Friday, October 28, 2011

MKUU WA MKOA WA RUKWA YUPO ZIARANI MKOANI RUVUMA IKIWA NI ZIARA YA KIKAZI YA KIBUNGE, AKIWA HUKO APOKELEWA KWA SHANGWE

Viongozi wa chama wa Wilaya ya Namtumbo wakimpokea Mbunge Mhandisi Stella Manyanya


Mama wa Kimasai akimpatia zawadi za kabila hilo Mhandisi
Stella Manyanya Mbunge baada ya kuwahutubia wananchi wa Songea Mjini katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji


  
Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakimkaribisha Mbunge na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya kwenye viwanja vya mkutano vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji SongeaKwenye ngoma pia anaweza, hapo akicheza ngoma baada ya kupokelewa Kata ya Kitanda Wilayani Namtumbo


Mhandisi Stella Manyanya ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma akimpatia Katibu wa UWT Wilaya ya Songea Mjini shillingi laki mbili kwa ajili ya mahitaji madogo madogo ya ofisi ya UWT Wilaya ya Songea Mjini,baada ya kupokea ripoti ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka 2011, katikati ni Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph
Diwani wa Kata ya Kitanda Vitus Ngoma akipokea jezi kwa ajili ya timu ya Kata kutoka kwa Mhandisi Stella Manyanya(Mb) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

Hapo akihutubia wananchi wa Songea Vijijini


Kwa matukio zaidi tembelea http://www.stephanomango.blogspot.com


Tuesday, October 25, 2011

MATUNDA YA KONGAMANO LA UWEKEZAJI YAANZA KUONEKANA - TPM WAANZA KUWEKEZA KWA KASI MPANDA

Huu ni moja ya mtambo ya kiwanda cha Tanzania Pema Mining Energy Company (TPM) cha kutengeneza madini ya shaba kinachojengwa mjini Mpanda tayari kwa kuanza kazi hiyo na ununuzi wa madini hayo wakati wowote kuanzia sasa, Mwenyekiti wa kiwanda hicho Bw. Servet Sukru Yazigi anasema kiwanda hicho kikikamilika kitaweza kutoa ajira ya watanzania wapatao 160 ambayo itakuwa ajira ya kudumu. na watanzania wengine zaidi ya 200 wataweza kupata ajira za muda mfupi. (PICHA NA KIBADA ERNEST WA MPANDA)

Monday, October 24, 2011

MKUU WA MKOA WA RUKWA ACHANGISHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 3.9 KUFANIKISHA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MWANARUKWA LITAKALOFANYIKA TAREHE 25-27 NOVEMBA 2011

Tangu mwaka 1994 Baraza la Makumusho la Taifa limekuwa likifanya matamasha mbalimbali ya kuhusisha makabila tofauti ya Kitanzania.

Matamasha hayo huwa na lengo la kuonyesha Utamaduni wa kimila na desturi za jamii fulani kwa kuhusisha maendeleo na mafundisho yake.

Mambo hayo ya kimila ni pamoja na Lugha, chakula, utamaduni, mavazi, sanaa, zana za kimila, na mambo mengine ya kijamii.

Mwaka huu kwa mara ya kwanza kabisa Jamii za wanarukwa zimepata fursa ya kuonyesha tamaduni zao kuanzia tarehe 25-27 Novemba 2011 katika viwanja vya makumbusho vilivyopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. (Pichani Mbunge wa Jimbo la Kwela Ndugu Ignas Malocha akitoa mchango wake kwa Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alilazimika kuendesha harambee ya kuchangishana ili kuweza kuharakisha maandalizi ya Tamasha hilo, Mwenyewe binafsi alianza kwa kutoa mchango wa Millioni moja na wadau wengine kuendelea kuchangia akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda aliyechangia kwa kujipiga faini baada ya kuchelewa kwenye kikao hicho ambapo aliahidi shilingi Milioni Mbili.

 Fedha alizoahidi Waziri Mkuu sio katika zile alizochangisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa bali ni sehemu ya mchango wake katika kufanikisha tamasha hilo.

