Thursday, May 31, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA - AFDB MJINI ARUSHA JANA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha jana Mei 31. 2012
 
Rais Kikwete akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana Mh Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa Dkt Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Morroco Bw Omar Kabbaj (kushoto) katika picha ya pamoja na Marais wastaafu wa Benki ya Afrika
 
Ukumbi wa AICC wakati wa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua Mkutano  Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha jana Mei 31. 2012.

Rais Kikwete akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana Mh Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa Dkt Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Morroco Bw Omar Kabbaj (kushoto) , Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (wa pili kushoto) muda mfupi kabla ya kuzindua mkutano huo jana. PICHA NA IKULU
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha.
 
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka(kulia) wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha.
 
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha.
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipongezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dr. Donald Kaberuka (kulia) mara baada ya kumaliza kutoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha . Katikati ni Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara.
 
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana mjini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (kushoto) wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Arusha

IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA IRAN NA MJUMBE WA RAIS WA BURUNDI IKULU DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 kutoka serikali ya Burundi alioletewa na Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran Mh Muhammad Reza Rahimi Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012. Kiongozi huyo yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 kutoka serikali ya Burundi alioletewa na Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 Mjumbe maalumu kutoka serikali ya Burundi, Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo. Kati ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma ujumbe alioupokea Ikulu jijini Dar es salaam leo May 30, 2012 toka kwa Mjumbe maalumu kutoka serikali ya Burundi, Mh Martin Nivyabandi, ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa nchi hiyo. shoto ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania.Picha na IKULU

Wednesday, May 30, 2012

WAKUU WA MIKOA WATEMBELEA MRADI WA NYUKI WA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA DODOMA

WaziriMkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu kifaa maalum kinachotumika kukamuwa asali kutoka kwenye masega wakati Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa walipotembelea mradi wake wa ufugaji nyuki, eneola Zuzu Dodoma, May 29,2012. Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa wakitembelea mradi wa ufugaji nyuki katika Shamba la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda lililopo eneo la Zuzu Dodoma May 29,2012. Viongozi hao wako Dodoma kwa semina.
 
Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa wakitembelea mradi wa ufugaji nyuki katika Shamba la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda lililopo eneo la Zuzu Dodoma May 29,2012. Viongozi hao wako Dodoma kwa semina. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, May 29, 2012

HII NDIO MFALME FC YA MAJENGO KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA

Kikosi cha Timu ya Mfalme fC ambacho makutano yake makuu yapo maeneo ya Kristo Mfalme katika kata ya Majengo Manispaa ya Sumbawanga. Timu hii inaundwa na vijana kutoka Majengo na baadhi kutoka katika kata ya Katandala. Kwenye timu hii wapo watumishi wawili kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, ambao ni Frank Mateny (hayupo pichani) na Hamza Temba wa kwanza kulia waliosimama. 

Mdau Hamza Temba, Winga Machachari wa timu husika. Pigana na maradhi yanaeyoweza kuepukika mfano shinikizo la damu kwa kushiriki kwenye michezo. Michezo Oyyeee!

Kijana Juma Michael, Kapteni wa timu husika. 

KAMA NA WEWE UNASHIRIKI KWENYE MICHEZO TUTUMIE PICHA YAKO NA TIMU YAKO IWEZE KUFAHAMIKA NA WADAU WA MTANDAO HUU.

MAKALA YETU: KWANINI WATU WENGI HATUFANIKIWI VYA KUTOSHA?

