Sunday, February 26, 2012

MKUU WA MKOA RUKWA AONANA NA DKT. GURISHA JOHN WILLIAM, AMTAKA KUDUMISHA USHIRIKIANO KATIKA NYANJA ZOTE KWA MAENDELEO YA SEKTA YA AFYA MKOANI RUKWA


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkaribisha Ofisini kwake Mganga Mkuu wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa (RMO) Dkt. Gurisha John William alipokuja kujitambulisha ofisini kwake juzi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Saadun Kabuma kustaafu kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi.

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Rukwa akimpongeza Mganga huyo kwa kuteuliwa na kukubali kuja Rukwa. Alimuhimiza juu ya ushirikiano baina ya uongozi mzima wa hospitali na Mkoa kwa ujumla kama nguzo kuu ya kuepuka migogoro na kuleta maendeleo katika sekta ya afya katika Mkoa wa Rukwa. "Usikae na tatizo peke yako, let us work as a team" Alisema Injinia Manyanya kumuambia Dkt. Gurisha John William.

Saturday, February 25, 2012

MKE WA MAKAMU WA RAIS MAMA ASHA BILLAL ATEMBELEA KITUO CHA MAYATIMA KATANDALA, AKABITHI TENKI LA KUHIFADHIA MAJI

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Billal akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakiwasili katika kituo cha Kulelea mayatima cha Katandala kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga jana.

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akicheza na mmoja ya watoto yatima wa kituo cha Katandala kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga huku Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Billal akiwa amembeba mtoto yatima wakati walipotembelea kituo hicho jana. 
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Billal akishikana mikono na Mkuu wa kituo cha kulelea mayatima cha Katandala Sr. Maria Goreth Chusu kama ishara ya kukabidhi Tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 5,000 lililonunuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kusaidia huduma ya maji katika kituo hicho. Anayeshuhudia kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal akiahidi mchango wake wa pampu ya maji na mabomba kwa ajili ya kutumika kwenye tenki alilokabidhi Mama Asha Billal katika kituo cha kulelea mayatima cha Katandala jana. Kulia ni Mama Naomi Nko Kaimu Mkurugenzi Halamashauri ya Wilaya ya Mpanda na Mama Joyce Mgana, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi. Kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Rukwa, Mke wa Makamu wa Rais Mama A sha Billal na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa na wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo wakimpungua Mgeni Rasmi Mama Asha Billal.

Friday, February 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AZINDUA KAMPENI YA USAFI KATIKA MJI WA SUMBAWANGA LEO NA KUKABIDHI VIFAA VYA USAFI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Kampeni ya usafi katika Manispaa ya Sumbawanga ijulikanayo kama "Sumbawanga Ng'ara". Kampeni hiyo ilianzishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Rukwa kwa nia ya kuufanya Mji huo uwe wa mfano na wakupendeza. Kushoto kwake aliyeshikilia utepe ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Kampeni hiyo inaenda sambasamba na Kauli Mbiu ya "Dumisha Usafi wa Mazingira, Dumisha Upandaji Miti na Dumisha Miundombinu Daima".  
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akiweka jiwe la Msingi katika moja ya barabara kuu za Mji wa Sumbawanga sehemu aliyozindulia Kampeni ya usafi kwa Mji wa Sumbawanga. Kushoto ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikabidhi vifaa vya usafi kwa kikundi cha usafi cha Manispaa ya Sumbawanga kama sehemu ya Kampeni ya usafi wa Mazingira katika Mji wa Sumbawanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kushoto na Mama Asha Billal  mara baada ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi katika kampeni hiyo. Pembeni kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.

Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais akifagia katika moja ya barabara za lami katika Mji wa Sumbawanga kama ishara ya kuhamasisha wanawake kushiriki kwenye usafi wa Mji huo.
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal akiwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni hiyo. Mhe. Aeshi alieleza kero kubwa ya wananchi wa jimboni kwake kuwa ni Maji na kumuomba Mhe. Makamu wa Rais kuifanyia kazi kero hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kandege.

