Wednesday, November 30, 2011

WAWEKEZAJI SIO LAZIMA WATOKE NJE, MIMI MWENYEWE NI MUWEKEZAJI, ASEMA WAZIRI MKUU PINDA

WAZIRI MKUU, Mhe. Mizengo Peter Pinda (MB) amesema suala la uwekezaji hapa nchini haliwalengi watu wa nje tu bali hata wa ndani wanaweza kuwekeza hata kama ni kwa kiwango kidogo.

Ametoa kauli hiyo siku ya Jumatatu, Novemba 29, 2011 wakati akizungumza na wakazi wa mikoa ya Rukwa, Ruvuma na mkoa tarajiwa wa Katavi katika chakula cha jioni ambacho aliwaandalia kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Wakazi hao zaidi ya 100 walikuwa wamealikwa kuja jijini Dar es Salaam kushiriki tamasha la Utamaduni la mikoa ya Rukwa na mkoa tarajiwa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tamasha hilo lilifanyika Novemba 25-27, 2011, katika kijiji cha Makumbusho jiini Dar es Salaam.

Akifafanua kuhusu uwekezaji Waziri Mkuu alisema yeye alipochukua mkopo waliopatiwa wabunge wa sh. milioni 90, hakuona haja ya kununua gari bali aliamua kuwekeza katika ujenzi wa nyumba ya kulala wageni kijijini kwao, Kibaoni wilayani Mpanda.

“Nilichukua mkopo mwingine benki ya NMB na kuamua kujenga vyumba 24 pale kijijini kwetu. Kama ningetaka ningechukua mafundi wazuri kutoka Kariakoo, (Dar es Salaam) lakini niliamua kutumia mafundi wa kijijini ili kutokana na zile fedha nao pia waweze kununua bati na kuezeka katika nyumba zao, jambo ambalo limewezekana,” alisema.

“Ujenzi wa vyumba 24 karibu unakamilika, … kiasi kingine cha fedha nililima shamba la mahindi na nikafanikiwa kuvuna magunia 380,” aliongeza.

Waziri Mkuu anasema aliamua kuuza magunia 300 kati ya hayo aliyovuna na kupata sh. milioni 11 ambazo aliziwekeza tena katika mradi wa ufugaji nyuki kijijini kwao na Dodoma.
“Nina mizinga 250 kule Dodoma na Kibaoni (kijijini kwao) nina mizinga 600, kila mzinga unauzwa sh. 50,000/- na kila mmoja una uwezo wa kutoa lita 10 za asali. Bei ya asali hapa mjini ni sh. 10,000/- kwa hiyo katika kila mzinga unaweza kupata sh. 100,000/-,” alisema.

Alisema suala la uwekezaji ni muhimu na haliepukiki na kumtaja Mbunge wa Mpanda Mjini, Bw. Said Arfi ambaye alikuwepo katika hafla hiyo kwamba ni miongoni mwa wawekezaji wadogo kwani ana ekari 200 za mahindi na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Kanali Antonio Mzurikwao kuwa naye ana ekari 100 za mahindi. “Hawa nao ni wawekezaji lakini tunawaita wawekezaji wadogo,” alisema.

Akifafanua kuhusu uwekezaji, Waziri Mkuu alisema nchi zote zilizoendelea zilifaulu kufiki hatua hiyo kwa kupunguza idadi ya wakulima wadogo na kuongeza idadi wa wakulima wakubwa. “Mkiona wakulima wadogo ni wengi mjue kuwa bado hamjapunguza umaskini,” aliongeza.

Alisema Taifa bado linakabiliwa na changamoto ya kupunguza umaskini kwa kuhahakikisha kwamba kuna uzalishaji wa chakula cha kutosha ili watu kwanza washibe lakini pia akaongeza kusema kwamba inabidi uzalishaji uwe na tija ili wakulima wapate mazao mengi na kujiongezea kipato.

Akitoa shukrani katika hafla hiyo, Mbunge wa Mpanda Mjini, Bw. Said Arfi aliwashukuru wajumbe wa Kamati za maandalizi katika mikoa ya Dar es Salaam na Rukwa kwa maandalizi mazuri hadi wakafanikisha tamasha la utamaduni wa mikoa hiyo miwili.

