Saturday, December 24, 2016

Mh. Zelote Stephen ameagiza duka la Dawa kufungwa baada ya Kugundua kuwa muuzaji hana sifa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameagiza duka la dawa hadi hapo muuzaji huyo atakapopata mafunzo ya ADO ili kuepusha madhara kwa wananchi anaowauzia dawa hizo.

Mh. Zelote aliagiza hayo baada ya kutembelea duka la dawa muhimu katika kijiji cha Mwela kata ya Mtowisa ambapo alitembelea watu waliopatwa na maafa katika kijiji hicho.

Duka hilo ambalo lilifanyiwa ukaguzi na watumishi kutoka Wizara ya Afya tangu tarehe 9.11.2016 nakubainika na makosa kadhaa ikiwemo muuza dawa hizo kutokuwa na sifa za kuuza dawa na “Shelf” za kuwekea dawa kutokuwa na ubora unaotakiwa, na kutolipia leseni ya mwaka 2016/2017.

Watumishi hao wa Wizara ya Afya waliagiza muuza dawa huyo kupelekwa kwenye mafunzo ya ADO, pamoja na kulipia leseni, na kurekebisha “Shelf”.
Makosa ambayo yalitakiwa kurekebishwa hadi kufikia tarehe 23.11.2016, lakini hadi Mh. Zelote anafika katika duka hilo, Muuzaji bado alikuwa anaendelea kutoa huduma bila ya kukamilisha agizo lolote kati ya maagizo yaliyotolewa na Wizara ya Afya.

Daktari Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Kabuga alithibitisha kuwa ukaguzi huo ulifanyika na maagizo hayo yalitolewa lakini hawakujua kama bado duka hilo linaendelea kutoa huduma.


Mmiliki wa duka hilo Bi. Leticia Mtama hakuweza kupatika na hatimae muuza duka kuachiwa maagizo ya kufunga duka hadi hapo atakapokamilisha maagizo hayo. 


No comments:

Post a Comment