Tuesday, July 24, 2012

TIPS ON HOW TO BROWSE IN THIS BLOG EFFECTIVELY (FAHAMU NAMNA YA KUTUMIA BLOGU HII KIUFASAHA)  1. Katika Blogu hii, hakuna picha au taarifa yeyote inayoondolewa baada ya kuonekana ukurasa wa kwanza, bali inahamia ukurasa wa pili au wa tatu na kuendelea kutokana na wingi wa taarifa zinazowekwa humu.
  2. Ukitaka kuhamia kurasa zingine zilizopita ambazo pengine hukuziona, nenda hadi chini kulia kwako bofya "Older Posts" kuona kurasa za nyuma zilizopita ambazo zimehamia kurasa za ndani. Fanya hivyo tena na tena kuona kurasa zote katika Blogu hii.
  3. Ukitaka kurudi mwanzo nenda chini kabisa, katikati bofya "Home" kurudi ukurasa wa mwanzo wa blogu hii.
  4. Ukitaka kutafuta habari kwa jina la mtu, sehemu au kitu nenda kulia utaona kisanduku juu yake kimeandikwa Tafuta/ Search andika unachikitaka hapo alafu bofya Search subiri kwa muda utaona majibu ya ulichokiandika. Mfano ukitaka kupata habari za mpanda andika"mpanda" alafu bofya search.
  5. Kama umevutiwa na habari, picha au kero na maoni yako unaweza kuandika kwa kubofya sehemu iliyoandikwa "comments" ambayo ipo chini ya kila habari (post) chagua annonymus kama hutaki ujulikane au chagua hizo nyingine kama unataka ufahamike.

Kwa yeyote mwenye maoni, ushauri, habari au picha nzuri za kuelimisha na kuhabarisha jamii unaweza kututumia kupitia tembs2001@gmail.com.


NAMNA YA KUTOA MAONI/ COMMENTS:
Chini ya kila POST utaona sehemu imeandikwa Comments, Bofya hapo mara moja, Shuka hadi chini ya hiyo POST utaona kisanduku kimeandikwa Post a Comment kama kinavyoonekana hapo chini.

0 comments:


Post a Comment


 
Andika Comments/ maoni yako hapo unaweza kuandika jina na contact zako kama ukipenda kisha chini ya hicho kisanduku utaona maneno haya " " Uchaguzi upo kwenye hicho kimshale kinachoangalia chini, chagua "Annonymus" kisha nakili maneno utakayopewa yaliyoandikwa kwa kificho kwenye kisanduku kinaochoonekana alafu Bofya Publish. Comment yako itakuwa hewani popote duniani katika mtandao huu na itaifikia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, kama inahitaji kufanyiwa kazi basi itafikishwa kwa wahusika na kufanyiwa kazi. Nawatakia kazi njema na Afya Bora.

Monday, July 23, 2012

MKUU WA MKOA RUKWA AMUOMBA WAZIRI WA MAJI KUUPA MKOA WAKE KIPAOMBELE KWENYE MIRADI YA MAJI

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya waziri wa maji Prof. Jumanne Maghembe (katikati) mkoani humo. kushoto ni katibu tawala wa mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Rukwa, Methew Sodoyeka, Sumbawanga (Kulia), Moshi Chang'a (Kalambo), na Iddi Kimanta (Nkasi) wakifuatilia hotuba ya waziri Prof. Maghembe kwenye majumuisho ya ziara yake Mkoani Rukwa.NA RAMADHANI JUMA
AFISA HABARI-HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA
MKUU wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ameiomba serikali kuupatia kipaumbele maalum mkoa huo katika miradi ya maji kutokana na kukabiliwa na upungufu wa muda mrefu wa huduma hiyo.
Alitoa ombi hilo kwa waziri wa Maji Mh. Profesa Jumanne Maghembe wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya waziri huyo mkoa humo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Thursday, July 19, 2012

AKIWA ZIARANI MKOANI RUKWA WAZIRI WA MAJI AAHIDI KUSHUGHULIKIA TATIZO LA MAJI, AWAASA WANANCHI KULINDA VYANZO VYA MAJII

Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe(kushoto) akisalimiana na Afisa Maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Crispin Luanda kulia.

Mkuu wa Wilaya  ya Kalambo Mkoani Moshi Mussa Chang'a akicheza ngoma ya Kifipa wakati wa mkutano katika Kijiji cha Ulumi wakati wa ziara ua Waziri wa Maji Wilayani Kalambo. Anayeshuhudia ni Katibu Tawala Mkoa Alhaj Salum Mohammed Chima.