Maandalizi ya Tamasha hilo bado yanaendelea na michango bado inaendelea kutolewa, kwa yeyote mwenye uwezo na nia anaombwa kuchangia kuweza kufanikisha Tamasha hilo muhimu.


Msanii Mkongwe Nchini Komandoo Hamza Kalala akionyesha mchango wake kwa wanajamii ya wanarukwa, Kulia nia Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kwa upande wa Dar es Salaam Mama Mwangaza na Katibu wake  Ndugu Santo.

Baadhi ya wadau waliohudhuria kwenye kikao hicho cha maandalizi

Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyemaliza muda wake Bw. Daniel Ole Njoolay na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyekabidhi kijiti kwa Injinia Manyanya (Daniel Ole Njoolay) akisalimiana na jamii ya wanarukwa wanaoishi Jijini Dar es Salaam

Waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma kuandika na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu Tamasha hilo, hapo wakimuhoji Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

MKOA WA RUKWA WATOA RAMBIRAMBI KWA WAHANGA WA AJALI YA MELI YA MV SPICE ISLANDER YA ZANZIBAR

Kufuatia ajali mbaya na ya kusikitisha iliyopelekea Meli ya MV Spice Islander kuzama na kusababisha vifo vya takribani watu 203 na majeruhi  619 huko Zanzibar, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa pamoja na Jamii ya wanarukwa imejumuika kwa pamoja kuwachangia wahanga wa ajali hiyo jumla ya mifuko 100 ya mchele kila mfuko ukiwa na jumla ya kilo hamsini.

Zawadi hiyo ilikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Maratin Manyanya (MB) kwa Mhe. Mizengo Kayanza Pinda (MB) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Viwanja vya Makumbusho Kijitonyama Jijini Dar es Salaam jana usiku.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa wao kama wanarukwa waliguswa sana na tukio hilo na kwamba njia mojawapo ya kuonyesha masikitiko yao ni pamoja na mchango walioutoa. Hata hivyo alisema kuwa mchango huo ni sehem tu ya masikitiko yao na kwamba wanawaombea wale wote walioguswa na msiba huo na kuwataka wawe na subira. 


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) akikabidhi gunia la mchele kati ya magunia hamsini yenye ujazo wa kilo mia moja kwa Mhe. Waziri Mkuu aliyekaa kushoto kwake katika ukumbi wa Makumbusho Kijitonyama Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander.
  

Sunday, October 23, 2011

RC RUKWA AKIWA SAFARINI DSM KIKAZI AKUTANA NA WAJASIRIAMALI WADOGO WA USAFIRISHAJI NA KUWAPA NASAHA ZAKE

Matrekta madogo aina ya Powerteallers yalitolewa na Serikali katika mpango wake wa kuboresha kilimo kwanza nchini huweza pia kutumika kwa shughuli mbalimbali kama kukokota mizigo na hata kuzungusha mashine za kusaga na kukoboa nafaka. Pichani wakulima wa kijiji cha Tunko katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakisafirisha karanga kutoka eneo moja kwenda eneo lingine la biashara.

Hapo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) alipokutana na wasafirishaji hao na kuwashauri kuwa makini kuepusha ajali na kuongeza ubora katika biashara zao kwani biashara yeyote ile bila kujali udogo au ukubwa wake cha muhimu ni kuiongezea ubora (thamani)

Punda nao ni sehem ya Usafirishaji kwa jamii ya wanarukwa. Zipo fursa nyingi za uwekezaji katika ukanda huu wa Ziwa Tanganyika ukizingatia kuwa barabara zote zinazoingia na kutoka katika mkoa huu zinajengwa kwa kiwango cha  lami. Tukiwa safarini Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akisalimiana na Ndugu Joakim Mwaniti alipokuwa kwenye shughuli zake za usafirishaji wa mkaa aliodai kuwa ameununua, alisema hayo baada ya kumtoa wasiwasi kuwa lengo letu sio kumuhoji kuhusu alikopata mkaa huo.

