Thursday, August 31, 2017

RC Rukwa atoa miezi miwili kukamilishwa kwa barabara Mollo - Songambele Azimio

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri ya Sumbawanga vijiji na Manispaa kuhakikisha wanamalizia ujenzi wa barabara ya Mollo - Songambele Azimio kabala ya Msimu wa Mvua kuanza.
Ametoa agizo hilo baada ya kutembelea katika kijiji hicho kuona maendeleo ya miti aliyoshiriki kuipanda pamoja na wanakijiji hao katika maadhimisho ya siku ya kupanda miti kimkoa tarehe 19/1/2017 ambapo siku hiyo aliahidi kuwajengea barabara hiyo.
"Wakurugenzi nataka kabla ya Mvua kunyesha barabara hiyo iwe tayari, Mkurugenzi wa Sumbawanga Vijiji kwakuwa wewe umesema kipande chako ni kidogo sana basi ukimaliza kesho nitafurahi sana." Alisema.
Nao kwa upande wao kila mmoja baada ya kupewa nafasi Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Suumbawanga Saad Mtambule alisema kuwa barabara hiyo imeshaanza matengenezo kwa kiwango cha changarawe na kuwa inaendelea vizuri.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini Nyangi Msema Kweli aliahidi kuwa ahizo hilo litatekelezwa kwani tangu ahadi itolewe mwanzoni mwa mwaka huu, halmashauri ilishaiweka barabara hiyo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 na kuwaahidi kuwa pesa ipo ya kufanaya matengenezo hayo.
msisitizo huo uliibuka baada ya Diwani  wa Msanda muungano Mh. Charles Kanoni kuanza kufanya mikutano na kuwaambia wananchi kuwa barabara hiyo haitatengenezwa kakuwa haikuwa kwenye bajeti yoyote ya halmashauri ya Sumbawanga Vijijini jambo ambalo lilimshtua Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule.
Dk. Haule alisisitiza kuwa alitegemea diwani kuwa mstari wa mbele kuhamasisha maendeleo na badala yake anakuwa kinyume na matarajio ya wanakijiji na kumuonya kutojihusisha na kusema uongo kwa wananchi ili ajitengenezee ulaji na kuongeza kuwa serikali ya awamu hii inatekeleza ahadi zake zote na hakuna ahadi itakayotolewa ambayo haitatekelezwa.
Ziara hiyo ilikuwa maalum kwaajili ya kuhamasisha upandaji wa miti katika kijiji hicho ili kiwe cha mfano katika Wilaya na Mkoa wa Ujumla juu ya upandaji wa Miti.
Aidha, Mh. Zelote pia aliahidi kukisaidia kikundi cha ngoma cha Mwalimu Nyerere cha kijiji hicho kuimarisha vifaa vyao na hatimae kuendelea kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kujiongezea kipato katika shughuli zao za kila siku.
"Kama nilivyoahidi nilipokuja mwanzoni mwa mwaka huu leo hii nimetoa shilingi 167000 kwa kikundi hiki ili waboreshe vifaa vyao vya kazi," RC alisema.
Na kuwaomba wadau mbalimbali wa utamaduni kujitokeza kusaidia kuuinua utamaduni wa wafipa na wa mkoa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa KamishnamStaafu Zelote Stephen akiwahakikishia wananchi wa kijiji cha Songambele Azimio ujenzi wa barabara 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa KamishnamStaafu Zelote Stephen akiwa amekaa na wanakijiji cha Songambele azimio. 

Kikundi cha ngoma za asili cha kina mama cha Mwalimu Nyerere cha Kijiji cha Songamebele Azimio wakipita kwa gwaride rasmi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa KamishnamStaafu Zelote Stephen.

Kikundi cha ngoma za asili cha kina mama cha Mwalimu Nyerere cha Kijiji cha Songamebele Azimio wakipita kwa gwaride rasmi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa KamishnamStaafu Zelote Stephen.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kulia) akihojiana na mtaalamu wa gwaride katika kijiji cha Songambele Azimio Bwana Kalikenya Kaziote (kushoto) huku wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule. 

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Halfan Haule akitoa tahadhari kwa wakulima waliolima kwenye vyanzo vya maji kuwa oresheni kali itafanyika kuwaondoa wakulima hao ili kulinda vyanzo vya maji na kuokoa mazingira. 


RC Rukwa aagiza wafanyabiashara kufunga maduka kufanya Usafi “Magufuli Day”

