Monday, October 10, 2016

"Njooni Kalambo Falls Kuwekeza" Kamishna Mstaafu Zelote Stephen.

Maporomoko   ya kalambo yapo katika Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa, Ni maporomoko ya pili kwa urefu Africa baada ya Victoria Falls. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen Zelote. anawaasa wawekezaji wote kuweza kupeleka nguvu zao katika Maporomoko hayo ili kuvutia wawekezaji.5 comments:

 1. Shukrani kwa taarifa na video ya maporomoko ya Kalambo, ambayo nimekuwa nikiyasikia tu kijuu juu. Mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Ruvuma, ambaye niko huku ughaibuni, na nina blogu zangu--ya ki-Swahili na ya ki-Ingereza--na hiyo ya ki-Ingereza huwa ninaitumia kutangaza vivutio vya mikoa yetu ya kusini. Sasa baada ya kuona taarifa hii ya maporomoko ya Kalambo, nataandika nami kuhusu maporomoko hayo kwa ki-Ingereza. Kila la heri.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Asante sana kwa kuweza kuunga mkono Kutangaza vya Nyumbani, Letu ni kuzidi kukuombea matangazo yako yapate washabiki wengi kwa lengo la kuvuta watalii na wawekezaji zaidi. Kwa pamoja Tunaweza.

   Delete
 2. Mto kalambo unaanzia ndani Ranchi ya Taifa ya kalambo baada ya vyanzo vingi kukutana hapo na ndipo jina la Mto Kalambo linaanzia hapo lakini wenzetu nchi jirani ya Zambia wanautumia sana kitalii zaidi yetu na hata wanadai chanzo chake ni Zambia hii ina maana inakuwa kama Mlima Kilimanjaro uko Kenya ili hali si sahihi.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Asante kwa historia na Maelezo mazuri Kaka Tamim. Natumai wengi wamefaidika na wamelezo yako kama sisi tulivyofaidika.

   Delete