Thursday, November 29, 2012

MATUKIO MBALIMBALI YA VIONGOZI WAKUU WA JUMUIYA YA NCHI WANACHAMA WA AFRIKA YA MASHARIKI NA UZINDUZI WA MAKAO MAKUU YA JUMUIYA HIYO JIJINI ARUSHA JANA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiangalia mfano wa jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na maelezo yake baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha.
 
Mfano wa jengo la Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wabunge wa Afrika Mashariki.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika chemba ya mikutano ya Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki katika jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika chemba ya mikutano ya Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki katika jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifunua pazia kufungua rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya Novemba 28, 2012 jijini Arusha.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitembelea sehemu mbali mbali za jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitembelea sehemu mbali mbali za jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha. Hapa ni katika chumba cha mahakama ya jumuiya hiyo
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishuhudia Mwenyekiti wa Jumuiya Rais Mwai Kibaki wa Kenya akizindua rasmi mfumo wa kisasa wa kuunganisha shughuli za ushuru wa forodha kwa njia ya mtandao katika jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha.
 
 Waandishi wa habari na wapiga picha wakiweka tukio hilo katika mashine zao kwa ajili ya kupeperusha habari hiyo na kuweka tukio hilo katika kumbukumbu muhimu za ofisi zao.
 

Tuesday, November 27, 2012

HOW TO TIE A TIE, JIFUNZE KUFUNGA TAI KAMA HUJUI


Watu walio wengi hasa mijini hupenda sana kuvaa tai na kuonekana Nadhifu. Ofisi katika Mabenki, Idara ya Kodi ndio wanaongoza hivi sasa kwa uvaaji wa tai na viongozi mbalimbali wa Serikali. Lakini ni Ukweli usio fichika kuwa katika kila kundi la watu 10 unaopishana nao wamevaa tai basi huenda ni wawili au mmoja ndie anajua kufunga tai kisasa na kitaalam. Nasema hivi kutokana na vile ilivyo kuwa wengi hufungiwa tai hizo na pindi ikifungwa haifunguliwi hadi ichakae.
 

Kawaida Tai ikifungwa na ukavuta ulimi mdogo haipaswi kuweka fundo, na pindi ikiweka fundo basi ujue hujafunga vyema. Leo Hii rukwareview blog imeona bora itoe somo hilo la ufungaji tai, ili wewe msomaji uweze kuifunga mwenyewe tai yako na si kwa domu au mtaalam mmoja wa hapo ofisini kwenu, na kama siku hayupo basi huwi smat. (Na Father Kidevu blog)

KILIO CHA MIAKA 50 YA UHURU NA BARABARA MKOANI RUKWA CHAELEKEA UKINGONI, LAMI YAENDELEA KUTANDAZWA KWA KASI

 
Hali ilivyo hivi sasa ya barabara ya Tunduma Sumbawanga. Na ujenzi bado unaendelea. Taarifa juu ya ujenzi wa barabara kuu inapatikana hapo chini. 
 
 
 Wakandarasi wakiendelea na ujenzi
 
 
TAARIFA FUPI YA MIRADI MIKUBWA YA BARABARA ZINAZOENDELEA KUJENGWA MKOANI RUKWA NA KATAVI
 
1. SEHEMU YA SUMBAWANGA – LAELA (95.31KM)
 
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya Aarsleff-BAM International Joint Venture V.O.F Kutoka Denmark na Uholanzi kwa gharama ya dola za Kimarekani 97 Milioni chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa yamefikia 49.9% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri na ulipangwa kwisha 31 Januari 2013 ingawa majadiliano kuhusu kuongeza muda wa kumaliza kazi bado yanaendelea.
 
 2. SEHEMU YA LAELA – IKANA (64.2KM)
Sehemu hii inajengwa na Kampuni ya China New Era International Engineering Corporation kutoka China kwa gharama ya Sh. bilioni 76.1 chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa na unategemea kukamilika 31 Mei 2013.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi 31 Octoba, 2012 yalikuwa yamefikia 64% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri.
 
 3. SEHEMU YA IKANA – TUNDUMA (63.7KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya Consolidated Contractors Group S. A (Offshore) (CCC) kutoka Ugiriki chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa kwa gharama ya Sh. bilioni 82.5. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi sasa yamefikia 43% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 9 Septemba 2012, hata hivyo muda wa kumaliza kazi uliongezwa hadi tarehe 31 May 2013.
 
 2. SUMBAWANGA – NAMANYERE – MPANDA NA KIZI – KIBAONI (245KM)
 
 2.1. SEHEMU YA SUMBAWANGA – KANAZI (75KM)
 
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania kwa gharama ya Sh. bilioni 78.8.
 
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 23.6% ya kazi zote zilizopangwa. Kasi ya maendeleo ya kazi inasuasua kwa madai kuwa mkandarasi hajalipwa kiasi chote anachodai. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba, 2012, hata hivyo muda wa kumaliza kazi bado unajadiliwa.
 