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wafanyabiashara hawafungui biashara zao bila ya kufanya usafi katika maeneo wanayofanyia biashara.
Agizo hilo lilitolewa baada ya Mkh. Zelote kufika katika soko kuu la mji wa Sumbawanga na kutokuta hata mfanyabiashara mmoja wa soko hilo akifanya usafi na huku uchafu katika eneo hilo ukiwa umekithiri katika siku hiyo ya usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi maarufu kama Magufuli day.
Aidha Mh. Zelote alikuta askari wa usalama wa raia wakiendelea na usafi wa soko hilo na maeneo yanayozunguka soko hilo na kutokuwa na hata afisa mtendaji wa mtaa aliyekuwa akisimamia ama kuhamasisha usafi katika maeneo hayo hali iliyomfanya kuagiza waitwe uongozi wa mtaa na Mkurugenzi ili kuwaonya.
“Siku hii imetungiwa sharia kabisa ili watanzania wote washiriki kwenye usafi, badala yake mnalala mnategemea jeshi ndio linawafanyie kazi, kwani jeshi wameajiriwa kwasababu hiyo, wanakazi nyingi za kufanya, kama Mkurugenzi wa Manispaa ni jukumu lako kuhakikisha Manispaa inakuwa safi, kwani imekuwa nafasi ya 17 si kwasababu ya msukumo tunaoufanya bila ya hivyo ingekuwaje,” Alisema.
Amesisitiza kuwa usafi ni kila siku na jumamosi ya mwisho wa mwezi imewekwa kama ukumbusho wa kuendelea na usafi Katika maeneo yote yam ji, majumbani na kwenye maeneo ya biashara.
Katika zoezi hilo Mh. Zelote alishiriki kufanya usafi na kukagua Soko kuu la Manispaa lililopo kata ya Mazwi pamoja na Soko la Sabasaba linalomilikiwa na Chama tawala cha CCM pamoja na kusikiliza kero kadhaa za wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Sabasaba.

Mtaa wa Soko Kuu, Sumbawanga, Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu zelote Stephen (kushoto) akiwa ameongozana na Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa ACP George Kyando, wakitembea kukagua usafi siku ya Usafi katika barabara ya Sumbawanga - Mpanda. Mjini Sumbawanga.

Usafi Uiendelea siku ya jumamosi ya Usafi. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu zelote Stephen akishiriki kwenye Usafi wa siku ya Usafi 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu zelote Stephen akishiriki kwenye Usafi wa siku ya Usafi 

Maduka ya Soko Kuu la Mji wa Sumbawanga yakiwa yamefungwa kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu zelote Stephen kwa wafanyabiashara kushiriki kwenye usafi. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen 


Wednesday, August 30, 2017

RC Rukwa atoa masaa 24 kutawanywa kwa vifaa vya afya vya Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna mstaafu Zelote Stephen amempa masaa 24 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo kuhakikisha vifaa vya huduma za Afya vilivyorundikwa katika zahanati ya Kasanga anavitawanya na kuanza kutumika katika zahanati hiyo na nyinginezo ili kusaidia upungufu wa vitanda uliopo kwenye zahanati hizo.
Vifaa vya Afya,  Msaada wa Rais vikiwa Stoo katika Zahanati ya Kasanga, Wilayani Kalambo, Mkoa wa Rukwa. 

Alitoa agizo hilo baada ya kuvikuta vitanda vitano, magodoro matano pamoja na mashuka kumi ya hospitali yakiwa yamehifadhiwa kwenye store ya dawa ya zahanati hiyo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea hali halisi ya iwepo wa madawa na huduma zinazopatikana katika zahanati hiyo inayohudumia wananchi zaidi ya 2000.

Vifaa hivyo ni miongoni mwa Vitanda 16 vyakuzalishia, Vitanda 80 vya Wagonjwa, Magodoro 80, na Mashuka 200 vilivyotolwa kwa Mkoa wa Rukwa ambavyo alivigawa Mh. Zelote tangu tarehe 27/7/2017 kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli aliyetoa vifaa hivyo kwenye halmashauri zote nchini ili kusaidia upungufu wa vifaa hivyo kwenye vituo vya afya na zahanati na kuboresha huduma za afya nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu zelote Stephen (Kulia) akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kalambo (kushoto)
“Mh. Rais hakutoa vifaa hivi ili vije kukaa kwenye stoo wakati kuna wananchi huko wanalala chini, mpaka kufikia kesho nitaagiza gari ije kuvibeba ili vikatumike kwa zahanati zenye shida zaidi maana ninyi hamna shida,” Mh. Zelote Alisema.
Pamoja na hayo Mh. Zelote aligundua kuwa Zahanati hiyo haina Mganga na baada ya kuhoji alijibiwa kuwa Mganga wa Hospitali hiyo yupo masomoni na tangu mwezi wa sita mwaka huu ameanza mitihani yake hali ambayo ilimstaajabisha Mh. Zelote na kuahidi kulishughulikia jambo hilo.

RC Rukwa azuia tani 2143 za madini kusafirishwa nje ya nchi

Katika kasi ya kuhakikisha madini ya watanzania yanawafaidisha watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya “Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda nje ya nchi hadi hapo atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.
Bandari ya Kasanga, Rukwa.

Sakata hilo liliibuka baada ya Mh. Zelote kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Kasanga Iliyopo Wilayani Kalambo mpakani  na nchi ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kupitia Ziwa Tanganyika.

