Friday, August 30, 2013

DANIEL OLE NJOOLAY BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI NIGERIA

Aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (2006-2011) Daniel Ole Njoolay na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wa sasa Eng. Stella Manyanya wakiteta jambo katika sherehe za kuwaapisha wakuu wa Mikoa zilizofanyika ikulu tarehe 16 Septemba 2011 . (Picha na MAKTABA)

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATOA MSAADA WA MASHINE YA KUFULIA KWA KITUO CHA KULELEA MAYATIMA CHA KATANDALA MKOANI RUKWA

Mashine maalum ya kufulia nguo aina ya HITACHI iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda kwa kituo cha kulelea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa na kukabidhiwa kituoni hapo na Katibu wake wa Jimbo Ndugu Charles Kanyanda leo tarehe 30, Agosti 2013. Msaada huo wenye thamani ya Tshs. Milioni moja na nusu (1.5) ni ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa alipotembelea kituoni hapo mapema mwaka huu.

Ndudu Charles Kanyanda Katibu wa Jimbo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Katavi akimkabidhi Mama Mkuu Mariastella Wampembe wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika ambao ni wamiliki wa kituo cha kulelea mayatima cha Katandala mashine maalum ya kufulia nguo iliyotolewa na Waziri Mkuu kwa kituo hicho leo tarehe 30, Agosti 2013.  

Mama Mkuu Mariastella Wampembe wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika wamiliki wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa akitoa shukrani zake za dhati kwa Waziri Mkuu kupitia kwa Katibu wake wa Jimbo Ndugu Charles Kanyanda kwa msaada huo wa mashine ya kufulia.

Monday, August 19, 2013

RAIS KIKWETE NA UJUMBE WAKE WAREJEA NCHINI BAADA YA MKUTANO WA 33 WA NCHI ZA SADC ULIOFANYIKA LILONGWE MALAWI


Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Katibu Mtendaji wa SADC Dkt.Stergomena Tax kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo wakati wa mkutano mkuu wa 33 wa viongozi wa nchi za SADC uliofanyika jijini Lilongwe Malawi mwishoni mwa wiki.Wapili kushoto ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik aliyefika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumlaki Rais na Ujumbe wake. (Picha na Ikulu)

ANGALIA MAPOKEZI YA RAIS KIKWETE NCHINI MALAWI


Tuesday, August 13, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA AWAPELEKA WATAALAM WA MAJENZI KUTOKA CHUO KIKUU MUST KWA AJILI YA KUANDAA MICHORO YA MAJENZI YA UWEKEZAJI WA KITALII KATIKA ENEO LA MAPOROMOKO YA MTO KALAMBO (KALAMBO FALLS)

 Njia panda kuelekea Kalambo Falls. Maporomoko hayo yanayopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo ni pili kwa ukubwa barani afrika yakiwa na urefu wa mita 235.  Maporomoko hayo yapo mpakani na nchi jirani ya Zambia.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa baadhi ya maelekezo kwa wataalam hao wa majenzi kutoka MUST na wale wa ardhi kutoka Halamashauri ya Wilaya ya Kalambo juu ya mpango wa majenzi wa eneo hilo la kitalii hivi karibuni. Mpango huo ni pamoja na kujenga geti la kukusanyia ushuru, eneo la mahoteli, na huduma nyingine muhimu.

 Wataalamu wa majenzi kutoka chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Kutoka kushoto Omary Mwenunge na Mark Nassary wakiwa kazini kupata taswiraya maeneo hayo na kuyafanyia kazi ikiwa ni kuweka michoro ya huduma mbalimbali zitakazokuwa zinapatikana katika eneo hilo la kitalii Mkoani Rukwa.

 Wataalam hao wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni walipotembelea eneo hilo. Nyuma yao ni Maporomoko ya Mto Kalambo yenye urefu wa mita 235.

 Wataalam hao kutoka MUST wakistaajabu maporomoko ya mto Kalambo.
 
Sehemu ya maangukio ya mto kalambo

Sehemu ya mapitio ya mto kalambo baada ya kupita kwenye maporomoko.
 
Picha ya maporomoko hayo ikionekana kwa urefu yakiwa na mita 235  (kutoka juu hadi chini)

KIPANYA LEO....TAFAKARI WAHI KUCHUKUA HATUA

Tuesday, August 6, 2013

TASO YAIVIMBIA SERIKALI YAGOMA KUAHIRISHA SHEREHE ZA NANENANE KUPISHA SIKUKUU YA IDDI

Mwenyekiti wa TASO Kanda ya nyanda za juu Kusini Kepten mstaafu Nkoswe.

 
Siku chache zikiwa zimebaki ili kufikia kilele cha maadhimisho ya s kumeibuka mgongano baina ya Chama cha wakulima (TASO) na serikali kuhusu maadhimisho hayo yafanyike Agosti 7 au 8, mwaka huu.