Baadhi ya wananchi waliokusanyika katika uzinduzi wa kampeni hiyo.
Makamu wa Rais akiagana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Mohammed Chima mara baada ya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa manispaa ya Sumbawanga. Makamu wa Rais ameondoka leo Mkoani Rukwa na kuelekea Mkoa jirani wa Mbeya ambapo atakuwa na ziara ya kikazi.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MAGHALA MAWILI YA KUHIFADHIA BIDHAA KATIKA BANDARI YA KASANGA NA KUTEMBELEA WAFANYABIASHARA WA SAMAKI KATIKA SOKO LA KASANGA JANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika moja ya jengo kati ya mawili ya Maghala ya kuhifadhia bidhaa yaliyopo katika Bandari ya Kasanga, kijiji cha Lusambo Wilaya ya Sumbawanga, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana februari 23, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Luteni Godfrey Semiono (Mkuu wa Kambi) kukagua kikosi cha Ulinzi wa Mipaka cha Kasanga kilichopo katika kijiji cha Lusambo, pembezoni mwa Wilaya ya Sumbawanga, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua maghala ya kuhifadhia bidhaa katika Bandari ya Kasanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua maeneo ya kufanyia biashara ya baadhi ya wafanyabiashara wa samaki katika Soko la Samaki la Kasanga, baada ya kuweka jiwe la msingi katika soko hilo akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua maeneo ya kufanyia biashara ya baadhi ya wafanyabiashara wa samaki
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuwaaga wananchi wa Kijiji cha Lusambo waliojitokeza katika mapokezi yake alipofika kuweka jiwe la msingi katika Soko la Kasanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana februari 23, 2012. Picha na OMR.

Thursday, February 23, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL ATEMBELEA KIWANDA CHA KISASA CHA NYAMA CHA SAAFI KILICHOPO SUMBAWANGA JANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi baada ya kuwasili kwenye kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Sumbawanga jana tarehe 22 Februari, 2012 akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi. Kiwanda hicho kinamilikiwa na Mbunge mstaafu wa Sumbawanga Dkt. Chrissant Mzindakaya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu uchinjaji wa Ng’ombe na matayarisho yake hadi kufikia nyama kamili kutoka kwa Meneja waKiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka, wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt. Mzindakaya, kilichopo Sumbawanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana Februari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu matayarisho na ufungaji wa nyama katika mifuko tayari kwa kuuzwa kwa wateja kutoka kwa Meneja waKiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka, wakati alipotembelelea Kiwanda hicho jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kuhusu vipimo vinavyotumika kabla ya Ng’ombe kuchinjwa kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi Dkt. Engelbert Bilashoboka wakati alipotembelelea Kiwanda hicho jana. Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na kulia kwa Makamu wa Rais ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu matayarisho na ufungaji wa nyama katika mifuko tayari kwa kuuzwa kwa wateja kutoka kwa Meneja waKiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka, wakati alipotembelelea Kiwanda hicho jana.  Picha zote na Muhidin Sofiani-OMR.

Wednesday, February 22, 2012

TIPS ON HOW TO BROWSE IN THIS BLOG EFFECTIVELY (FAHAMU NAMNA YA KUTUMIA BLOGU HII KIUFASAHA)


