Sunday, June 23, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONGOZA WAUMINI WA KANISA KATOLIKI EMAUS CENTRE UBUNGO JIJINI DAR KATIKA IBADA YA KUPANDA MBEGU NA NA KUFANIKIWA KUPANDA SHILINGI MILIONI 41

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar es Salaam  ambapo aliwaasa  juu ya umuhimu wa kutunza amani iliyopo nchini kwa kujiepusha na mambo madogomadogo yanayoweza kuondoa amani iliyopo ikiwemo mijadala ya kuchinja ambayo ilishaanza kufanya machafuko nchini. Hata hivyo aliwaomba waumini hao kuwaombea wanasiasa wafanye kazi zao vizuri kwa haki, usawa na uwajibikaji badala ya kuishia kuwatupia lawama ambazo hazijengi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akishiriki kukusanya sadaka zilizokuwa zikitolewa na waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akinadi kitabu cha Sumbawanga Ng'ara alichoandika yeye mwenyewe kwa waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar (hawako pichani) walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni, kitabu hicho kinachoelezea juu ya usafi na udhibiti wa mazingira Mkoani Rukwa na taifani kwa ujumla kilitumika pia kupandia mbegu. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.

Waumini wa kanisa katoliki kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam waliokuwa wamekusanyika "Emaus Centre" Ubungo kwa ajili ya ibada ya kupanda mbegu iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni.

Saturday, June 15, 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA KITABU CHA SUMBAWANGA NG'ARA KILICHOANDIKWA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA MHANDISI STELLA MANYANYA MJINI DODOMA

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu cha "Sumbawanga Ng'ara" kilichoandikwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (wa katikati) katika ukumbi wa Dodoma Hoteli Mjini Dodoma, kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa. Kitabu hicho kinaelezea na kutoa muongozo juu ya usafi na uhifadhi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla. Kitabu hicho kinauzwa Tsh. 3,500 kwa lengo la kukusanya fedha ya kuchapisha machapisho mengine zaidi.
 
 Zoezi la uzinduzi likiendelea. SOMA ITABU HICHO HAPO CHINI........
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho alitoa wito kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa mpango waliouanzisha wa Sumbawanga Ng'ara kwa kuweka mikakati na kutengeneza sheria ndogondogo za kusimamia mpango huo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akisoma hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu kuzindua kitabu cha Sumbawnga Ng'ara ambapo alimshuru kiongozi huyo Mkuu katika nchi kwa kutenga muda wake pamoja na waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya uzinduzi. Zaidi ya vitabu 175 vilinunuliwa baada ya uzinduzi huo.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitambulisha viongozi mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakiwemo baadhi ya mawaziri, wabunge, madiwani kutoka Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wengine wa chama na Serikali.
 
 Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mzengo Kayanza Peter Pinda akizungumza katika hafla hiyo ambapo alimpongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya kwa kuanzisha mpango wa Sumbawanga Ng'ara pamoja na kuandikia kitabu. Alisema viongozi kama hawa wanaofanya mambo kwa vitendo ndio viongozi wa mfano wanaotakiwa katika taifa letu.
 
 Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anaeshugulia Elimu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla hiyo. Kwa upande wake alisema kama Wizara wanaipongeza Serikali na wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kuanzisha mpango huo wa Sumbawanga Ng'ara na kuunga mkono. Alisema halmashauri zingine zinatakiwa zijifunze kwa kuanzisha mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya utunzaji wa mazingira. Mhe. Majaliwa aliahaidi kununua vitabu 10 vya Sumbawanga Ng'ara.
 
Mhe. Pindi Chana, Mbunge Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Njombe akizungumza katika hafla hiyo. Alimsifu mwandishi wa kitabu hicho cha Sumbawanga Ng'ara ambaye pia ni muasisi wa mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na kusema ni mchapakazi wa kuigwa. Mhe. Chana aliahidi kununua vitabu 30 vya Sumabwanga Ng'ara kwa ajili ya kuhamasisha usafi Mkoani Njombe.
 
