Friday, December 9, 2016

Mkuu wa Mkoa ahimiza upandaji wa miti siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen Zelote amewaagiza wakuu wa ke wa wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri zao pamoja na wananchi kuwa na kiwanda angalau kimoja ili kutekeleza kauli mbiu ya maadhimisho miaka 55 Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vitendo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akipanda Mti katika siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Jamhuri ya Muu ngano wa Tanzania. 
Ameyasema hayo wakati alipomaliza kupanda mti kama ishara ya maadhimisho ya siku ya uhuru yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na watumishi wote wa ofisi yake.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Ndugu Tixon Nzunda pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen wakipanda miti katika kuadhimisha miaka 55 ya uhuru wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
amewataka watumishi wote kila mmoja kuwa na mti wake ambao atauhudumia hadi kukua kwa mti huo, hii ikiwa ni mwanzo wa kampeni ya upandaji miti ili kuuokoa Mkoa wa Rukwa kugeuka kuwa jangwa.

Katika kutekeleza Kauli mbiu ya siku ya Uhuru wa Vitendo Mkuu wa Mkoa amezitahadharisha Halmashauri hasa idara ya ardhi, elimu, afya na mahakama juu ya kukithiri kwa rushwa.
Watumishi mbalimbali wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Rukwa walivyoshiriki katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupanda miti. 
"Tunajua kwamba rushwa ni kirusi kwa haya maendeleo ambayo serikali yetu imepania kuyaleta, hatutakubali yawepo," Mkuu wa Mkoa alisisitiza.

Pia amewataka wananchi kuwa huru kuitumia taasisi ya kupambana na rushwa katika kuripoti mtukio mbalimbali yenye harufu ya rushwa na kusisitiza kuwa wananchi wasitoe taarifa baada ya rushwa. 
Watumishi mbalimbali wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Rukwa walivyoshiriki katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupanda miti.
"Wananchi wasitoe taarifa baada ya rushwa maana aliyetoa na aliyepokea wote ni wahalifu, kwa maana hiyo tuhakikishe tunatoa taarifa za vitendo vya rushwa mapema," Mkuu wa Mkoa alifafanua. 


No comments:

Post a Comment