Wednesday, June 28, 2017

AJALI YA GARI KUGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA RUKWA
                         KWA VYOMBO VYA HABARI.
“PRESS RELEASE TAREHE 28.06.2017”

Mnamo tarehe 27/06/2017 majira ya saa 10:05 huko Kipundu Kala, tarafa ya Namanyere, wilaya ya Nkasi mkoa wa Rukwa.
Gari No.T 790 DEM TATA Truck mali ya ASSIF ASHRAF HASSAM ikiendeshwa na JOSEPHAT SALYA, Ilimgonga mtembea kwa miguu aitwaye ELIUD STEVEN, mwenye umri wa miaka 5,Mfipa, Mkazi wa Kipundu Kala na kumsababishia kifo cha papo hapo.
Chanzo cha ajalia ni uzembe wa dereva kushindwa kujali watumiaji wengine wa barabara.
Mwili wa marehemu  imekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi.
Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi GEORGE SIMBA KYANDO   anatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara kuwa makini hasa kwa kufuata na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepukana  ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani.

Imesainiwa na;

(G.S.KYANDO  -ACP )

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUKWA

No comments:

Post a Comment