Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa Shilingi
150,000/= kwa vikundi vitatu vya muziki ikiwa ni kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na vikundi hivyo katika kukuza utamaduni na sanaa ya mtanzania.
“Kila kikundi kilichokuja hapa, vile vitatu
navipa shilingi 50,000/=, na hii ni chachu tu kwa makundi mengine, waweze kuona
uzito wa kutunza na kuimarisha tamaduni zetu lazima tuendeleze tamaduni zetu,
taifa lisilokuwa na utamaduni limelala, na sawa na kufa kabisa,” Alisema.
Aidha, aliwataka vijana kujishughulisha na sanaa
za utamaduni ili kulinda na kuenzi na kutopoteza nembo ya taifa na utambulisho
kama watanzania na kasha kutumia nafasi hiyo kivipongeza vikundi vitatu; kikundi
cha Kwaya ya Sopa, kikundi cha ngoma za utamaduni cha maporomoko na kikundi cha
muziki wa kisasa cha Wasafi boys.
Alitoa zawadi hiyo katika maadhimisho ya siku ya
utundikaji mizinga kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kijiji cha kisumba,
kata ya kisumba, Wilayani Kalambo.
No comments:
Post a Comment