HAYA NDIYO YATOKANAYO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MTANZANIA KWA JAMII ZA WANARUKWA NA KATAVI

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (MB) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania lililowasilishwa na Jamii za wanaRukwa na Katavi katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam.

Lilikuwa ni tamasha la aina yake lililodumu kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 25-27 Novemba 2011 katika Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Tamasha la aina hii huandaliwa kila mwaka kwa ushirikiano wa Makumbusho ya Taifa na Jamii husika. Mwaka huu ilikuwa ni zamu ya jamii za wanaRukwa na Katavi.
Katika Tamasha hili la aina yake lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakuu Serikalini na wageni kutoka nje ya nchi tofauti na inavyokuwaga katika miaka mingine iliyopita. Katika maonesho hayo jamii za wanaRukwa na Katavi zilipata fursa pana ya kuonyesha tamaduni zao zikiwepo mila za jadi, vyakula vya asili, zana mbalimbali, ngoma, nyimbo, tiba asilia, na mambo mengine mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB) ambaye pia ni mwanaRukwa alisema kuwa, miogoni mwa mambo tuliyojifunza katika Tamasha hilo na ambayo tunatakiwa tuondoke nayokwenda kuyafanyia kazi ni pamoja na:-
ü  Umuhimu wa kuenzi na kuendeleza mila zetu.
ü  Umuhimu wa kuhifadhi mila na desturi zetu vizuri.
ü  Kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kuhifadhi tamaduni, mila na desturi zetu (Makumbusho).
ü  Kuwa na siku maalum ya utamaduni wa mwanaRukwa na Katavi kwa ajili ya kudumisha tamaduni zetu .
ü  Umuhimu wa kuhusisha masuala ya Utamaduni na Utalii.
ü  Kuwepo na Kamati maalum itakayosaidia na kusimamia yaliyojifunzwa wakati wa Tamasha hilo.
Aidha katika hotuba yake ya kufunga Waziri Mkuu alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) kuwa mstari wa mbele kusimamia hayo mambo katika utekelezaji wake. Kwa upande wa wanaRukwa waishio Dar es Salaam  aliwomba na kuwapa jukumu la kuanzisha umoja wa wanaRukwa na Katavi (UMARUKA) kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano amabao umekuwa ukilegalega.

KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA NA MKUU WA WILAYA YA MPANDA KWA PAMOJA WALIWASILISHA TAARIFA YA FURSA ZA UWEKEZAJI ZINAZOPATIKANA MKOANI RUKWA WAKATI WA KILELE CHA TAMASHA HILO.

Fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Rukwa zilinadiwa wakati wote wa Tamasha hilo. Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima (kulia) na Dkt. Rajab Rutengwe wakifanya kazi hiyo wakati wa kilele cha Tamasha hilo.

Ze Orijino Komedi walikuwepo kutoa burudani motomoto.

Ubunifu ni Nguzo ya Tamaduni zetu. Hizo ni baadhi ya ngoma zilizokuwa zinatumika kuburudisha wakati wa tamasha hilo. 

Tuesday, November 29, 2011

KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA APATA AJALI MBAYA YA GARI, HAKUNA MAJERUHI, GARI NDIO LILILOUMIA

Wananchi wakiangalia gari lenye namba za usajili STK 5925 alilokuwa amepanda Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima mara baada ya kupata ajali mbaya katika maeneo ya Kibamba CCM nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Ajali hiyo ililihusisha gari hilo na gari lingine lenye namba za usajili T 701 BWY ambalo ndilo lililogonga gari la Kiongozi huyo wa Serikali kwa nyuma na kulisukumia kwenye mtaro kama inavyoonekana pichani. Hakukuwepo na majeruhi yeyote katika ajali hiyo.

Monday, November 28, 2011

WAKE WA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI WATEMBELEA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MTANZANIA LINALOWAKILISHWA NA JAMII ZA WANARUKWA NA KATAVI KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO

Mama Zakia Gharib Bilal, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) wakati alipowasili kutembelea Tamasha la Mtanzania lililowakilishwa na Jamii za WanaRukwa na Katavi katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Katika msafara mwenyekiti alikuwa Mama Zakia Bilal akiongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda, Mke wa Makamu wa Pili wa Zanzibar Mama Asha Seif Ali Iddi, Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2011 (Miss Vodacom 2011) Salha Israel na Wake wa mawaziri mbalimbali.

