Wednesday, February 27, 2013

MWENYEKITI WA WAMA MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA HOSPITALI KUU YA MKOA WA RUKWA

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha orodha ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013 hospitalini hapo. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani na vina thamani ya shilingi milioni mia saba.
 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha moja ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013. Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine za Ulta Sound, X-Ray, Upasuaji, tiba ya macho, tiba ya kinywa na meno, mgongo, mifupa, mashine ya dawa za usingizi, vitanda maalum (TCU beds) n.k. Kushoto anaeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
 
Baadhi ya vifaa tiba alivyokabidhi Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia saba. Vifaa hivo pamoja na vingine ambavyo bado vipo kwenye kontena vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani.
 
Mama Salma Kikwete akiongea na wadau wa sekta ya afya na wananchi waliokusanyika katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkaribisha Mama Salma Kikwete kuzungumza na wadau wa afya katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ambapo alikabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Mama Salma kwa jitihada anazozifanya yeye na taasisi yake katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha huduma za afya nchini, alimuhakikishia kuwa Serikali yake ya Mkoa itahakikisha inasimamia vizuri sekta ya afya kutimiza ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2010-2015 ambazo ni pamoja na kuimarisha huduma za afya nchini.
 
 
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daudi Nasib akielezea kwa kifupi kazi na majukumu ya taasisi hiyo kwa wadau wa afya waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka WAMA kwa uongozi wa hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa. Miongoni mwa malengo makuu ya taasisi hiyo ni kuimarisha afya ya mama na mtoto na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini.
 
 Ndugu Abdul Kimario wa shirika la Project C.U.R.E kutoka Marekani ambae shirika lake limeshirikiana na WAMA kuleta vifaa tiba hivyo hapa nchini akitoa ufafanuzi wa matumizi ya baadhi ya vifaa hivyo kwa wadau wa afya waliokusanyika kushuhudia makabidhiano hayo.
 
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mzee Protas Kimario kitambulisho cha matibabu ya uzeeni kuwakilisha wazee wengine 458 zoezi lililoenda sambamba na kukabidhi vifaa vya tiba kwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.02.2013. Jumla ya vitambulisho 4356 sawa na asilimia 96% katika Manispaa ya Sumbawanga vimeshatengenezwa kwa ajili ya matibabu ya wazee.
 
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta funguo za pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya vya Wilaya hiyo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Jumla ya Pikipiki kumi kutoka Water Rid zilikabidhiwa kwa ajili ya huduma hizo katika Mikoa ya Rukwa na Katavi.

Monday, February 25, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AWASILI MKOANI RUKWA KWA ZIARA YA SIKU TATU

Mama Salma Kikwete (MNEC) Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA) akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga leo. Anaemuongoza ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Atakuwepo Mkoani Rukwa kwa ziara ya siku tatu ambapo atakabidhi msaada wa vifaa vya hospitali kutoka WAMA, atafanya mkutano na wanawake, atakabidhi pikipiki za mradi wa PMTCT katika tarafa ya Matai Wilaya mpya ya Kalambo, atakabidhi pia vitambulisho vya matibabu ya wazee wa Manispaa ya Sumbawanga, na vilelvile kabla ya kuondoka atafanya mkutano na wanajumuiya wa shule ya St. Theresia ya Mjini Sumbawanga.
 
Mama Salma akiveshwa Skafu na moja ya Skauti mara baada ya kuwasili Mkoani rukwa.
 
Mama Salma akifurahi na vikundi vya ngoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
 
Mama Salma akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal ambae pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini CCM. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Ignas Malocha.
 
Mama Salma Kikwete akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika Ikulu ndogo ya Sumbawanga Mkoani Rukwa leo mara baada ya kuwasili katika ikulu hiyo kwa ajili ya mapumziko mafupi, chakula na kusomewa taarifa ya Mkoa.
 
Mama Salma Kikwete Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakati akimsomea taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika sekta ya afya.
 