Usafirishaji wa madini hayo umekuwa ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini Mbeya tangu mwezi wa pili mwaka 2017 kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini Bujumbura, ambapo mpaka Mh. Zelote anazuia uuzwaji huo, tayari walikuwa wameshauza tani 4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa dola za kimarekani 128.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akikagua shehena ya mifuko ya Saruji iliyokwama katika bandari ya Kasanga, Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
Wakati Mh. Zelote akiendelea na ukaguzi  katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya Mbeya Cement ina mzigo wa tani 2050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo tangu mwezi November mwaka 2016 na alipoulizwa mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Mbeya Sabas Sokoni alisema kuwa Saruji hiyo imekosa wateja.
“Sisi tunajuwa kwamba bandari hii inapokea Simenti na kuuzwa nchi za jirani, haya ni madini, Haiwezekani tukadanya kwamba tunapeleka madini kumbe tunapeleka “raw materials” kutoka Tanzania kwajili ya kutengeneza simenti, kila siku tunazungumza suala la kuongeza thamani ya vitu vyetu ili tuuze “finished products” na sio “raw materilas.” Mh. Zelote alisema.
Na kuongeza kuwa Utaratibu uliopo ni kwamba Simenti inazalishwa Tanzania na kuuzwa nje ya nchi na sio utaratibu wa kusafirisha udongo wa kutengenezea Simenti na kuhoiji kuwa kwanini udongo huo uwe na soko zaidi kuliko Simenti yenyewe.  
Wakati Mh. Zelote akitoa zuio hilo tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye namba za usajili BY 0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi.
Kwa upande wake afisa wa bandari hiyo Suleiman Kalugendo hakuona tatizo mbali na vibali vya usafirishaji wa madini hayo kuwa na mashaka.

RC Rukwa Kuuza chakula nchi nzima

Mkuu wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameitaka mikoa yenye upungufu wa chakula nchini kuorodhesha mahitaji yao kupitia ngazi zilizopo ili wanunue bidhaa hiyo ili kuondokana na hofu ya upungufu wa chakula nchini.
Moja ya Mashine ya kutenga pumba na mahindi katika Shamba la Msipazi. 

Pia aliwaomba wakuu wa mikoa kuwahamasisha wafanyabiashara wao wafike Mkoani kwake kununua bidhaa hiyo badala ya wakulima kuanza kukimbiza chakula hicho nje ya nchi, ambapo kwa msimu wa mwaka wa mavuno 2016/2017 Mkoa umevuna tani Milioni 1.1 za chakula huku zao la mahindi peke yake likiwa ni tani 710,652.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (suti ya Bluu - katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wataalamu mbalimbali wa Mkoa na Halmashauri zake. 
“Nichukue nafasi hii kuthubutu kuiambia mikoa mingine ambayo haijapata bahati ya kuvuna kama kama tulivyovuna sisi watumie fursa hii watuambie kupitia ngazi zilizopo kwamba wanahitaji nini, hili ni kwa Tanzania bara na visiwani, tunawakaribisha kufanya biashara na sisi,” Alisema.
Shehena ya Mahindi iliyopo katika Ghala la shamba la Msipazi ni miongozi 
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kilimo cha kisasa yaliyoshirikisha uongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri zake katika shamba la Msipazi lenye ukubwa wa ekari 4,420 lililopo katika Kijiji cha China, Kata ya Kate,Wilayani Nkasi mali ya Salum Summry.
Mh. Zelote ameonya kuwa hakuna  mwananchi atakayepewa chakula cha msaada kutoka serikalini kutokana na njaa, hivyo aliwaonya wanannchi wa mkoa huo kuachana na tabia ya kuuza chakula na badala yake waache akiba katika nyumba zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (suti ya Bluu) akitoa maelekezo kwa viongozi na wataalamu mbali mbali wa Mkoa juu ya kuboresha huduma za kilimo katika Mkoa. 
“Sisi siyo wachoyo, uchoyo wetu ni kuhakikisha wananchi wetu wanakuwa na akiba ndani ya nyumba zao, na wale wanaouza mazao wahakikishe wanatenga fedha zinazotokana na mauzo hayo kwaajili ya kununua pembejeo za msimu wa kilimo unaofuata,” Amesema.
Katika kuhakikisha wakulima wanaondokana na adha ya mbegu feki na ubabaishwaji wa bei za pembejeo Mh. Zelote amewaagiza wauzaji wa pembejeo hizo kuweka mabango ya bei nje ya maduka yao na kuwaagiza wakuu wa wilaya kuwachukulia hatua wale wote watakaogundulika kuuza mbegu feki.
Mbali na hayo Mh. Zelote amesema kuwa anataka kusikia mkoa wa Rukwa unakuwa wa kwanza nchini kwa uzalishaji wa chakula baada ya kuwa wa tatu ukitanguliwa na Ruvuma na Mbeya, hivyo aliwataka wale ambao hawalimi kuonja utamu wa kilimo kwa kulima japo ekari moja.
“Naambia Mkoa wa Mbeya umekuwa wa Kwanza, tujiulize wametuzidi nini, mkoa wa Ruvuma umekuwa wa Pili, wametuzidi nini, sasa mwaka huu nataka kusikia mkoa wa Rukwa umekuwa wa kwanza ama wote watatu tushike namba moja,” alimalizia.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (suti ya Bluu) akiwa na uongozi mzima wa Mkoa wa Rukwa walipofanya ziara katika shamba la Msimpazi linalomilikiwa na Salum Summry ili kujione ana kujifunza kilimo bora na cha kisasa ili kuboresha miundo mbinu ya kilimo katika Mkoa. 
Awali alipokuwa akisoma taarifa ya shammba hilo, Mkurugenzi wa Shamba la Msipazi Salum Summry amesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazorudisha nyuma juhudi za wakulima katika Mkoa wa Rukwa ni uwepo wa mbegu zisizo na ubora “Fake” pamoja na wadudu waharibifu wa mazao.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa suala la mbegu feki limekuwa likirudisha nyuma juhudi zetu kama wakulima ambao tunaanza kuchipukia, na pia msimu huu tulishambuliwa na wadudu jamii ya viwavi jeshi lakini nichukue nafasi hii kukushukuru wewe binafsi, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri kwa mlivyotusaidia kukabiliana na wadudu hao kwa kuwezesha kupata ndege ya kunyunyizia madawa n ahata mafuta ya ndege kwaajili ya kazi hiyo,” Salum Summry alisema.
Naye Mstahiki Meya wa manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwahamasisha wananchi wa Rukwa kulima na kuongeza thamani katika mazao yao.