Mbunge wa Kilindi CCM Mhe. Beatrace Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo ambaye naye alipewa fursa na Waziri Mkuu aweze kuzungumza ambapo alisema Mkoa wa Rukwa umepata kiongozi thabiti ambaye angetamani afanye kazi katika Mkoa wake wa Tanga. Mhe. Selukindo alinunua vitabu 20 kwa ajili ya madiwani wa Korogwe ili awape wivu wa kufanya kazi katika maeneo yao.
 
 Mama Anne wa UNDP akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu cha Sumbawanga Ng'ara ambapo alifurahishwa na kitendo hicho na kusema yeye pia ni mdau wa mazingira na hivyo akaahidi kununua vitabu 10 kwa ajili ya kuviweka katika maktaba yake.
 
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa akielezea kwa kifupi Mpango wa Sumbwanga Ng'ara ambapo alisema tangu mpango huo uanzishwe na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya wananchi wengi wameupokea vizuri na tayari Mji wa Sumbawanga umeshanza kubadilika ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
 
 Wajukuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wanaosoma nchini Marekeani wakijitambulisha katika hafla hiyo baada ya kupewa fursa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiendelea na hotuba yake.
 
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akimkadhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima kitabu cha Sumbawanga Ng'ara mara baada ya kukizindua rasmi.
 

Friday, June 7, 2013

HASSAN MAAJAR TRUST YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 320 KUSAIDIA ELIMU MKOANI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiandika kwenye daftari la mwananfunzi aliyekaa pembeni yake kama ishara ya matumizi ya madawati 320 yaliyokabidhiwa na taasisi ya Hassan Maajar Trust ya jijini Dar es Salaam tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense ikiwa ni jitihada za taasisi hiyo kusaidia elimu nchini.  Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilamu Serikali na huduma zilizopo badala ya kutoa mchango wowote. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga na Makamu Mwenyekiti Ndugu Shariff Maajar. Wa tatu kutoka kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
 
Wanafunzi wa shule ya msingi Kasense wakiwa wamekalia baadhi ya madawati yaliyotolewa shuleni hapo na taasisi ya Maajar Trust. Jumla ya shule nane (8) za Mkoa wa Rukwa kutoka kila Wilaya zenye upungufu mkubwa wa madawati zimepata madawati arobaini (40) kila moja kuondoa upungufu unaowakabili.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajr Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilaumu Serikali badala ya kusaidia katika huduma za jamii. Aliendelea kusema kuwa katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaboreka atakuwa dikteta kuhakikisha kila mtu wakiwemo wazazi wanatimiza wajibu wao katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaimarika. Kulia  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitoa taarifa fupi ya madawati kwa shule za msingi Mkoani Rukwa katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule hizo Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Aliishukuru taasisi hiyo na kusema kuwa Rukwa ina uhaba wa madawati 33,638 sawa na asilimia 50.2%.
 
Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense. Mwenyekiti huyo alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuboresha mazingira ya kusomea watoto nchini Tanzania. Aliwaasa wadau wa elimu Mkoani Rukwa kuchangia katika sekta hiyo kwa maendeleo ya taifa.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense. Katika hotuba yake hiyo alisema lengo la taasisi hiyo ni kuboresha mazingira ya kusomea kwa watoto wa Tanzania na kuhamasisha jamii kutambua wajibu wa kuchangia ili kuweka mazingira ya shule zetu kuwa mahali bora kwa watoto kusomea. 
 
Mkurugenzi Mtendaji wa  Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga akisoma houtuba yake kwenye hafla hiyo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar shilingi laki moja na nusu ili aikabidhi kwa mwalimu mkuu shule ya msingi Kasense ikiwa ni sehemu ya azimio alilolianzisha na kuliita "Azimio la Kasense" KADARU (Kampeni ya Dawati Rukwa) katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013.
 
Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akipima uelewa wa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kasense Mkoani Rukwa kwa kuwapa mtihani wa kuandika wakati wa hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule hiyo, Kulia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.
 
Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti Hassan Maajar Trsut Bw. Shariff Maajar, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa na Mkurugenzi Mtendaji Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga wakifurahia Ngonjera ya wanafunzi wa shule ya msingi Kasense katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati. 

Picha  ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wa taasisi ya Hasaan Maajar Trust.
 
Picha ya pamoja.