Thursday, October 20, 2011

ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA RUKWA AAGWA RASMI

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Daniel Ole Njoolay akiwa na Mama Njoolay usiku wa jana alipokuwa akiagwa katika ukumbi wa Upendo View Wilayani Sumbawanga 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Daniel Ole Njoolay ameagwa rasmi jana katika ukumbi wa Upendo View uliopo wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo ilikuwa pia ya kumkaribisha rasmi Mkuu mpya wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB).
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali na sekta binafsi katika Mkoa wa Rukwa. Bw. Daniel Ole Njoolay alishukuru kwa ushirikiano aliopewa kwa kipindi chote alichokuwa madarakani akiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Alisema kuwa "Maendeleo haya ya Mkoa wa Rukwa siyo ya kwangu peke yangu bali ni yetu sote"
Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa Mkuu wa Mkoa aliyemaliza muda wake na yule aliyechukua nafasi. Kwa upande wake Injinia Manyanya ambaye ndiye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa sasa alisema "Zawadi hizi mlizotoa hapa leo ni za aina mbili, moja ya kumpongeza Bw. Njoolay lakini ya kwangu mimi ni deni na ninaahidi kulilipa kwa kuwafanyia kazi nnachoomba kwenu ni ushirikiano".
Aliendelea kusema kuwa watu wengi huogopa kuishi ndani ya mabadiliko, akawaasa wanarukwa kutokuogopa mabadiliko na kuwasihi kuonyesha ushirikiano, kudumisha amani na kuepuka misuguano ya kisiasa kwakuwa itamuongezea mzigo usiokuwa na ulazima.  
Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa aliyemaliza muda wake Bw. Daniel Ole Njoolay aliaga kwa kuwaachia wanarukwa changamoto nne, moja ikiwa ni elimu kwani wananchi wengi wa Rukwa elimu kwao sio kipaumbele aliwaasa wanarukwa kuikumbatia elimu.
Changamoto nyingine ni uharibifu wa mazingira hususani uchomaji moto misitu, tatizo la masoko na fursa iliyotolewa na Rais ya kuuza mazao nje itumike kutafuta masoko katika nchi jirani. Nyingine ni uboreshaji wa michango kwa ajili maendeleo ya Rukwa, Halmashauri na wadau wengine wa maendeleo wameelekea kusuasua kuchangia kitu ambacho kitazorotesha maendeleo ya Rukwa.
Alimalizia kwa kusema kuwa changamoto hizo pamoja na nyingine za miundombinu ambazo zishaanza kupatiwa ufumbuzi zikikamilika na kufanyiwa kazi ipasavyo basi kuna matuamaini makubwa kuwa katika miaka kumi (10) ijayo Mkoa wa Rukwa ndio utakaoongoza kiuchumi nchi nzima.

Wednesday, October 19, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI MPANDA, AREJEA DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katika uwanja wa ndege wa Mpanda muda mfupi kabla kuondoka, nyuma yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Col. Mst. Issa Machibya. 
Rais Kikwete akisalimiana na viongizi muda mfupi kabla ya kuondoka. Kushoto kwake ni Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hilal

 Rais Kikwete akipungia wananchi muda mfupi kabla ya kuondoka

Rais kikwete akiwapungia wananchi mkono tayari kwa kuondoka kurejea Dar es Salaam

MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA NA KONGAMANO LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA KUTOA TASWIRA MPYA YA UWEKEZAJI KATIKA UKANDA HUO


