Thursday, October 11, 2018

DC Kalambo awataka wasichana kuanza kijilinda wenyewe kupunguza mimba za utotoni


Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura amewataka wasichana wa shule za msingi na sekondari kuhakikisha wanaanza kujilinda wenyewe kwa kutojiweka na kujihusisha na mazingira tatanishi wanapotoka shuleni na badala yake waendelee kusaidi kazi za nyumbani na kujisomea wakiwa nyumbani.
Wawakilishi wa watoto wa kike Mkoa wa Rukwa wakionyesha idadi ya watu wanaounga mkono kubadilishwa kwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 na 17 katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa kike Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nelson Mandela mjini Sumbawanga. 


Mwanafunzi Beatrice James akisoma maombi ya kubadilishwa kwa sheria ya ndoaya mwaka 1971 kifungu cha 13 na 17 katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa kike Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nelson Mandela mjini Sumbawanga. 


Mwanafunzi Beatrice James akimkabidhi maombi ya kubadilishwa kwa sheria ya ndoa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika Maadhimisho ya Siku ya mtoto wa Kike Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mandela Mjini Sumbawanga. 

Watoto waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa kike Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nelson Mandela mjini Sumbawanga. 
Watoto waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa kike Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nelson Mandela mjini Sumbawanga. 


Ameyasema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga huku akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kama mgeni rasmi wa maadhimisho hayo.

Pia ametoa wito kwa wazazi na walezi mkoani humo kuhakikisha wanawalinda watoto wa kike lakini ili kupunguza vitendo vya ukatili amewaomba wazazi kushirikiana kujenga mabweni ili kuwahakikishia ulinzi watoto hao.

“Kauli mbiu inasema tuwalinde watoto wa kike, ni kweli tuwalinde kwani tusipofanya hivyo, tutahatarisha nchi yetu na kuhatarisha dunia nzima kwa watoto kukosa maadili mazuri, maadili yanatoka kwetu wazazi, nawaomba wananchi qwote wa Mkoa wa Rukwa tuwalinde watoto wetu wanapokuwa mashuleni na majumbani,” Alisisitiza.

 Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mwanafunzi Amina Suleiman amesema kuwa ingawa katika familia nyingi hawatoi kipaumbele cha kuwasomesha watoto wa kike lakini imeshuhudiwa mara kadhaa watoto hao wa kike ndio wanaowalea wazazi.

“Utafiti uliofanywa na wadau mbalimbali wa haki za watoto, umebaini kuwa hali duni ya kiuchumi ya wazazi wengi umechangia watoto wao wa kike kukatisha masomo kwa lengo la kuwaoza au kuwapeleka kufanya kazi za ndani ili waweze kuwasaidia kipato kidogo wanachokipata,” Alibainisha

Halikadhalika aliongeza kuwa shirikala maendeleo ya wasichana linasema kuwa wasichana milioni 39 kati ya umri wa miaka 11 hadi 15 hawamalizi masomo yao.

Kuanzia Julai 2017 hadi Mei 2018 jumla ya wanafunzi 149 wamepata ujauzito katika mkoa wa Rukwa, huku wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa 59 na sekondari ni 98. Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na watendaji wa kata kufikisha kesi hizo polisi na mahakamani kwa hatua Zaidi na mapaka sasa matukio yote 149yameripotiwa polisi na 7 yapo mahakamani.


No comments:

Post a Comment