Sunday, August 20, 2017

SERIKALI imesema inaendelea kuboresha huduma za afya ya uzazi namtoto ili wajawazito wanaohudhuria kliniki na kujifungulia katika vituovinavyotoa huduma ya afya 2020.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wananwake jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akifafanua namna mkoa wa Rukwa Ulivyofanikiwa katika kuboresha huduma ya mama na mtoto

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu mjini Nkasi akiwa katika ziara ya kikaziya siku mbili katika mkoa wa Rukwa. Alisema wajawazito wanaohudhuria nakujifungulia kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya imefikia asilimia 95 hukukitaifa ikiwa asilimia 64.
“Niwapongezeni Rukwa maana tayari mmefikia asilimia 95 yawajawazito wanaojifungulia katika vituo vinavyotoa huduma za afya hata kabla ya2020 hongereni sana ndio maana vifo vya wajawazito mkoani hapavinavyosababishwa na matatizo ya uzazi viko chini,” alisema.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wananwake jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika picha pamoja na viongozi wa mkoa wa Rukwa pamoja na viongozi wa Hospitali teule ya Wilaya ya Sumbawanga Dk. Atman. 
Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Boniface Magangaalimueleza Waziri Mwalimu kuwa vituo 214 kati ya 223 vilivyopo mkoani humovinatoa huduma muhimu ya uzazi na mtoto ambapo wajawazito 161,089 walihudhuriakliniki mwaka 2016.
Aliongeza kuwa katika kipindi hicho wajawazito 43, 938 kati yao41,698 ikiwa ni sawa na asilimia 95 walijifungulia katika vituo vinavyotoahuduma ya afya ambapo 2,240 sawa na asilimia 15 walijifungulia nje ya vituo hivyo.Aidha, watoto wapatao 47,268 wenye umri chini ya mwaka mmoja walipatiwa chanjoikiwa ni asilimia 93 ya watoto 50,728 waliotarajiwa kupewa chanjo.

Mh. Ummy awaagiza watendaji wa afya kuwa na takwimu sahihi muda wote.Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Rukwa. 
Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazeena watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ameiagiza timu ya uendeshaji wa huduma zaafya ya mkoa wa Rukwa, kusimamia utendaji wa vituo vyote vya kutolea huduma yaafya ili kudhibiti takwimu zisizokuwa sahihi, ambazo zinasababisha bajeti yadawa isiwe halisi na kuendelea kuwepo upungufu mkubwa wa dawa.

Waziri huyo Ummy Mwalimu akiongea kwenye kituo cha afya chaMatai wilayani Kalambo, ameshangazwa kuona menejimenti ya kituo hicho cha afyaambacho hivi sasa kinatumika kama hospitali ya wilaya hiyo, inakuwa haijui kwauhalisi bajeti ya dawa, na huku wakiendelea kupata bajeti ya kiwango cha katakwa idadi ya watu elfu tatu, wakati sasa matai ni makao makuu ya wilaya naidadi ya watu ni zaidi ya 10,000 jambo ambalo haliendani na upatikanaji wa dawa.

Nae katibu tawala wa Wilaya ya Kalambo Bw. Frank Sichalwe, aliilalamikia boharikuu ya dawa MSD kanda ya Mbeya, kwa kuwapelekea dawa nyingi ambazo zinazokaribia kuisha muda wa matumizi, na kuongeza kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la kutokuwa na gari la wagonjwa kabisa jambo ambalo linasababisha serikali kushindwa kufikisha huduma katika vijiji vilivyo mbali na makao makuu ya mji. 

Kwa kujibu hilo Mh. Ummy Mwalimu aliwatahadharisha watendaji wa Afya katika kituo hicho kuhakikisha wanaagiza dawa wanazohitaji mapema na kusisitiza kuwa bohari ya dawa haiwezi kuwapelekea dawa bila ya kujua mahitaji yao. 

Wednesday, August 16, 2017

Kilio cha Wananchi nane nane chasababisha agizo la RC Rukwa.