NA RAMADHANI JUMA,
AFISA HABARI - H/W SUMBAWANGA

SERIKALI imewataka wananchi kuacha utamaduni wa kuchoma misitu moto

ili kuhifadhi mazingira, ikiwa ni pamoja na kuwa na vyanzo endelevu
vya ikiwemo mito ya asili.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maji Mheshimiwa Profesa Jumanne

Maghembe wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ulumi Kata ya
Ulumi wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, wakati wa ziara yake mkoani humo
kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma hiyo.

Alisema hayo baada ya kupokea taarifa ya mradi wa maji unaotarajiwa

kutekelezwa na Halmshauri ya wilaya ya Sumbawanga kijijini hapo,
ambapo chanzo cha maji ya mradi huo ni mto Kapoka.

Alisema endapo wakazi wa kijiji hicho hawataacha uharibifu wa misiti

katika maeneo ya mto huo, huenda ukakauka katika kipindi kifupi
kijacho, hali itakayosababisha tatizo la upungufu wa huduma ya maji
kuendelea katika kijiji hicho.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Maghembe aliwashauri wataalamu wa Maji

wa Halmashuri ya Sumbawanga ambayo inahudumia wilaya mbili za
Sumbawanga Vijijini na Kalambo kufanya utafiti ili kubaini vyanzo
vingine vya maji kijijini hapo kuliko kutegemea mto huo pekee ambao
uhai wake uko mashakani endapo uharibifu wa mazingira hautadhibitiwa
kikamilifu.

Waziri huyo wa Maji aliahidi kupambana na tatizo la upungufu wa maji

linalowakabili wakazi 4791 wa kijiji hicho, ambao kwa sasa wanategemea
chanzo kimoja tu cha maji hali inayopelekea upungufu wa huduma hiyo.

Aliwaahidi wakazi hao kuwa, katika kipindi cha wiki moja ijayo

wataalamu wa maji wataanza kazi ya kutafiti vyanzo vingine vya maji
kijijini hapo, ambapo alisema eneo hilo linaoekana kuwa na maji mengi
ardhini.

Alisema kuwa, kazi ya utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji vya

Laela, Matai, na Nankanga pia utaanza mara moja, na kwamba nia ya
serikali ni kusambaza maji katika maeneo yote nchini ambayo
yanakabiliwa na upungufu wa huduma hiyo muhimu

Wednesday, July 11, 2012

BARAZA LA MADAKTARI LAFUTA USAJILI WA MUDA WA MADAKTARI WOTE WALIOGOMATAARIFA KWA UMMA

Baraza la Madaktari Tanganyika limepokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba, baadhi ya Madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kati ya tarehe 23 na 29 mwezi Juni 2012. Madaktari hao walipangiwa kutoa huduma kwa wagonjwa katika hospitali za Muhimbili, K.C.M.C, Rufaa Mbeya, Bugando, Amana, Temeke,St. Francis- Ifakara, Mwananyamala, Sekou Toure, Haydom na Dodoma. Kufuatia mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika kwamba, Madaktari waliogoma walikataa kutoa huduma za kitaalamu, ikiwa ni wajibu wao, na kwamba kitendo hicho kilihatarisha maisha ya wagonjwa katika hospitali husika na pia ni kinyume na maadili ya taaluma ya udaktari.
Kufuatia malalamiko hayo, Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la Kufanya Uchunguzi (Preliminary Examination) dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baraza la Madaktari Tanganyika limebaini kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, Madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda (Provisional Registration).
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhika kwamba madaktari wote ambao majina yao yameorodheshwa katika Taarifa hii, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo, usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012. Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya tarehe 17 Julai, 2012.
KUONA MAJINA YA MADAKTARI HAO BOFYA READ MORE CHINI KUSHOTO

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ASHIRIKI KWENYE MAZISHI YA SHEMEJI YAKE WILAYANI MPANDA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka udongo kwenye kaburi la shemeji yake, Mzee Sadik Ismail Katila katika mazishi yaliyofanyika mjini Mpanda Julai 10,2012.
 
Viboko wakiwa kwenye dimbwi kwenye Hifadhi ya `Taifa ya Katavi Mkoani Katavi, Julai 11,2012.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, July 9, 2012

DR. ASHA-ROSE MIGIRO: “FURSA YENYE TIJA: TAFAKURI YA UTUMISHI WANGU KAMA NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA”

Dk Asha -Rose Migiro
--
Hakika kila chenye mwanzo hakikosi mwisho, na kila mwisho wa jambo moja huwa mwanzo wa jingine. Ingawa huenda ni mapema sana kwangu kutoa tafakuri kamili ya muhula wangu katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hapana shaka kabisa kuwa nafasi hiyo imenipa uzoefu maridhawa. Namshukuru Katibu Mkuu BAN Ki-moon kwa kunipa fursa hii, kuniamini na kwa ushirikiano mkubwa wakati wote wa utumishi wangu.