Katika ziara yao hiyo walipata kujionea mambo mbalimbali ya utamaduni wa MwanaRukwa na Katavi yakiwemo vyakula vya asili, vifaa vya kutengenezea chuma, silaha za jadi na tiba asilia.

Kutoka kushoto ni Mama Asha Seif Ali Iddi Mke wa Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mama Zakia Gharib Billal Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mzee Zeno Nkoswe ambaye ndiye mwenyeji wa sherehe hizo kimila. Nyuma ya Mzee Nkoswe ni Miss Tanzania 2011 Salha Israel wakijitambulisha kwa kwenye tamasha hilo.

Mama Zakia Gharib Billal (katikati) na Mama Tunu Pinda wakionyeshwa aina ya udongo maalum uliokuwa ukitumika katika kutengenezea chuma. Jamii za WanaRukwa na Katavi zilikuwa na Teknolojia ya kuyeyusha na kutenegeneza chuma.
Kikundi cha Uyeye kutoka Mpanda kikitoa burudani. Kikundi hiki kinasifika kwa kucheza na nyoka. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya, Chifu Kayamba wa Inyonga na Miss Tanzania 2011 Salha Israel.
 
Ilungu ni aina ya mtambo uliokuwa ukitumika na Jamii za WanaRukwa katika harakati zao za kutengeneza Chuma. Mtambo huo ulikuwa ukiyeyusha udongo maalum na baadae kuundwa chuma kamili. Mtambo huo umejengwa katika Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama ili kuhifadhi kumbukumbu na Tamaduni za Mtanzania. 

Saturday, November 26, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILLAL AZINDUA TAMASHA LA SIKU YA MTANZANIA LA WATU WA MKOA WA RUKWA NA KATAVI JIJINI DAR

Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania likiwasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi, linalofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 25-27.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya nyumba ya asili ya watu wa Kabila la Wafipa, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi, Wanaomshuhudia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayaza Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimshudia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda , akinywa kinywa cha asili aina ya Chimpumu ‘Pombe ya Isute’ kinachotengenezwa  na Kabila la watu wa Katavi na Rukwa, wakati wa  uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiangalia jinsi watu wa Rukwa na Katavi wanavyofua na kuandaa Chuma cha asili wakati uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakitembelea mabanda ya maonyesho na kujionea Bidhaa za Vyakula vya asili vinavyotumiwa zaidi na watu wa Mikoya ya Rukwa na Katavi, wakati  wa uzinduzi wa Tamasha hilo

Wednesday, November 23, 2011

VODACOM YATOA FLANA 1000 KUFANIKISHA TAMASHA LA WANARUKWA NA KATAVI DAR ES SALAAM

Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel akifurahia jambo wakati  akimkabidhi flana Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la   utamaduni wa watu wa Mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi  Mwangaza  Msongole. Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Bw. Salum Mwalim.  Vodacom imekabidhi flana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni kumi na nne kusaidia hamasa ya tamasha hilo litakalofanyika kuanzia tarehe 15-17/11/2011 katika Kijiji cha Makumbusho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Tamasha la  Utamaduni wa watu wa mkoa  wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi  Mwangaza Msongole kulia akiongea  na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa  wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa katavi litakalofanyika ijumaa katika  kijiji cha makumbusho. Katikati ni Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha  Israel na kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim.

Friday, November 18, 2011

MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA WA 2011 WAPITISHWA BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda na Mbungewa Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Emmanuel Nchimbi wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Novemba 18,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Katiba na Sheria, Celiina Kombani (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari (katikati) wakifurahia baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2011 kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Novemba 18,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DEREVA WA BODABODA ANUSURIKA KUFA LEO BAADA YA KUGOGWA NA GARI NDOGO MAENEO YA CHANJI WILAYANI SUMBAWANGA

Ni ajali mbaya iliyohusisha gari ndogo aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T814 BUW na Pikipiki yenye namba za usajili T742 BQT. Inasemekana kuwa dereva aliyekuwa akiendesha Pikipiki ndiye aliyeumia na hali yake bado ni mbaya na alipelekwa katika hospitali ya Mkoa Rukwa kwa matibabu zaidi.

