Sunday, December 21, 2014

KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA MKOA WA RUKWA...

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati akizungumza katika kikao cha baraza la biashara Mkoa wa Rukwa kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa RDC Mkoani humo.
Mwanasiasa mkongwe nchini na Mbunge wa zamani wa jimbo la kwela Ndugu Chrissant Mzindakaya akichangia mawazo yake katika kikao hicho ambapo alitilia mkazo uwekezaji katika maporomoko ya mto kalambo katika kukuza utalii na uwekezaji Mkoani Rukwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara nchini aliyejulikana kwa jina moja la Bwana Mbilinyi akichangia mawazo yake katika kuinua biashara Mkoani Rukwa.
 Afisa katika Dawati la Uwekezaji Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Ndugu Misasi Marco akiwasilisha moja ya mada katika kikao hicho.

Saturday, December 13, 2014

GARI LA MBUNGE WA JIMBO LA KWELA (CCM) IGNAS MALOCHA LAVAMIWA NA KUVUNJWA VIOO

Hii ni gari ya mbunge wa jimbo la kwela Ignas Malocha ambayo imevunjwa vioo na wafuasi wanaosadikiwa kuwa wa vyama vya upinzani ktk kijiji cha Kapenta jioni ya tarehe 12 /12/2014. Mbunge huyo alikuwa akitokea kijiji cha Kaoze aliposhiriki mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa za CCM, kundi la vijana walitanda barabarani kisha kuanza kutoa lugha chafu kuona hivyo dereva aligeuza gari huku mawe yakirushwa ambayo alivunja vioo hivyo. Kimsingi hakuna aliyejeruhiwa ktk tukio hilo.
Picha na habari hii kwa hisani ya matandao wa Facebook na Mussa Mwangoka Sumbawnga.

Thursday, December 11, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AONGOZA WATUMISHI WA JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA HUO KATIKA USAFI WA MAZINGIRA (SUMBAWANGA NG'ARA)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akishiki kwa vitendo katika usafi wa mazingira kwa kusafisha choo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo ikiwa ni utaratibu wa kawaida uliowekwa kwa wafanyakazi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kushiriki katika usafi wa mazingira  unaobebwa na kaulimbiu ya "Sumbawanga Ng'ara" katika kila Alhamisi ya wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ofisi Bw. David Mlongo juu kuboresha usafi katika mazingira ya vyoo na jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo.
PICHA NA FRANK MATENY WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA.

Saturday, November 1, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILLAL AFUNGA KONGAMANO LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA MJINI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA JANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa ziwa Tanganyika lililojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. kongamano hilo limefungwa jana tarehe 01 Nov 2014  katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga, Mkoani Rukwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi na tano kwa wajasiriamali wadogo wadogo wa Sumbawanga kwenye Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya ambaye Mkoa wake ndio mwenyeji wa Kongamano hilo kwa mwaka huu 2014.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi  kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya Mpanda mjini kwenye Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Dkt. Rajb Rutengwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia mashati ya vitenge alipotembelea banda la Mkoa wa Katavi kwenye maonesho wakati wa Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Col. Mstaafu Issa Machibya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ndizi za aina mbalimbali alipotembelea banda la Mkoa wa Kigoma kwenye maonesho wakati wa Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa ziwa Tanganyika linalojumuisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.  kongamano hilo llimefungwa jana tarehe 01 Nov 2014  katika Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga Mkoani Rukwa. Picha na OMR.

Friday, October 17, 2014

TANGAZO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya anapenda kuwatangazia na kuwakaribisha wananchi wote katika Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika – Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi litakalofanyika Mkoani Rukwa kuanzia tarehe 26, Oktoba hadi 01, Novemba 2014.

