Sunday, October 7, 2018

Kaimu Balozi wa Marekani aahidi kusaidia kupambana na Udumavu Rukwa.


Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Patterson amesikitishwa na hali mbaya ya udumavu iliyopo katika mkoa wa Rukwa na kuahidi namna ya kusaidia kupunguza udumavu huo uliopo ili kuokoa maisha ya watoto na hatimae kuwa na kizazi chenye akili ili kuifikia Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akiongea na Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Patterson. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) akiongea na Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Patterson (Kushoto) na Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard MakaliInmi amesema kuwa siku 1000 za mwanzo ni muhimu sana kwa mtoto mdogo katika kujenga afya ya mwili na akili na endapo mtoto huyo atakosa chakula bora katika siku hizo basi itakuwa ni hasara kwa mtoto lakini kwa taifa pia.

“Kuna maneno mawili ya Kiswahili siyapendi; UDUMAVU na UTAPIAMLO, nchini Tanzania haipendezi kuwa na udumavu na utapiamlo kwasababu chakula kipo cha kutosha, udumavu ni uhalifu, sisi sote tuna wajibu wa kufanya kazi pamoja kupunguza udumavu mpaka sifuri, huu udumavu unaiumiza sana,” Alisema

Kwa upnde wake mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema kuwa Halmashauri kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wanao mpango kabambe wa kuhakikisha kuwa udumavu huo unapungua kama sio kuisha kabisa na kutanguliza shukrani kwa kaimu balozi juu ya fikra yake ya kutaka kuusaidia mkoa wa Rukwa kuondokana na udumavu kabisa.

Hali ya udumavu kitaifa ni asilimia 34 na katika mkoa wa Rukwa ni asilimia 56.3.

Halikadhalika kaimu Balozi huyo alisifu serikali ya mkoa wa Rukwa kwa kupambana na kupunguza maambukizi ya kiwango kutoka asilimia 6.2 mpaka asilimia 4.4 na kuwaomba wajitahidi hadi kufikia asilimia 0.  

No comments:

Post a Comment