Monday, April 30, 2012

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AONGOZA KIKAO CHA SAGCOT LOCAL INVESTORS LEO OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongoza kikao cha Investment Forum SAGCOT Local Investors, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo Aprili 30, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sunday, April 29, 2012

RAIS KIKWETE AWA MWENYEJI WA MKUTANO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA JANA

Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.
PICHA NA IKULU
 
Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionesha hati baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.
 
Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikaribishwa chakula cha mchana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Richard Sezibera baada ya picha ya pamoja kufuatia kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Saturday, April 28, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AWAOMBA WADAU WA MPANGO WA UZAZI SALAMA KUONGEZA NGUVU ZAIDI KUSAIDIA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Mashirika binafsi ya RFSU ya Sweden na taasisi ya RODI ya Mkoani Rukwa Ofisini kwake jana alipotembelewa na wadau hao ambao kwa pamoja wako Mkoani Rukwa katika kusadia mpango wa Uzazi Salama kwa afya ya Mama na Mtoto. Mkuu huyo wa Mkoa amezipongeza taasisi hizo kwa kazi nzuri wanazofanya na kuwaomba waongeze nguvu pamoja na kuzishawishi taasisi zingine na wafadhili waweze kusaidia kwenye mpango huo ambao ni muhimu kwa Afya ya Mama na Mtoto nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliamua kusimama na kujitambulisha kuwa yeye ni mdau mkubwa wa afya ya mama na mtoto katika mpango wa uzazi salama nchini, alifurahia ujio wa wageni hao kutoka Sweden Mkoani Rukwa na kusema kuwa ni faraja kubwa kwake yeye kama mdau kuona wafadhili hao wameamua pia kusaidia Rukwa. Wakwanza kushoto kwake ni Ndugu Mpina kutoka taasisi ya RODI, Olov Boggia wa RFSU ya Sweden na Agneta Falck RFSU kutoka Stockholm Sweden.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiendelea na mazungumzo na wadau hao (RODI ya Rukwa na RFSU ya Sweden) ambao walifika Ofisini kwake kujitambulisha kama wadau wa mpango wa uzazi salama nchini unaolenga usalama kwa mama na mtoto.

Friday, April 27, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA MKUU WA MAJESHI YA AKIBA NCHINI BRIGEDIA GENERALI R.M MUHUZA OFISINI KWAKE LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia Generali R.M Muhuza hayupo pichani katika ofisi yake leo alipomtembelea kujitambulisha na kueleza juu ya ujio wake Mkoani Rukwa ambapo ni kuona matayarisho ya kikosi cha mgambo cha Mkoa wa Rukwa ambacho kitashiriki kwenye zoezi la kijeshi litakalohusisha Vikosi vya JWTZ vilivyopo katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa, Lindi, Mtwara, Njombe na Katavi) ifikapo tarehe 15 Septemba 2012. Zoezi hilo la kijeshi litaandaliwa na Brigedi ya 401 KV iliyopo Songea Mkoani Ruvuma. Jumla ya Wanamgambo 60 kutoka Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kushiki zoezi hilo litakalojumuisha vikundi toka Kamandi zingine za Ndege za Kivita, Wahandisi, Mizinga na Vifaru.

Kutoka kushoto ni Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia Generali R.M Muhuza, Msaidizi wake Kanali A.Y Amasi na Katibu wake Meja A.R Gumbo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Dar es Salaam wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa walipomtembelea Ofisini kwake leo.

 Miongoni mwa mambo aliyosisitiza Mkuu huyo wa Mkoa ni uboreshwaji wa sekta muhimu nchini kama sekta ya ulinzi ili kuepusha uvunjifu wa amani iliyodumu nchini kwa muda mrefu. Alisema Jeshi la Wananchi lina jukumu kubwa la kuhakikisha amani inakuwepo nchini na sio kutokana na hatari zinazoweza kutoka nje bali kwa hatari zinazoweza kusababishwa na wananchi wenyewe.