Kukitumikia chombo hiki cha kimataifa kwa muda wa miaka mitano na nusu mfululizo ni heshima ya pekee ambayo daima nitaienzi kama kilele kimojawapo cha maisha yangu ya utumishi wa umma. Kila siku niliyoitumia katika Umoja huo ilikuwa ni darasa la kusukuma mbele mipaka ya ujuzi na elimu. Nimepata kufahamu mengi zaidi kuhusu Shirika lenyewe; kuhusu dunia na watu wake, lakini pia kufahamu ukomo wa uwezo wa Umoja wa Mataifa katika kushughulikia changamoto mbali mbali zinazoikabili dunia yetu.

Utumishi wangu katika Umoja wa mataifa ulikuwa fursa adhimu iliyonipa uzoefu wa pekee. Kazi hii imeujaza moyo wangu na unyenyekevu wa dhati kwani niliingia Umoja wa Mataifa wakati ambapo dunia inachagizwa na madhila makubwa makubwa yakiwemo maradhi, umaskini wa kupindukia, kutokuwapo kwa usawa wa kijinsia, kuongezeka kwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto; na changamoto nyingine nyingi. Kwa muktadha huu ilikuwa fursa ya pekee kuchangia juhudi za pamoja za kuimarisha Umoja wa Mataifa katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi cha mazingira magumu ya kimataifa yaliyojaa changamoto za kipekee kabisa.

Daima nitaendelea kushukuru na kuthamini kwa dhati jinsi Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali na Watanzania wenzangu walivyonitia moyo na kunienzi katika kipindi chote nilichokuwa Umoja wa Mataifa. Familia yangu, ndugu na marafiki walikuwa karibu nami kwa dua na kunitia nguvu wakati wote wa utumishi wangu. Nawashukuru sana.

Hapana shaka kazi yangu katika Umoja wa Mataifa imeniwezesha kufahamiana kwa karibu na viongozi wengi wa kimataifa na pia watu mbali mbali waliopata mafanikio makubwa duniani. Nimeweza kufahamu kwa undani thamani ya michango yao katika kujenga amani na ustawi wa dunia.

Zaidi ya yote, sitasahau hisia nilizopata kila nilipokutana na watu wanyonge waliokuwa wanahitaji msaada wa Umoja wa Mataifa. Nitakumbuka daima tabasamu ya mwanamke mmoja niliyekutana naye katika moja ya ziara zangu barani Afrika nilipotembelea zahanati mojawapo kati ya kadhaa zinazofadhiliwa na Umoja wa Mataifa. Mama huyo mwenye watoto sita, alikuwa amekikumbatia kitoto chake kimoja kilichokuwa nyonde nyonde; lakini alikuwa na tabasamu iliyojaa faraja na matumaini kwa kuwa alikuwa amefanikiwa kupata bure dawa za kunusuru maisha ya mwanawe.

Maendeleo

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliasisiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1997 kwa madhumuni ya kuongeza ufanisi wa utendaji wa Sekretariati na kuimarisha uongozi wa Umoja Mataifa katika medani za uchumi na maendeleo ya jamii. Majukumu ya Naibu Katibu Mkuu yaliongezeka kadri Shirika lilivyokuwa linapanua shughuli zake. Hatimaye Naibu Katibu Mkuu akakabidhiwa jukumu la kuoanisha na kuratibu idara zote zilizo chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa. Jukumu hili lilikuwa na manufaa makubwa, hususan tulipoingia katika utekelezaji wa dhana ya “Huduma ya Pamoja ” (Delivering as One - DaO) ili kuleta ufanisi zaidi katika kazi zetu hususan za maendeleo.

Kwa bahati nzuri, ninamaliza kipindi changu kukiwa na maendeleo mazuri yanayotokana na jitihada za kimataifa za kupambana na umaskini. Takwimu za kuaminika za hivi karibuni zinatuambia kuwa juhudi zetu za kupunguza idadi ya watu maskini duniani kufikia angalau nusu ya viwango vya sasa zimeanza kuzaa matunda. Taarifa hii ni ya kutia moyo licha ya ukweli kwamba dunia inapitia dhahama kubwa ya kiuchumi kuliko wakati mwingine wowote katika miaka ya hivi karibuni. Pamoja na majukumu mengine,nguvu zetu tulizielekeza zaidi kwenye kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia na malengo mengine ya maendeleo yaliyokubaliwa kimataifa. Nilihamasika sana na dhamira waliyoionesha wadau na washirika wetu wa maendeleo: serikali, mashirika ya kiraia na mashirika ya biashara. Kwani wote kwa pamoja waliyatumia malengo hayo kama kilingo cha msingi katika kutokomeza umaskini.