Wananchi wa Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wamemuomba mkuu wa Mkoa huo kamishna Mstaafu Zelote Stephen Kufanya maonyesho ya Nane nane Kimkoa ili wakulima na wafugaji wasioweza kufika katika ngazi ya kanda wapate fursa ya kuelimika na kuonesha bidhaa zao Kimkoa.
 Maombi hayo yametolewa na wananchi wa Manispaa hiyo baada ya Mh. Zelote Stephen kutembelea mabanda kadhaa ya maonesho ya nanenane yaliyofanyika katika Manispaa hiyo kwenye kituo cha kilimo katika Kijiji cha Katumba azimio ili kutoa fursa kwa wakulima na wafugaji wadogo kuonyesha bidhaa zao.

“mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wanaokwenda kwenye maonyeshoi ya nanenane kanda ni wachache sana na wengi tuliopo hatuna vipato vya kutosha kutufikisha huko, hivyo tunaomba tufanye nane nane ya Kimkoa ili nasi tuweze kuonyesha bidhaa zetu na tuweze kujifunza kwa wenzetu,” Alisema Pscal Mwanisawa Mkulima wa Kijiji cha Ulinji Manispaa ya Sumbawanga.


Kuwepo kwa maonyesho hayo ni utekelezaji wa pendekezo la Mh. Zelote aliyetaka kila halmashauri kufanya maonesho ili wakulima na wafugaji waweze kuelimishana na kutambulika katika maeneo yao ili wapate msaada kutoka kwa maafisa ugani ili kuongeza tija katika kilimo na ufugaji na hatimae kuongeza thamani katika mazao yao.

Akipokea maombi hayo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amesema kuwa ili wananchi waweze kujikwamua ni muhimu kuungana na kuwa na utambulisho wa aina moja wenye bidhaa tofauti katika makundi yao ili kuwa na nguvu.


“Muitikio wa wakulima na wafugaji katika Mkoa wa Rukwa upo juu sana, ila hawapewei nafasi, sasa mwakani ni lazima kwa Halmashauri zote kufanya nane nane katika Halmashauri zao. Nitasimamia kila mtu apate nafasi ili kujifunza teknolojia mpya na tuachane na mambo ya zamani,” Mh. Zelote alisema.

Katika kuunga mkono ombi la wananchi hao Mbunge wa Viti maalum Mh. Silafi Maufi, alipongeza juhudi za Mh. Zelote kwa kuhakikisha wananchi wa Halmashauri wanapata nafasi ya kuonesha bidhaa zao mbali na kuongeza kuwa ni jambo linalowezekana kufanya “Nane nane” ya kimkoa.


“ mheshimiwa mkuu wa Mkoa umekuwa shahidi kwa namna maonyesho yalivyofana ni Dhahiri kuwa inawezekana kufanya nane nane ya kimkoa katika mkoa wetu wa Rukwa,” Mh. Maufi alimalizia. 

RC Rukwa ashauri Nanenane nyanda za juu kusini kushirikisha nchi za SADC

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa KamishnMstaafu Zelote Stephen ameishauri kamati ya maandalizi ya nanenane nyanda za juu kusini kufikiria kushirikisha nchi za SADC ili kuongeza hamasa na kuleta ushindani kwa watanzania wafahamu yanayofanyika katika nchi za jirani.Ametoa ushauri alipokuwa akifanya majumuisho baada ya kutembelea mabanda 16 ya bidhaa mbalimbali za kilimo katika maonesho ya nane nane kwa kanda ya nyanda za juu kusini yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya ambapo Mh. Zelote Stephen alikuwa mgeni rasmi wa siku ya tatu tangu ufunguzi wa maonesho hayo.


“Tuachane na mazoea, maonyesho haya yana miaka 25 sasa tuyaboreshe zaidi, isiswe ni mikoa hii tu saba, tupanue wigo, kwakiwa huku ni nyanda za juu kusini basi tufikirie kuzishirikisha nchi za SADC ambazo zitasaidia kubadilishana biashara na teknolojia pamoja na kutafuta masoko,” Alifafanua.


Akisisitiza suala hilo Mh. Zelote alibainisha kuwa nchi ya Tanzania inafikika kwa njia zote, ardhini, majini na angani huku akitaja meli mbili zilizozinduliwa Mkoani Mbeya na Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa, treni ya TAZARA pamoja na ndege zinazomilikiwa na nchi yetu.   

Aidha amezishauri halmashauri kuanza maandalizi kwa kuwa na siku maalum kwaajili ya maadhimisho hayo kihalmashauri ili kuwapa ujuzi na kujua ubora wa vitu ambavyo vinaweza kupelekwa kwenye maadhimisho ya nanenane kikanda ili kuimarisha ushindani na kumpa kila mwananchi nafasi ya kuelimika ili kuwa na kilimo chenye tija.


Akiunga Mkono Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kilolo Ntila alityekuwemo katika msafara huo alisisitiza kuwa maonesho ya nanenane yanayofanyika kikanda yanalenga watu wenye kipato cha kutoka katika halmashauri zao na kukusanyika jijini Mbeya huku wakulima wasio na uwezo wakikosa elimu inayopatikana kutokana na maonyesho hayo.

“Nikiongezea aliyoyasema Mheshimiwa Mkuu wangu wa Mkoa, kwa nafasi yake namuomba aweze kushawishi haya makampuni makubwa kuweza kusambaza wataalamu wao katika Halmashauri zetu ambapo kuna uhitaji mkubwa wa elimu hii inayotolewa hapa katika viwanja hivi vya nanenane na wao ndio walengwa wakubwa wa shughuli hii,” alisema.