Mazungumzo yakiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akifafanua jambo

Wednesday, April 25, 2012

BAADHI COMMENTS ZILIZOTOLEWA NA WADAU WA RUKWAREVIEW NDANI NA NJE YA NCHI TANGU MTANDAO HUU UANZISHWE

1-17 of 17
Anonymous
on 4/18/12
Nampongeza sana sana Mkuu Wa Mkoa Inj.Manyanya kwa uamuzi aliotoa kuhusu uwanja wa ndege wa Kisumba kujengwa badala ya kuendeleza Uwanja uliopo katikati ya mji. napendekeza uwanja wa sasa upimwe viwanja na kupewa Shirika La Nyumba ili zijengwe nyumba za kukopesha na kuuza kwa wananchi kwani shirika la nyumba litajenga nyumba bora nzuri na kuleta sura nzuri ya mji....Tamim Said on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 2/14/12
This RC is doing terrific job. She is great lady and I am impressed with her dedication and hard-work. She makes me remember General T. Kiwelu. on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 1/22/12
Ukijengwa uwanja mpya wa ndege, huo wa sasa utengenezwe kama bustani na eneo la mapumziko. We need open spaces to relax! Nawakilisha. on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 1/22/12
It makes sense to have a new airport in Kisumba. The existing airport is small and it is dangerous for the pedestrians who cross the airport. Mdau wa Edeni A on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 1/22/12
Habari za kazi mimi huwa ni msomaji ya blog hii na nimeguswa sana na utendaji kazi ya mkuu wa mkoa wa sumbawanga.Huyu Mheshimiwa ni mfano mzuri wa uongozi bora ambao nchi hii inahitaji viongozi wanaongoza kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa.Ushahidi unaonyesha Mkubwa wa serikali akishika ufagio na kufagia barabara na kuingia ndani ya mtaro kuondoa maji machafu, hawa ndio viongozi ambao tunawahitji watuongoze.Mungu akubariki sana mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Sumbawanga.Sisi watanzania wenzako tunatambua jinsi unafanyakazi kwa bidii.WEWE NI MFANO MZURI UNAOFAA KUIGWA.Serikali iangalie viongozi wa aina hii ili kuwapa nafasi nyeti kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla. on MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA MJINI SUMBAWANGA LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA JANA
Anonymous
on 1/18/12
Habari za kazi mimi huwa ni msomaji ya blog hii na nimeguswa sana na utendaji kazi ya mkuu wa mkoa wa sumbawanga.Huyu Mheshimiwa ni mfano mzuri wa uongozi bora ambao nchi hii inahitaji viongozi wanaongoza kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa.Ushahidi unaonyesha Mkubwa wa serikali akishika ufagio na kufagia barabara na kuingia ndani ya mtaro kuondoa maji machafu, hawa ndio viongozi ambao tunawahitji watuongoze.Mungu akubariki sana mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Sumbawanga.Sisi watanzania wenzako tunatambua jinsi unafanyakazi kwa bidii.WEWE NI MFANO MZURI UNAOFAA KUIGWA.Serikali iangalie viongozi wa aina hii ili kuwapa nafasi nyeti kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla. on MKUU WA MKOA WA RUKWA ATOA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA WAFUGWA WA MAHABUSU MKOANI HUMO
Anonymous
on 1/18/12
Anonymous
on 1/13/12
Wapelekeshe hao na wa Dar waige mfano sio kujifungia maofisini wakati jiji limeoza. Nafikiri hii kampeni isambae nchi nzima! on MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA MJINI SUMBAWANGA LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA JANA
Anonymous
on 1/13/12
Anonymous
on 1/13/12
Shukrani kwa taarifa hizi na zingine unazoweka katika blogu hii. Navutiwa kuona taarifa za mkoa ambao sijawahi kufika na taarifa zake hazikuwa zinapatikana kirahisi, hata mtandaoni. Sasa mambo ni mazuri kutosha. Napenda tu nigusie hili suala la hao waTuruki kuagiza vyakula kutoka nchini kwao. Ni kweli, ingekuwa bora wanunue vyakula hapa hapa Tanzania. Mimi ni mtafiti na mwandishi katika masuala ya tofauti za tamaduni hapa duniani. Suala la chakula linapambanua utamaduni moja na mwingine. Hata kwetu ni hivyo hivyo. Vyakula vya Mchagga, kwa mfano, kwa ujumla ni tofauti na vile vya Mpemba. Sasa hao wa-Turuki isije ikawa wanaagiza kutoka kwao kwa msingi huo. Ingefaa tupate taarifa zaidi. Mwarabu akiwa hapa Mpanda, sitashangaa akiagiza tende kutoka Arabuni. Pamoja na kuwa ingekuwa vema iwapo hao wa-Turuki wangenunua vyakula vya kwetu, kuna pia jambo ambalo tunaweza kujifunza kutoka kwao. Mimi ni m-Tanzania ambaye niko hapa ughaibuni, lakini huwa natafuta vyakula kwenye maduka ya on YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA WILAYANI MPANDA HIVI KARIBUNI