Lengo kuu la Kongamano hili ni kunadi fursa nyingi za uwekezaji ambazo bado hazijawekezwa ipasavyo Mkoani Rukwa na katika ukanda huu wa Ziwa Tanganyika. Mkoani Rukwa fursa hizi zipo katika Sekta za Viwanda, Madini, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Afya, Elimu, Utamaduni, Michezo, Usafiri na Usafirishaji katika maeneo ya Barabara, Anga na Majini katika Ziwa Rukwa na Tanganyika; ikiwa ni pamoja na vivutio vingi vya kihistoria vinavyohitaji kuhifadhiwa na kuendelezwa. Mkoa wetu pia una vivutio kadhaa vya Kitalii ambavyo havijaendelezwa yakiwemo Maporomoko ya Kalambo, samaki wa mapambo “ornamental fish”, Mbuga ya Lwafi, pamoja na mabwawa ya asili ya Kwela na Sundu.

Kwa upande wa Mkoa wa Rukwa Kongamano hili litakuwa la kipekee ikilinganishwa na Makongamano yaliyotangulia kwa sababu litafanyika sanjari na mambo yafuatayo:-

a)                 Kufanya tathmini ya shughuli za Uwekezaji Kikanda na Kimkoa na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizojitokeza,

b)                 Kufanya tathimini ya Mafanikio ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa Mkoa wa Rukwa (1974 - 2014),

c)                 Kutangaza fursa za uwekezaji za Mkoa wa Rukwa katika kipindi hiki,

d)                Kuzindua Wilaya Mpya ya Kalambo, pamoja na fursa za Uwekezaji wa Ndani na Nje za Wilaya hii,

e)                 Kufanya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Wawekezaji walioanza kuwekeza Mkoani Rukwa,

f)                  Kutathimini ubora wa wawekezaji waliojitokeza hadi sasa na kutoa tuzo kwa Wawekezaji bora

g)                 Maonyesho ya SIDO ya  wajasiriamali wa Kanda ya nyanda za juu Kusini inayojumuisha Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Katavi na Njombe.

h)                Kutumia fursa hii kuwaalika Wajasiriamali wa Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini, kutumia fursa zilizopo za kuwekeza katika Mkoa wa Rukwa ikiwemo Wilaya mpya ya Kalambo.

i)                   Kutangaza fursa za biashara za Kimataifa. Kutokana na mazingira ya mahali Mkoa ulipo kijiografia na Ukanda wa Ziwa Tanganyika kwa ujumla, ipo fursa kubwa ya kufanya biashara za kimataifa kati ya Tanzania (Kupitia Mkoa wa Rukwa), Kongo, Burundi na Zambia. Nchi yetu iko katika mchakato wa kuipanua bandari ya Kasanga ambayo itatumiwa na Nchi za Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia na Burundi katika kusafirisha mizigo na abiria.


Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki na kujifunza mengi katika Kongamano hili.

Sunday, September 14, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AIBUKA NA MBINU MPYA KUPUNGUZA VIFO VYA KINAMAMA WAJAWAZITO MKOANI HUMO

WATENDAJI wa Serikali kuanzia ngazi za wilaya, tarafa na kata mkoani Rukwa wamekula kiapo mbele ya mkuu wa mkoa huo, Mhandisi Stella Manyanya kwamba wapo tayari kuwajibika iwapo katika maeneo yao ya utawala kitatokea kifo cha mama mjamzito kitakachosababishwa na uzembe
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akisisitiza jambo jana katika kikao cha kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya wajawazito, sambamba na kuhimiza jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kilichowajumuisha wananchi, wakunga wa jadi,watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya kata, tarafa, wilaya na mkoa ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga. 