Kongamano la Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika limefanyika tarehe 17 Oktoba  2011 Wilayani Mpanda na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya mia 300. Mgeni rasmi katika Kongamano hilo alikuwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye aliyefungua Kongamano hilo rasmi.
Mwenyekiti wa Kongamano hilo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (MB). Kongamano hilo lilihudhuriwa na mawaziri mbalimbali, mabalozi, wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na wadau mbalimbali wa uwekezaji wakiwemo wajasiriamali na viongozi wa chama na serikali.
Yalikuwepo maonyesho kwa njia ya mabanda ambayo wajasiriamali tofauti na baadhi ya wawekezaji walinadi bidhaa na fursa mbalimbali za uwekezaji. Maonyesho hayo yalikuwa ya siku nne (4) kuanzi tarehe 15-18 Oktoba 2011. Mada mbalimbali ziliwasilishwa katika kuonyesha fursa zilizopo kwenye Ukanda wa Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, Aidha Halmashauri zote za Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi zilipata fursa ya kunadi miradi yake ambayo inahitaji uwekezaji.
Ili kufanikisha adhma ya kufungua Ukanda wa Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, Kongamano hilo lilifikia makubaliano kadhaa ambayo yakifanyiwa kazi ipasavyo itarahisisha na kufanikisha uwekeza kwa njia rahisi, Makubaliano hayo ni kama ifuatavyo:
 • Halmashauri zote kutenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji.
 • Hakuna maendeleo ya kiuchumi bila uwekezaji.
 • Kuinua rasilimali zilizopo kwa kuongeza uzalishaji.
 • Uwekezaji katika sekta ya nishati upewe kipaumbele cha kwanza.
 • Ianzishwe ofisi ya Uwekezaji (TIC) katika Ukanda wa Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika.
 • Awepo mtu maalum (One Stop Centre) ambaye atakuwa kiunganishi kwa Mikoa yote mitatu (Rukwa, Kigoma na Katavi)
 • Kujenga mfumo mmoja unaokubalika na wote kwa ajili ya uwekezaji tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo kuna baadhi ya watu wanaukubali uwekezaji na wengine wanaukataa.
 • Jamii ishirikishwe ipasavyo katika kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji kwa mujibu wa sheria (Act No: 48.5) ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya msingi.
 • Kuvutia uwekezaji katika sekta ya ufugaji wa nyuki.
 • Mikoa yote kushawishi wawekezaji wa ndani.
 • Kutambua na kuainisha maeneo kwa ajili ya huduma za mawasiliano
 • Kuwaongezea uwezo watendaji katika Serikali za Mitaa na Halmashauri ili waweze kufanya mambo kwa ufanisi zaidi.
 • TIB (Benki ya Uwekezaji Tanzania) ipitie sera zake za mikopo upya kuwawezesha watanzania wa hali ya chini kupata mikopo na kuwekeza.
 • Kuandaa mpango mkakati wa matumizi bora ya ardhi kwa mkoa mpya wa Katavi.
 • Kuandaa mipaka sahihi katika Ziwa Tanganyika kuweza kuruhusu uchimbaji wa mafuta kirahisi.
Makubaliano hayo yalifikiwa na wajumbe wote wa mkutano huo ili kufanikisha uwekezaji wenye tija na wa kudumu katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Makubaliano hayo yalipata Baraka zote kutoka kwa wajumbe wakiongozwa na mwenyekiti wa Konagamano hilo Mhe. Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda. Makubaliano hayo yakifanyiwakazi ipasavyo ni wazi kuwa Ukanda wa Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika utapata taswira tofauti na mafanikio makubwa.  