on 12/26/11
Anonymous
on 11/29/11
Naishukuru sana serikali kwa jitihada zake za uwekezaji nchini Tanzania. Hii inaonyesha nia njema kabisa na thabiti ya kuwainua wananchi wake kwa kipato.Pamoja na shukrani hizi naona kuna sababu za msingi za kuangalia aina ya uwekezaji tunaouruhusu kwenye maeneo husika na athari zake kwa wananchi wetu. Nasema hivi kwa sababu uwekezaji ambao serikali imeuridhia wa Mpanda ambao ni kwenye sekta ya kilimo naona unaathari kwetu. Dunia kwa sasa imekuwa na tatizo kubwa sana la kiuchumi. Mtikisiko ambao sasa unazikumba nchi za Ugiriki, Italia, Marekani, Ufaraansa, Uingereza na nchi nyingine zinazotumia sarafu ya euro ungetumik kama sababu ya kutufanya tukajifunza na sisi pamoja na umasikini wetu. Uzalishaji wa mazao ya chakula kwenye nchi za ulaya ni mdogo na una gharama kubwa sana za uzalishaji. Wakulima wanatumia mtaji mkubwa zaidi kuliko wanachopata na hivyo kufanya mazao yao kuuzwa kwa bei ya ghali sana. Sasa wanakuja kwetu kuwatumia raia wetu kuzalisha kwa gharama ndogo na hivyo kupata on HAKUNA MAENDELEO BILA UWEKEZAJI - RAIS KIKWETE
on 11/12/11
Tunakupongeza sana mheshimiwa Njoolay kwa kazi yako nzuri iliyotukuka ya kuuongoza mkoa wa rukwa. Upendo,uchapakazi na moyo wako wa ukarimu ulioonyesha wanarukwa tutazidi kukukumbuka daima. Umekuwa nasi katika shida na raha na daima ulikuwa mstari wa mbele jutusaidia na kutuongoza. Unaondoka rukwa lakini tunakukaribisha sana rukwa. Eng Manyanya karibu rukwa mkoa wenye fursa nyingi za maendeleo. Ahsante George - UK on ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA RUKWA AAGWA RASMI
on 11/12/11
Naanza sasa kuingiwa na matumaini makubwa sana kwenye mwelekeo mzima wa wanarukwa kwenye ulimwengu wa utandawazi. Fursa hii imechelewa kutufikia kwa kweli. Tumekuwa na historia nyingi japo zimekuwa zikivalishwa gamba la kutisha mfano Uchawi,mazingaombwe,uganga wa jadi nk. Sasa naingiwa na furaha kwani maana halisi ya tafsiri hizo haikuwa kama unavyotakiwa kuwa. Huo ni utamaduni wetu na ndio asili yetu wana rukwa.Makabila mengine yamekuwa yakijitokeza tangu zamani sana na sasa wamekuwa mbali sana na sanaa zao zimekuwa kwenye makumbusho na kununuliwa kwa thamani kubwa sana. Nakuombea mafanikio mema mkuu wa mkoa na wana rukwa kwa ujumla Ahsante sana. George Nkwera - UK on MKUU WA MKOA WA RUKWA ACHANGISHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 3.9 KUFANIKISHA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MWANARUKWA LITAKALOFANYIKA TAREHE 25-27 NOVEMBA 2011
on 11/12/11
Nakushukuru sana kwa kutuhabarisha habari hizi muhimu sana kwa maendeleo yetu wana rukwa. Binafsi naona kumekuwa na jitihada nzuri sana upande wa serikali na taasisi zake katika kusukuma maendeleo ya rukwa tatizo naliona ni upande wa mwananchi mmojammoja. Watu bado tunaendeleo kugubikwa na blanketi la kihistoria kuwa rukwa ni mkoa usio na maendeleo. Mengi yamefanyika na mazuri sana. jitihada zielekezwe kwenye uhamasishaji wa watu kuongeza bidii katika kufanya kazi za maendeleo na kujitolea. Uamuzi wa kupeleka sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kimkoa wilayani Nkasi naupongeza sana kwani hii itakuwa fursa kwa wana nkasi kujivunia na kujikumbusha tulikotoka wapi tupo na wapi tunataka Nkasi,Rukwa na Tanzania kwa ujumla tunataka tuwe miaka 50 ijayo. Mkuu wa Wilaya mama Mgana jitihada zake wote tunazijua katika kuhimiza maendeleo ya wilaya na mkoa kwa ujumla. Ahsante sana na endelea kutuhabarisha hususan sisi ambao tuko nje ya nchi kwa sasa. George Nkwera Sumbawanga - on KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA RUKWA KUFANYIKA WILAYANI NKASI
on 11/12/11
Nawashukuru sana wajasiriamali wa Rukwa na wengine ambao wamejitokeza kwenye maonyesho ya SIDO Sumbawanga kuonyesha ubunifu wao na jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.Hii ni nafasi ya kuonekana na kujitambulisha kwenye mtandao wa masoko ndani ya nchi na kwingineko duniani. Nawatakia mafanikio mema katika maonesho George Nkwera Sumbawanga - kwa sasa UK on NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA
 