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, wa tatu ni Ndugu Aeshi Hillal Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa Rukwa, Iddi Kimanta Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na Mussa Chang'a Mkuu wa Wilaya ya Kalmbo wakifuatilia taarifa hiyo iliyokuwa ikiosmwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
 
Mganga Mkuu Hospitali Kuu ya Mkoa Rukwa Dkt. Gurisha Richard akifafanua jambo kwa Mama Salma Kikwete juu ya vifo vya mama na mtoto Mkoani Rukwa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa InjiNIA Stella Manyanya akimkabidhi Mama Salma Kikwete taarifa hiyo ya Mkoa wa Rukwa kuhusu sekta ya Afya. Katika taarifa hiyo Mama Salma kikwete aliutaka uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuendelea kutoa elimu kwa kina mama kabla na baada ya kujifungua ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo vingi husababishwa na uelewa mdogo wa akinamama juu ya afya zao na watoto. SOMA TAARIFA HIYO HAPA CHINI. Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

Saturday, February 23, 2013

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2005-2012 YA MKOA WA RUKWA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akisoma taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mapema hii leo. Taarifa hiyo hiyo iliyodumu kwa zaidi ya saa moja na nusu ilirushwa moja kwa moja (LIVE) na Radio Chemchem FM ya Hapa mjini Sumbawanga.

Thursday, February 21, 2013

KITAIFA: RAIS MWAI KIBAKI WA KENYA AZINDUA BARABARA YA MWAI KIBAKI JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akizindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jina la barabara ya Old Bagamoyo jana kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo jana Februari 21, 2013.
 

Sehemu ya barabara iliyopewa rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo jana kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo jana Februari 21, 2013. (Picha na Ikulu)

WANAOTUHUMIWA KUNYOFOA MKONO WA MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) MARIA CHAMBANENGE HAWA HAPA


Watuhumiwa watano wakiwa katika Mahakama ya Hakimu wa Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kwa tuhuma za kumnyofoa mkono mwanamke mlemavu wa ngozi (Maria Chambanenge (39) (pichani chini) na kutokomea nao na kumjeruhi vibaya kichwani kisha kuufukia porini kijijini Miangalua. Picha na Juddy Ngonyani.
 
Mama Maria Chambanenge (39) mlemavu wa ngozi aliyenyofolewa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa pichani juu akiwa anaendelea vizuri huku akipatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa. (Picha na Rukwareview)

WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO WAPEWA SEMINA YA PAPO KWA PAPO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa semina kwa baadhi ya kina mama wajasiriamali Mkoani Rukwa waliofika ofisini kwake kwa ajili ya msaada wa fikra na mtaji kuendeleza biashara zao ndogo ndogo. Kina mama ho wanaojishugulisha na bishara za kuuza karanga, mahindi ya kuchoma, mayai na mama lishe walipata somo kidogo juu ya kuendeleza biashara zao ambapo pia waliahidiwa kusaidiwa kuendeleza biashara zao. Miongoni mwa mafunzo waliyopewa ni utunzaji mzuri wa hesabu, usafi wa mwili, nguo na eneo la biashara, kujiwekea malengo pamoja na uchangamfu kwa wateja na ubunifu zaidi wa kuongezea thamani biashara zao. 
 
Injinia Stella Manyanya akitoa darasa kwa wajasiriamali hao wadogo wadogo akiamini kuwa hata wafanyabiashara wakubwa walianzia chini na hivyo kuwapa moyo kinamama hao kuwa mstari wa mbele kujikwamua kiuchumi.

Darasa likiendelea...zoezi hili la kuelimisha na kuwahamasisha kinamama wajasiriamali wadogo wadogo ni katika malengo waliojiwekea umoja wa wanawake mkoa wa Rukwa (RUWA) kuhakikisha mwanamke wa Rukwa anakua kiuchumi na kuondokana na umaskini. 
 
Mama Fausta Malenga mama wa watoto wa tano anajishughulisha na biashara ya uuuzaji mahindi ya kuchoma.
 