 
Mgongano huo umekuja baada ya serikali kutaka maadhimisho hayo yafanyike Agosti 7 mwaka huu huku chama cha wakulima kikiweka msimamo wake wa kusherehekea maadhimisho hayo agosti, 8 mwaka huu .

 
Akizungumza jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale Mwenyekiti wa Chama cha wakulima (TASO) kanda ya nyanda za juu kusini,Kapten Mstaafu Noel Nkoswe wakati wa majumuisho na waandishi wa habari baada ya kuibuka vuta nikuvute na serikali kuhusu kilelele cha maadhimisho hayo ya wakulima.

 
Kapten Nkoswe amesema kuwa wao kama chama cha wakulima msimamo wao upo pale pale wa sherehe hiyo ya wakulima kufanyika Agosti 8 mwaka huu kama ilivyopangwa kila mwaka.

Amesema Wakulima wao lazima l washerekee sikukuu yao kama kawaida hivyo mpango wa kubadilisha tarehe haupo ambapo chama hicho kwa msimao wake kitafanya tarehe 8 na zawadi za wakulima kutolewa agosti 8 kama ilivyo pangwa.

 
Kapten mstaafu Nkoswe amesema mwenyekiti wa TASO taifa aliyemtaja kwa jina moja amemwelekeza kuwa maadhimisho ya kilele cha sikukuu hiyo yatafanyika kitaifa katika kanda ya kati Dodoma Agosti 7 mwaka huu ambapo katika kanda zingine zitafanya kama kawaida Agosti 8 mwaka huu.

 
Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma amesema kuwa wamepokea barua ya serikali inayotaarifu sherehe za kilele cha nane nane zifanyike Agosti 7 mwaka huu kutokana na sikukuu ya Idd kuwa agosti 8 mwaka huu .

 
Hata hivyo katika barua iliyotumwa na wizara ya kilimo chakula na ushirika yenye kumbu kumbu namba AE 18/196/01 ya julai 30 mwaka huu kwenda kwa waziri wa nchi sera uratibu na bunge ofisi ya waziri mkuu iliyoandikwa na waziri wa kilimo na chakula Eng Christopher Chiza na nakala kwa wakuu wa mikoa yote minne ya kanda ya nyanda za juu kusini.

 
Aidha nakala ya barua hyo iliyotumwa kwa katibu mtendaji Taifa imesema kuwa sherehe za kilele cha nane nane imeamliwa zifanyike Agosti 7 mwaka huu kutokana na mwingiliano wa sikukuu ya Idd ambapo Waziri wa nchi Mh.William Lukuvi atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.

 
NA mbeya Yetu Blog.

Monday, August 5, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA ATEMBELEA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA, RUKWA DAY YAPAMBWA NA SIKU YAKE YA KUZALIWA


 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (katikati) akikagua mfumo wa umwagiliaji bustani za mbogamboga katika maonesho yanayoendelea ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
  

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) juu ya gari iliyotengenezewa mfumo wa nishati ya gesi katika maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
 

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua bidhaa mbalimbali kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi katika maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya. Mkuu huyo wa Mkoa ameridhishwa na vifungashio vingi vilivyotumika katika maonesho hayo mwaka huu na wajasiriamali wa Mkoa wa Rukwa.
 

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiangalia "shamba jiko" ambalo staili yake ni ya kupanda mbogamboga nyumbani katika eneo dogo kwenye maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua maji aina ya Dew Drop, maji pekee yanayotengenezwa Mkoani Rukwa Mjini Sumbawanga na Mjasiriamali wa ndani, maji ambayo wananchi na wadau wengi wanasifia ubora wake kuwa ni ya kiwango cha juu. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.
 


 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima wakikagua banda la Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga ambalo limesifika kwa umaridadi wake.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua samaki mbalimbali waliopo katika moja ya banda la Wilaya ya Nkasi katika maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya. Samaki hao wamekaushwa kitaalam na wana uwezo wa kukaa mda mrefu bila kuharibika.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima wakipata maelezo kwa mtaalam wa hali ya hewa walipotembelea kituo cha hali ya hewa kilichopo katika maonesho hayo. Kifaa kinachoonekana kinatumika kupima wingi wa mvua.
 
 TanSeed wakitangaza bidhaa zao za mbegu kwa staili ya aina yake.
 
 Ebony Fm Radio ya nyanda za juu kusini ambayo makao makuu yake ni Mjini Iringa ikifanya mahojiano ya moja kwa moja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya mara baada ya kiongozi huyo kuzungukia mabanda kuzungumzia maonesho hayo kwa ujumla wake.
 
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na baadhi wafanyakazi wa Radio ya Ebony FM ya Mjini Iringa maara baada ya Interview.
 