Pamoja na hayo Mh. Zelote alitoa wito kwa wananchi wote wenye nafasi wajitokeze kwa wingi kwenye maonyesho hayo ili waweze kuelimika kutokana na mafunzo mbalimbali yanayotolewa viwanja hivyo vya nanenane na kusifu maandalizi ya sherehe hizo.


Vijiji 111 kuwa na Umeme Mkoani Rukwa Kufikia 2019

Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani ameendelea na ziara za uzinduzi wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA PHASE III) ambapo Agosti 14, 2017 alikuwa Mikoani Rukwa katika Kijiji cha Kabwe Wilaya ya Nkasi.
Dkt. Kalemani alisema jumla ya Shilingi Bilioni 42.5 zitatumika kupeleka umeme katika Mkoa huo na kuongeza Mradi huo utatekelezwa katika vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 111. 
"Sehemu ya pili itahusisha vijiji 145 ambapo itaanza baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza. Kufikia mwaka 2021 vijiji vyote vya Mkoa wa Rukwa vitakuwa vimepatiwa umeme".Alisema Dk. Kalemani.
Aidha, Dkt. Kalemani alimtambulisha Mkandarasi atakayejenga Mradi wa REA Mikoani humo Kampuni ya Kitanzania ya Nakuroi Investment Company Limited.
Alimwagiza Mkandarasi kuhakikisha anapeleka umeme Kijiji kwa Kijiji na Kitongoji kwa Kitongoji bila kuruka na sehemu zinazotoa huduma za Kijamii kama Mashule, Zahanati, Magereza, Visima vya maji, Nyumba za Ibada na sehemu mbalimbali. 
Pia alitoa maagizo kwa TANESCO kupeleka Ofisi katika Kijiji cha Kabwe na katika maeneo yote yenye Wateja wengi lakini wapo mbali na Huduma za TANESCO.
Aliongeza kwa kuwataka Mameneja na Watalaamu wa TANESCO kutokukaa Ofisini bali wawafuate Wateja.Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCo, Dkt. Tito E. Mwinuka aliwaomba Wananchi hao wa Kabwe kuwa waaminifu na kutoa ushirikiano kwa Watendaji wa TANESCO kabla na hata baada ya Mradi kukamilika. 
"Muitunze miundombinu ya umeme, msiihujum wala kuichoma moto". Alisema Dkt. Mwinuka.Alisema TANESCO imejipanga kuhakikisha Wananchi hao wanapata huduma ya umeme iliyobora na ya uhakika.  
Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy aliwaeleza Wananchi kuwa mradi huo wa usambazaji umeme vijijini hauna malipo ya fidia hivyo watoe ushirikiano kwa wakandarasi hao wakati wanatekeleza mradi huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Nkansi Mheshimiwa Saidi Mtanda aliushukuru Uongozi wa TANESCO kwa kwani umekuwa ukitoa ushirikiano pale unapohitajika. 
"Mheshimiwa Mgeni Rasmi katika Kijiji cha Nyamare kwenye chanzo cha maji tulileta Mkandarasi akatukadilia bei ya Transifoma milioni 60, tuliwasiliana na uongozi wa TANESCO wametufungia Transfoma kwa pesa zao milioni 24". Alisema Mheshimiwa Mtanda.
Mh,Dkt Medard Kalemani alimalizia uzinduzi Mkoani Rukwa kwa kukakabidhi kifaa cha UMETA kwa wazee 10 wa Kijiji hicho ambao hawana uwezo wa kumiliki ikiwa ni nia ya wamu ya serikali ya awamu ya tano kuwainua waliochini. 

“Hatuhitaji Kupeleka mahindi Dar es Salaam, tunahitaji kupeleka unga,” RAS Rukwa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Benard Makali amewasisitizia wafanyabiashara wadogo na wakubwa wa mahindi kuachana na tabia ya kusafirisha mahindi kwenda mikoani na badala yake waongeze thamani ya mazao hayo na kusafirisha unga kwenda kwenye mikoa hiyo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Benard Makali 