 2.2. SEHEMU YA KANAZI – KIZI – KIBAONI (76.6KM)
 
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya China Hunan Construction Engineering Group Corporation kutoka China, chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania, kwa gharama ya Sh. 82.84 bilioni.
 
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 30% ya kazi zote zilizopangwa. Mkandarasi anaendelea na kazi ingawa kwa kasi ndogo kwa madai ya kuchelewa kulipwa. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba, 2012, lakini haitawezekana. Hivyo muda wa kumaliza bado unajadiliwa.
 
 3. SUMBAWANGA – MATAI – KASANGA PORT (112KM)
 
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G)/ Newcentry Company Ltd. chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd, kutoka Tanzania. Gharama ya Mradi ni Sh. 133.30 bilioni.
 
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufika tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 28% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu unatekelezwa kwa mkataba wa Usanifu na Ujenzi (Design and Build Contract). Kwa sasa kazi zinaendelea vizuri baada ya kusuasua siku za nyuma. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 13 Januari, 2013 lakini itabidi muda wa utekelezaji kuongezeka kutokana sababu mbalimbali.
 

 
Kwa lugha isiyo rasmi tunasema "Mkeka"


Kazi bado inaendelea

Monday, November 26, 2012

MCHEKESHAJI SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza akiwa katika gari lenye namba za usajili T478 BVR Toyota Harrier, majira ya saa mbili usiku, ambapo pia ndio nyumbani kwao.
R.I.P Sharomilonea. Maiti ya Sharo Milionea imehifadhiwa hospitali ya Teule Muheza.

INSPITE OF PROMOTING OUR ENDOWED INVESTMENT POTENTIALS, ENVIROMENTAL CLEANESS IS ALSO OUR PRIORTIY POWERED BY SUMBAWANGA NG'ARA COMPAIGN

Sumbawanga Nga'ra Compaign was initiated by the currently Rukwa Regional Commissioner Hon. Engineer Stella Manyanya (MP) in collaboration with other leaders in the Region. The Compaign gained a great support from citizens in the Region that loves to see their town in a good shape of cleanness. The Compaign was officially launched by the Vice President of the United Republic of Tanzania Hon. Dr. Mohammed Gharib Billal on 24th February 2012 where he cut the ribbon to announce the beggining of the compaign and distributed some equipments for cleanness. Since the Compaign got into service, the Sumbawanga town has changed with a new outlook that impress people to stay. The streets and Roads for pedestrians and Vehicles are clean as can be seen on the displayed pictures. For us, investment goes together with cleaness and environmental conservation. KEEP OUR TOWN CLEAN FOR A GOOD STAY.


Vodacom Tanzania has supported the Compaign by installing the Street Lights as they can be seen. Bravo to Vodacom but the Citizens in town are still asking when they should expect to see them working (lighting the town).

VIONGOZI IRINGA WATAKIWA KUWA MFANO KWA KULIMA ZAO LA MTAMA

Na. Dennis Gondwe, IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma ameagiza viongozi katika ngazi zote kulima zao la mtama katika harakati za mkoa kuhakikisha wilaya zake zote zinajitosheleza kwa chakula.
Agizo hilo amelitoa wakati akiongea na viongozi wa baraza la maendeleo la kata ya Nduli katika ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kilimo cha mtama na elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kijiji cha Kising’a.
Dk. Christine amesema “tunaingia katika msimu wa kilimo lazima tujiulize kwa nini bado tunaendelea kukabiliwa na upungufu wa chjakula katika baadhi ya maeneo na kwa nini tuendelee kulima mahindi wakati yanaharibiwa na hali ya hewa?.” Amesema “viongozi wote lazima tushiriki katika kampeni ondoa njaa Isimani na lazima viongozi tuwe viongozi wa mfano kwa kulima zao la mtama katika mashamba yetu angalau heka mbili” alisisitiza Dk Christine.
Amesema ili wakulima waweze kunufaika na mvua ni vizuri wakazitumia vizuri mvua za kwanza kwa kupanda mtama. Amesema ili kunufaika na mvua hizo lazima mashamba yaandaliwe mapema ili mvua zinapoanza kunyesha zikute mashamba yapo tayari kwa kupanda. Aidha, amewataka Maafisa kilimo na watendaji kuwa walimu kwa kuwaelimisha wakulima juu ya kanuni za kilimo bora cha mtama ili kuweza kupata mazao bora. 
Akiwa katika kijiji cha Ilambilole katika mkutano wa hadhara Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewashauri wakulima wa kijiji hicho kulima hekari chache watakazoweza kuzihudumia vizuri tofauti na utaratibu wa mazoea wa kulima hekari nyingi na kushindwa kuzihudumia na hatimae mkulima kupata hasara. Amesema “ni vizuri mkulima kulima hekari chache atakazoweza kuzihudimia vizuri kwa kufuata kanuni bora za kilimo ili aweze kupata mazao mazuri”. 
Akifafanua sababu zinazowafanya wakulima kuendelea kulipa kipaumbele zao la mahidi pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, Afisa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa Wilaya ya Iringa, Lucy Nyalu amesema kuwa changamoto iliyopo ni kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa wakulima ili wawe kukubaliana na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo kwa takribani miaka mitano mfululizo hali ya hewa imekuwa si nzuri kwa kilimo cha mahindi jambo lilosababisha eneo kubwa la tarafa ya Isimani kukumbwa na upungufu wa chakula. Amesema kuwa ni Halmashauri yake itaendelea kuhamasisha wakulima kuzitumia mvua za kwanza kwa ajili ya kupanda zao la mtama pamoja na kufuata kanuni za kilimo bora.