on 11/12/11
 
HATA WEWE UNAWEZA KUTOA MAONI YAKO YENYE NIA NJEMA NA MKOA WETU PAMOJA NA MTANDAO WETU HUU KWA LENGO LA KUJENGA NA KUBORESHA. TUMIA LUGHA SAFI ISIYOCHAFUA HALI YA HEWA.
 
NAMNA YA KUTOA MAONI/ COMMENTS:
 
Chini ya kila POST utaona sehemu imeandikwa Comments, Bofya hapo mara moja, Shuka hadi chini ya hiyo POST utaona kisanduku kimeandikwa Post a Comment kama kinavyoonekana hapo chini.

0 comments:

Post a Comment


 
 
Andika Comments/ maoni yako hapo unaweza kuandika jina na contact zako kama ukipenda kisha chini ya hicho kisanduku utaona maneno haya "  " Uchaguzi upo kwenye hicho kimshale kinachoangalia chini, chagua "Annonymus" kisha nakili maneno utakayopewa yaliyoandikwa kwa kificho kwenye kisanduku kinaochoonekana alafu Bofya Publish. Comment yako itakuwa hewani popote duniani katika mtandao huu na itaifikia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, kama inahitaji kufanyiwa kazi basi itafikishwa kwa wahusika na kufanyiwa kazi. Nawatakia kazi njema na Afya Bora.

Tuesday, April 24, 2012

ANAYEDAIWA KUWA MTOTO WA STEVEN KANUMBA AIBULIWA SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

Mtoto aitwaye Johnson Steven Kanumba  mwenye   umri  wa  miaka   mitatu na miezi  minne juzi   akiwa na mama  yake  mzazi  Paskalia Macha (20)  mkazi  wa kitongoji  cha Bangwe  mjini  Sumbawanga  wakiwa katika eneo la nyumba ya mama yake mzazi na Paskalia katika kitongoji cha Mafulala nje kidogo ya mji wa Sumbawanga. Mama huyo anadai  baba  mzazi  wa mtoto  huyo  ni  msanii maarufu  wa  tasnia   ya  filamu nchini, Steven Kanumba.

Mtoto Johnson Steven Kanumba akiwa amepakatwa na   bibi yake  aitwaye  Viginia Makungu (69) ambaye  ni  mama  mzazi  wa  Paskalia Macha (20) katika  eneo  la  nyumba  ya  bibi   huyo   katika   kitongoji  cha  Mafulala  nje kidogo ya  mji  wa Sumbawanga.

Na Peti Siyame - Rukwa

SAKATA la kujitokeza kwa wanawake wanaodai kuzaa na  aliyekuwa msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba, limezidi kushika kasi  baada ya mwanamke mwingine Paskalia Macha (20) mkazi wa kitongoji cha Bangwe  mjini hapa kudai kuzaa na msanii huyo.
  Mwanamke huyo amevuta hisia za wakazi wengi mjini hapa alipojitokeza  hadharani na kudai kuwa mtoto wake wa kiume aliyemzaa miaka mitatu na miezi  minne iliyopita, baba yake mzazi ni Kanumba aliyefariki dunia hivi karibuni.