  1. Katika Blogu hii, hakuna picha au taarifa yeyote inayoondolewa baada ya kuonekana ukurasa wa kwanza, bali inahamia ukurasa wa pili au wa tatu na kuendelea kutokana na wingi wa taarifa zinazowekwa humu.
  2.  
  3. Ukitaka kuhamia kurasa zingine zilizopita ambazo pengine hukuziona, nenda hadi chini kulia kwako bofya "Older Posts" kuona kurasa za nyuma zilizopita ambazo zimehamia kurasa za ndani. Fanya hivyo tena na tena kuona kurasa zote katika Blogu hii.
  4. Ukitaka kurudi mwanzo nenda chini kabisa, katikati bofya "Home" kurudi ukurasa wa mwanzo wa blogu hii.
  5.  
  6. Ukitaka kutafuta habari kwa jina la mtu, sehemu au kitu nenda kulia utaona kisanduku juu yake kimeandikwa Tafuta/ Search andika unachikitaka hapo alafu bofya Search subiri kwa muda utaona majibu ya ulichokiandika. Mfano ukitaka kupata habari za mpanda andika"mpanda" alafu bofya search.
  7.  
  8. Kama umevutiwa na habari, picha au kero na maoni yako unaweza kuandika kwa kubofya sehemu iliyoandikwa "comments" ambayo ipo chini ya kila habari (post) chagua annonymus kama hutaki ujulikane au chagua hizo nyingine kama unataka ufahamike.
Kwa yeyote mwenye maoni, ushauri, habari au picha nzuri za kuelimisha na kuhabarisha jamii unaweza kututumia kupitia tembs2001@gmail.com.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA NYUMBA 11 ZA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NKASI NKOMOLO LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi nyumba 11 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi zilizopo katika Kijiji cha Nkomolo wilayani humo leo. Kushoto anayemshikilia utepe ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akiweka jiwe la msingi kwenye moja ya nyumba hizo za watumishi alizozizindua leo Wilayani Nkasi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akipanda Mti wa kumbukumbu nje ya nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi alizozizundua leo. Makamu wa Rais amehitimisha ziara yake Wilayani humo leo na tayari amaeshaanza ziara nyingine ya kikazi Wilayani Sumbawanga ambayo ndiyo Wilaya ya mwisho kwa ziara yake Mkoani Rukwa na Katavi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais naye akipanda mti wa kumbukumbu nje ya nyumba hizo za watumishi.
Miongoni mwa nyumba 11 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambazo zipo katika Kijiji cha Nkomolo zimezinduliwa leo na Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal.

