Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga James Mtalitinya
ameendelea kuwahamasisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuhakikisha
wanajiunga katika vikundi ili kuweza kupata fursa ya kupewa mikopo ili kuweza
kujiajiri hali itakayopelekea kupunga wimbi la wasio na ajira na hatimae
kujiongezea kipato.
Amesema kuwa moja ya majukumu ya Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga ni kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye
ulemavu na kuongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri ilitoa
shilingi milioni 253 na kusisitiza kuwa bado kuna milioni 32 zilizovuka mwaka
ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri inatakiwa kutoa shilingi
milioni 230.
“Kufikia Mwezi wa 10 tarehe 15 tunategemea kutoa kiasi cha
shilingi milino 120 ikiwa ni makusanyo ya robo ya kwanza kwa maana ya Julai –
Septemba, kwahiyo tunaomba wananchi wa bangwe pamoja na wananchi wa Sumbawanga
wajiunge katika vikundi visivypongua watu watano mpaka kumi halafu waainishe
shughuli wanayofanya na waje waombe mkopo wa kiasi chochote, tutawakagua na
baada ya hapo tutawapatia mkopo,” alimalizia.
![]() |
Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya |
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.
Joachim Wangabo walipokuwa wakitembelea masoko yaliyopo katika mji wa
Sumbawanga ili kujionea hali halisi ya maendeleo ya biashara na kujua changamoto
mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi katika masoko hayo.
No comments:
Post a Comment