Maria Kilongozi Mjasiriamali biashara ya Mama Lishe
 
Magreth Otolo mjasiriamali biashara ya kuuza karanga...
 
Ester Sundu biashara ya kuuza mayai na machungwa....kwa ujumla wajasiriamali hao walimshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutojali udogo wao na kutumia muda wake kubadilishana nao mawazo juu ya shughuli ndogondogo wanazofanya, walisema kuwa wamefarijika sana na watayanyia kazi mawazo waliyopewa.

Wednesday, February 20, 2013

JAMII YETU

What is your comments?.....................!

HABARI KATIKA PICHA KUTOKA "NOTICE BOARD" YA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Kamera ya rukwareview imepita katika ubao wa matangazo na taarifa mbalimbali uliopo ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na kukuta picha hii iliyowekwa na kiongozi huyo. Umeelewa nini kwenye picha hii. Comment...... 

TIPS ON HOW TO BROWSE AND USE OUR BLOG EFFECTIVELY/ NAMNA YA KUTUMIA BLOG HII KIUFASAHA


Katika Blogu hii, hakuna picha au taarifa yeyote inayoondolewa baada ya kuonekana ukurasa wa kwanza, bali inahamia ukurasa wa pili au wa tatu na kuendelea kutokana na wingi wa taarifa zinazowekwa humu.
  1. Ukitaka kuhamia kurasa zingine zilizopita ambazo pengine hukuziona, nenda hadi chini kulia kwako bofya "Older Posts" kuona kurasa za nyuma zilizopita ambazo zimehamia kurasa za ndani. Fanya hivyo tena na tena kuona kurasa zote katika Blogu hii.

  2. Ukitaka kurudi mwanzo nenda chini kabisa, katikati bofya "Home" kurudi ukurasa wa mwanzo wa blogu hii.
  3. Ukitaka kutafuta habari kwa jina la mtu, sehemu au kitu nenda kulia utaona kisanduku juu yake kimeandikwa Tafuta/ Search andika unachikitaka hapo alafu bofya Search subiri kwa muda utaona majibu ya ulichokiandika. Mfano ukitaka kupata habari za mpanda andika"mpanda" alafu bofya search.
  4. Kama umevutiwa na habari, picha au kero na maoni yako unaweza kuandika kwa kubofya sehemu iliyoandikwa "comments" ambayo ipo chini ya kila habari (post) chagua annonymus kama hutaki ujulikane au chagua hizo nyingine kama unataka ufahamike.
Kwa yeyote mwenye maoni, ushauri, habari au picha nzuri za kuelimisha na kuhabarisha jamii unaweza kututumia kupitia tembs2001@gmail.com.NAMNA YA KUTOA MAONI/ COMMENTS:

Chini ya kila POST utaona sehemu imeandikwa Comments, Bofya hapo mara moja, Shuka hadi chini ya hiyo POST utaona kisanduku kimeandikwa Post a Comment kama kinavyoonekana hapo chini.

0 comments:


Post a Comment 
Andika Comments/ maoni yako hapo unaweza kuandika jina na contact zako kama ukipenda kisha chini ya hicho kisanduku utaona maneno haya " " Uchaguzi upo kwenye hicho kimshale kinachoangalia chini, chagua "Annonymus" kisha nakili maneno utakayopewa yaliyoandikwa kwa kificho kwenye kisanduku kinaochoonekana alafu Bofya Publish. Comment yako itakuwa hewani popote duniani katika mtandao huu na itaifikia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, kama inahitaji kufanyiwa kazi basi itafikishwa kwa wahusika na kufanyiwa kazi. Nawatakia kazi njema na Afya Bora.

Tuesday, February 19, 2013

PATA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 HAPA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
1.0 UTANGULIZI
Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012. Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0 MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1 Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2 Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
3.0 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.
 
