Saturday, December 24, 2016

"Tuko mbioni kumalizia mahakama 10 za kisasa," Mh. Mohamed Chande Othman

Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Cahnde Othman amesema Tanzania iko mbioni kumalizia ujenzi wa mahakama 10 za teknolojia ya kisasa, za ujenzi wa bei nafuu na zenye uimara ili ziwe za mfano. katika kutoa huduma kwa teknolojia ya kisasa.
Kutoka kushoto, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Otheman, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kanda ya Sumbawanga Mh. Mgeta, Mtendaji Mkuu wa watumishi wa Mahakama, Emanuel Munda.

Mh. Chande ameyasema hayo alipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika ziara yake ya siku mbili Mkoani hapa.

Katika ziara hiyo Mh. Chande amekiri kuwa mahakama zina mzigo mzito wa kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutoa hukumu mapema ili wananchi wawe na imani na mfumo wa kupata haki zao.

Katika kusherehesha hilo Mh. Chande hakuacha kulishukuru jeshi la polisi kwa kuhakikisha upepelezi unamalizika mapema na pia aliupongeza MKoa wa Rukwa kwa kutokuwa na malalamiko mengi ya wahukumiwa kupata nakala zao za hukumu pindi tu hukumu inapofikiwa.
Kutoka kushoto, Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Otheman, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kanda ya Sumbawanga Mh. Mgeta, 
Mh. Chande aliongeza kuwa pamoja na Tanzania kuwa na mahaka za mwanzo 960 ambazo zinashikilia asilimia 72 mashauri ya kesi za nchi nzima, bado mhimili wa mahakama unahitaji kupewa nguvu zaidi ili kuweza kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.

Jambo ambalo lilimfanya amsifu Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuweza kuliona hilo na kuwapatia shilingi Bilioni 12.3 ili kuweza kuanza kuimarisha mhimili huo.

Mh. Chande aliyazungumza hayo baaada ya kusikiliza risala fupi iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ambaye alielezea upungufu wa mahakimu katika mahakama za mwanzo jambo ambalo linapelekea ucheleshwaji wa kesi na kuleta hisia mbaya kwa wananchi na kuwafanya wahisi kesi ambazo hucheleshwa ni kwasababu ya rushwa.No comments:

Post a Comment