Tuesday, February 21, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AIOMBA SERIKALI KUSAIDIA KUHAKIKISHA BARABARA ZA LAMI ZINAZOJENGWA MKOANI HUMO ZINAKAMILIKA KWA WAKATI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akizungumza Wilayani Mpanda. Kushoto ni Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal na Mke wake Mama Asha Billal.
Mkuuwa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ameiomba Serikali kupitia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal kusaidia kuhakikisha ujenzi wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa Mkoani Rukwa zinakamilika kwa wakati.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa ombi hilo jana mara baada ya kusomwa taarifa ya ujenzi wa barabara za lami zinazoendela kujengwa Mkoani humo kwa Mhe. Makamu wa Rais ambapo taarifa hiyo ilielezea changamoto zinazokabili ujenzi huo ambazo zinatishia kukamilika kwa ujenzi huo katika muda uliopangwa.
Taarifa hiyo iliyowasilishwa na Meneja wa Tanroads Mkoa wa Rukwa Ndugu Florian Kabaka jana iliweza kuainisha changamoto mbalimbali zinazoukabili ujenzi huo ikiwemo ucheleweshwaji wa malipo ya fedha kwa ile miradi inayotemea fedha za ndani hususani barabara za Sumbawanga-Kasanga na Sumbawanga-Mpanda.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo changamoto nyingine ni baadhi ya wakandarasi wanaojenga barabara hizo kukimbiwa na wafanyakazi wao kutokana na ukosefu wa fedha za kuwalipa hali inayopelekea kuzorota kwa ujenzi huo.
Mbali na changamoto hizo, nyingine ni kuchelewa kulipwa fidia wananchi waliothibitika kustahili malipo hayo ili kuepusha shughuli za ujenzi katika maeneo wanayotakiwa kuhama.
Pamoja na changamoto hizo nyingine ni wizi wa vifaa vya ujenzi wa barabara hizo zikiwepo nondo, mafuta, simenti, vyuma na hata mabati. Kwa mujibu wa Meneja huyo wa Tanroads ujenzi huo unatakiwa kukamilika mwakani 2013 lakini kama hali itaendelea kuwa hivyo basi huenda ukamilishaji wa miradi hiyo ukachelewa.
Baada ya kusomwa taarifa hiyo ilifika wakati kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kumkaribisha na kumtambulisha Mhe. Makamu wa Rais kwa wananchi wa Wilaya ya Nkasi ambapo amenza ziara akitokea Wilayani Mpanda. Kabla ya kufanya hivyo alilazimika kutumia fursa hiyo kutoa ombi lake rasmi kwa Makamu wa Rais kuhusu ujenzi unaondelea na kuhakikisha kuwa changamoto zinzozikabili barabara hizo zinapatiwa ufumbuzi.
"Wananchi wote wa Mkoa wa Rukwa wanaishukuru sana Serikali yao kwa hatua yake kubwa ya kuleta miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za lami Mkoani hapa kitu ambacho ni cha kujivunia kwa wanarukwa wote, Nitumie fursa hii kuiomba Serikali itusaidie kuondokana na changamoto zinazoikabili miradi hii ili iweze kuakamilika kwa wakati" Alisema Injinia Manyanya.
Serikali imesaini mikataba ya ujenzi wa barabara za lami Mkoani Rukwa kwa barabara za Tunduma-Ikana-Laela, laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Kasanga na Sumbawanga-Mpanda. Hadi hivi sasa ujenzi wa barabara kwa baadhi ya maeneo hayo unaendelea na maeneo mengine yamesimama kwa muda kutokana na uhaba wa fedha.
Mhe. Makamu wa Rais yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku saba ambapo, ameshatembelea Wilaya ya Mpanda, Sasa yupo Wilayani Nkasi na baadae atamalizia ziara yake Wilayani Sumbawanga amabap atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuizindua na kuweka mawe ya msingi. Ziara yake hiyo itakamilika tarehe 24 Februari 2012 ambapo ataenda Mkoa jirani wa Mbeya kwa ziara kama hiyo ya kikazi.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AWATEMBELEA WAZAZI WA WAZIRI MKUU KIJIJINI KWAO KIBAONI WILAYANI MPANDA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal, akisalimiana na Baba mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Exavery Kayanza Pinda, wakati alipokuwa akipita kuelekea Kijiji cha Mwamapuli akiwa katika ziara yake ya Mkoani Rukwa na Katavi jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya.

Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa Waziri Mkuu wa kwanza kulia na kushoto waliokaa nyumbani kwao Kijiji cha Kibaoni Wilayani Mpanda jana. Wa pili kulia waliokaa ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Billal. Kushoto waliosimama ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Mhe. Hiporatus Matete, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe.

Monday, February 20, 2012

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS YAENDELEA MKOANI RUKWA, ATEMBELEA MASHAMBA YA MHE. WAZIRI MKUU KIJIJINI KWAKE KIBAONI LEO

Makamu wa Rais Mhe. Mohammed Gharib Billal akipokea taarifa ya maendeleo ya shamba la mahindi na nyuki la Mhe. Mizengo Kayanza Pinda Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Kijijini kwake Kibaoni Wilayani Mpanda, taarifa hiyo iliwasilishwa na Katibu wa Waziri Mkuu Jimbo Ndugu Kanyanda. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais. Makamu wa Rais alifarijika kwa kuona kazi anayofanya Waziri Mkuu ya kuhamasisha kilimo na ufugaji wa nyuki na kusema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wenyewe kwani wao ndio kioo cha jamii.
 Hapo akiangalia shamba la nyuki la Waziri Mkuu nyumbani kwake Kibaoni. Makamu wa Rais alifurahia kazi hiyo na kusema kuwa atahakikisha naye anafuga nyuki kwani faida zake ni niyngi.
Makamu wa Rais alipata pia fursa ya kuona (Shamba) bwawa la samaki la Mhe. Waziri Mkuu.