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa uwekezaji kwenye sekta ya Viwanda Mkoani hapa iliyohudhuriwa na wakurugenzi wa Halmashauri, Mameneja kutoka TANROADS, TANESCO, SIDO na wamiliki wa viwanda katika mkoa.
“Mkoa kama wa Dar es Salaama hawahitaji mahindi wanahitaji mazao yanayotokana na mahindi kama ni unga, ama pumba kwaajili ya chakula cha mifugo lakini utaona kuna malori yamejaza magunia ya mahindi yakielekea Dar es salaam badala ya kupeleka unga.” Amesema.
Awali alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya mkuu wa Mkoa, Benard Makali alisema kuwa Mkoa wa Rukwa unaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kila mwenye nafasi na awezo ashiriki kikamilifu katika kuzalisha bidhaa kwa kuzingatia viwango na ubora wa mahitaji ya Soko.
Aliongeza kuwa Mkoa wa Rukwa una fursa nyingi za uwekezaji katika maeneo ya kilimo, mifugo na uvuvi hiuvyo basi aliwaasa wakurugenzi wa Halmshauri kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa kujikita katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika Halmashauri zao ili kuvutia wawekezaji wakubwa na wadogo ili waweze kuwekeza katika sekta hizo.
Kwa mujibu wa orodha ya viwanda Tanzania Bara ya mwaka 2015 kutoka  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mkoa wa Rukwa una takribani viwanda 950 huku viwanda vidogo sana 869 vyenye uwezo wa kuajiri watu kuanzia 1 hadi 4 vikichukua asilimia 91.5,  na viwanda vidogo 78 ambavyo ni sawa na asilimia 8.2 ,Viwanda vya kati 2 ambavyo ni sawa na asilimia 0.2 na kiwanda kikubwa  1.  
Serikali Mkoani Rukwa imefanya kikao na wadau wa sekta ya viwanda mkoani humo ili kuzungumzia namna ya kuziimarisha fursa zilizopo katika Mkoa na hatimae kuwavutia wawekezaji kutoka mikoani na nje ya nchi kuwekeza katika mkoa Ili kufuikia azma ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.

RC Rukwa atoa wito ufuatiliaji wa karibu katika ugawaji wa vyandarua kwa Mkoa mzima

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ametoa wito kwa watekelezaji wa mpango wa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria katika Mkoa kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuepuka matatizo yaliyojitokeza katika mfumo uliotangulia.
Ametoa wito huo alipokuwa akifungua mkutano wa uhamasishaji kuhusu mpango wa ugawaji wa vyandarua kupitia vituo vya kutolea huduma za afya uliowashirikisha wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri na Mkoa.
Ugawaji huu wa vyandarua ulikuwa ukijulikana kwa jina la Hati Punguzo uliokuwa ukitumia vocha maaluma na kulipia Shilingi 500, mpango ambao ulisitishwa mwaka 2014 kutokana na ubadhirifu uliotokea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ambapo watopa huduma walikuwa wakishirikiana na wakala kuandika vocha hewa na wakala kuchukua fedha bila ya kutoa huduma.
“kutokana na umuhimu wa kuwakinga wajawazito na watoto chini yam waka mmoja Serikali imeamua kuanzisha utaratibu wa ugawaji wa vyandarua kwa mjamzito na mtoto chini yam waka mmoja, moja kwa moja kutoka kwa mtoa huduma ya afya bila ya malipo yoyote wala uwakala,” Mh. Zelote alisema.
Aliongeza kuwa lengo la mpango huu ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na ugonjwa wa malaria. Pia kuongeza upatikanaji na utumiaji wa vyandarua katika ngazi ya kaya na jamii kwa asilimia 85 au zaidi na mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka 2017 vyandarua hivyo vitaanza kugaiwa kwa mkoa wa Rukwa.
Kwa upande wake muuguzi mkuu mwandamizi kutoka wizara ya afya Bi. Epiphania Malingumu alisema kuwa mgawo wa vyandarua hivyo utafanyika kupitia bohari ya dawa (MSD) na vituo vya serikali pekee ndivyo vitaweza kutoa vyandarua hivyo kwakuwa vina namba maalum kwaajili ya malipo, hivyo vituo binafsi havitaweza kutoa huduma hii.
“Mama mjamzito atapata chandarua katika hudhurio la kwanza kliniki haijtajalisha ni mimba ya miezi mingapi, kama amehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza akiwa na ujauzito wa miezi nane basi atapewa chandarua na mtoto akizaliwa atapewa tena chandarua na kama amejifungua mapacha basi atapewa vyandarua viwili,” Alisema.
Tafiti za mwaka 2015/2016 zinaonesha maambukizi ya ugonjwa wa malaria ni alimia 14.8 kitaifa na kwa Mkoa wa Rukwa ni asilimia 2.7. kwa mwaka 2012 maambukizi yalikuwa asilimia 9.5 kitaifa na kimkoa ilikuwa asilimia 4.5 ambayo imepungua kwa asilimia 1.8.

Mh. Maghembe aeleza mikakati yake kuboresha utalii Mkoani Rukwa.Wazi

Waziri wa Maliasili na Utalii mh. Jumanne Magembe ameeleza umuhimu wa kuimarisha utalii katika Mkoa wa Rukwa kwa kuwa na kivutio kikubwa cha maporormoko ya Mto Kalambo ambapo maporomoko hayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika.
Amesema kuwa imefika wakati sasa kuondokana na fikra ya utalii katika mikoa ya kaskazini peke yake na kuamua kuelekeza nguvu za uwekezaji katika mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini kama Rukwa na Katavi.
Ameeleza kuwa mikoa hii inavivutio vingi sana na tayari kuna wawekezaji kadhaa ambao wameomba kujenga nyumba za kupumzikia katika maeneo kadhaa ya vivutio yaliyoko katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
“Ni Imani yetu kuwa hawa ambao watajenga hizi nyumba za kupumzikia watahitaji watalii wa kuja kuzitumia hivyo kwa kuwatumia wao tunaweza kutangaza maeneo yetu haya ya utalii,” Alimalizia.
Aliamua kueleza mikakati hiyo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen kuongelea shauku yake ya kutaka nchi na dunia nzima ifahamu maporomoko ya mto Kalambo ambayo yanapatikana mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Hayo yalisemwa wakati Mh. Zelote alipokuwa akitoa historia fupi ya mkoa kabla ya Mh. Magembe kuanza ziara yake ya siku tano katika mkoa wa Rukwa.
Waziri wa maliasili na Utalii Mh. Prof. Jumanne Maghembe (Mb) akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa wa rukwa Kmaishna mstaafu Zelote Stephen (aliyekaa) ofisini kwa Mkuu wa mkoa.

