Sunday, February 26, 2017

Mh. Zelote Stephen aagiza Dosari zirekebishwe ujenzi wa barabara ya Ntendo - Muze

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amishna Mstaafu Zelote Stephen amemuagiza Meneja wa TANROAD Mkoa Eng. Masuka Mkian kusimamia kwa makini ujenzi wa barabara ya Ntendo - Muze ili kuepuka kurudia ujenzi wa barabara hiyo na kupoteza pesa za serikali.

Ameyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo barabara za Kalambazite - ilemba, Miangalua - Kipeta, Mtowisa - Ilemba,  Kasansa - Muze, Kaoze - Kilyamatundu, na Ilemba - Kaoze.

Mh. Zelote amewataka TANROADS kuwa makini na pia kufanya kazi na wakandarasi ambao ni waaminifu wasiowababaishaji ili kutolipua ujenzi wa barabara hizo na kuisababishia serikali hasara na kuwapa tabu wananchi wanaozitegemea barabara hizo katika kukuza uchumi wao.

No comments:

Post a Comment