Katika kufanikisha utekelezaji madhubuti wa malengo ya maendeleo ya milenia nilipewa jukumu la kukamilisha ahadi ya Katibu Mkuu aliyoitoa kwa nchi wanachama ya kuunda Mfumo Kamilifu wa Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs Integrated Implementation Framework ). Ninaona fahari kwamba naondoka Umoja wa Mataifa mfumo huu ukiwa umekamilika ambapo Katibu Mkuu aliuzindua mwezi Juni mwaka huu. Kwa mara ya kwanza mfumo huu umeweka utaratibu ambao utauwezesha Umoja wa Mataifa na wadau wote kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa ahadi za kisera na kifedha. Hapana shaka utaratibu huu utaongeza uwajibikaji wa wadau na upimaji sahihi wa hatua za maendeleo.

Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) Barani Afrika

Kwa mwelekeo huo huo, Katibu Mkuu alizindua Jopo la Viongozi la Kuhimiza Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia Barani Afrika (MDG Africa Steering Group) mwezi September 2007. Kikundi hiki kinajumuisha taasisi zote kuu duniani zilizo mstari wa mbele katika kuchochea kasi ya maendeleo ya Afrika. Nilipata bahati ya kukiongoza kikosi-kazi (MDG Africa Working Group) kilichokuwa mhimili wa Jopo hilo la viongozi. Baada ya miaka mitano ya majadiliano ya kina, Jopo hilo likiongozwa na Katibu Mkuu limetoa mapendekezo kamambe ya utekelezaji. Endapo mapendekezo haya yatazingatiwa basi yatakuwa nyenzo muhimu ya kuweka sera na mikakati madhubuti itakayosaidia maendeleo katika nchi husika na duniani kwa ujumla. Napenda kutoa mwito kwa wadau wote kuyapa umuhimu mapendekezo haya.

Ninafahamu kwamba tathmini kamili ya mafanikio ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia imepangwa kufanyika Septemba mwaka 2013. Hata hivyo tayari tunaweza kusema kuwa Malengo haya yameleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu wa kawaida sehemu nyingi duniani, hususan barani Afrika. Ni dhahiri kuwa jamii nyingi zimenufaika na utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia sio kwa kufanyiwa hisani bali kwa wao wenyewe kuwa na mikakati maalum ya kupiga hatua madhubuti za kujiletea maendeleo stahimilivu na yaliyolenga kuleta usawa baina ya watu.


Mkutano wa Rio + 20

Ni jambo la kutia moyo kwamba maendeleo shirikishi na yenye kuleta usawa ni baadhi ya masuala muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano wa Rio +20 uliomalizika hivi karibuni. Suala hili litachukua nafasi kubwa pia katika kuandaa mfumo wa maendeleo unaotarajiwa baada ya mwaka 2015, mwaka uliokusudiwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia. Nilipokabidhiwa jukumu la kuratibu maandilizi ya ushiriki wetu kwenye mkutano wa Rio+20 nilitiwa moyo na nia ya dhati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kubuni mkakati wa pamoja wa kutekeleza maazimio ya Rio+20. Napenda kuzishukuru nchi wanachama kwa kufikia makubaliano katika masuala mengi yaliyojadiliwa Rio licha ya changamoto nyingi zinazotokana na mtikisiko wa uchumi duniani. Ninafurahi kwamba maazimio ya mkutano huu yatachangia upatikanaji wa maendeleo stahimilivu, shirikishi na yenye kuleta usawa na hususan kuhakikisha kunakuwa na mustakabali mzuri kwa wanawake na wasichana.

