Tuesday, October 31, 2017

RC Rukwa aahidi kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Rukwa katika Sekta zote.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo amewatahadharisha watumishi kutobweteka baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen kustaafu na kumkabidhi yeye kijiti cha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya mkoa.

Amesema kuwa hatomwangusha Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumkabidhi madaraka hayo na kuahidi kuwa ataimarisha elimu inayoonekana bado ipo chini kwa ufaulu lakini pia kuendeleza kasi ya uzalishaji katika kilimo.

“Baada ya kusoma kabrasha hili la kukabidhiana ofisi kuna mambo mengi ya kuyazingatia ikiwemo, elimu, kilimo, ulinzi na usalama, utunzaji wa mazingira, uvuvi na uwekezaji katika viwanda. Hasa katika elimu maana mimba ni nyingi, kuna upungufu wa madawati, upungufu wa vyumba vya madarasa lakini pia kiwango cha ufaulu hakijafikia kile kilichopo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo ni asilimia 80 kwa darasa la saba,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo katika makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mapema leo hii tarehe 31/10/2017 katika ukumbi wa ofisi hiyo, jambo lililoshuhudiwa na watumishi wa sekretariet ya Mkoa pamoja na baadha ya Halamashauri.

Katika kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufanisi Mh. Wangabo amesema kuwa hupemda kusikiliza mipango ya watendaji inayotekelezeka ili waweze kuitekeleza kama walivyoipanga nay eye ataisimamia na kutoa ushauri wa kuongeza kasi ya utekelezaji pale inapobidi ili kuyafikia malengo waliyojiwekea kwa wakati.


Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewashukuru watumishi wote wa serikali katika Mkoa wa Rukwa pamoja na wananchi wa mkoa kwa kumpa ushirikiano katika kipindi chote alichokuwepo na kuwaomba waendeleze kumpa ushirikiano huo huo Mkuu wa Mkoa mpya ili naye aweze kufanya majukumu yake kwa ufanisi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Leonard Wangabo (kushoto) na Mh. Zelote Stephen (Waliokaa) katika picha ya pamoja na watumishi wa Sekretariet ya Mkoa pamoja na taasisi za serikali Mkoani Rukwa. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Leonard Wangabo (kushoto) na Mh. Zelote Stephen (Waliokaa) katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Mwenyekiti wa CCM Mkoa.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) akimkabidhi nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo. katika makabidhiano ya ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

Mkuu nwa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Leonard Wangabo akisalimiana na Meneja wa PS3 Mkoa wa Rukwa Bi. Rose wakati wa kumkaribisha Mh. Wangabo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tayari kwaajili ya Kuanza kazi

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) akisaini nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa kwaajili ya Kumkabidhi ofisi hiyo Rukwa Mh. Joackim Wangabo. 
Monday, October 23, 2017

