Sunday, January 8, 2017

Mh. Zelote awatahadharisha wananchi kujiwekea akiba ya chakula baada ya mavuno

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kutouza mazao yote watakayopata baada ya mavuno na badala yake wajiwekee akiba ya chakula cha kutosha.
aliyasema hayo alipokuwa akimalizia ziara yake ya kupita kwa maafisa kilimo ili kujua utendaji wao wa kazi katika kuwasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija.
Pamoja na hayo aliwaasa kupanda mazao yenye kuhimili ukame, kama mihogo, viazi, karanga n.k. alipotembelea kijiji cha malagano na kukutaa kvikundi vya wakulima katika kijiji hicho.No comments:

Post a Comment