Uwezeshaji wa wanawake na usawa wa kijinsia

Tukirejea kwenye suala hili, hata baada ya Mkutano wa Rio + 20 tutawajibika kuendelea na juhudi za uwezeshaji wa wanawake na kuleta usawa wa kijinsia. Wakati wa utumishi wangu Umoja wa Mataifa tumefanya bidii kubwa na kutumia muda mwingi kushughulikia suala hii. Tumetumia hadhi na ushawishi wa ofisi yetu kupaza sauti za wanawake na wasichana na kukuza ushiriki wao katika jamii. Tumeendesha kampeni za kupiga vita ukatili kwa wanawake na wasichana. Tumezihimiza mamlaka katika ngazi za kitaifa na kimataifa kutunga sera na sheria zinazozingatia haki za wanawake na usawa wa kijinsia, na tumetaka wapewe fursa kushika nafasi za uongozi katika jamii. Ndiyo maana kwa upande wetu hatukuweka koleo chini hadi pale tulipokamilisha uanzishwaji wa idara inayojulikana kwa kifupi kama “UN Women” mnamo Julai 2010. Hii ni idara ya Umoja wa Mataifa iliyoundwa kwa madhumuni ya kuongoza masuala ya wanawake na usawa wa kijinsia kwa umakini na ufanisi zaidi kuliko hapo awali. Tumefanya jitihada hizi kwa kuamini kuwa hakuna uamuzi wowote ule, uwe mdogo au mkubwa, unaofanywa na Umoja wa Mataifa bila ya kuzingatia maendeleo na ustawi wa wanawake na wasichana.

Huduma ya Pamoja

Kwa upande mwingine ninapenda kuwapongeza kwa dhati wenzangu wote waliomo katika utumishi wa Umoja wa Mataifa,wake kwa waume,walioutumia ujuzi na weledi wao wote kuchangia maendeleo ya nchi na jamii tunazozihudumia. Natoa shukrani za pekee kwa wale wote waliopo kwenye ofisi na vituo vya Umoja wa Mataifa nje ya Makao Makuu na ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu na yenye changamo nyingi. Hao wote wanadhihirisha umuhimu wa kuwapo kwa Shirika hili kama chombo cha kuhimiza maendeleo katika ngazi zote za kitaifa, kikanda na kimataifa. Katika kutekeleza dhana ya “Huduma ya Pamoja” (Delivering as One) Waratibu Wakaazi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa na mchango muhimu sana.Uratibu wao umeongeza ubora na wepesi wa utoaji huduma kwa nchi wanamowakilisha Shirika. Hatuna budi kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha dhana ya “Huduma ya Pamoja”. Ni dhahiri kwamba uwezo wa nchi mwanachama kumiliki mchakato wa maendeleo yake unakuwa imara zaidi pale ambapo kuna mtiririko mzuri wa huduma za Umoja wa Mataifa na fursa za kukuza ushirikiano endelevu na wadau wengine wa maendeleo. Wakati uamuzi rasmi kuhusu maendeleo ya dhana hii ukisubiri kukamilika kwa majadiliano ya nchi wanachama, ninaamini kwa dhati kuwa utaratibu wa kutoa “Huduma ya Pamoja” kupitia mpango mmoja uliokubaliwa na wote ni mwelekeo sahihi na wenye tija.

Nchini mwetu Tanzania, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu sana toka mwaka 2011 kupitia mpango mmoja uitwao “Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kusaidia Maendeleo” (United Nations Development Plan – UNDAP). Mpango huu unakwenda sambamba na mwaka wa fedha wa Serikali yaani Julai 1 hadi Juni 30 na kwa mantiki hiyo kuuwezesha kuzingatia vipaumbele vya Serikali. Kupitia mpango huu Umoja wa Mataifa umejiwekea utaratibu wa kujipima na kujitathmini ambao unatoa fursa kwa hatua za haraka kuchukuliwa inapobidi. Utaratibu huu unapatikana kwenye tovuti. Kwa upande wa uendeshaji, mfumo huu wa utendaji kazi kwa pamoja umetuwezesha kutekeleza majukumu mengi kwa kutumia raslimali chache ambapo“ziada” iliyopatikana imeelekezwa kwenye shughuli nyingine za maendeleo.

Afya ya Jamii

Katika eneo la afya, ambamo wanawake na watoto ndiyo wanaathirika zaidi, hatua muhimu zinachukuliwa kupunguza vifo nakuhakikisha kwamba kila mwanamke na kila mtoto anakingwa na maradhi, hususan kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Tukiwa Nairobi Aprili mwaka 2011, Katibu Mkuu Ban Ki-moon, Michel Sidibe, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) pamoja nami tulishuhudia mfano hai wa jitihada za Umoja wa Mataifa. Tulipata fursa ya kukutana na mwanamke aliyeathirika na virusi ambaye alijaaliwa kupata mapacha watatu waliozaliwa bila ya maambukizi. Nikiwa mjumbe wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa iliyoshughulikia taarifa na uwajibikaji katika masuala ya afya ya mama na mtoto (Commission on Information and Accountability on Women's and Children's Health) ambayo iliendeshwa kwa umahiri na Rais Kikwete wa Tanzania na Waziri Mkuu Harper wa Canada, nina imani kwamba jumuiya ya kimataifa hivi sasa imepata mfumo madhubuti utakaohakikisha kwamba kunakuwa na ufuatiliaji, usimamizi na uwajibikaji kuhusu afya ya mama na mtoto. Hakuna shaka kwamba mfumo huu utafikia hatua ya utekelezwaji siku za hivi karibuni.