SHAMBA LA MALONJE KURUDISHWA SERIKALINI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameagiza eneo lililokuwa shamba la mifugo la Malonje wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa lenye ukubwa wa ekari 12,750, lirejeshwe serikalini kwa vile utaratibu wa kuligawa umekiukwa kwa kiwango kikubwa, na masharti ya uendeshaji hayajazingatiwa kabisa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi 
ameyasema hayo alipofanya ziara wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa alpoenda kutatua mgogoro wa ardhi huo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 20 jambo ambalo limekuwa likizua sintofahamu baina ya wananchi na wawekezaji wa shamba hilo.
Mhe. William Lukuvi amesema Serikali imekusudia kuwanyang’anya mashamba watu wote waliokopeshwa kwa kuyatumia kama dhamana kwa ajili ya kupata mikopo kutoka kwenye mabenki ndani na nje ya nchi lakini mikopo hiyo hawaitumii kuinufaisha nchi wala kuiendeleza ardhi waliyoitumia kama dhamana.
Waziri Lukuvi ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya wawekezaji wengi wenye mashamba makubwa kutumia ardhi kama dhamana kwa ajili ya kupata mikopo kutoka kwenye mabenki ndani na nje ya nchi lakini mikopo hiyo wanaitumia kuwekeza nje ya nchi na kujenga majengo nchi za Ulaya, dubai na kwingine duniani.
Lukuvi amesema Haiwezekani mtu atumie ardhi yetu kujipatia fedha halafu fedha hizo azitumie kuendeleza nchi nyingine na kuiacha ardhi yetu kama pori jambo ambalo linaleta migogoro mikubwa katika jamii inayoyazunguka maeneo hayo.
“Kwa hiyo Wizara yangu imekusudia mwezi ujao kupeleka Bungeni marekebisho ya sheria namba 24 ya mwaka 1999 ili kuongeza vifungu ambavyo vitadhibiti mikopo inayopatikana kwa kutumia ardhi kama dhamana” amesema Waziri Lukuvi.
Marekebisho haya tunalenga kuwezesha fedha zinazopatikana kutokana na mikopo iliyotolewa itumike kuendeleza sehemu ya ardhi husika iliyotumika kama dhamana ya kuomba mkopo katika mabenki. Kwa kuwa Tathmini iliyopo inaonesha, baada ya wekezaji hao kupata mikopo kwa kutumia ardhi kama dhamana fedha hizo hawazitumii kuendeleza ardhi husika au katika uwekezaji wowote hapa nchini.
Lukuvi amesema, kuanzia mwezi Novemba tatizo hilo litakwisha kabisa kwa kuwa jukumu hili yatapewa mabenki na wakopeshaji wote ambao watafuatilia kwa karibu maombi ya mikopo kutokana na mpango mkakati uliowasilishwa katika Benki husika.
“na kama Benki husika haitowafuatilia na kuamua kumuachia mtu huyo kwa kuwekeza fedha hizo anavyotaka bila kuendeleza ardhi husika, basi Serikali itamyang’anya mkopeshwaji huyo shamba hilo kwa kuwa atakua amekiuka sheria halafu Benki ambayo itamuachia mtu achukue fedha na asiendeleza shamba lile itakuwa imekula hasara yenyewe” amesema Waziri Lukuvi.
Aidha katika hatua nyingine Serikali imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka alama za x na kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao bila kibali na yale yanayojengwa katika viwanja vya watu wengine walio na hati miliki zao za ardhi kwa dhuruma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema tatizo la ujenzi holela lianaanza pale ambapo Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji wanawaacha majengo yanaibuka katika miji yao bila kujua ujenzi huo una kibali au unajengwa katika kiwanja chenye hati na muhusika wa hati hiyo ndio anayejenga.
“Hatuwezi kuendelea na zoezi la kufanya urasimishaji wa makazi kila siku wakati chanzo cha tatizo hilo kinajulikana, kwa hiyo naagiza Wakurugenzi, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka x katika majengo yote yanayojengwa bila vibali na ujenzi unaofanywa kwenye viwanja vya watu masikini kwa dhuruma” amesema Lukuvi.
Lukuvi amesema atapambana na viongozi hao pale ambapo atakuta majengo yamekithiri katika miji yao na hayana vibali vya ujenzi na baya zaidi majengo hayo yamejengwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kujenga au yamejengwa katika kiwanja cha mtu mwingine na viongozi hao wameshindwa kufuatilia kwa kuyavunja au kuyaweka alama ya x majengo hayo, kwa kuwa huu ni uzembe unaotokea nchi nzima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amemhakikishia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuwa atayafanyia kazi mapendekezo yake kikamilifu na kwa haraka ili kuondoa migogoro na kero zinazoukabili mkoa wake katika masuala yote ya ardhi.

UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA KUANZA KUJENGWA DISEMBA

Akizungumza na wananchi wanaozunguka Uwanja huo Prof. Mbarawa amewahakikishia wananchi wote wanaostahili kulipwa fidia kutokana na kupisha ujenzi huo watalipwa fidia zao katika kipindi kisichozidi miezi miwili kuanzia sasa.
“Jumla ya wananchi 97, ndio wanaostahili kulipwa fidia na kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kimetengwa na wataanza kulipwa hivi karibuni kabla ya zoezi la ujenzi wa uwanja huo kuanza” amesema Prof. Mbarawa.
Amewataka wananchi hao kuacha kupita katika uwanja huo kwani ni hatari kwa usalama wa ndege na usalama wa wananchi wenyewe.
Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga unajengwa kwa kiwango cha lami na kuongezwa urefu kutoka kilomita 1.5 had 1.7 ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutumia uwanja huo na hivyo kuufungua mkoa wa Rukwa na mikoa mingine hali itakayochochea maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa mkoa huo.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mkoa wa Rukwa, Mussa Mchola amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa hatua ya kulipa fidia na kumhakikishia kuwa watamsimamia mkandarasi huyo kikamilifu ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati na kwa ubora unaostahili.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Mbarawa amekagua Ujenzi wa Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port KM 112 na mizani ya Singiwe na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ambapo amemtaka mkandarasi China Railway 15, Bereau Group Corporation (CR15G) na Henan Provincial Newcentry Road na Bridge Consultants Limited JV anaejenga kuongeza kasi katika maeneo korofi kabla ya Mvua za masika kuanza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mwl. Julieth Binyura amezungumzia umuhimu wa ukamilishaji wa barabara hiyo utakavyonufaisha wilaya hiyo kwa kuwa inaunganisha Wilaya hiyo na bandari ya Kasanga na mpaka wa Kasesha unaounganisha Tanzania na Zambia na hivyo kuchochea uzalishaji na uchukuzi kati ya Tanzania, Kongo na Zambia.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iko katika mchakato wa kuunganisha kwa kiwango cha lami barabara zinazoingia katika bandari za mipakani ili kukuza huduma za uchukuzi kati ya Tanzania na nchi jirani kwa njia za magari, ndege na meli.

RC Rukwa awaagiza Wakuu wa Wilaya kufanya Vikao vya DCC katika Wilaya zao.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanafanya vikao vya kamati ya ushauri ya maendeleo ya wilaya (DCC) kabla ya kufanya kikao cha kamati ya ushauri ya maendeleo ya mkoa.

Amesema kuwa kwa muda mrefu wakuu wa wilaya wamekuwa wakisubiri kikao cha RCC bila ya kuwa na taarifa kamili ya vikao vya DCC kwakuwa hawavitekelezi kama inavyotakiwa.
“Vikao hivi vipo kisheria na ni mara mbili tu kwa mwaka, sasa kila siku tunakutana ngazi ya Mkoa tu na kujadili mambo ya mkoa bila ya kujua yaliyojiri katika ngazi ya wilaya na sioni kama ni muafaka kuendelea na utaratibu huu, hivyo maagizo yangu ni kwamba kabla ya kikao hiki nataka kupata mrejesho wa vikao vya DCC ndipo tuendelee na kikao hiki,”Alisema
Mh. Zelote alisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo ndipo ngazi ya mkoa itaelewa eneo ambalo ngazi ya wilaya imeshindwa kulitekeleza kwa ufanisi na kuhitaji msaada kutoka katika ngazi ya mkoa ili kwa pamoja kuweza kusaidiana namna ya kutatua matatizo hayo na hatimaye kufikisha hudmua bora kwa wananchi.

RC Rukwa aitahadharisha TARURA kutorudia makosa ya Halmashauri.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameutahadharisha Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa yanafanywa na Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.

Amesema kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo kujengwa chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya matengenezo ya mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali imeamua kuzitafutia ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.
“Ukiitwa Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka hata sisi ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya kiwango, na hapo mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana kwenye barabara lakini kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua zinataka kuanza ndio utaona mkandarasi anaingia barabarani kwenda kutengeneza barabara,” Mh. Zelote alifafanua.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Amesisitiza kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua za kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.
Hivyo ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu na kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano. 