Sunday, November 25, 2012

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKOA MPYA WA KATAVI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa Katavi.
 
Makamuwa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akimkaribisha Makamu wa Rais Dt. Gharib Bilal ili kuongea na wananchi wa kijiji cha Kabungu.

Msafara wa magari ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal ukiwasili katika eneo lilipowekwa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa mkoa wa Katavi katika kilima cha kijiji cha Kabungu Mkoani Katavi.
 
Wazee waasisi wa kijiji cha Kabungu wakinyanyua matawi ya miti juu kama ishara ya kumpokea Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati alipowasili katika kijiji hicho leo.

Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa mkoa wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili kulia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt. Mary Nagu.
 
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya wakiwa katika sherehe za uzinduzi huo.
 
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
 
Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
 
Mama Aisha Bilal akisalimia wananchi wa katavi katika sherehe hizo.
 
Kwaya ya Vijana ya Moravian mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.
 
Martha Mbogo mwimbaji wa kundi la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika uzinduzi huo mjini Mpanda.
 
Wananchi wa Mpandawakinyanyua mkono yao juu kama ishara ya kushangilia kuazinduliwa kwa mkoa wao wa Katavi uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
 
Wananchi wakiwa wanashangilia
 
Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Veta Chuo cha Veta Mpanda Trojemsi Bashato wakati alipotembelea banda la Veta.

Makamu wa Rais akisikiliza maelezo kutoka kwa Thomas Lemunge mfanyakazi wa kampuni ya simu ya TTCL wakati alipotembelea Banda la kampuni hiyo, kulia ni Bw Huphrey Ngowi mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa huduma Mwandamizi wa benki ya Wanawake TWB BiMargaret Msengi wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
 

Makamu wa Rais Akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea katika banda hilo leo njini Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo. PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM.

Saturday, November 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AWAISILI MKOANI KATAVI LEO NA KUZINDUA MIRADI MBALIMBALI PAMOJA NA TATHMINI YA KONGAMANO LA UWEKEZAJI LA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Mpanda leo kwa ajili ya kuzindua Tathmini ya Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika lililofanyika Wilayani Mpanda tarehe 17 Oktoba Mwaka 2011. Pamoja na Kongamano hilo atazindua pia Mkoa mpya wa Katavi na miradi mbalimbali ya maendeleo inayoenda sambamba na shughuli za uwekezaji.
 
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa Katavi
 
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda katika sherehe fupi za kuzindua uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya maboresho makubwa yaliyofanyika katika uwanja huo ambao sasa una uwezo wa kutumiwa na ndege za abiria wasiopungua sabini.

Mama Zakhia Billal akiteta jambo na Mama Tunu Pinda katika jukwaa kuu kwenye uwanja wa ndege wa Katavi kabla ya uwanja huo kuzinduliwa leo na Makamu wa Rais.
 
 Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kukamilika kwa maborsho ya uwanja huo, kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Mama Zakia Bilal mke wa Makamu wa Rais.


 Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akizindua rasmi uwanja huo uliogharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 30 ambapo katika hizo bilioni 28 ikitolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na bilioni 2 zikitolewa na Shirikia la Kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akiteta jambo na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Chizeba katika uwanja wa ndege wa Katavi leo.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akimkaribisha Makamu wa Rais ili kuongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa uwanja huo mjini Mpanda leo.
 

 Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo mchana.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba muda mfupi kabla ya mapokezi ya Mkamu wa Rais leo Mjini Mpanda.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Chadema Said Alfi katika uwanja wa ndege wa Mpanda muda mfupi kabla ya mapokezi ya Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Billal.

 Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mst. Issa Machibya wakijadiliana jambo leo katika katika mapokezi ya Makamu wa Rais katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta muda mfupi baada ya mapokezi ya Mhe. Makamu Rais katika uwanja wa ndege wa Mpanda leo.
 

 Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Mary Nagu akifurahia jambo na Mkuu wa  Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika mapokezi ya Mhe. Makamu wa Rais katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza katika kongamano hilo kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda na kukaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo.
 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na kutoa taarifa ya mkoa wake wa Rukwa katika maendeleo ya uwekezaji.
 
Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Mary Nagu akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika mjini Mpanda leo.

 Mabalozi mbalimbali wamehudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mkoa wa Katavi kutoka Burundi, Zambia, Misri, Japan na DRC Kongo.