweshwaji wa pesa kutoka katika halmashauri umekuwa moja ya sababu ya wao kushindwa kufikisha dawa kwa wakati na kuongeza kuwa tangu kuagizwa kwa dawa hadi kupatikana kwake huchukua miezi sita, hivyo aliziomba halmashauri kupeleka pesa mapema ili dawa zipatikane mapema.

Mkuu wa mkoa pia alitaka kujua fedha za mfuko wa Basket Fund, CHF na NHIF zinapokwenda kama fehda hizo hazipo kwaajili ya kutatua matatizo ya wananchi pamoja na wanachama wa bima za afya.No comments:

Post a Comment