Chanzo cha ajali hiyo inasemakana kuwa ni mwendo kasi wa dereva wa gari hilo pamoja na dereva wa pikipiki kutokuonyesha ishara (Indicator) ya uelekeo aliokuwa akielekea na hivyo kupelekea kugogwa na kuburuzwa hadi pembeni ya barabara wakati akijaribu kukata kulia bila kuonyesha ishara yeyote. Hata hivo dereva wa gari hilo hakuumia kabisa.

Wananchi waliokuwepo katika eneo hilo walilamikia madereva wa pikipiki na kusema kuwa hawako makini jambo linalosababisha ajali za pikipiki kuongezeka mara kwa mara.

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa katika eneo la tukio

MIAKA 50 YA UHURU NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI RUKWA 2011


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Col. Mst. Issa Machibya akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) tayari kwa kwa Mwenge huo kuanza mbio zake Mkoani Rukwa tarehe 5-7/11/2011. 

Wanafunzi waliupokea Mwenge kwa Mabango mbalimbali

Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu kitaifa Ndg. Mtumwa Rashid Khalfan akizungumza na wananchi mkoani Rukwa.

Vikundi vya ngoma vilikuwepo kutoa burudani na kusindikiza Mwenge wa Uhuru

Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa katika wilaya zote tatu za Mkoa wa Rukwa, hapo ukisubiriwa Wilayani Nkasi

Katibu Tawala Wilaya ya Mpanda Ndg.Lauten Canon akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Joyce Mgana Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza mbio zake wilayani Mpanda tayari kwa kuanza mbio hizo wilayani Nkasi


Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu kitaifa Ndg. Mtumwa Rashid Khalfan akiweka jiwe la msingi katika nyumba kumi za watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga tarehe 5/11/2011


Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Joyce Mgana akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Col. John Antonyo Mzurikwao Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza mbio zake wilayani Nkasi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi wakifurahi kwa pamoja na kikundi cha Ngoma cha Kanondo wakati wa Mbio za Mwenge Wilayani Sumbawanga

Kikundi cha Chanji nacho hakikuwa nyuma kuhakikisha masuala ya burudani yanakwenda vizuri

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abas Kandoro eneo la Makutano mpakani mwa Mbeya na Rukwa baada ya Mwenge huo kumaliza mbio zake Mkoani Rukwa tarehe 07/11/2011


Timu ilifanikisha mbio za Mwenge mkoani Rukwa ikiongozwa Ndg. Festo Chonya, Eng. Maulid Mbelwa, Alex Nkenyenge na SSP. Mutalemwa 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) akihutubia wananchi

Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe. Sabas Katepa akiwa sambamba na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Mtumwa Rashid Khalfan nyuma yake ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. Silvia Siriwa

Afisa Tawala Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Ndg. Festo Chonya akiushuhudia Mwenge wa Uhuru uso kwa usoKiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu kitaifa Ndg. Mtumwa Rashid Khalfan akizungumza na wananchi mkoani Rukwa.

Sunday, November 13, 2011

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA MIPYA KABLA YA DESEMBA MOSI MWAKA HUU ASEMA RAIS KIKWETE


Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa uteuzi wa wakuu wa wilaya utafanyika hivi karibuni ambapo katika uteuzi huo utakwenda sanjari na uteuzi wa wakuu wa mikoa mipya na wilaya mpya na kuwa hadi desemba mosi uteuzi huo utakuwa umefanyika na wilaya Mpya zitaanza kazi Januari mwakani. Alisema kuwa hatateua wakuu wa mikoa pekee bali atateua na wasaidizi wake wa wilaya na mikoa na kusema kuwa lengo la serikali ni kuharakisha maendeleo yanasonga mbele na kuonya viongozi wa wilaya  mpya ya Wanging'ombe kupendekeza mapeni makao makuu ya wilaya vinginevyo atateua yeye. Rais Kikwete amesema hayo leo mjini Njombe wakati akifungua mradi wa maji katika kata ya Mtwango katika wilaya ya Njombe. Picha kwa hisani ya Fullshangwe blog

KAIMU MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA CHANJO YA SURUA, POLIO, MINYOO NA VITAMIN A KWA MKOA WA RUKWA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Mhe. Joyce Mgana akimuweka alama mtoto Rajabu Wangoma, mwenye umri wa miaka mitatu na miezi minne mara baada ya kupata matone ya Vitamini A, wakati wa uzinduzi wa zoezi la Chanjo ya Surua, Polio, Minyoo na Vitamini A, uliofanyika katika kitongoji cha Mazwi mjini Sumbawanga.