Hali kadhalika, kazi nzuri imekuwa ikifanywa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Mpango wa Uzazi Duniani (UNFPA), Babatunde Osotimehin, na Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kuboresha afya ya mama na mtoto. Matokeo ya jitihada za wenzangu hawa yalikuwa chachu ya utekelezaji wa majukumu ya Naibu Katibu Mkuu katika nyanja zote za maendeleo. Ama kwa hakika matunda ya kazi zao yanaimarisha imani yangu kuwa Umoja wa Mataifa ni Shirika lenye umuhimu mkubwa; na kwamba mchango wetu, japo mdogo, unasaidia sana katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia. Nilijawa na imani kama hiyo nikiwa katika ziara nyingine za kikazi. Kwa mfano nikiwa Montevideo, Uruguay, Novemba 2011, pamoja na wenzangu Michelle Bachelet, Helen Clark na Alicia Barcena, tulisimama kidete kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kupiga vita vitendo vya ukatili kwa wanawake.

Nilipozuru Haiti mwezi Aprili2010, miezi michache baada ya tetemeko ambalo lilikuwa kubwa kuliko yote yaliyowahi kutokea nchini humo kwa kipindi cha takriban karne moja, nilikutana na watu ambao walikuwa wameathirika vibaya sana: waliopoteza familia nzima, waliopata ulemavu wa maisha, waliopoteza mali zao zote! Lakini bado watu hawa walikuwa na nyuso za matumaini wakitarajia mchango wa Umoja wa Mataifa na wa wadau wengine wa jumuiya ya kimataifa. Mnamo Novemba 2010 tulizuru Laos, ambako Umoja wa Mataifa unashirikiana kwa karibu na Serikali na wadau wengine wengi katika utoaji wa misaada muhimu ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuisaidia Laos kupambana na janga la mabaki ya mabomu ya“cluster munitions”.

Hii ni mifano michache tu inayojibu hoja za wakosoaji wa Umoja wa Mataifa.Ujumbe wangu kwao ni huu: wanyonge na wenye kutaabika sehemu zote duniani ni mashuhuda na watetezi wakubwa wa Umoja wa Mataifa. Kwa wanyonge na wahitaji walio wengi Shirika hili ni nguzo ya kutumainiwa katika jitihada zao za kila siku za kujiletea maisha yenye utu na heshima.

Mageuzi katika menejimenti na usimamizi wa mabadiliko

Ukweli huu haumaanishi kuwa Umoja wa Mataifa hauna kasoro au upungufu. La hasha! Ndiyo maana wakati wa utumishi wangu tulijielekeza kikamilifu kwenye kuboresha masuala ya utawala, uendeshaji na namna tunavyofanya kazi. Ni wazi kwamba hivi sasa Umoja wa Mataifa umebadilika kutoka chombo cha huduma za mikutano na kuwa mtendaji mwenye majukumu muhimu nje ya kumbi za mikutano. Kwa ushirikiano na msaada maridhawa wa wafanyakazi wenzangu, tulijikita katika kuhamasisha mabadiliko ya kiutendaji katika Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na kujenga desturi ya uwajibikaji, uadilifu na kufanya kazi kwa tija zaidi huku tukitumia rasilmali chache.

Ilitubidi pia kuweka mifumo thabiti ya kusimamia mabadiliko yaliyokuwa yakijitokeza. Katika kufanya hivyo tulitambua wazi kwamba hakukuwa na njia ya mkato wala njia mbadala ya kuliimarisha Shirika letu na kulifanya liwe la kisasa zaidi katika kutekeleza majukumu yake.Tulihakikisha kwamba utendaji kazi wetu unakwenda sambamba na changamoto zilizopo, lakini pia tulizingatia ufinyu wa bajeti, misimamo tofauti na wakati mwingine inayaokinzana ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Katika hali hii ilitulazimu kuwa wabunifu zaidi ili kuleta muafaka baina ya nchi wanachama na kuhakikisha kwamba raslimali chache zilizopo zinatoa tija kubwa zaidi.

