Tuesday, November 8, 2016

Mkuu wa Mkoa atoa siku 7 kwa Manispaa kuwa safi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amempa siku 7 Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kuusafisha  mji wa Sumbawanga ikiwemo kuwachukulia hatua watu wote wanaochangia kuuchafua mji wa Sumbawanga kwa kutiririsha maji machafu kwenye mitaro.

Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo alipotembelea stendi kuu ya mabasi ya mji wa Sumbawanga wakati alipokuwa akifuatilia suala la usafi na hatimae kufanya mkutano wa dharura na wananchi wanaotumia stendi hiyo na kuamua kusikiliza vilio vyao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Saad Mtambule wakiongozana na wananchi katika kukagua usafi wa kituo cha mabasi yaendayo mikoa mbalimbali nchini pamoja na mapato  ya kituo hicho..

Katika mkutano huo wanachi mbalimbali walitoa madukuduu yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wakimtaka msaada awasaidie kwa matatizo wanayopambana nayo kila siku kutoka kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga pamoja na jeshi la polisi.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda (mwenye tai) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen wakikagua mapato ya Choo kilichopo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani ambacho ilikuwa kikifurika na hatimae kupelekea watumishi wanne wa Manispaa kuwekwa ndani wa muda wa masaa 24.

Mmoja wa wananchi hao bwana Stanslaus Lushanga aliomba dustbin la kuwekea uchafu kutolewa ndani ya stendi na kuhamishiwa nje, jambo ambalo lilipatiwa majibu hapo hapo na Afisa Mazingira wa Manispaa na kumwabia Mkuu wa Mkoa kuwa dustbin hilo likiondolewa wanachi hawataweza tena kutumia kituo hicho cha mabasi kwkuwa uchafu utasambaa kwa wingi bila ya uwa na sehemu ya kuhifadhia. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa kwaza kushoto,), Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, (wa pili kushoto) na  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Saad Mtambule wakimsikiliza kwa makini mwananchi Imani Fungo akitoa malalmiko yake juu ya ukarabati wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Manispaa ya Sumbawanga.

Nae mwendesha bodaboda Pascal Silvanus alimuomba mkuu wa mkoa awaelimishe kuhusu faini ya shilingi 30,000/= kwa wanaendesha bodaboda wanaopaki pikipiki zao ndani ya kituo hicho cha mabasi na kujibiwa kuwa bodaboda zote zinazopaki mlangoni zinpoingilia au kutokea mabasi ndizo hupigwa faini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisikiliza vilio vya wananchi.

“Natoa siku 7 sitaki kuona uchafu katika mji wa Sumbawanga, na nawaomba wananchi wote tushirikiane katika hili, sitaki mtu akamatwe kwa kuonewa, na watu wanaochafua mazingira wanajuana,” Mkuu wa Mkoa alisema.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephe (wa kati kati) akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Saad Mtambule pamoja na Afisa Mazingira wa Manispaa Hamidu Masare. 

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa suala la usafi ni la muhimu na ni la lazima, na kutoa mfano kuwa pindi tu Mheshimiwa Rais alipoingia ofisini jambo la kwanza alilolifanya ilikuwa ni usafi.

Kamishna MStaafu Zelote Stephen pia aliagiza dusbin kubwa linalotumiwa na wananchi wa hapo stendi kuondolewa kila linapojaa ili kuepusha uchafuzi wa mazingira katika stendi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maelekezo.

“Sasa agizo, asubuhi shughuli zinapoanza haya makontena yawe safi” Mkuu wa Mkoa aliagiza.
Katika Msafara huo wa kukagua usafi Kamishna MStaafu Zelote Stephen aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule.

Zoezi hili la kufuatilia usafi lilianza jana (tarehe 7/11/2016) ambapo Mkuu wa Mkoa alimuagiza Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule kuwachukulia hatua watumishi wote wa Manispaa ya Sumbawanga wanaohusika na usafi wa Manispaa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maelekezo.

“Mi nasema wachukuliwe hatua, cha kwanza na cha pili eneo hili libadilike, cha tatu kama hawafai kwenye nafasi zao watoe, huwezi ukawa na orodha ya watu ambao hawafanyi kazi,” Kamishna MStaafu Zelote Stephen aliagiza.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maagizo.
Baada ya Agizo hilo nae Dk. Haule aliliagiza jeshi la polisi kuwasimamia maafisa wanne wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya usafi katika eneo la Choo cha stendi kuu ya mabasi ya mji wa Sumbawanga na baada ya kumaliza wawekwe ndani.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiendelea na ukaguzi wa Usafi pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.


Maafisa hao waliochukuliwa hatua ni afisa mazingira wa Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Masare, Afisa Mtendaji wa kata ya Katandala, Charles kalulunga, Afisa Mtendaji wa Mtaa, Maria Ntura pamoja na Afisa Afya wa Kata, Edes Kakusa.

No comments:

Post a Comment