Kusoma zaidi Bofya Read More chini kushoto kwako

Saturday, April 21, 2012

BE CAREFUL WITH THIS KIND OF MESSAGE. SIMILAR MESSAGES WERE USED TO STEAL PEOPLE'S PERSONAL INFORMATION. UNLESS YOU TRUST THE SENDER, DON'T CLICK LINKS OR REPLY WITH PERSONAL INFORMATION

2012 Toyota International Promotion Program
Customer Service Department.
Toyota Motor Manufacturing (UK) Ltd,
Burnaston Derbyshire
East Midlands DE1 9TA
United Kingdom.
Dear Beneficiary,
We are pleased to inform you of the announcement made on this month of April, That you are among the winners of the 2012 Toyota International Promotion Program, Participants were  selected through a computer ballot system drawn from 6,500,000 email addresses of individuals and companies from all part of the world as part of our Electronic business Promotions Program.
As a result of your visiting various websites we are running the E-business promotions for You/Your Company email address, attached to ticket number 719-226-1319, with serial number 902-66 drew the lucky numbers 05,12,30,11,17,43 and Bonus number 10 , Your Insurance Number: FLS433 /GMSA and consequently you won in the Second Category of the 2012 Toyota International Promotion Program. You have therefore been approved the payment of the sum of £1, 500, 000.00 in cash. {One Million Five Hundred Thousand British Pounds.}
CONGRATULATIONS!!!
Please be informed that your winning fund of £1, 500, 000.00 is now with the payee center.
Contact our agent and give them your full names so that they will re-insure your winning fund under your full names. To begin your claim.
1. Full name...
2. Address...
3. Telephone...
4. Fax....
5. Occupation....
6. Age....
7. Sex.....
8. Nationality.....
9. Country of residence....
10.Your email.............
Send above information in your correspondences with your claims agent /online consultant.

Congratulations once again from all our staffs and thank you for being
part of our promotions program.

Agent Name: Mr. Mark Foster
Tel: +44-703-590-13-05
Email:
redeemprize02@m77.cc
WARNING
For security reasons, we advise all winners to keep this information confidential from the public until your claim is processed and your prize released to you. This is part of our security protocol to avoid double claiming and unwarranted taking advantage of this program by non-selected winner or unofficial personnel.

Thursday, April 19, 2012

FAHAMU FUKWE ZA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA MKOANI RUKWA ZILIZOHIFADHIWA KUVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA

Ukanda wa Ziwa Tanganyika unajumuisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Mikoa hii kwa pamoja ni Mikoa iliyopitiwa na Ziwa Tanganyika ambalo fukwe zake ni sehemu ya Utawala katika Mikoa hiyo. Ziwa hilo kwa upande wa pili limepakana na Nchi jirani za Kongo, Zambia na Burundi pamoja na Rwanda. Miongoni mwa fursa kuu zinazopatikana humo ni pamoja na uvuvi, usafirishaji katika Mikoa na nchi hizo. Fukwe zake ambazo zimehifadhiwa ni fursa pekee ya Ujenzi wa Hoteli za Kitalii kutokana na Watalii wengi kupenda kutembelea maeneo hayo. Hali kadhalika kuna samaki wa mapambo. Kubwa zaidi kunakadiriwa kuwepo kwa mafuta ya Petroli na Gesi, Utafiti bado unaendelea kufanywa na Kampuni ya Beach Petroleum kwa kushirikiana na TPDC Tanzania kubaini uwepo wa rasilimali hizo. Katika Ziwa hili ndiko inakopatikana Meli Kongwe kuliko Meli zote Duniani, Meli ya MV Liemba inakadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 100 huku bado ikiwa inafanya kazi.
 Fukwe za Ziwa Tanganyika kwa Mkoa wa Rukwa ni fursa pekee ambayo bado haijaharibiwa au kutumiwa vya kutosha. Ukanda huu ni kielelezo tosha cha mandhari na fursa nzuri za uwekezaji katika eneo hili ambalo kwa kiasi kikubwa linachochewa na ujenzi wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa katika Mikoa hii itakayounganisha Mikoa hiyo na Ziwa Tanganyika pamoja na Nchi jirani zilizopakana na Ziwa hilo. 