Tamaa ya mafanikio katika maisha ni safari ndefu. Kwa wengi wetu ni safari ya kudumu. Kila mara tunataka zaidi. Tunataka kuwa kama fulani au fulani.Tunatamani kuwa na kiasi cha fedha kama au kuliko fulani. Kuwa na mke au mume mzuri na mwenye heshima kama fulani. Na kwa wale ambao maisha yao huendeshwa na tamaa za kuwa maarufu basi kila leo huwa wanataka kuwa kama mwanamuziki,muigizaji filamu,mwanasiasa fulani na vitu kama hivyo.
Mafanikio
Ingawa ni vigumu sana kwa binadamu kufikia mahali ambapo anaweza kusema kwamba amesharidhika vya kutosha na alichonacho na hataki nyongeza yeyote zaidi, yawezekana kabisa mtu akafikia mahali pa kuridhisha ingawa hiyo haimaanishi kwamba akipata nafasi ya kupata zaidi hatoitumia. Hapa tunaweza kusema mtu anakuwa ameridhika kwa kiasi cha hali ya juu.


Lakini kwanini basi baadhi yetu tunashindwa kufikia japo robo tu ya mafanikio tunayoyatamani? Ni mambo gani yanatukwamisha? Leo nimeona tuongelee kidogo sababu kadhaa ambazo zinatufanywa wengi wetu tukwame na hata kuishia kulaumu watu wengine bila kutambua kwamba yawezekana sababu sio ukosefu wa elimu ya kutosha,mtaji wala chochote kile bali sisi wenyewe;
 • Hujiamini vya kutosha: Ukijaribu kuangalia au kufuatilia maisha ya watu ambao sote tunaamini kwamba wana mafanikio zaidi yetu utagundua jambo moja muhimu;Wanajiamini. Wanaamini kwamba wanalo jambo au mambo ya msingi wanayoweza kuchangia katika jamii. Wanajiamini na wana madhumuni ya makusudi kuhakikisha kwamba jamii itawakumbuka. Watu hao pia huwa ni wajuzi wa kuketi chini wakajikosoa wenyewe na kisha kusonga mbele zaidi na zaidi.
  Je wewe hapo ulipo una kitu gani cha kipekee? Unayo maarifa au ujuzi (skill or talent) gani maalumu ambao hujaufanyia kazi kwa sababu ya kutojiamini tu? Kwanini usiamke leo ukaanza kujiamini zaidi kisha uone jinsi utakavyobadilisha muelekeo?

 • Hujui malengo yako: Hili ni tatizo kubwa miongoni mwetu. Tunafanya mambo mengi bila malengo maalumu.Akitokea mtu akakuuliza kuhusu malengo yako hapa duniani na kisha ukapatwa na kigugumizi,ujue pana tatizo hapo. Ni kwa sababu hujawahi kuketi chini na kuandika malengo yako. Matokeo yake ni kwamba kila kukicha unarukia lengo tofauti. Ni muhimu ukawa na uhakika na malengo yako.Nashauri uyaandike mahali.Ukishaandika nenda kwenye hatua ya pili ambayo ni kupanga jinsi ya kutimiza malengo yako. Yawezekana una malengo ya kuwa tajiri wa mali,kuwa mke au mume bora,kuwa na afya njema,kuwa na kazi nzuri au kufanya vizuri katika biashara. Vyovyote vile,ni lazima uwe na malengo ya uhakika.Unaweza kuyarekebisha malengo yako inapobidi. Lakini cha msingi hapa ni kujiuliza;una malengo gani hapa duniani?Una mpango gani katika kuyatimiza?

 • Umeridhika kupita kiasi na ulichonacho: Binadamu tuna tabia ya kuridhika. Hilo sio jambo baya. Linakuwa baya pale kuridhika kwetu kunapotufanya tushindwe kuendelea mbele zaidi,kupata zaidi ili pengine kusaidia watu wengi zaidi.
  Wengine hufikia hata hatua ya kujiuliza; kwanini nijisukume mbele zaidi wakati tayari nafanya vizuri hapa nilipo? Kwanini nifungue duka lingine wakati hili nililonalo tayari lina wateja wa kutosha? Wakutosha??Jiulize tena. Watu wanaofanikiwa zaidi hufanya zaidi. Huwa wanajaribu zaidi. Wanakabiliana na mitihani migumu zaidi. Jiulize; umeridhika kupita kiasi na hapo ulipo,ulichonacho? Kwanini usijaribu zaidi?