MAKAMU WA RAIS ASIMIKWA UCHIFU WA KABILA LA WAKONONGO ZIARANI TARAFA YA INYONGA WILAYANI MPANDA JANA

Chifu Kayamba wa Inyonga akimsimika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Billal uchifu wa kabila la wakonongo. Kulia kwake ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya.

Sunday, February 19, 2012

WANANCHI WA MPANDA WAJITOKEZA KWA WINGI KUMLAKI KIONGOZI WAO MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILLAL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akihutubia umati wa wananchi wa Mpanda katika uwanja wa Kashaulili uliopo katika wilaya hiyo.

 Wengine wakaona juu ya miti ndio pahala murua kwa wao kumuona kiongozi wao live bila ya chenga, japo usalama kwao ulikuwa mdogo.

 Muitikio wa wananchi kumuona kiongozi wao Makamu wa Rais ulikuwa mkubwa kwani walihudhuria mamia kwa mamia katika mikutano ya hadhara. Hapa ni katika uwanja wa Kashaulili uliopo Mji Mpanda.

Sehemu ya umati wa wananchi wakisubiri kusikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal Inyonga Leo.

DKT. BILLAL AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA INYONGA LEO, AWAASA KINAMAMA WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA KWENYE KITUO HICHO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akiweka jiwe la msingi katika Kituo Kikuu cha Afya Tarafa ya Inyonga Leo. Kituo hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 64 pamoja na nyumba za watumishi 24.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Emmanuel Kalobelo akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Mhe. Makamu wa Rais. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya na kushoto kwake ni Mke wake Mama Asha Billal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Mhe. Hiporatus Matete.

Makamu wa Rais akikagua jengo la kituo hicho

Saturday, February 18, 2012

AKIWA ZIARANI MKOANI RUKWA MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MTAFITI BIGWA WA SOKWE DUNIANI AMBAYE PIA NI MTAALAMU WA MAZINGIRA JANE GOODALL IKULU NDOGO YA MPANDA

Si mwingine bali ni Dkt. Jane Goodall ambaye ana zaidi ya miaka 73 mwanamama mtafifiti bigwa wa masokwe duniani kutoka Uingereza ambaye pia ni mtaalamu wa mazingira kwa pamoja Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal anayeonyesha kitabu cha mwanamama huyo kiitwacho "Reason for Hope" kwa baadhi ya waandishi wa habari waliojumuika nao kwenye chakula cha jioni Ikulu ndogo ya Mpanda jana. Mama Jane ametumia zaidi ya miaka 40 ya utafiti wake katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyopo Mkoani Kigoma akitafiti maisha na tabia za Sokwe wanaopatikana kwa wingi katika mbuga hiyo.
.
Mtafiti Jane Goodall akimuonyesha Mhe. makamu wa Rais moja ya tabia za nyani ambayo ni salamu inayotumiwa na mnyama huyo ambaye hushika kichwa kama ishara ya maamkizi. Dkt. Jane Goodal pia ni balozi wa mazingira na viumbe hai duniani katika kuhamasisha umuhimu wa uhai wa vitu hivyo pamoja na ustawi misitu.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bllal akishika mdoli wa nyani ambao unamilikiwa na Mama Jane Goodgall  kwa takribani miaka 15 sasa. Alisema kuwa anamiliki mdoli huo kutokana na hisia zake juu ya nyani ambao amekuwa akiwatafiti katika kipindi chote cha maisha yake.
Mama Asha Billal Mke wa Makam wa Rais na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakiwa wameshikilia mdoli huo ambao kwa hakika anavutia pamoja na historia yake.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe naye hakuwa nyuma kwani alimtia mkononi mdoli huyo wa kihistoria.
Dkt. Jane Goodall akikumbatiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kabla ya kuondoka katika Ikulu hiyo ndogo ya Mpanda jana usiku.
Picha ya pamoja kati Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal na Dkt. Jane Goodal. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, wa pili anayefuata na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima. Kushoto kwa Dkt. Jane Goodall ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe.