Wednesday, November 30, 2016

Sita wauawa katika ajali wakitokea Nkasi kwenda Sumbawanga mjini.

Gari iliyopata ajali.


Gari iliyopata ajali.


Gari iliyopata ajali


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) akipata maelezo ya kina ya majeruhi wa ajali akiwa na  Daktari Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa John Lawi 


Siti za Mbele kwa Dereva za gari hiyo


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh. Said Mtanda kushoto pamoja na RTO Sadik Msangi wakiwa katika eneo la tukio la ajali


Katika tukio la jali

Mauaji ya Mfugaji Mmoja Mwimbi


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen alipokwenda katika Kijiji cha Mwimbi, Wilaya ya Kalambo kuangalia eneo ambalo Mfugaji aliuawa  kwasababu ya kwenda kulishia mifugo yake kwenye shamba la Mkulima. 

Tuesday, November 22, 2016

Video: Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alipoongoza kikao cha maendeleo ya Elimu cha Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameendesha mkutano uliowajumuisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na waalimu wengine na wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa. ili kutafuta ufumbuzi wa kuusogeza mbele kielimu Mkoa wa Rukwa. 

Kikao hicho kilifanyika 5.7.2016.


Video: Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa alipojibu mabango ya wana Mandela - SumbawangaVideo: Mkuu wa Mkoa alipofanya Ziara ya Usafi wa Stendi Kuu: part 2


Monday, November 21, 2016

Mkuu wa Mkoa asisitiza upandaji miti Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamisna Mstaafu Zelote Stephen amesisitiza upandaji wa miti kwa wananchi wa moa wa Rukwa alipokuwa akipokea madawati 420 yaliyotolewa na mamlaka ya uhifadhi wa misitu nchini.

"Miti ni Uhai, Miti ni Ajira, Miti ni Uchumi, bila ya miti hatuwezi kuwa na madawati" Kamishna Mstaafu Zelote Stephen alisisitiza.

Karibu Mh. Makamba

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Sptehen alipomkaribisha Waziri za Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano. Mh. Januari Makamba katika Mkoa wa Rukwa. 


"Zingatieni upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mkoa" Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameishauri bodi ya ushauri wa hospitali ya rufaa kuwa makini na matumizi yanayotokana na mapato ya hospitali hiyo.

Mkuu wa Mkoa alishauri hayo alipokuwa akizindua bodi hiyo ambayo wajumbe wake waliteuliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ambao watadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa aliwakumbusha wajumbe wa bodi hiyo majukumu yao kuwa ni pamoja na kuboresha usimamizi wa Hospitali kupitia mpango wa mabadiliko ya hospitali "hospital reform", ushirikishwaji wa wananchi katika kusimamia huduma za Afya na kuleta uwiano wa kijinsia na uwakilishi wa watumiaji wa huduma katika usimamizi na maamuzi.

"Ndugu Wajumbe ninaimani kutoka na utaalamu na uzoefu wenu mliokuwa nao mtaweza kutekeleza majukumu mliyopewa na serikali". Mkuu wa Mkoa alisisitiza. 

Mkuu wa Mkoa pia alisisitiza upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo kwa kuimarisha duka lililopo ili kuepusha wananchi kuzunguka kutafuta huduma za madawa.

pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa aliwasisitiza washauri hao kuwasimamia na kuwachunga wafanyakazi ambao wanakauli chafu, wazembe, na kutowajali wagonjwa basi wasifumbiwe macho.

"Tungependa kuwa na watumishi waadilifu wenye kauli nzuri, wazalendo, kwasababu siku ya kwenda kutafuta kazi aliithamini na hivyo ni heri aiheshemu kazi, na aipende, kwani hospitali ni mahali pa kujali, kuwa na huruma kuokoa maisha ya watu, ni bora kuwa na watu wachache ambao wana maadili kuliko kuwa na wengi ambao hawafanyi kazi nzuri". Mkuu wa Mkoa alisisitiza.


Wednesday, November 16, 2016

Tuesday, November 8, 2016

Mkuu wa Mkoa atoa siku 7 kwa Manispaa kuwa safi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amempa siku 7 Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kuusafisha  mji wa Sumbawanga ikiwemo kuwachukulia hatua watu wote wanaochangia kuuchafua mji wa Sumbawanga kwa kutiririsha maji machafu kwenye mitaro.

Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo alipotembelea stendi kuu ya mabasi ya mji wa Sumbawanga wakati alipokuwa akifuatilia suala la usafi na hatimae kufanya mkutano wa dharura na wananchi wanaotumia stendi hiyo na kuamua kusikiliza vilio vyao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Saad Mtambule wakiongozana na wananchi katika kukagua usafi wa kituo cha mabasi yaendayo mikoa mbalimbali nchini pamoja na mapato  ya kituo hicho..

Katika mkutano huo wanachi mbalimbali walitoa madukuduu yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wakimtaka msaada awasaidie kwa matatizo wanayopambana nayo kila siku kutoka kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga pamoja na jeshi la polisi.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda (mwenye tai) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen wakikagua mapato ya Choo kilichopo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani ambacho ilikuwa kikifurika na hatimae kupelekea watumishi wanne wa Manispaa kuwekwa ndani wa muda wa masaa 24.

Mmoja wa wananchi hao bwana Stanslaus Lushanga aliomba dustbin la kuwekea uchafu kutolewa ndani ya stendi na kuhamishiwa nje, jambo ambalo lilipatiwa majibu hapo hapo na Afisa Mazingira wa Manispaa na kumwabia Mkuu wa Mkoa kuwa dustbin hilo likiondolewa wanachi hawataweza tena kutumia kituo hicho cha mabasi kwkuwa uchafu utasambaa kwa wingi bila ya uwa na sehemu ya kuhifadhia. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa kwaza kushoto,), Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, (wa pili kushoto) na  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Saad Mtambule wakimsikiliza kwa makini mwananchi Imani Fungo akitoa malalmiko yake juu ya ukarabati wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Manispaa ya Sumbawanga.

Nae mwendesha bodaboda Pascal Silvanus alimuomba mkuu wa mkoa awaelimishe kuhusu faini ya shilingi 30,000/= kwa wanaendesha bodaboda wanaopaki pikipiki zao ndani ya kituo hicho cha mabasi na kujibiwa kuwa bodaboda zote zinazopaki mlangoni zinpoingilia au kutokea mabasi ndizo hupigwa faini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisikiliza vilio vya wananchi.

“Natoa siku 7 sitaki kuona uchafu katika mji wa Sumbawanga, na nawaomba wananchi wote tushirikiane katika hili, sitaki mtu akamatwe kwa kuonewa, na watu wanaochafua mazingira wanajuana,” Mkuu wa Mkoa alisema.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephe (wa kati kati) akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Saad Mtambule pamoja na Afisa Mazingira wa Manispaa Hamidu Masare. 

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa suala la usafi ni la muhimu na ni la lazima, na kutoa mfano kuwa pindi tu Mheshimiwa Rais alipoingia ofisini jambo la kwanza alilolifanya ilikuwa ni usafi.

Kamishna MStaafu Zelote Stephen pia aliagiza dusbin kubwa linalotumiwa na wananchi wa hapo stendi kuondolewa kila linapojaa ili kuepusha uchafuzi wa mazingira katika stendi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maelekezo.

“Sasa agizo, asubuhi shughuli zinapoanza haya makontena yawe safi” Mkuu wa Mkoa aliagiza.
Katika Msafara huo wa kukagua usafi Kamishna MStaafu Zelote Stephen aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule.

Zoezi hili la kufuatilia usafi lilianza jana (tarehe 7/11/2016) ambapo Mkuu wa Mkoa alimuagiza Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule kuwachukulia hatua watumishi wote wa Manispaa ya Sumbawanga wanaohusika na usafi wa Manispaa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maelekezo.

“Mi nasema wachukuliwe hatua, cha kwanza na cha pili eneo hili libadilike, cha tatu kama hawafai kwenye nafasi zao watoe, huwezi ukawa na orodha ya watu ambao hawafanyi kazi,” Kamishna MStaafu Zelote Stephen aliagiza.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maagizo.
Baada ya Agizo hilo nae Dk. Haule aliliagiza jeshi la polisi kuwasimamia maafisa wanne wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya usafi katika eneo la Choo cha stendi kuu ya mabasi ya mji wa Sumbawanga na baada ya kumaliza wawekwe ndani.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiendelea na ukaguzi wa Usafi pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.


Maafisa hao waliochukuliwa hatua ni afisa mazingira wa Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Masare, Afisa Mtendaji wa kata ya Katandala, Charles kalulunga, Afisa Mtendaji wa Mtaa, Maria Ntura pamoja na Afisa Afya wa Kata, Edes Kakusa.

Tuesday, November 1, 2016

Muu wa Mkoa aingia shule ya Msingi Kufuatilia Mahudhurio


Mkuu wa Mkoa atoa pole kwa wafanyabiashara wa soko la MandelaMkuu wa Mkoa atoa maelekezo ya mgao wa Pembejeo msimu huu

Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa Mikoa 25 ya Tanzania Bara itakayonufaika na ruzuku ya pembejeo kwa maana ya Mbolea na Mbegu bora itakayotolewa na Serikali katika Msimu wa Mwaka 2016/2017. Ruzuku hii itatolewa kwa mazao mawili tu ya Mahindi na Mpunga kwa maana ya kufidia asilimia 30 ya bei ya soko kwa Mbolea na Mbegu bora za Mazao hayo.