 Baadhi ya makazi ya wananchi wanaozunguka Ziwa Tanganyika. Shughuli kubwa za wakazi hawa ni uvuvi na kilimo. Katika shughuli zao za uvuvi bado wanatumia zana duni ikiwepo mitumbwi ya mbao na nyambu zilizo chini ya kiwango. Fursa za uwekezaji kwenye eneo hili pia zinapatikana. Samaki wakuu wanaopatikana katika Ziwa hili wanaitwa Migebuka. Kuna Kampuni chache ambazo zimewekeza katika mradi huu na huuza bidhaa hiyo hadi nje ya nchi.
 Baadhi ya Hoteli zinazopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Nkasi katika Tarafa ya Kipili. Boti zinazoonekana ni kwa ajili ya wateja watakaohitaji kwenda kucruise ndani ya Ziwa. Bado yapo maeneo maalum ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za Kitalii katika ukanda huu.
 Mandhari ya Hoteli ya Kipili iliyopo Mkoani Rukwa
 Sehemu ya maegesho ya Boti kwa ajili ya wateja na watalii wanaotembelea ukanda huo hususani katika Hoteli ya Kipili.
 Hakika mandhari haya yanavutia na hivyo ni baadhi ya vyumba katika Hoteli hiyo ya Kipili.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Kushoto na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana wakiwa wamejipumzisha katika moja ya maeneo ya mapumziko kwenye Hoteli ya Kipili baada ziara ya kuzungukia fukwe za Ziwa Tanganyika.

 Sehemu za maegesho ya Boti katika Hoteli ya Kipili.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana (Kushoto) wakiongea na watalii waliofikia katika Hoteli ya Kipili Wilayani Nkasi siku za hivi karibuni walipoenda kutembelea fukwe hizo.
Uwepo wa fukwe hizi ni fursa nzuri za ujenzi wa Hoteli za kitalii na shughuli nyingine zinazohusiana na uwekezaji na Utalii katika ukanda huu wa Ziwa Tanganyika. 
 Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nkasi wakimaliza ziara ya kukagua Fukwe za Ziwa Tanganyika huku wakielekea kwenye Hoteli ya Kipili ambayo kwa kiasi kikubwa hupata wageni wa kitalii.
Vyumba vya Hoteli ya Kipili. Hoteli hii ipo katika ukingo wa Ziwa Tanganyika.
Sehemu kubwa ya Hoteli hii ya Kipili imeezekwa kwa makuti.
Watalii hutembelea ukanda huu. Kulia Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injiania Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana.

Tuesday, April 17, 2012

RAIS KIKWETE AKIWA ZIARANI NCHINI BRAZIL: AONANA NA RAIS MSTAAFU WA NCHI HIYO PAMOJA NA KOCHA ALIYEWAHI KUIFUNDISHA STARS MARCIO MAXIMO


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais Mstaafu wa Brazil Mh Luis Inancio Lula da Silva baada ya mazungumzo yao alipokwenda kumjulia hali jijini Sao Paulo April 16, 2012.
(PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na na Rais Mstaafu wa Brazil Mh Luis Inancio Lula da Silva mara baada ya mazungumzo yao alipokwenda kumjulia hali jijini Sao Paulo April 16, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Mstaafu wa Brazil Mh Luis Inancio Lula da Silva alipokwenda kumjulia hali jijini Sao Paulo April 16, 2012.

Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimsalimu mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete alipokwenda kuwasalimia katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akisalimiana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.

Friday, April 13, 2012

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA MPYA IKULU JANA

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Joseph Sinde Warioba, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Muhidin Sufiani. OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Agustino Ramadhan, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Muhidin Sufiani. OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Salim Ahmed Salim, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Muhidin Sufiani. OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha, Abdallah Ali Saleh, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Muhidin Sufiani. OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mbunge wa Viti Maalum, Al-shymaa Kwegiyr, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Muhidin Sufiani. OMR
Kwa Picha zaidi bofya "Read More" chini kushoto