Tuesday, August 1, 2017

RC Rukwa azionya Halmashauri dhidi ya matumizi mabovu ya mashine za EFD

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amezionya halmashauri zote mkoani Rukwa kuhakikisha wanazitumia vizuri manshine za EFD kwa kuongeza mapato katika halmashauri zao.

Ametoa onyo hilo kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa madiwani wa  Manispaa ya Sumbawanga katika kumalizia ziara yake maalum kwa halmashauri zote mkoani humo kujua namna Halmashauri zilivyojipanga ili hoja hizo zisijirudie miaka inayofuata.  

Akiongea huku akionesha risiti alizozikamata katika maeneo mbalimbali ya mauzo alisema kuwa serikali inafanya kila liwezalo katika kuhakikisha inakusanya maopato lakini bado kuna watumishi wanatafuta namna ya kuiskosesha serikali mapato hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akionesha risiti ambazo zimeshakatwa kabla ya matumizi.

“katika kila sehemu za mauzo lazima mashine hizi ziwepo na kuwepo sio mtindo huu (akionesha msururu wa risiti zilizokatwa tayari kwa matumizi) hizi nimezikamata maeneo anajua Mkurugenzi, asubuhi watu wanagawana, ndio mchezo uliopo, pamoja na jitihada tunazofanya bado watu wanatafuta mbinu za kuiba, hii sio kwamba nimeleta iwe mfano, hapana, nimezikamata na mfahamu kuwa mimi ni mtaalamu wa kukamata,”Alisema.

Katika Kusisitiza suala la uwazi wa matumizi ya fedha za halmashauri kwa waheshimiwa madiwani Mh. Zelote alitaja majukumu kadhaa ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kusema kuwa moja ya kazi za Mkurugenzi ni kuhakikisha kuwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halmashauri.

“Hapa mmezungumza na mmenionyesha kwa kiasi kikubwa kwamba hamnazo taarifa na nikiangalia kazi moja wapo ya waheshimkwa madiwani ni kiusimamia matumizi ya fedha za halmashauri zao sasa mtasimamiaje ikiwa hamna taarifa,” Alisema

Na kukumbusha kuwa Mkurugenzi ndio katibu wa kamati ya fedha ya halmashauri lakini na kuonya kuwa kamati hiyo ibebe sura ya halmashauri na sio sura ya kamati na kuwasisitiza kufuata taratibu nyingine za ikiwa kurudisha mrejesho kwa wengine juu ya mipango na maazimio yaliyofikiwa.

Katika kikao hicho Mh. Zelote alimtambulisha mtaalamu wa TEHAMA ili awaelezee waheshimiwa madiwani namna mifumo ya fedha inavyofanya kazi ili nao wawe na uelewa mpana katika kufuatilia mapato na matumizi ya halmashauri.

“Suala la kukusanya mapato limekuwa likiimbwa asubuhi, mchana na usiku, kuwa tuhakikishe tunajipanga vyema kukusanya mapato ya halmashauri kwa kupitia utaratibu uliopo, suala la kutumia hizi mashine sio la kuhoji tena mwisho ulikuwa mwezi wa tatu ndio agizo lililopo kwa wakurugenzi kuwa mashine hizi ziwepo na zinafanya kazi,” Alisema

Na katika kuhakikisha kuwa vitabu hivyo havipati nafasi Mh. Zelote alitoa siku saba vitabu hivyo kurudishwa maghalani na kuongeza kuwa watumishi wanaokiuka miiko ya kazi zao kuwajibishwa kulingana na madhara waliyosababisha na kuwaasa kujenga uaminifu katika utumishi ndani ya halmashauri.

“Sitaki kusikia tena kuwa kwenye mkoa wangu kuna halmashauri inanyooshewa kidole, mmeshanyooshewa kidole mara moja sitaki kuona tena hicho kidole,” alimalizia.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya nSumbawanga Mh. Julieth Binyura alishanngazwa na wataalamu hao kushindwa kudhiti hoja na hatimae wao kuwa chanzo kikuu cha kuzalisha hoja.

“Mtu kama unaitwa mtaalamu na serikali imekuamini kwanini tena unaizalishia serikali hoja, na suala la fedha ni suala nyeti sana hivyo linahitaji umakini wa haloi ya juu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili na si vinguinevyo,” Alisema.


Akifunga kikao hicho Mstahiki meya wa Manispaa ya Sumbwanga Mh. Justin Malisawa alimuahidi Mkuu wa Mkoa kusimamia yale yote aliyoyaelekeza na kuomba msaada wake pindi pale watakapokwama.