Kiapo hicho wamekula jana mara baada ya kikao cha siku nzima kilichokuwa na lengo la kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya wajawazito, sambamba na kuhimiza jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kilichowajumuisha baadhi ya wananchi, wakunga wa jadi na watendaji hao wa serikali kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga mjini hapa

Watendaji wa Serikali waliokula kiapo hicho ni wakurugenzi wa halmashauri, maofisa tarafa na watendaji wa kata ambao wana jukumu la kuhakikisha hakuna mama mjamzito ambaye itatokea anafariki dunia kutokana na sababu ambazo zinaweza kuzuilika kwenye maeneo yao

"tumedhamiria kupunguza vifo vya wakina mama wajawazito.....na hilo linawezekana sasa kuna mikakati tumejiwekea kama mkoa ya kuhakikisha tunafuta vifo vyote vinavyotokana na uzembe wa watawala wa eneo husika au wataalam wa idara ya afya, hatutaki kusikia mama mjamzito ameshindwa kufikishwa kituo cha afya au hospitali kwa sababu ukosefu wa gari ya kubeba wagonjwa au kitu kingine ambacho kipo ndani ya uwezo wa utawala" alisema Manyanya

Baadhi ya viongozi wa Serikali na wadau wengine wa maendeleo wakifuatilia kwa makini mada katika kikao hicho.

Manyanya aliongeza kuwa iwapo kitatokea kifo uchunguzi utafanyika na ikibainika kulikuwa na uzembe uliosababishwa na mtendaji yoyote kati ya hao waliokula kiapo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi ili we fundisho kwa watendaji wengine

Pia Manyanya alisema kuwa mkoa unajipanga kuona uwezekano wa kuwapatia simu za mkononi wakunga wa jadi ambao watawasiliana na wataamu wa afya na watawala wa eneo husika ili wafike kuwachukua wajawazito wanakwenda kwao kujifungulia badala ya kwenye vituo vinavyotoa huduma ya afya

Awali, Kaimu Mganga mkuu wa mkoa, Emmanuel Mtika alisema kuwa tangu januari 2014 hadi mwezi agosti kumeripotiwa kutokea vifo vya wajawazito 33 hali ambayo inasababishwa na changamoto kadhaa ikiwemo matumizi ya dawa za asili kwa wajawazito ili kuongeza uchungu wakati wa kujifungua hivyo kusababisha kizazi kufumuka na kupasuka sambamba na upungufu wa wataalamu wenye ujuzi

Naye, Gasper Materu ambaye ni mratibu wa mradi wa Wazazi na Mwana ulio chini ya mashirika ya Africare, Jhpiego na Plan International wenye lengo la kupunguza vifo vya wajawazito katika mkoa huo kwa asilimia 75 ifikapo mwakani
Mratibu wa mradi wa Wazazi na Mwana ulio chini ya mashirika ya Africare, Jhpiego na Plan International, Gasper Materu akitoa mada katika hicho.

Alisema kuwa  mradi huo umefanya kazi kubwa ikwemo kutoa elimu kwa wahudumu wa afya vijijini wapatao 3032 katika vijiji 288 ambao wanawajibu wa kutembelea kaya zilizopo katika maeneo yao ili kuwaelimisha wakina mama wajawazito kuhusu umuhimu wa kuhudhuria kliniki kwa ajili ya kupata elimu ya afya ya uzazi kabla na baada ya kujifungua

Materu aliongeza kuwa kupitia mradi huo umetoa gari la wagonjwa katika vituo vya afya Mtowisa na Wampembe maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki kirahisi hivyo wajawazito wengi kupoteza maisha kutokana na umbali ili waweze kufikia hospitali kwa ajili ya kupata huduma ya kujifungua

Takwimu zinaonyesha kwamba kwa mkoa wa Rukwa wakinamama wajawazito 138 kwa wastani wa 100,000 ufariki kila mwaka kutoka na matatizo ya uzazi. (Habari hii ni kwa hisani ya pembezoni kabisa blog)