Friday, November 11, 2011

NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu (MB) akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi maonyesho ya 9 ya SIDO ya nyanda za juu kusini inayoshirikisha mikoa ya Rukwa, Iringa na Mbeya. Kulia kwake anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana. Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa  kwa kushirikisha wajasiriamali kutoka zaidi ya mikoa 14 nchini na wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Burundi.


Naibu Waziri akisalimiana na Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa ambao ndio wenyeji Ndugu Martin Chang'a mara baada ya kuwaili katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzindua rasmi maonesho hayo. Kwa mujibu wa Meneja huyo wa SIDO maonyesho hayo yatadumu kwa mda wa siku 6 kuuanzi tarehe 9-14 ambapo ndio itakuwa kilele na atakefunga maonesho hayo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.  

Mkurugenzi Mkuu wa SIDO nchini Ndugu Mike Laizer akifafanua jambo kwa Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye banda la SIDO. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana.

Naibu Waziri akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana akimpokea na kumkaribisha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.

Wajasiriamali wa Rukwa wakinadi bidhaa zao za Asali na Nta. Asali inayopatikana Mkoani Rukwa ni asali yenye ubora mkubwa (Grade One), kwa wale watakaopata bahari ya kutembelea maonyesho haya wanaweza kujipatia bidhaa hiyo na nyinginezo nyingi. 

Uhifadhi wa Mazingira nao umepewa kipaumbele Mkoani Rukwa, Mjasiriamali wa uhifadhi wa Mazingira wa kikundi cha REYO akinadi miti aina mbalimbali inayofaa kwa uhifadhi wa mazingira na matumizi mengineyo katika maonesho hayo.

Mjasiriamali Mama Grace Masawe kutoka Arusha anayejishughulisha na kazi za mikono akionyesha cheti alichozawadiwa kama Mjasiriamali mwenye banda bora katika maonesho hayo, alikabidhiwa Cheti hicho na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu. Mama Grace Mkurugenzi Mtendaji wa Masawe Curio and Crafts kutoka Arusha.

Maonyesho hayo yakiendelea

Tiba asilia pia zinapatikana katika maonyesho hayo

Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa Ndg. Frank Mateny kushoto, Makatibu Tawala Wasaidizi  Ndugu Samson Mashalla Utawala,  Ndugu Sebastian J. Mundia Menejimenti ya Serikali za Mitaa na Ndugu Willy Mzava Uchumi na Uwezeshaji wakisubiri kumuaga Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga

Utamaduni wa Kimasai nao unapatikana katika maonesho hayo

Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa kulia Ndugu  Martin Augustino Chang'a pamoja Katibu wa Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Frank Mateny wakisubiri kumuaga Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga.

Haya mambo ya ajabu pia yapo, inadaiwa ni Mtu wa ajabu kutoka Burundi aliyezaliwa kichwa kitupu, ana uwezo wa kuzungumza lugha tofauti na wakati wa kumuhoji alidai kuwa chakula chake ni Sindano maalum. Katika akili ya kawaida haifikiriki na wengi wa watu waliomtembelea huyu bwana ikiwa ni pamoja na mimi walisema haya ni MAZINGAUBWE. Huyu bwana anapatikana kwenye banda moja na ili kuweza kumuona inatakiwa kulipia shillingi mia tano tu. Nilishuhudia baadhi ya watoto waliopata bahati ya kumuona wakilia kwa hofu na wengine wakiwa na mshangao mkubwa.

Vikundi vya ngoma vilikuwepo kutoa burudani

Mjasiriamali wa Rukwa anayejishughulisha na utengenezaji wa viatu kwa kutumia ngozi mbalimbali. Chipawas Leather Tunning wanapatikana maeneo ya Jangwani Wilayani Sumbawanga, wapo pia kwenye maonesho hayo.