Katika Msimu huu, ruzuku ya Pembejeo haitatolewa kwa mfumo wa Vocha kama ilivyokuwa imezoeleka, badala yake Mkulima atanunua moja kwa moja Pembejeo kutoka kwa Msambazaji kwa bei elekezi itakayopangwa na Wilaya. Kampuni ya Mbolea TFC, Wakala wa Mbegu ASA pamoja na Makampuni mengine ya Mbegu kupitia mawakala wao walioko Wilayani watakuwa na jukumu la kusambaza pembejeo kwa bei yenye ruzuku ya asilimia 30 hadi kwa Mkulima.

Mfumo huu wa utoaji wa Ruzuku ya Pembejeo unalenga kuongeza tija katika mazao ya Kilimo na kuhakikisha kuwa Mkoa unajitosheleza kwa chakula kwa kumuwezesha hata Mkulima mwenye kipato cha chini sana ambaye hawezi kupata pembejeo kwa bei ya soko aweze kupata mbolea na mbegu bora. Kwa kuzingatia hilo Mkoa wa Rukwa Msimu huu umepata mgao wa Tani 2,444 za Mbolea ya Kupandia, Tani 2,444 za Mbolea ya kukuzia na Tani 489 za Mbegu bora za Mahindi.

Natambua kwamba kiasi hiki cha pembejeo hakitoshi kwa mahitaji ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wapatao Kaya 250,952. Kiasi hiki cha Pembejeo kinatosha tu kunufaisha Kaya zipatazo 48,880 sawa na asilimia 19.47 ya kaya zote. Pia natambua kwamba sio maeneo yote ya Mkoa wa Rukwa yanafaa kwa kilimo chenye tija cha zao la Mahindi.


Kwa kuzingatia ratiba ya Kilimo natambua kwamba Mkoani Rukwa Mvua zitaanza kunyesha Mwanzoni mwa Mwezi Novemba kuanzia tarehe 10 hadi 15. Na pia Wataalam wa hali ya hewa wametuambia kwamba Mvua za Msimu huu zitakuwa kidogo. Hivyo, kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba taratibu za maandalizi ya kufikisha Pembejeo kwa Mkulima zinafanyika haraka sana kuanzia sasa. Kwa sababu hiyo napenda kuwaagiza Wakuu wa Wilaya wote Mkoani Rukwa Kuhakikisha Vikao vya Kamati za Pembejeo za Wilaya vinafanyika kati ya Tarehe 1-4 Novemba, 2016 kwa ajili ya maandalizi,

Kuhakikisha kwamba Vikao vya Kamati za Pembejeo za Vijiji Vinafanyika kati ya Tarehe 5-8 Novemba, 2016 hususan kuainisha Majina ya Wanufaika,Kuhakikisha kwamba hadi kufikia Tarehe 10 Novemba, 2016 Taarifa za Vikao vya Kamati za Pembejeo katika Ngazi za Vijiji zinawasilishwa Wilayani,Kuhakikisha kwamba hadi kufikia Tarehe 12 Novemba, 2016 Taarifa za Kamati ya Pembejeo ya Wilaya zinawasilishwa katika Ngazi ya Mkoa.

Kusimamia kikamilifu zoezi la usambazaji wa Pembejeo za Kilimo na kuhakikisha kwamba Wanufaika walioainishwa na Kamati za Pembejeo za Vijiji ndio wanatumia Pembejeo zenye ruzuku na sio wajanja wachache wenye pesa kushambulia pembejeo hizo.
Kuhakikisha kuwa elimu kwa wananchi juu ya uwepo wa mvua kidogo kwa mwaka huu inatolewa ili wakulima wetu waweze kuitumia vizuri na kuzalisha mazao ya kutosha. 

Wakulima wetu ambao hawatafikiwa na pembejeo hizo kuhakikisha wanajiunga katika Vikundi mbalimbali vya Kilimo kama AMCOS, SACCOS na Vikundi vinginevyo, ili kupitia Vikundi hivyo waweze kujipatia Mikopo ya Pembejeo zitakazotosheleza mahitaji yao badala ya kutegemea pembejeo zenye Ruzuku ambazo hazitoshelezi. Lengo ni kuona kwamba kila Mkulima anapata pembejeo ili Kilimo chetu kiwe na tija kwa maisha ya Wakulima wetu na taifa kwa jumla.

zaidi angalia video