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE HAPO CHINI

Monday, February 18, 2013

MWENYEKITI CHAMA CHA ALBINO TANZANIA (TAS) AIOMBA SERIKALI KUPITISHA ADHABU YA KIFO KWA WANAOWATENDEA ALBINO UNYAMA IWE FUNDISHO KWA WENGINE

 Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) "Tanzania Albino Society" ndugu Ernest Kimaya akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Pichani chini) kuelezea juu ya tukio la kinyama alilofanyiwa Maria Chambanenge (39) la kukatwa mkono wake wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kwa imani za kishirikina kuwa ni kupata utajiri. Watuhumiwa waliohusika na tukio hilo ambao pia yupo mume wake na muathirika wameshakamatwa na polisi na kuonyesha mkono huo, taratibu za mashitaka zinaendelea ili haki iweze kupatikana. Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kufkiria adhabu kali kwa watuhumiwa kama ho ikiwepo kunyongwa ili fundisho kwa wengine na Albino waweze kuishi katika nchi yao kwa amani.
 
 Mwenyekiti wa TAS akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Mohammed Chanzi.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwa uchungu na kutoa onyo kali kuwa vitendo hivyo vya kinyama havitavumiliwa. Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo hivyo.

 Kabla ya kwenda kumtembelea mgongwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliandaa chakula kwa wageni wake.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na msafara wake pamoja na viongozi wa chama cha Albino Tanzania (TAS) wakimfariji Mama Maria Chambanenge walipomtembelea katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa ambapo hali yake kwa sasa inaendelea vizuri japo ameongezewa ulemavu mwingine wa viungo kwa kukatwa mkono wake wa kushoto. 
 
 Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya akimfariji Mama Maria Chambanenge ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao tayari wapo mikononi mwa polisi.
 
..............................................................
 
Mwenyekiti wa chama watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania "Tanzania Albino Society" (TAS) ndugu Ernest Kimaya ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki ya kuishi kwa kuwapatia adhabu kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa vitendo vya kinyama dhidi ya albino ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika katika imani za kishirikina kuwa ni kujipatia utajiri.
 
Aliyasema hayo jana akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ofisini kwake alipomtembelea akiongozana na viongozi wengine wa chama hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa kile alichosema ni mfano wa kuigwa kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini kwa muda wa miaka mitano iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa kuwakamata wahalifu wa namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi usiozidi siku tatu.
 
Amesema kuwa maalbino wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na amani kama watu wengine jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam. "Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa huru, wabanwe hata kuchomwa moto wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni mmoja na inatia uchungu sana kwa sisi maalbino" alisema mwenyekiti huyo.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wenzake kwa kufika Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya kuskika kwa matukio hayo ya kinyama kwa Albino wenzao na pia kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri walioutoa kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki iweze kutendeka. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza kuvumilika Mkoani kwake.
 
Kumekuwepo na matukio ya kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo mama mlemavu wa ngozi Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga alivamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa ambao wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao zinaendelea.
 
Vilevile katika bonde la ziwa Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba ameshambuliwa na vijana watatu waliovaa kininja na kumkata mkono wake mmoja na kutokomea na kusikojulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.
 
Matukio yote hayo yanahusishwa na wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo vitendo hivi vya imani za kishirikina vimeshamiri. 

ALICHOSEMA MKUU WA MKOA WA RUKWA BAADA YA MKONO WA ALBINO KUPATIKANA


Friday, February 15, 2013

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA PONGEZI KWA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KWA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOMKATA MKONO MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) NA KIZIBITI HICHO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (Albino) Vicky Mketema kulia na wajumbe wenzake wa shirika hilo watatu waliosimama nyuma. Kulia waliosimama ni katibu wa Mkuu huyo wa Mkoa Frank Mateni na kushoto aliyekaa ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Deonisya Njuyui.
 
 Mama Maria Chambanenge mlemavu wa ngozi anayenyonyesha mtoto wa miezi mitano alikatwa mkono na watuhumiwa ambao wameshatiwa nguvuni na jeshi la polisi Mkoa wa Rukwa na Mkono wake uliokatwa umeshapatikana. Upelelezi bado unaendelea kuwapata watuhumiwa zaidi wanaohusika na vitendo hivyo.
 