MC MIMA, Misasi Marco akipaisha vokali zake.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitangaza rasmi kuzaliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya katika usiku wa maonesho ya nanenane "Rukwa Day" katika ukumbi wa JKT Nanenane Jijini Mbeya saa 12:01 Usiku wa tarehe 04/08/2013. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa amebebwa juujuu na wananchi pamoja na watumishi walioshiriki hafla fupi ya "Rukwa Day" katika maonesha ya nanene nyanda za juu kusini Jijini Mbeya ikiwa ni pongezi kwake katika siku yake ya kuzaliwa ya tarehe 04/08.
 
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Respich Maengo akimpongeza Mhe. Manyanya kwa siku yake ya kuzaliwa.
 
Simon Mutabazi Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akimpongeza Mhe. Manyanya kwa siku yake ya kuzaliwa.


Friday, August 2, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA STELLA MANYANYA AONANA NA WALIMU WA KIKE WA MANISPAA YA SUMBAWANGA LEO KUJADILI KERO ZAO MBALIMBALI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na walimu wa kike wa Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 02 Agosti 2013 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la mkutano huo likiwa kujadili kero mbalimbali za walimu pamoja na kuzitaftia ufumbuzi. Pamoja na kero mbalimbali zilizowasilishwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa maelekezo kwa Halmsahauri ya Manispaa kushughulikia kero zinazowezekana ikiwepo madai ya likizo na mengineyo. Kwa yale yaliyo nje ya uwezo wa Manispaa aliahidi kuyachukua na kuyafikisha panapohusika ili yaweze kutaftiwa ufumbuzi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Kushoto ni Afsa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa Bi Catherine Mashalla. 
 
 Katika kikao hicho walimu walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kufuta chama cha waalim (CWT) kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiwakata waalim mishahara kwa mda mrefu bila kuwa na msaada wowote kwao pindi wanapouhitaji. Mapendekezo mengine ni kupunguza idadi ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka tisa hivi sasa na kuwawekea masomo yatakayowawezesha kusoma na kuandika kuliko hivi sasa ambapo masomo ni mengi na huwachanganya watoto. Hata hivo Mkuu wa Mkoa aliweka bayana kuwa ni vyema chama hicho kikaona ni jinsi gani ya kuwanufaisha zaidi walimu kwa kujiwekea utaratibu wa kuwakopesha au kuwasaidia kwa njia nyingine kiuchumi.
 
Sehemu ya waalimu waliohudhuria katika Mkutano huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwashauri waalim kutokopa katika taasisi zisizo rasmi ambazo riba zake ni kubwa kupita kiasi. Alisema taasisi nyingi za namna hiyo zimechangia kufanya maisha ya walimu wengi kuwa magumu na badala ya kuwa msaada kwao inageuka na kuwa kero.

 
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi Witness Maeda akitoa kero mbalimbali wanazokabiliana nazo waalim ikiwepo uhaba madarasa, mabweni, bwalo na maabara chuoni hapo. Kwa ujumla kero zilizowasilishwa ziligusia mishahara hafifu ya walimu, uhaba na ubovu wa vyumba vya madarasa, kucheleweshewa madai yao ya mishahara na nauli (Salary Arears), kupandiswa madaraja na uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kuweza kukabiliana ni mabadiliko ya mitaala mipya. 

Thursday, August 1, 2013

ABBASIYYA YA MVIMWA MKOANI RUKWA YAPATA ABATE MPYA

Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa Ndugu Martin Augustino Chang'a akimpongeza Abate Denis Ndomba kwa kutunukiwa cheo cha Uabate katika Abasiyya ya Mvimwa iliyopo Mkoani Rukwa jana tarehe 01 Agosti 2013. Abate Ndomba alisimikwa cheo hicho na Askofu Damian Kiaruzi wa Kanisa Katoliki Sumbawanga. Hafla hio ilitanguliwa na Misa maalum ya kuliombea Kanisa ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwepo mapadre na mabruda kutoka nyanda za juu kusini, viongozi mbalimbali wa vyama na Seriakali, na wananchi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimpongeza kwa zawadi Abate Denis Ndomba kwa kuchaguliwa kuwa Abate mpya wa Abbasiyya ya Mvimwa iliyopo Mkoani Rukwa.
 
Baba Askofu Damian Kiaruzi wa Kanisa Katoliki Sumbawanga, Abate Denis Ndomba aliyechaguliwa kuwa Abate mpya wa Ababasiyya ya Mvimwa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta wakifurahia onesho la wanafunzi mara baada ya ibada maalum ya kumsimika Uabate Padre Denis Ndomba. 

Wanafunzi wakionyesha umahiri wao wa kuimba na kufanya maonesho katika hafla hiyo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aiktoa salam zake katika hafla hiyo.