Monday, November 21, 2016

"Zingatieni upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mkoa" Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameishauri bodi ya ushauri wa hospitali ya rufaa kuwa makini na matumizi yanayotokana na mapato ya hospitali hiyo.

Mkuu wa Mkoa alishauri hayo alipokuwa akizindua bodi hiyo ambayo wajumbe wake waliteuliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ambao watadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa aliwakumbusha wajumbe wa bodi hiyo majukumu yao kuwa ni pamoja na kuboresha usimamizi wa Hospitali kupitia mpango wa mabadiliko ya hospitali "hospital reform", ushirikishwaji wa wananchi katika kusimamia huduma za Afya na kuleta uwiano wa kijinsia na uwakilishi wa watumiaji wa huduma katika usimamizi na maamuzi.

"Ndugu Wajumbe ninaimani kutoka na utaalamu na uzoefu wenu mliokuwa nao mtaweza kutekeleza majukumu mliyopewa na serikali". Mkuu wa Mkoa alisisitiza. 

Mkuu wa Mkoa pia alisisitiza upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo kwa kuimarisha duka lililopo ili kuepusha wananchi kuzunguka kutafuta huduma za madawa.

pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa aliwasisitiza washauri hao kuwasimamia na kuwachunga wafanyakazi ambao wanakauli chafu, wazembe, na kutowajali wagonjwa basi wasifumbiwe macho.

"Tungependa kuwa na watumishi waadilifu wenye kauli nzuri, wazalendo, kwasababu siku ya kwenda kutafuta kazi aliithamini na hivyo ni heri aiheshemu kazi, na aipende, kwani hospitali ni mahali pa kujali, kuwa na huruma kuokoa maisha ya watu, ni bora kuwa na watu wachache ambao wana maadili kuliko kuwa na wengi ambao hawafanyi kazi nzuri". Mkuu wa Mkoa alisisitiza.


No comments:

Post a Comment