“Kwa gharama yoyote ile michezo lazima ikue Rukwa” RAS Rukwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bernard Makali akikabidhi mipira kwa vilabu vya michezo Rukwa. 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali ameahidi kusimamia michezo katika Mkoa wa Rukwa na kuhakikisha Mkoa haubaki nyuma katika mashindano mbalimbali ya kitaifa ikiwemo ligi kuu ya soka Tanzania bara
Bernard Makali ambaye pia ni Mwenhyekiti wa baraza la Michezo la Mkoa amesema kuwa michezo yote itasimamiwa kuanzia ngazi ya mtaa, kata na wilaya na kuwashirikisha wadau wote kuanzia mwananchi wa kawaida, madiwani, wabunge na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali zilizopo katika mkoa ili kusukuma maendeleo ya michezo katika Mkoa.
“Michezo yote itasimamiwa, siyo mpira peke yake, lazima wadau wote washirikishwe katika mkoa ili kukuza michezo katika mkoa wetu, kuna mama hapa amelalamika wanawake hawachezi, lakini kuna chama cha netiboli tumekiwezesha kwenda Dodoma kwenye uchaguzi wao na wamefanikiwa, hivyo wote wanawake kwa wanaume watashiriki kwenye michezo,” Makali alisisitiza
Aliyaongea maneno hayo alipoitisha kikao cha wadau wa michezo wa mkoa kabla ya kukabidhi mipira 100 iliyotolewa na chama cha mpira wa miguu taifa (TFF) kwa vilabu 20 vya watoto vilivyopo katika Mkoa wa Rukwa.
Pia aliviagiza vilabu vyote na viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo waliohudhuria kikao hicho kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kutekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Nchi mama Samia Suluhu la kufanya mazoezi kila jumamosi ya pili ya mwezi ili kuhamasisha michezo pamoja na kuimarisha afya za wanarukwa.
“Mkoa huu hatuhamasishi wananchi kufanya mazoezi katika jumamosi ya pili ya mwezi, sasa naagiza sisi tuliopo ndani hapa tuwahamasishe wananchi huko tunapoishi kufanya mazoezi, na nataka kuona ratiba ya kila kilabu kujua wanapofanyia mazoezi kila siku hna hasa jumamosi ya pili ya mwezi,” Alimalizia.
Katika kikao hicho wadau hao walielezea changamoto mbali mbali za michezo mkoani Rukwa ikiwemo kutokuwa na ushirikiano kati ya chama cah mpira cha Mkoa pamoja na vyama vya mpira vya Wilaya jambo linalopelekea kudhoofisha maendeleo ya mpira katika mkoa.
Akizungumzia migogoro iliyopo katika vyama hivyo na namna wanavyoendelea kuitafutia ufumbuzi Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) Bw. Blas Kiondo amesema kuwa tangu aingie madarakani mwaka 2013 amekuwa akikabiliana na changamoto hiyo na kuahidi kuimaliza kabisa.
Kwa upande wake Afisa michezo wa Mkoa Gabrieli Hokororo ametahadharisha kuwa si vyema kuyafufua makovu na badala yake wadau waungane pamoja ili kupeleka maendeleo ya michezo mbele na hatimae Mkoa wa Rukwa usikike kwenye ramani ya michezo katika taifa.

Wednesday, October 11, 2017

RC Rukwa aitahadharisha TARURA kutorudia makosa ya Halmashauri.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameutahadharisha Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa yanafanywa na Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto)  wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara, 
(katikati) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule pamoja na Katibu tawala wa Mkoa waRukwa Bernard Makali. 

Amesema kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo kujengwa chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya matengenezo ya mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali imeamua kuzitafutia ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.

“Ukiitwa Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka hata sisi ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya kiwango, na hapo mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana kwenye barabara lakini kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua zinataka kuanza ndio utaona mkandarasi anaingia barabarani kwenda kutengeneza barabara,” Mh. Zelote alifafanua.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Amesisitiza kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua za kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.


Hivyo ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu na kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano. 

Rukwa wajipanga kuzalisha malighafi nyingi za viwanda kuvutia wawekezaji.

Katika kujiandaa na msimu wa kilimo Uongozi wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen wamezuru Taasisi ya Utafiti Kilimo (ARI) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) nyanda za juu kusini - Uyole, Mkoani Mbeya.