Mkurugenzi wa shirika la under the same sun Vicky Mketema ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kushughulikia tatizo hilo kikamilifu na kwa haraka na kufanikiwa kupata kiungo hicho na watuhumiwa waliohusika kwa muda wa siku mbili. Alisema endapo mikoa yote ingekuwa inashughulikia matatizo kama hayo kwa muda mfupi kama huo basi uhalifu na namna hii ungekuwa umeshatoweka nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa onyo kali kwa wale wote watakaohusika na vitendo vya uvunjifu wa amani Mkoani humo ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi pale wanapowashuku wahalifu wa vitendo hivyo. Amewato hofu wananchi kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili yo.

Muathirika huyo anaendelea kupata huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na hali yake inaendelea vizuri.

MKUU WA MKOA WA RUKWA AAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI WALANGUZI WA NISHATI YA MAFUTA MKOANI HUMO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pongezi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa nishati ya mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao vizuri. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
 
Mwenyekiti wa baraza la ushauri watumiaji wa maji na nishati nchini Eng. Profesa Katima akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni kutetea na kulinda haki za watumiaji wa maji na nishati ambayo ni maji safi na maji taka, umeme, petroli na gesi asilia.
 
Baadhi ya wadau wa mkutano huo ambao ni vyombo vya ulinzi na usalama, Tanesco, EWURA Mkoa wa Rukwa, wawakilishi wa sheli za mafuta na shirika la Maji safi na Maji taka Mkoa wa Rukwa (SUWASA) 
 
Wawakilishi wa baraza hilo Mkoani Rukwa
 
Picha ya pamoja.

Wednesday, February 13, 2013

TANZANIA YASHINDA VIVUTIO VITATU MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA, NI MLIMA KILIMANJARO, NGORONGORO CRATER NA MBUGA YA SERENGETI

 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda
kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro,
Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo
imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi,
Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika
ukanda wa Afrika Mashariki
Katika picha kulia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa
wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crater  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya Afrika iliyofanyika juzi jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. (Na Fullshangwe Blog)

Friday, February 8, 2013

RAIS KIKWETE ASEMA VITAMBULISHO VYA TAIFA KUTUMIKA UCHAGUZI UJAO

NA SHAKILA GALUS - MAELEZO
……………………………
RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amehahidi kuwasaidia Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kwa kuiwezesha kupata fedha kwa ajili Vitambulisho vya Taifa ili kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 watu wote wawe wamepata vitambulisho hivyo vitakavyo tumika katika uchaguzi huo.
 
images Aidha Rais Kikwete aliitaka NIDA kutoa vitambulisho kwa watu wanaotakiwa na kuwachukulia hatua za kisheria wale watakaokiuka sheria ya usajili wa vitambulisho hivyo.
 
Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais Kikwete wakati uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 
Rais Kikwete aliwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa zao kwa uaminifu na kutoa ushirikiano ili kurahisisha zoezi hilo.
 
Aliwataka viongozi wa dini, serikali na waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano huo.
 
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi alisema ni muhimu kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la msingi ambalo litaweza kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo mikubwa ya usajili ya kitaifa.
 
Baadhi ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi (TRA), Mfumo wa vizazi na vifo (RITA), Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa POLISI, Mifumo ya mawasiliano ya simu(Vodacom,Tigo,Zantel,Airtel,TTCL),Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za kijamii,Mifumo ya Taasisi za kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan Board),n.k.
 
Mkurugezi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto mbalimbali za kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu vya kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.
 
Aliyataja mahitaji halisi ya zoezi hilo kuwa ni vifaa vya kuchukulia alama za vidole, picha saini takribani 12,000, rasilimali watu wa muda 114,000 na wakudumu 3000 ili kukukamilisha mpango huo kwa muda utaotakiwa.