Wednesday, June 5, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AONGOZA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA KITAIFA NAMANYERE MKOANI RUKWA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akihutubia wananchi katika viwanja vya sabasaba Mji mdogo wa Namanyere Mkoani Rukwa katika kuhitimisha siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa leo tarehe 05.06.2013. Katika hotuba yake hiyo alisisitizia juu ya uhifadhi wa mazingira kwa kutunza vyanzo vya maji, milima na misitu ya asili, kuhifadhi ardhi na kupanda miti katika maeneo yaliyoathirika na usafi wa mazingira kwa ujumla.
 
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua kitalu cha miche ya miti mbalimbali ya mjasriamali ndugu Kidevu (kushoto) katika maonyesho kwenye kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa katika Mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi leo tarehe 05.06.2013, Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akisoma moja ya vitabu vya uhifadhi wa mazingira wakati akikagua banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwenye kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa katika Mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi leo tarehe 05.06.2013, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akimkabidhi kikombe na cheti Ndugu Leonard Kapini Makamu mwenyekiti Halmashauri ya Mji Mpanda kwa Halmashauri hiyo kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika usafi wa Miji nchini. Zawadi nyengine waliyopewa ni Pikipiki moja. Jiji la Nyamagana limekuwa la kwanza kitaifa na Manispaa ya Moshi ikiwa Manispaa ya kwanza kitaifa katika usafi wa Mazingira mwaka huu 2013
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji Mpanda wakifurahia kwa pamoja ushindi kwa halmashauri yao kuwa ya kwanza kitaifa katika usafi wa Miji nchini mwaka 2013. Halmashauri hiyo imezawaidiwa cheti, kikombe na pikipiki moja.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua mtambo asilia wa kuzalisha umeme kwa kutumia upepo uliobuniwa na mjasiriamali kutoka Mkoani Rukwa wa kampuni ya Ulaya Hydro and Windmill Technology (Kulia), Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima mara baada ya kuwasili kwa helkopta katika viwanja vya Sabasaba katika Mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasi kwa ajili kushiriki katika kilele cha siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akipanda mti wa kumbukumbu katika kampeni ya uhifadhi wa mazingira mbele ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi leo tarehe 05.06.2013 ikiwa ni kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa.
 
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akizindua kwa kuwasha mashine mpya ya maji katika bwawa la maji Mphiri ambalo ni chanzo kikuu cha Maji katika Mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasi leo tarehe 05.06.2013. Serikali imetenga jumla ya Tshs bilioni nne (4) kuendeleza chanzo hicho muhimu ambacho asili yake ni chemchem. 
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa akihutubia wananchi ambapo alikemea uharibifu wa vyanzo vya maji na kuwaasa wanasiasa kutofanya siasa zitakazopelekea kuhatarisha uhai wa vyanzo vya maji kwani umuhimu wa maji hauna mbadala. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kuwatambulisha baadhi ya viongozi wakuu waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa. 
 
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Suleiman Rashid akiwataja washindi mbalimbali wa usafi wa mazingira kitaifa katika ngazi ya majiji, manispaa, miji na wilaya ambao walipewa zawadi mbali mbali. Walioongoza ni Halmashauri ya Jiji la Nyamagana (Majiji), Halmashauri ya Manispaa ya Moshi (Manispaa), Halmashauri ya Mji Mpanda (Miji) na Halmashauri ya Wilaya Njombe (Wilaya). 
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Msema Chochote (MC) machachari ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a.
 
MC Machachari ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a akisherehesha mambo kwa ufasaha kabisa. Nyuma yake ni kundi la taarab la TOT ambalo limekuwa likinogesha sherehe hizo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Galikunga wakijadili jambo katika maadhimisho hayo. Hawa ndio viongozi wakuu wa Wilaya ya Nkasi na wenyeji wa maadhimisho ya siku hiyo ya mazingira kitaifa mwaka huu 2013. 
 
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa akicheza muziki na kundi la Tanzania One Theatre (TOT) waliokuwepo kutumbuiza katika maadhimisho hayo. TOT wakiongozwa na muimbaji wao mahiri Khadija Kopa "Heshima Pesa Shkamoo Makelele".....
 
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakiwa katika banda  lao la maonesho.