Wafanyakazi ndiyo rasilmali kubwa kupita zote. Hivyo kila tulipoendelea na jitihada za kuboresha Shirika ilitubidi kuwekeza vilivyo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia fursa za mafunzo na msingi imara wa maendeleo yao kazini. Ni jambo lililo dhahiri kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanatekeleza majukumu yao katika mazingira hatarishi na yenye kubadilika mara kwa mara. Tunafahamu, tena kwa uchungu mkubwa, kuwa Bendera ya Umoja wa Mataifa - “bendera ya bluu” - hivi sasa si kinga tena. Haituhakikishii usalama kwani wengi wa watumishi wetu mahiri wamekuwa wahanga wa matukio ya kikatili ya ugaidi. Nilishuhudia tukio la aina hii huko Abuja, Nigeria, ambako watumishi wenzetu walipoteza maisha kutokana na shambulio la kigaidi la tarehe 26 Agosti 2011. Na mara nyingi wenzetu wanapotangulia mbele ya haki, wapendwa wao wanaachwa katika hali ngumu ya maisha. Ni faraja kubwa kwangu kuwa miongoni mwa masuala ambayo tuliyasimamia kabla ya kumaliza utumishi wangu ni kuanzisha mchakato wa kubaini namna bora ya kuwasaidia wahanga wa majanga hayo pamoja na familia zao.Utawala wa sheria

Mojawapo ya majukumu ya Umoja wa Mataifa ni kukuza sera zinazolenga kulinda haki za binadamu na kuendeleza utawala wa sheria katika ngazi za kitaifa na kimataifa. Leo hii, nchi nyingi zimelipa kipaumbele suala la kuimarisha utawala wa sheria, hususan kufuatia umuhimu wake katika ajenda za ujenzi wa amani (peace-building) na maendeleo stahimilivu. Kwa mantiki hiyo, nilifurahi nilipopata fursa ya kusimamia ujenzi wa mfumo madhubuti wa sera na mwongozo wa utekelezaji wa shughuli za utawala wa sheria nikishirikiana na nchi wanachama. Kwa upande wao nchi wanachama zimepanga kufanya mkutano wa ngazi ya juu wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba 2012. Nia kubwa ni kuendeleza jitihada katika suala hili ili kukuza heshima ya watu wote duniani na kujenga amani kati ya mataifa.
Hitimisho

Japokuwa muda wangu wa utumishi katika Umoja wa Mataifa umefikia tamati, naamini hakuna tamati katika utekelezaji wa malengo, misingi na maadili ya Umoja wa Mataifa. Ili mradi bado kuna umaskini duniani na mahitaji ya chakula; bado kuna changamoto ya kutunza utu na heshima ya binadamu na haja ya kuimarisha amani duniani basi hakika nitaendelea kuunga mkono jitihada, misingi na malengo ya Umoja wa Mataifa popote pale nitakapokuwa. Kwani ni dhahiri kwamba njia bora ya kukabiliana na changamoto kubwa zilizo mbele yetu ni kujenga ubia na ushirikiano wa karibu baina ya serikali, asasi za kiraia, wafanyabiashara, mashirika ya hisani, taasisi za kitaaluma na watu binafsi.

Aidha, ninaaamini kuwa vijana, kizazi ambacho kina kila sababu ya kuwa na kiu ya kuishi kwenye dunia yenye utu, usawa, haki na amani, watauchukulia Umoja wa Mataifa kuwa mbia wa kuaminika katika kujenga mustakabali wao.


Asha-Rose Migiro

Thursday, July 5, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA LEO


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi serikalini baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.

PICHA NA IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na baadhi ya mawaziri na viongozi waandamizi serikalini baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo July 5, 2012 katika ukumbi wa TAMISEMI Dodoma.


WAKAZI 8000 KUPATIWA MAJI SAFI WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA, NI KWA UDHAMINI WA BENKI YA DUNIA

Diwani kata ya MWIMBI wilaya MPYA ya KALAMBO Mkoa wa Rukwa Leonard Shalamwana (wa tatu kulia)akimuonesha Mkuu wa wilaya Moshi Mussa Chang'a(wa tatu kushoto) chanzo cha Mradi wa maji utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 158.3 na kunufaisha takribani wakazi 8,000. Mradi huo unadhaminiwa na benki ya dunia, wananchi pamoja na mfuko wa maendeleo wa jimbo la Kalambo. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Miradi ya TASAF wilaya John Kiondo na Kaimu Mkurugenzi wilaya Sumbawanga Crispin Luanda.
NA RAMADHANI JUMA,
AFISA HABARI - HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA
 
WAKAZI wapatao 8,000 wa vijiji viwili vya Majengo na Mwimbi katika Kata ya Mwimbi wilaya mpya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi unatekelezwa katika kata hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 158.3.
 
