Monday, April 22, 2013

MHE. CHANG'A AMUWAKILISHA MKUU WA MKOA WA RUKWA KWENYE MAHAFALI YA PILI YA CHUO CHA UALIMU ST. AGGREY CHANJI

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a akizungumza katika mahafali ya pili ya chuo cha ulaimu St. Aggrey Chanji. Katika hotuba yake aliwataka wanafunzi wanaomaliza kusoma vizuri waweze kufaulu mitihani yao pamoja na kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho kwa kukiletea sifa nzuri. Aliwaasa wananchi wa Rukwa kubadilika kimtazamo na kuwaendeleza watoto wao kieleimu.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a akimkabidhi cheti mshindi wa jumla Bonavencha Ngasa katika taaluma kwa wanafunzi wa ualimu wa Stashahada, daraja la III A na Ualimu wa Awali.
 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flavour" maarufu kama Dogo Janja alialikwa kutoa burudani.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo akimbadilishia "Mike" Dogo janja ili apate kutoa burudani vizuri.

Baadhi ya wanafunzi waliohitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
 

Picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu chuoni hapo.

Tuesday, April 16, 2013

MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA BUNENGI YA AFRIKA KUSINI KWA URATIBU WA NDC AONANA NA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KWA LENGO LA KUSAIDIA KATIKA UWEKEZAJI MKOANI HUMO

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Bunengi ya Afrika Kusini Bi. Savannah Maziya akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NDC (National Development Coorporation) ambaye pia Mbunge Mstaafu wa Jimbo la KwelaNdugu Chrissant Mzindakaya walipoonana na uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kujadili namna Kampuni hiyo kwa kushirikiana na NDC katika uratibu watakavyosaidia katika kuwekeza kwenye miundombinu ya bandari, reli na barabara kuunganisha Mkoa wa Rukwa Mikoa pamoja na Nchi jirani kuwezesha rasilimali zilizopo Mkoani Rukwa zinapata masoko yakiwemo mazao, madini na utalii. Utalii huo ni pamoja na Kalambo Falls maporomoko ya maji makubwa barani Afika na Bismark Fort iliyokuwa ngome ya wajerumani iliyopo hapa Mkoani Rukwa.
 
 Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akiongoza kikao hicho kilichohudhuriwa na muwekezaji huyo, wawakilishi wa NDC, Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa na Halmashauri za Wilaya ya Kalmbo na Sumbawanga.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta akiwa anazungumza katika kikao hicho.
 
 Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwa anatoa mchango wake juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa muwekezaji huyo.
 
Afisa katika dawati la Uwekezaji Ndugu Misasi Marco akimwaga sera kutoka katika dawati lake uwekezaji.

Wednesday, April 10, 2013

RUKWA REGIONAL MUSEUM (LOCATED AT REGIONAL COMMISSIONER'S OFFICE, GROUND FLOOR)

It is a small museum founded by the Rukwa Regional Commissioner Engineer Stella Manyanya to concur with the instruction given by the Prime Minister Mizengo Kayanza Pinda during the function of Tanzania Cultural Day, Rukwa and Katavi Community held in Dar es Salaam at Makumbusho square last year 2012. The instruction by the Prime Minister went to Rukwa and Katavi leaders to establish Regional Museums that will serve together with tourism  industry in the respective Regions.

 Just by start, the Rukwa Regional Commissioner decieded to establish a small museum at his office as a steping stone towards the achievement of having a Regional Museum where later on will be shifted elsewhere as a full Regional Museum. The area has already alocated where in the future will be transformed into a Rukwa Regional Museum.   
 

 Some collections of informations and crafts has already being made as can be seen on the pictures.

 Various trophies that were given to the Rukwa Regional Commissioner's Office in previous years on a different achievements can also be found here.
 
 Information of all Regional Commissioner's lead Rukwa Region since its establishment in the yaear 1974 can also be found here. 
 
 
Rukwa Regional Commissioner Engineer Stella Manyanya working handly with carpenters in the process of establishing the Museum. It was not an easy task, this day it took over 20 hours a day to accomplish the initial stages of the Museum.
 

Thursday, April 4, 2013

HII NDIO MASHINE YA KWANZA YA ATM NCHINI TANZANIA

MASHINE HIYO IMEHIFADHIWA KATIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.

Wednesday, April 3, 2013

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANAZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31, MACHI, 2013

Ndugu Wananchi;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi. Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.
Ziara ya Rais wa China Nchini Tanzania
Ndugu wananchi;
Jambo la kwanza ni ziara ya Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China aliyoifanya nchini kwetu kati ya tarehe 24 na 25 Machi, 2013. Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa kumpokea vizuri mgeni wetu na ujumbe wake. Wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.

Kwa niaba yenu, nimepokea salamu za shukrani kutoka kwa Rais Xi Jinping akielezea kufurahishwa na mapokezi mazuri tuliyowapatia. Naomba tuendelee kuonesha moyo wa upendo na ukarimu kwa wageni wetu wengine mashuhuri watakaotutembelea siku za usoni.

Ndugu wananchi;
Nami pia, nimemshukuru sana Mheshimiwa Xi Jinping kwa kukubali mwaliko wangu na kufanya ziara ya kihistoria na yenye mafanikio makubwa kwa nchi yetu. Ameifanyia nchi yetu jambo la heshima kubwa na kumbukumbu isiyosahaulika. Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kuitembelea, tena siku kumi tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi yake. Na, kubwa zaidi ni kutumia fursa ya ziara yake hapa nchini kutangazia dunia Sera ya China kwa Afrika katika kipindi cha uongozi wake. 
Tumefarijika sana kusikia kuwa uhusiano na Afrika bado unapewa kipaumbele cha juu na viongozi wapya wa China. Pia, kuwa China itaendelea kukuza biashara na uwekezaji na kuongeza misaada ya maendeleo kwa Afrika ikiwemo kutoa nafasi 18,000 za mafunzo kwa vijana wa Kiafrika. Kama mtakumbuka nchi zetu mbili zilitiliana saini mikataka 16 ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Misaada ya maendekeo kwa maeneo yetu ya kipaumbele nayo imejumuishwa.
Ndugu Wananchi;
Rais Xi Jinping alielezea na kusisitiza dhamira yake na ya Serikali na Chama cha Kikomunisti cha China ya kudumisha na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China. Kama mjuavyo uhusiano huo ulianzishwa mwaka 1964 na waasisi wa nchi zetu, yaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na Mwenyekiti Mao Zedong aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa China na Waziri Mkuu wake Chou En Lai.
Rais wa China aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika medani ya kimataifa na kuchangia katika jitihada zetu za kujiletea maendeleo kwa kuongeza misaada ya maendeleo. Katika miaka 49 ya uhusiano na ushirikiano na China nchi yetu imepata misaada mingi ya maendeleo ikiwemo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere ambao ulizinduliwa na Rais Xi Jinping wakati wa ziara yake.
Ndugu wananchi;
Kuna miradi kadhaa mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini, Bara na Zanzibar, kwa msaada wa Serikali ya China. Wakati wa ziara yake, Rais Xi Jinping iliahidi kuendelea kutusaidia miradi mingine ya maendeleo kama tulivyoomba wakati wa mazungumzo yetu licha ya ile ambayo ilitiwa saini siku ile.
Ajali ya Kuporomoka Jengo la Ghorofa
Jijini Dar es Salaam
 
KUSOMA ZAIDI BOFYA read more CHINI