Monday, December 26, 2016

Mh. Zelote Stephen Awapa pole na kuwatahadharisha wananchi kujenga nyumba Imara kuepuka maafa.Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akielezea namna nyumba zilivyokuwa hazina uimara katika moja ya nyumba iliyopata maafa katika kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen amewatahadharisha wananchi wa mkoa wa Rukwa kujenga nyumba zenye kufuata taratibu za kitaalamu ili kuweza kuhimili mvua za upepo

Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo alipokwenda kutembelea na kuwapa pole wanakijiji wa kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga, waliopotelewa na nyumba zaidi ya Ishirini zilizoezuliwa paa pamoja na kuanguka kwa kuta za nyumba hizo.

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa mbali na kujenga nyumba imara lakini pia wananchi wanapaswa kuzingatia kupanda miti kwa wingi ili upepo upambane na miti kabla ya kukutana na nyumba.

"Ukiangalia nyumba nyingi zinajengwa kwa udongo wa kawaida bila ya kutumia udongo ulaya (cement), sasa hapa unakaribisha hatari na tofari zenyewe ni nzito sana, zinashikiliwa na udongo kidogo, halafu miti pia hakuna ambayo inazunguka nyumba ili kuweza kupambana na upepo mkali" Mkuu wa Mkoa alifafanua. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa katika moja ya nyumba iliyopata maafa katika kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga.

Moja ya Nyumba iliyopata maaafa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa katika moja ya nyumba iliyopata maafa katika kijiji cha Mwela, Kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga. 
No comments:

Post a Comment