Ziara hiyo iliyobeba Katibu Tawala wa Mkoa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Rukwa na makatibu tawala wao walioambatana na wakulima, maafisa kilimo na mifugo wa wilaya pamoja na wenyeviti wa Halmashauri nne za Mkoa huo, na wataalamu wa kilimo na mifugo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Katika ziara hiyo mada mbalimbali zilitolewa kuhusu aina ya mazao yanayoweza kustawi katika Mkoa wa Rukwa, wadudu wanaoweza kushambulia mazao hayo na namna ya kuwadhibiti ili kuongeza uzalishaji, utafiti wa udongo pamoja na kilimo cha nyasi kwaajili ya mifugo na ufugaji wa kisasa.

Mh. Zelote alisema kuwa kwa miongo kadhaa Mkoa wa Rukwa umekuwa katika mikoa inayoongoza kwa kilimo lakini haikuwahi kuwa namba moja hivyo ziara hiyo ndio mwanzo wa kuiendea Rukwa mpya yenye kuzalisha mazao yenye kuleta tija kwa wakulima, mkoa na taifa kwa ujumla.

 “Lengo la kufunga safari kutoka Rukwa hadi hapa ni kwa lengo la kuleta mabadiliko ya Kilimo na mifugo, Rukwa kupitia kilimo ndio litakuwa ni chimbuko la viwanda, kama wataalamu walivyosema kuwa kilimo ndio chimbuko la viwanda,tunahitaji kuboresha kilimo katika Mkoa wa Rukwa ili tuwe na viwanda vya uhakika” Amesema.

Amesema kuwa ili kuwakomboa wananchi wa hali ya chini ambalo ndio lengo la Rais Dk. John Pombe Magufuli Hakuna budi kuimarisha kilimo na hatimae kuinuka kutoka katika uchumi wa viwanda vidogo kwenda viwanda vya kati na kutoka katika uchumi mdogo kwenda uchumi wa kati.

Kwa upande wake mratibu wa ziara hiyo Benjamin Kiwozele alimshukuru Mh. Zelote kwa kuona umuhimu wa kuzitumia taasisi hizo kwa malengo yaliyowekwa na serikali.


Kabla ya Kumkaribisha Mh. Zelote, Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tulole Bucheyeki alisema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa heshima kubwa walioionyesha kwa kufika kwenye Taasisi hiyo na kuweza kukutana na wataalamu wao kwa nia ya kuboresha uwekezaji na vipato vya wananchi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani-kaundasuti) akiwa katika picha ya pamoja na watafiti mbalimbali katika Taaisi ya Utafiti wa Kilimo – uyole, Mbeya pamoja na baadhi ya wataalamu wa Kilimo na Mifugo kutoka Rukwa. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani-kaundasuti) akipewa maelezo ya kilimo cha maharage na mtafiti hifadhi ya mimea Reinfred Maganga (shati nyeupe) katika moja ya bustani ya mifano yaliyopo kwenye viwanja vya taasisi hiyo. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani-kaundasuti) pamoja na uongozi wa Mkoa wa Rukwa wakipewa maelezo ya kilimo cha maparachichi na mtafiti hifadhi ya mimea Reinfred Maganga (shati nyeupe- kushoto) katika moja ya vitalu vilivyopo kwenye viwanja vya taasisi hiyo. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (wa tatu kutoka kulia) akisikiliza uwasilishaji kutoka kwa mtafiti rasilimali za mifugo Dk. Pius Mwambene (wa kwanza kulia) kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI)

Dk. Denis Mwakilembe (kulia) akielezea namna mabua ya zao la mahindi kuwa nia chakula bora cha mifugo mbele ya ujumbe mzima wa Mkoa wa Rukwa ulioongozwa na Mh. Zelote Stephen.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen akiangalia baadhi ya mifugo iliyopo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa mifugo (TALIRI)-Uyole. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa ameshika mbegu za nyasi wanazotakiwa kupatiwa ng’ombe zilizofanyiwa utafiti na TALIRI ili kuepukana na kuhama hama kwa wafugaji, Wa kwanza kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa TALIRI Suleiman Nasibu Masola.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen akipewa maelezo ya namna maabara ya udongo inavyofanya kazi na mtafiti wa udongo Daudi Mujuni katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-Uyole

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (wa pili Kulia) akioneshwa madawa mbalimbali yanayotumika kuzuia uharibifu wa mazao shambani. 