Tuesday, October 18, 2011

HAKUNA MAENDELEO BILA UWEKEZAJI - RAIS KIKWETE

RAIS Jakaya Kikwete amesema hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana nchini kama hakuna uwekezaji wowote utakaofanyika kwa sababu hakuna Taifa lolote linaloendelea bila kukaribisha uwekezaji wa nje.
“Hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana kama hakuna uwekezaji, penye maendeleo ni lazima kuwe na utoaji wa huduma za jamii... kama hukuwekeza hakuna utakachozalisha, na kama hukuwekeza hakuna huduma utakayotoa,” alisema na kusisitiza kuwa ajenda kubwa ya serikali ni kuvutia uwekezaji nchini.
Katika hotuba yake iliyodumu kwa saa moja na nusu wakati akifungua mkutano wa siku moja wa uwekezaji wa Kanda ya Uwekezaji ya Ziwa Tanganyika, Rais Kikwete alisema Serikali itaendelea na jukumu lake la kutengeneza mazingira ya kukuza uchumi ili sekta binafsi iweze kutekeleza majukumu yake.
Alisema mikoa ya Kanda ya Ziwa Tanganyika inayojumuisha Rukwa, Kigoma na mkoa tarajiwa wa Katavi imekuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu ya uwekezaji mdogo uliokuwepo miaka ya nyuma.
Alibainisha kwamba hali sasa itabadilika kwa sababu Serikali imeamua kuwekeza katika miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na bandari ili kuifungua mikoa hiyo. “Katika mkoa wa Rukwa peke yake, mbali ya uwekezaji katika maeneo mengine, Serikali imewekeza sh. bilioni 490/- kwa ajili ya ujenzi wa barabara, wakati katika mkoa wa Kigoma fedha zilizowekezwa kwenye barabara ni mara mbili ya hizo,” alisema.
Akizungumza na washiriki wa kongamano hilo ambao ni mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, wawekezaji, wafanyabiashara, wakuu wa taasisi za Serikali, wabunge na baadhi ya wakuu wa mikoa, Rais Kikwete alisema angependa kuona kanda ya Ziwa Tanganyika ikishamiri kimaendeleo. (I would like to see this sleeping giant - Lake Tanganyika Zone - awakening).
Aliwataka washiriki wa mkutano huo waangalie fursa za uwekezaji zilizopo katika madini, uvuvi, safari za majini, utalii, kilimo, viwanda, usafiri wa anga na barabara, ufugaji na hata kilimo cha miwa hasa katika maeneo ya Kigoma.
Alitumia fursa hiyo kuwathibitishia wakazi wa wilaya Mpanda ambao walikuwa wakifuatilia mkutano huo kwenye mahema nje ya ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwamba kabla ya mwisho wa mwezi huu, mkoa mpya wa Katavi utakuwa umetangazwa baada ya taratibu zote kukamilika. Wilaya ya Mpanda ni mojawapo ya wilaya zitakazounda mkoa mpya wa Katavi.
Kuhusu bandari, Rais Kikwete alisema bandari tano kati ya 19 zilizopo katika Ziwa Tanganyika tayari ziko katika mpango wa kufanyiwa ukarabati wakati meli ya siku nyingi ya MV Lihemba iko mbioni kukarabatiwa ili kutunza historia yake ya zaidi ya miaka 100.
“Bandari za Kigoma na Kasanga zitapanuliwa na kuboreshwa ili ziwe na hadhi ya kimataifa, bandari nyingine za Kirando, Karema na nyinginezo, zitakarabatiwa kadri tunavyoendelea,” aliongeza.
Kuhusu viwanda vya ndege vya Rukwa, alisema baada ya kukamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, Serikali itafanya ukabati mwingine katika kiwanja kidogo cha ndege cha Sumbawanga (airstrip).
Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma, Rais Kikwete alisema mkandarasi amekwishapatikana na ukarabati wake utaanza hivi karibuni. “Ninatamani kuona uwanja wa ndege wa Kigoma ukiwa ni kitovu cha mawasiliano ya ndege zote katika ukanda wa maziwa makuu...,” alisema.
Mkutano huo ambao kaulimbiu yake ilikuwa “Kuibua Fursa za Uwekezaji katika Kanda ya Ziwa Tanganyika” (Unleashing Potentials for Lake Tanganyika Zone) ulikuwa na lengo la kuinua fursa za uwekezaji katika Kanda ya Uwekezaji ya Ziwa Tanganyika ambayo inaihusisha mikoa ya Rukwa, Kigoma na mkoa mpya-tarajiwa wa Katavi ambayo yote kwa pamoja imejaliwa maliasili nyingi zikiwemo madini, vivutio vya utalii, ardhi nzuri ya kilimo na maeneo ya uvuvi.
Rais Kikwete ameondoka Mpanda jana kurejea jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA MJINI MPANDA

Picha ya Pamoja kati ya Rais Jakaya Kikwete na mabalozi mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo, waliokaa kulia ni Mhe. Mary Nagu waziri wa viwanda na biashara, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kushoto waliokaa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Col. (Mst) Issa Machibya. 

Rais Jakaya Kikwete akihutubia ukumbini. Kongamano hili lilihudhuriwa na mabalozi mbalimbali, mawaziri, wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.