 • U-mvivu: Uliwahi kusikia uvivu ni adui kwa ujenzi wa taifa.Ni kweli. Ni adui pia wa mafanikio. Unaweza kuwa na mipango mizuri na mawazo mazuri.Lakini mipango bila vitendo havimfikishi mtu popote pale. Wengi wetu hupoteza muda mwingi katika mambo ambayo hayana msingi,ni ya kivivu. Ni muhimu kujiuliza maswali kuhusu jinsi unavyotumia muda wako na hatua unayopiga katika kuelekea kwenye mafanikio unayoyatamani. Kama wewe unataka kufanikiwa zaidi kama mwandishi;unaandika vya kutosha?Unasoma vya kutosha?(mwandishi mzuri ni msomaji mzuri pia) Kama wewe ni mtu wa masoko; je unauza vya kutosha? Kama wewe ni mkulima; je unalima vya kutosha? Epuka uvivu.

 • Hujichanganyi na watu waliofanikiwa: Ukweli lazima usemwe.Ndugu,jamaa na marafiki zako wanakupenda sana na ni watu wazuri sana. Lakini yaweza kutokea bahati mbaya wakawa hawakuchochei kufanikiwa zaidi.Ukiwaangalia unaona umefanikiwa vya kutosha wakati kumbe tukikuchanganya na wengine,unaweza kuonekana mwanafunzi! Sasa sikwambii usiambatane na ndugu,jamaa na marafiki zako.Hapana. Ninachotaka kukuambia ni kwamba, mara kwa mara jitahidi kuwa karibu na watu waliofanikiwa zaidi na zaidi.Watu wenye mawazo chanya. Watu wanaoelewa maana na tamaa ya mafanikio. Ukiwapata watu wa namna hiyo usisite kuwashirikisha katika mawazo na ndoto zako. Mara nyingi watakuunga mkono.Kwanini? Kwa sababu wao wameshafikia hayo malengo.Wanaamini inawezekana kwa sababu wameshaweza. Hali ni tofauti na ukimuuliza mtu ambaye hajafanikiwa. Mara nyingi anakuwa haamini kwamba inawezekana. Atakachokwambia ni ah…haiwezekani usipoteze muda wako.Achana na watu wa namna hiyo.
Kwa kumalizia kumbuka yafuatayo; mtu ambaye anatamani mafanikio zaidi ni wewe. Wewe pia ndio wa kuyafanyia kazi. Jitume zaidi.Usiogope kushindwa.Ni sehemu ya maisha.Kwa hiyo jaribu kufanikiwa zaidi.

Monday, May 28, 2012

KESI YA LULU KUSIKILIZWA JUNI 16

Lulu akiwasili katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam jana.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.

Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.

Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.

Alidai walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.

Aliwashauri mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.

Mawakili wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.

Aliusoma upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Baada ya kusikiliza mabishano hayo ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.

RAIS KIKWETE AWAHUTUBIA WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA JANA MJINI DODOMA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea katika ukumbi wa St. Gaspar Mjini Dodoma jana. (Picha na Ikulu)


TIPS ON HOW TO BROWSE IN THIS BLOG EFFECTIVELY (FAHAMU NAMNA YA KUTUMIA BLOGU HII KIUFASAHA)