Viongozi wa Mkoa wa Rukwa wakiendelea kupata somo kutoka kwa watafiti mbalimbali wa Kilimo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nyanda za juu kusini -Uyole.
Baadhi ya Wataalamu na wakulima wakiendelea kusikiliza kwa makini mawasilisho ya tafiti mbali mbali za kilimo yaliyofanya na watafiti katika Taasisi ya Utafiti wa kilimo nyanda za juu kusini – uyole. 

(Kutoka kulia) Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen. Tuesday, October 10, 2017

RC Rukwa aishauri benki ya NMB kufungua tawi bonde la ziwa Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameishauri benki ya NMB kufungua tawi katika bonde la Ziwa Rukwa ili kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi ambao shughuli zao kubwa za kiuchumi ni kilimo cha mahindi, mpunga pamoja na uvuvi.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutaepusha matukio ya uvamizi na mauaji yanayofanywa na baadhi ya watu wanaowavizia wakulima na wafanyabiashara wanaoweka fedha majumbani mara tu baada ya mauzo ya mazao yao.

“Mimi nashauri Benki ya NMB muwe na Tawi huku, si lazima kuwa na jengo, hata ile Mobile Banking ambayo mwananchi anaweza kupata huduma zote za kuweka na kutoa fedha katika gari hiyo, ili fedha zao hawa ziwe katika mikono salama,” Mh. Zelote Alisema.

Ametoa ushauri huo katika ufunguzi wa siku ya huduma kwa wateja iliyofanywa na benki ya NMB kanda ya nyanda za juu katika Kijiji cha Mfinga, kata ya Mfinga, Wilaya ya Sumbawanga, kabla ya kukabidhi vifaa vya shule pamoja na hospitali vyenye thamani ya Shilingi milioni 20.

Sambamba na hilo Mh.Zelote amewahamasisha wakulima pamoja na wafanyabiashara wa Kata ya Mfinga kufungua akaunti benki na pia kujiunga katika vikundi ili kuwa na urahisi wa kupata mikopo  na kuweza kuwainua kiuchumi.

“Mbali na kuhifadhi fedha pia benki inatoa mikopo kwaajili ya kujiendeleza na hatimae kuwainua wakulima waweze kuongeza thamani ya mazao yao na kupata soko pana hasa katika awamu hii inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli inayohamasisha uchumi wa viwanda kwa taifa,” Alisema.

Aidha aliwataka viongozi wa Kijiji na wanufaika wa vifaa hivyo kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na ikiwemo kuwahudumia wananchi bila ya bugudha na kuonya kuwa wananchi wasiogope kuwashitaki watumishi wanaowahudumia kwa viburi.

Awali akisoma taarifa fupi ya Benki ya NMB Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja makao makuu ya benki hiyo Richard Makungwa alisema kuwa Benki ya NMB hutenga asilimia moja ya mapato kwa mwaka ili kuirudishia jamii na kuweza kuisaidia katika mambo mbalimbali ikiwemo elimu na afya.

“Kwa kuunga mkono juhudi za Rais wetu tumeamua kama Benki kutoa kompyuta 7, vitanda 8 vya kulalia, vitanda 4 vya kujifungulia, magodoro 8 pamoja na mabati 204 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 20 vilivyotolewa na benki hiyo kama marejesho ya faida kwa wateja watu,” Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akikabidhi Kompyuta kwa Afisa Elimu Manispa ya Sumbawanga Silvestor Mwenekitete katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji cha Mfinga, Wilayani Sumbawanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akikabidhi Kompyuta kwa Afisa Elimu Manispa ya Sumbawanga Silvestor Mwenekitete katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji cha Mfinga, Wilayani Sumbawanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akikabidhi vitanda kwa mganga mfawidhi zahanati ya Mfinga Ephraim Matekele (shati ya draft) katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji cha Mfinga, Wilayani Sumbawanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akikabidhi vitanda kwa mganga mfawidhi zahanati ya Mfinga Ephraim Matekele (shati ya draft) katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja katika Kijiji cha Mfinga, Wilayani Sumbawanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) akiendeleza ujenzi kwa kuweka tofali katika jengo la shule ya msingi Mfinga waliopewa mabati 204 na Benki ya NMB.

