Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametaka
kupewa mpango kazi wa ujenzi unaoendelea wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha
Mkoa, kinachojengwa katika mtaa wa Kaswepepe, kata ya Sumbawanga asilia,
Wilayani Sumbawanga ili kufuatilia kwa ukaribu na kuweza kukosoa pale
mkandarasi atakapokwenda kinyume na alichokiandaa.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo, itasaidia kukosoa
maendeleo ya ujenzi mapema kabla mambo hayajaharibika na si kulalamika baada ya
kukamilika kwa ujenzi na kulaumu ubadhirifu uliojitokeza wakati fursa ya
kufuatilia ilikuwepo.
“Ningependa nipatiwe “Work plan” mpango kazi ambao
mnao, hatua kwa hatua ili na mimi nikikaa kule najua mwezi lazima mko hatua
Fulani, nikiona inafaa ntakuja kukagua, mwenyekiti wa ulinzi na usalama Wilaya
nae apewe mpango kazi, Mstahiki Meya nae apewe ili tufuatilie kwa pamoja ili
kama kuna mapungufu tuambiane mapema, tusingoje kuviziana kwamba hili
limeharibika,” Alisisitiza.
Ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele kulia) akitoa akitaka ufafanuzi juu ya uwakilishi wa majengo kwa mashimo yaliyochimbwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akitaka ufafanuzi juu ya uwakilishi wa majengo kwa mashimo yaliyochimbwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiangalia ubora wa matofali yatakayotumika katika ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ambapo Mkandarasi alisemakuwa anatumia mfuko mmoja wa saruji kutoa matofali 20.
Ameongeza kuwa kwenda vibaya kwa mambo na kufika mwisho
itashindikana kurudisha nyuma na matokeo yake ni kumfunga mhusika
aliyesababisha uharibifu wakati fedha za serikali zimekwishapotea na huku
wananchi bado wanahitaji maendeleo. Ameyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua
ujenzi wa chuo hicho.
Kwa upande wake akisoma taarifa ya ujenzi Mkadiriaji
majengo wa ujenzi huo Faraji Selemani alisema kuwa ujenzi huo utagharimu
shilingi bilioni 10.7 hadi kukamilika kwake ambapo kutakuwa na majengo tisa
yatakayohusisha fani mbalimbali pamoja na jengo la utawala.
“mradi utakuwa na majengo yafuatayo, majengo ya
utawala, madarasa pamoja na maktaba, “workshops” mbali mbali 9, mabweni ya
wanafunzi wa kike na wakiume, vyumba vya waalimu na makazi yao na sehemu ya
kufanyia mazoezi kwa vitendo,” Alimalizia.
Ujenzi huo ambao
umeanza mapema mwezi wa tisa mwaka huu baada ya makabidhiano baina ya VETA
makao makuu Dar es Salaam, VETA kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya pamoja na
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kumkabidhi mkandarasi TENDER Intarnational
kwaajili ya ujenzi wa chuo hicho huku mshauri elekezi akiwa Sky Architect
Consultancy Ltd.
Ujenzi ukikamilika chuo kitaweza kuchukua wanafunzi 900
wa kozi ndefu na 600 wa kozi fupi hivyo, kitakuwa na uwezo wa kuchukua jumla ya
wanafunzi 1,500.
No comments:
Post a Comment