 1. Katika Blogu hii, hakuna picha au taarifa yeyote inayoondolewa baada ya kuonekana ukurasa wa kwanza, bali inahamia ukurasa wa pili au wa tatu na kuendelea kutokana na wingi wa taarifa zinazowekwa humu.
 2. Ukitaka kuhamia kurasa zingine zilizopita ambazo pengine hukuziona, nenda hadi chini kulia kwako bofya "Older Posts" kuona kurasa za nyuma zilizopita ambazo zimehamia kurasa za ndani. Fanya hivyo tena na tena kuona kurasa zote katika Blogu hii.
 3. Ukitaka kurudi mwanzo nenda chini kabisa, katikati bofya "Home" kurudi ukurasa wa mwanzo wa blogu hii.
 4. Ukitaka kutafuta habari kwa jina la mtu, sehemu au kitu nenda kulia utaona kisanduku juu yake kimeandikwa Tafuta/ Search andika unachikitaka hapo alafu bofya Search subiri kwa muda utaona majibu ya ulichokiandika. Mfano ukitaka kupata habari za mpanda andika"mpanda" alafu bofya search.
 5. Kama umevutiwa na habari, picha au kero na maoni yako unaweza kuandika kwa kubofya sehemu iliyoandikwa "comments" ambayo ipo chini ya kila habari (post) chagua annonymus kama hutaki ujulikane au chagua hizo nyingine kama unataka ufahamike.
Kwa yeyote mwenye maoni, ushauri, habari au picha nzuri za kuelimisha na kuhabarisha jamii unaweza kututumia kupitia tembs2001@gmail.com.

NAMNA YA KUTOA MAONI/ COMMENTS:
Chini ya kila POST utaona sehemu imeandikwa Comments, Bofya hapo mara moja, Shuka hadi chini ya hiyo POST utaona kisanduku kimeandikwa Post a Comment kama kinavyoonekana hapo chini.

0 comments:


Post a Comment


 
 
 
Andika Comments/ maoni yako hapo unaweza kuandika jina na contact zako kama ukipenda kisha chini ya hicho kisanduku utaona maneno haya " " Uchaguzi upo kwenye hicho kimshale kinachoangalia chini, chagua "Annonymus" kisha nakili maneno utakayopewa yaliyoandikwa kwa kificho kwenye kisanduku kinaochoonekana alafu Bofya Publish. Comment yako itakuwa hewani popote duniani katika mtandao huu na itaifikia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, kama inahitaji kufanyiwa kazi basi itafikishwa kwa wahusika na kufanyiwa kazi. Nawatakia kazi njema na Afya Bora.

Thursday, May 24, 2012

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MIRADI MKOANI RUKWA

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu akisalimiana na wakandarasi wa Makampuni ya Aasleaff na Bam International wanaojenga barabara ya Laela-Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Kamati hiyo ya Bunge ipo Mkoani Rukwa kwa zaira ya siku mbili ambapo itakagua miradi mbalimbali ikiwemo barabara za Tunduma-Ikana-Laela, Laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Kasanga, Bandari ya Kasanga na Miundombinu ya Anga ambapo wataona eneo la Kisumba lililotengwa tangu mwaka 1984 kwa ajili ya kujengwa uwanja mkubwa wa ndege na pia wataona uwanja wa ndege wa Sumbawanga. 

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu wa tatu kushoto Meneja wa Tanroad Mkoa wa Rukwa Florence Kabaka na wajumbe wengine wa Kamati hiyo ya Bunge wakishika udongo uliochanganywa na Cement na kushindiliwa ikiwa ni mojawapo ya hatua kuelekea ujenzi wa kiwango cha lami katika barabara ya Laela Sumbawanga eneo la kyanda walipokagua ujenzi wa barabara hiyo.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Aasleff na Bam International wakiendelea na ujenzi wa barabara hiyo. Mpaka sasa kilomita zaidi ya 10 zimeshawekwa lami ya majaribio na kazi nzima katika barabara hii ya Laela - Sumbwawanga imeshafikia asilimia 37 hadi kukamilika kwake.

Umwagiliaji kuimarisha ujenzi ukiendelea.

Wafanyakazi wakiendelea kuchapa kazi, hapo wakiondoa kokoto kwa ajili ya kuweka surface nyingine.

Mhe. Shekifu na Kamati yake wakiangalia moja ya eneo lililoanza kupata nyufa katika baadhi ya maeneo yaliyoanza kuwekwa lami. Mwenyekiti huyo alimuasa Mkandarasi huyo mambo matatu moja ikiwa ni kupata taarifa rasmi yenye uhakika kutoka kwao kuwa ni lini mradi huo utakamilika ili wawatangazie wananchi wenye kiu kubwa na barabara hizo. Pili wahakikishe ubora wa barabara hizo unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo yaliyowekwa lami. Na mwisho ni kuhakikisha suala la fidia kwa wananchi wanaostahiki linakamilika kuepusha usumbufu wowote ule.  

Mhandisi Msaidizi Mkazi wa Aasleff Bam International Paul Grument akitoa maelezo kuhusu nyufa zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo yaliyoanza kuwekwa lami, amesema tatizo hilo limeonekana katika baadhi ya maeneo kutoka Laela kuelekea Sumbawanga hali wanayoihisi kuwa ni kutokana na asili ya udongo wa maeneo hayo. Aliendelea kuseama kuwa kwa maeneo yote tatizo hilo lilipojitokeza wameshachukua udongo na kuusafirisha kwenda Afrika Kusini na Ufaransa kwa ajili ya kuufanyia utafiti kujua tatizo ni nini ili waweze kupata ufumbuzi. Alieleza kuwa viwango vyote vya ujenzi katika kutengeneza ngazi zote za barabara hizo vimezingatiwa cha ajabu nyufa hizo zimejitokeza jambo ambalo wanalifanyia utafiti na katika wiki mbili zijazo majibu yatakuwa yamepatikana na hapo watajua nini cha kufanya kunusuru hali hiyo.

Kamati ikiangalia eneo lililochimbwa mchanga katika eneo la Kyanda ambao umepelekwa maabara za nje kufanyiwa utafiti utakaobainisha chanzo cha mipasuko iliyoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo kwenye barabara hayo. Mhe. Shekifu aliwataka wakandarasi hao waharakishe kupata majibu ya utafiti huo kwani wananchi wa Rukwa wana kiu kubwa ya kupata barabara za lami. Mwenyekiti huo aliwataka Tanroads Mkoa wa Rukwa washirikiane kwa ukaribu na wakandarasi hao kwa kuweka utaifa mbele ili tatizo hilo liweze kupata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Rukwa Florence Kabaka akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Lami inayojengwa na Kampuni ya Aasleaf Bam International ya Laela- Sumbawanga. Alisema kuwa mpaka sasa barabara hiyo imeshajengwa kwa kiwango cha asilimia 37. Alieleza changamoto kubwa zinazokabili ujenzi huo kuwa ni kuchelewa kwa vifaa kufika katika eneo la mradi, nyufa ambazo zimeanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo katika kilomita 13 za mfano ambazo zimeshaanza kuwekwa lami, na Mkandarasi kuchelewa kuhamisha maji ya mvua kandokando ya barabara yaliyosababisha mmomonyoko wa ardhi kwenye barabara hizo. Hata hivyo Mkandarasia alishaanza kuhamisha maji hayo na kazi imenza kuimarika. Kuhusu nyufa Mkandarasi huyo amesema wamechukua sample za udongo katika sehemu zilizoathirika na kuzipeleka Afrika Kusini na Ufaransa kwa ajili kuzifanyia utaifiti na kupata suluhisho la tatizo hilo.

Picha ya pamoja kati ya Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye ni Katibu Tawala Masaidizi Miundombinu Francis Kilawe wa tatu kulia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Dkt. Henry D. Shekifu (Mb) Lushoto katikati. Wengine ni wajumbe wa Kamati hiyo kutoka kulia ni Haroub Shamis (Mb) Chonga Zanzibar, Eng. Ramo Makani (Mb) Tunduru, Juma Sururu Juma (Mb) Bububu Zanzibar, Rukia Kassim Ahmed (Mb) Viti Maalum Kusini Pemba na Herbert James Mntangi (Mb)Muheza.    

Picha ya pamoja kati ya Kamati ya Bunge, Uongozi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, na Tanroads Mkoa wa Rukwa.