Picha ya pamoja 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Kaunda Suti ya Ugoro) katika picha ya pamoja na viongozi wa NMB pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mfinga, Wilayani Sumbawanga. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Godfrey Kalungwizi aliahidi kuvisimamia vifaa hivyo na kuendelea kuwahamasisha wananchi kuchangia katika shughuli za kimaendeleo. 

Uongozi wa Mkoa wa Rukwa waungana kuwafariji wafiwa ajali iliyoua 15 na kujeruhi 9

Uongozi wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi 9 na wafiwa wa vifo vya watu 15 vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso eneo la Ntembwa, Wilayani Nkasi.
Gari iliyopata ajali na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi 9
Gari iliyopata ajali na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi 9

Gari iliyopata ajali na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi 9

Gari iliyopata ajali na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi 9


Katika kuhakikihsa tukio hilo halijirudii Mh. Zelote amepiga marufuku ukiukwaji wa sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na kuonya kuwa yeyote atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.

“Nimekataza binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na wananchi wetu salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema tutumie zile chai maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.

Mh. Zelote alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari hiyo ili kuweza kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa huduma stahiki na kufanikisha zoezi la uokoaji.

Ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425 BFF kuacha njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliochangiwa na ugeni wa barabara hiyo.

Lori hiyo mali ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya mahindi na watu iliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15 kati yao wanawake 10 na wanaume 05.

Waliofariki katika ajali hiyo ni

1.   Domona Tenganamba, 41yrs, mfipa mkulima.
2.     Emmanuel Rashid 84yrs, mfipa mkulima, mkazi wa ntemba
3.     Restuta Sunga , 35yrs, mfipa mkazi wa ntemba
4.     Salula Revana 64yrs, mfipa mkazi wa mtapenda isale
5.     Ferisia Tenganamba , miaka 1 – 6/12
6.     Prisca Madeni, 45yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa china
7.     Richard Chikwangara, 24yrs, mfipa, mwalimu mkazi wa kalambanzite
8.     Yusta Somambuto, 36yrs, mfipa, mkulima mkazi wa kizumbi
9.     Gilesi Ramadhan, 24yrs, mfipa, mkulima mkazi wa sumbawanga
10. Odetha Madirisha 46yrs, mfipa mkulima wa kizumbi
11. Megi Nalunguli, 52yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
12. Abuu Amani @ mandevu, 37yrs, muha, biashara, mkazi wa liapinda
13. Nyandindi Batrahamu, 35yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa sumbawanga
14. Magdalena Mbalamwezi, 50yrs, mfipa, mkulima mkazi wa ntuchi
15. Mtoto mchanga wa wiki mbili, mwanaume ambaye hajapewa jina
Majeruhi wa ajali hiyo ni:-
1.     Dismas Clement, 26yrs, mfipa, mkulima mkazi wa mwinza
2.     Sema Savery 25yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
3.     Ally Haruna, 33yrs, mfipa, mkazi wa namanyere
4.     Yusta Mfundimwa, 50yrs, mkulima mkazi wa izinga
5.     Tenesfory Oscar, 36yrs, mfipa mkazi wa wampembe
6.     Amos Kitambale, 25yrs, mfipa, mkazi wa wampembe
7.     Neema Mwanandenje, 21yrs, mfipa, mkazi wa mlambo
8.     Joseph Sungula, 28yrs, mfipa, mkulima.
9.     Majeruhi mmoja mwanamke ambaye hajafahamika kwa jina yuko icu

Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva alitoroka lakini juduhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea kufanyika.