Kongamano hili lilirushwa LIVE na Televisheni ya Taifa TBC 1, Muongozaji wa matangazo hayo akiwa kazini.

Zito Kabwe naye alikuwepo. Hapo akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda.

Rais Jakaya Kikwete wakibadishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya Nje ya Ukumbi wa Mkutano wa Idaya ya Maji Mjini Mpanda palipofanyika Mkutano huo wa Uwekezaji.

Rais Jakaya Kikwete akizindua Tovuti (Website) ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika, wanaoshuhudia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Viwanda na Biashara Marry Nagu (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Col. Mst. Issa Machibya (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya. Tovuti hiyo ni www.laketanganyikazone.go.tz

Rais Jakaya Kikwete akihutubia kwenye Kongamano la Uwekezaji. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Col. Mst. Issa Machibya na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimkaribisha Mhe. Rais Jakaya Kikwete aweze kuhutubia wadau wa uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Rais Kikwete akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya akiwasili kwenye eneo la ukumbi wa Idara ya Maji wilayani Mpanda kwa ajili ya kufungua Kongamano la Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika.
  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda tayari kufungua kongamano la Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.

Sunday, October 16, 2011

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MABANDA YA UWEKEZAJI MJINI MPANDA, ASEMA UWEKEZAJI UWANUFAISHE ZAIDI WANANCHI


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dr. Rajab Rutengwe alipotembelea mabanda ya uwekezaji na wajasiriamali katika eneo la Idara ya Maji Mjini Mpanda. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) wakibadilishana maneno na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw. Salum Mohammed Chima.Waziri Mkuu alipotembelea banda la Ofisi y mkuu wa Mkoa Rukwa. Katikati ni mchumi Bw. Florence Chrisant na Daktari wa Mifugo Bw. Respich Maengo wataalam wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa waliokuwa mstari wa mbele kutoa elimu na taarifa mbalimbali kuhusu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

Waziri Mkuu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mabanda ya uwekezaji na wajasiriamali mjini Mpanda. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB). Miongoni mwa mambo muhimu aliyozungumza ni kuona kuwa uwekezaji unawanufaisha wananchi hususani wakulima wadogo kwa kuwapatia zana bora za kilimo, mbegu bora na masoko ya uhakika.

Saturday, October 15, 2011

UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI TUNDUMA-SUMBAWANGA-MPANDA NA KASANGA WAENDELEA...

Baadhi ya maeneo ya Kaengesa kuelekea mpui tayari wakandarasi hao wameshaanza kujenga kwa kiwango cha lami kama inavyoonekana barabara baada ya kuweka lami ya awali.
Picha kwa hisani ya http:// fullshangwe.blogspot.com
Hapa ni maeneo ya Kaengesa ambapo wakandarasi wanajitahidi kuhakikisha wanajenga barabara hiyo kwa kiwango bora kabisa.
Hili ni daraja maeneo ya Mpui kama unavyoona wakandarasi wakiendelea na ujenziwa barabara.

Hapa kuna mwamba mkubwa barabarani hivyo wakandarasi wamelazimika kuvunja mwamba huo ili kujenga barabara bia matatizo.
Hapa ni maandalizi ya ujenzi a daraja.
Hapa inasemekana hali ya ardhi yake siyo nzuri kwani kuna maji mengi hivyo wakandarasi wa barabara hiyo wamelazimika kutandaza turubai zito kabla ya kuweka udongo na kokoto na kisha kumwaga lami katika eneo hilo.
Hapa ni baada ya kutoka Tunduma maroli haya yanayofanya kazi ya ujenzi wa barabara kati ya Tunduma na Laela yakiwa yameegeswa katika moja ya vijiji ambavyo barabara hiyo inapitia.

Thursday, October 13, 2011

NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju wa pili kulia alipoenda kutambulishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kanda ya Sumbawanga muda mfupi kabla ya kuondoka.   
Injinia na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuondoka.  

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akipokea maneno ya mwisho kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kanda ya Sumbawanga kabla ya kuondoka kuelekea Mbeya kwa ziara nyingine ya kikazi.