Wednesday, May 23, 2012

PETROL STATION

Hapa ni Laela Mji mdogo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kamera yetu jana iliona tukio hili la aina yake ambalo mjasiriamali katika Mji huu wa Laela ameamua kuweka mafuta ya petroli kwenye vikontena hivyo na kuuza kwa wateja wenye mahitajio mbalimbali wakiwemo wa pikipiki, majenereta na hata magari. Kilichonivutia zaidi ni huo msemo wake alioandika kwenye biashara yake hiyo "Ya ngoswe mwachie ngoswe". Kwa picha hiyo ni wazi kuwa kuna fursa ya uwekezaji wa Sheli za kuuzia mafuta katika eneo hili, kwa wale wafanyabiashara wa mafuta wanaweza kutumia fursa hiyo. Asubuhi njema.

Monday, May 21, 2012

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWATAKA MA-RC NA MA-DC KUJITOA ZAIDI KATIKA KUTAFUTA SULUHISHO LA MATATIZO YA WANANCHI NA SIO KUWA SEHEMU YA MATATIZO HAYO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia (kushoto) na Waziri wa Zamani na mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Kikao cha Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Kituo cha mikutano cha St. Gaspar Mjini Dodoma May 21,2012. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
Waziri wa zamani na Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akitoa mada katika Kikao cha Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Kituo cha Mikutano cha St.Gaspar Mjini Dodoma May 21, 2012.
 
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua kikao chao kwenye Kituo cha Mikutano cha St. Gaspar Mjini Dodoma May 21, 2012.
 
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya wote nchini wajitoe zaidi katika kutafuta suluhisho la matatizo yanayowakabili wananchi wanaowaongoza badala ya wao pia kuwa sehemu ya matatizo hayo.
Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Mei 20, 2012) wakati akifungua mafunzo maalum ya siku 10 kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya yanayoanza leo kwenye ukumbi wa St. Gaspar mjini Dodoma.

Akinukuu maneno ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, Waziri Mkuu alisema: “Kiongozi anayetakiwa kwa Taifa letu, lazima awe anakerwa na matatizo ya wananchi” na kwa maana hiyo anatarajia kuwa viongozi hao watakuwa viongozi wa aina hiyo baada ya kumaliza mafunzo hayo.

“Ninyi kama viongozi na watendaji wakuu katika maeneo yenu ni timu muhimu katika kufahamu changamoto, matatizo na kero walizonazo wananchi hasa wale wanaoishi vijijini ambao ni asilimia 80 ya Watanzania wote,” alisema.

Alisema ili kuwasaidia wananchi kuondokana na umaskini, viongozi hao wanategemewa kuonesha njia ya nini kifanyike ili kukabiliana na changamoto na malalamiko ya wananchi.

“Mnapaswa kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili badala ya kuwa sehemu ya matatizo yao. Ili muweze kuyafanikisha haya yote sharti kila mmoja wenu atambue na kukubali kuwa uongozi ni kufanya kazi zaidi na kwa hiyo mnapaswa kujitolea zaidi kwa umma na wala siyo nafasi ya kujinufaisha binafsi au kuona mmpata ofisi ya kupiga mbwembwe,” alisisitiza.

Aliwataka mara baada ya kumaliza mafunzo haya, awe ni Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya, kila mmoja mmoja anapaswa kujiuliza kuna kiwango gani cha umaskini katika eneo aliliopangiwa; aangalie pia pato la wastani la mwananchi katika wilaya au mkoa wake likoje na kuainisha kama ongezeko la idadi ya watu katika mkoa au wilaya yake linaendana na ukuaji wa uchumi katika eneo husika.

“Mnapaswa pia kuzijua na kuzitambua fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya mkoa au wilaya husika; mziainishe ni fursa zipi za kuichumi za haraka (quick wins) zinazoweza kumtoa mwananchi kwenye umaskini; na zaidi ya yote muangalie ni kwa namna gani mwananchi wa kawaida atawezeshwa kutumia fursa zilizopo kuondoa umaskini unaomzunguka,” aliongeza.

Alisema wanatakiwa kuhakikisha kuwa maeneo yao yanakuwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa viwango stahiki na kwamba thamani ya fedha inaonekana. Vilevile alisisitiza kuwepo kwa nidhamu katika ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma na kujiridhisha kuwa zinatumika kwa manufaa ya wananchi.