Mradi huo unadhaminiwa na Benki ya Dunia iliyotoa zaidi ya shilingi milioni 154.4, wakazi wa kata hiyo wamechangia shilingi 2,709,000 na mfuko wa jimbo la Kalambo umetoa shilingi 1,200,000 ili kufanikisha mradi huo.
Akielezea mradi huo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Mussa Chang’a, diwani wa Kata ya Mwimbi Leonard Shalamwana alisema kwa sasa mradi huo uko katika hatua ya nne ambayo ni usambazaji wa maji katika vituo vikuu.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Mosses Nkinda alisema mradi huo utaongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi hao na kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza hali ya kiuchumi mara utakapokamilika.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo Moshi Mussa Chang’a alipongeza utekelezaji wa mradi huo na kuwataka viongozi wa kata hiyo kuhakikisha kuwa unakamilika haraka ili wakazi hao waanze kunufaika nao kama ilivyokusudiwa.

Monday, July 2, 2012

MKUU WA WILAYA MPYA YA KALAMBO APOKELEWA KWA SHANGWE, AANZA KAZI YA KUWAAGIZA VIONGOZI KUWACHUKULIA HATUA WAZAZI WA WANAFUNZI WALIOFAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA NA AMBAO BADO HAWAJARIPO​TI

Na Ramadhan Juma - Afisa Mawasiliano wa Serikali Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

MKUU wa wilaya mpya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Moshi MussaChang’a amewaagiza viongozi wa kata za wilaya hiyo kuhakikisha wanawachukuliahatua kali za kisheria wazazi wa wanafunzi ambao walifaulu na kuchaguliwa kuingiakidato cha kwanza mwaka huu lakini hawajaripoti shuleni mpaka sasa ambapomuhula wa kwanza masomo umemalizika.
Chang’a ametoa maagizo hayo katika ziara yake yakujitambulisha katika wilaya hiyo ambapo anatembelea kata zote 17 za wilaya yaKalambo iliyozaliwa baada ya ya wilaya mama ya Sumbawanga kugawanywa.

Katika maagizo yake, Chang’a pia amewataka viongozi haowanafunzi ambao hawakuripo mpaka sasa, wanaripoti shuleni mara baada ya shuleza sekondari kufunguliwa mapema mwezi Julai, ambapo katika kata ya Kasangailiyopo mwambao wa ziwa Tanganyikawanafunzi 40 hawakuripoti kidato cha kwanza kati ya 80 waliochaguliwa ikiwa nisawa na asilimia 50, huku wengine 56 wakishindwa kuripoti katika Kata ya Mkowe.

“Katika hili la elimu sitaki mchezo kabisa…ni bora tuonanewabaya kwa sababu kumkosesha mtoto elimu ni sawa na kumuua”  alisema Mkuu huyo wa wilaya ambapo aliwatakawatendaji wa Kata na Vijiji kushirikiana na walimu wakuu wa shule za sekondarikumaliza tatizo hilomara moja.

Mkuu huyo wa wilaya ameanza ziara hiyo siku mbili tu baadaya kuripoti katika kituo chake cha kazi, ambapo amekuwa akiwaeleza wakazi wawilaya hiyo utajiri wa fursa zilizopo na kuwataka wazitumie kwa ipasavyo ilizisaidie kuleta maendeleo ya haraka ndani na nje wilaya hiyo.

Amezitaja baadhi ya fursa za kiuchumi kuwa ni pamoja naKilimo cha mazao mbalimbali kama vile mahindi, alizeti,maharage, mihogo, napamoja na ufugaji wa nyuki kwa njia ya kisasa kwa kuweka mizinga ya nyukikuzunguka mashamba ya alizeti ili wasadie kuchavusha alizeti na pia kupataasali nyeupe ambayo bei yake ni kubwa katika soko la dunia.

“Asali nyeupe ni utajiri mkubwa kwa sasa, kuna makampuniyanayoinunua kwa bei ya shilingi 150,000 kwa lita moja tu…na mimi ninamawasiliano na makampuni haya kwa hiyo nawapa hii changamoto, kila mkulimaatakayelima alizeti aweke na mizinga ya nyuki kuzunguka shamba lake”alisisitiza.

Kwa upande wao, wakazi wa wilaya hiyo wamemwelezea Mkuu wawilaya yao kuwa tumaini jipya katika kuletamaendeleo ya wilaya yaona kwamba watashirikiana naye katika kuchapa kazi, huku wakiishukuru Serikalikukubali ombi la kuwapatia wilaya hiyo.