“Ninawasihi sana Wakuu wa Mikoa na Wilaya mkasimamie vizuri ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zenu kwa sababu ndiko viliko vyanzo vikuu vya mapato. Katika bajeti iliyopita, Halmashauri zilipanga kukusanya sh. bilioni 320/- lakini hadi kufikia Januari mwaka huu, ni sh. bilioni 90/- tu ambazo zilikuwa zimekusanywa.”

“Ni lazima RC na DC mlione hili… lazima muweke mbinu za kufuatilia ukusanyaji wa mapato katika mamlaka zenu za Serikali za Mitaa ili kusaidia kuleta maendeleo katika maeneo yenu kwa kutumia vyanzo mlivyonavyo,” alisisitiza.

Akifafanunua kuhusu majukumu ya jumla ya viongozi hao, Waziri Mkuu aliwataka wakapambane na rushwa, dawa za kulevya, tatizo la ajira kwa vijana na kuhakikisha kuwa mikoa na wailaya zao zina akiba ya chakula cha kutosha.

“Ni aibu kwa RC au DC kuomba chakula kwani si kweli kwamba hapakuwa na fursa nyingine za kuepuka hali hiyo. Fursa za kuzalisha mazao mbadala zipo, himizeni watu wenu walime mazao yanayostahimili ukame, yanayokomaa kwa muda mfupi, na ikibidi muwasisitize wazalishe chakula cha ziada ili wawe na akiba ya kutosha na pia waweze kuuza na kupata fedha,” aliongeza.

Aliwataka wahimize dhana ufugaji nyuki katika maeneo ya kilimo na ufugaji ambako wamepangiwa kwani ni eneo ambalo halijapewa msukumo licha ya kuwa lina fursa kubwa ya kuongeza kipato kwa wananchi wanaowaongoza.

“Wasaidieni wananchi kuongeza kipato kwa kujiingiza katika ufugaji nyuki… bei ya asali inapanda kila siku. Ethiopia ni nchi ya jangwa lakini wenzetu wamefika mbali kiuchumi kutokana na ufugaji nyuki na urinaji asali,” alifafanua.

Mafunzo hayo yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133. Jumla ya watoa mada 39 wanatarajiwa kutoa mada katika mafunzo hayo wakiwemo mawaziri 17.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 998,
DODOMA.
JUMATATU, MEI 20, 2012.
 

PICTURE OF THE DAY

 Viongozi wa G-8 wakiwa Camp David nchini Marekani walipata nafasi ya kuangalia fainali za kombe la mabingwa Ulaya wakati Chelsea wakiwafunga Bayern Munich na kutwaa ubingwa. Anayeshangilia ni Waziri Mkuu wa Uingereza Bw David Cameron akisaidiwa na Rais Barak Obama wa Marekani. Kiongozi wa Ujerumani Mama Angela Merkel haamini kinachotokea...

Friday, May 18, 2012

PRESIDENT JAKAYA MRISHO KIKWETE IN WASHINTON DC TODAY

President Jakaya Mrisho kikwete speaks during a high level breakfast briefing on scaling up nutrition at the Dirksen office building in Washington DC May 17, 2012. Together with him at the High table are the minister of international Cooperation of Canada Ms Beverly J. Oda, UNFP Executive Director Ms Ertharin Cousin and the CEO of Concern Worldwide, Mr Tom Arnold.
President Jakaya Mrisho kikwete speaks during a high level breakfast briefing on scaling up nutrition at the Dirksen office building in Washington DC May 17, 2012.

President Jakaya Mrisho kikwete greets the USAID Administrator Dr Raj Shah after taking part in a high level breakfast briefing on scaling up nutrition at the Dirksen office building in Washington DC May 17, 2012. right is the Tanzania Ambassador to the US Ms Mwanaidi sinare Maajar and second right is Ms Liberata Mulamula, Personal Assistant to the President (Diplomatic Affairs)-Photo by State House.