Thursday, September 11, 2014

TAARIFA KWA UMMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

RATIBA YA TUME YA RAIS YA UCHUNGUZI WA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI KUTEMBELEA MIKOA YA KIGOMA, KATAVI, RUKWA NA MBEYA
_______________________________
Tume inatoa taarifa kwa Umma kuwa itatembelea Mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya kukusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili kuanzia tarehe 17/9/2014 mpaka 6/10/2014 kama ratiba inavyoonesha:-
Na.
Tarehe
Mkoa/Wilaya
1.
Jumatano 17/9/2014
Kigoma

Alhamisi
18/9/2014
Kibondo

Ijumaa
19/9/2014
Kibondo

Jumamosi
20/9/2014
Kasulu

2.
Jumatatu
22/9/2014
Kasulu

Jumanne
23/9/2014
Uvinza

Jumatano
24/9/2014
Uvinza

3.
Alhamisi
25/9/2014
Mpanda

Ijumaa
26/9/2014
Mpanda

Jumamosi
27/9/2014
Mpanda

4.
Jumapili
28/9/2014


Jumatatu
29/9/2014
Sumbawanga

Jumanne
30/9/2014
Sumbawanga

5.
Jumatano
1/10/2014


Alhamisi
2/10/2014
Mbozi

Ijumaa
3/10/2014
Mbeya

Jumamosi
4/10/2014
Mbarali

Jumapili
5/10/2014
Mbarali

6/10/2014


Aidha Tume inaendelea kupokea taarifa na malalamiko kwa njia ya barua, simu na barua pepe kwa anwani ifuatayo:-

                                i.            Katibu wa Tume
Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili
SLP 9050
Kivukoni Front
Dar es Salaam

                              ii.            Barua Pepe: opereshenitokomeza@agctz.go.tz

                            iii.            Namba za simu:

Tigo:               0714 826826
Vodacom:       0767 826826
Airtel:             0787 826826
Zantel:            0773 826826

Imetolewa Na:

Frederick K.Manyanda
KATIBU WA TUME
9 Septemba, 2014


Tuesday, August 12, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA RAIS UHURU KENYATTA MJINI DUBAI

 Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia  ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama.
  Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
 walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda na Rais Jakaya Kikwete wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia  ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
Balozi wa Tanzania  katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe.Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na balozi wa Kenya katika UAE Mhe Mohamed Gello katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai ambapo mabalozi hawa walifika kuwapokea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta waliosimama kwa muda mjini hapo wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi za Afrika ulioandaliwa na Rais BArack Obama wa Marekani.Picha na IKULU

Wednesday, August 6, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AUFAGILIA MTANDAO (BLOG) WA RUKWA REVIEW

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akipokea maelezo ya jinsi mtanadao (Blog) wa Rukwa Review unavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katika maonyesho ya Nane nane kanda ya nyanda za juu kusini yanayoendelea Jijini Mbeya. Mhe. Waziri Mkuu alifurahishwa kuona Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa inafanya mambo yake kisasa kupitia mtandao huo ambapo alisema "...haya ndiyo mambo tunayoyataka, mnaweka taarifa zenu humo watu duniani kote wanaona na wanapata fursa ya kutoa maoni yao...". Kulia anaefanya mambo ni muendeshaji wa mtandao huo Ndugu Hamza Temba.

UONGOZI WA MKOA WA RUKWA WADHAMIRIA KUFUNGUA UTALII "KALAMBO FALLS"

Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya ya Kalambo Ndugu Makwasa Biswalo (katikati) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya eneo lililopimwa katika kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza Utalii katika Kijiji hicho ambacho kina maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls), maporomoko ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika yakiwa na urefu wa mita 235. 

Uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya umeonyesha jitihada za makusudi kuhakikisha unafungua fursa za utalii katika maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls) ambayo ni maporomoko ya pili kwa urefu barani Afrika yakiwa na urefu wa mita 235.

Maporomoko hayo ambayo yanahitaji kuwekewa mazingira mazuri kuvutia watalii wa nje na wa ndani yapo mpakani mwa Tanzania na Zambia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo na yanafikika katika umbali usiozidi Km 110 kutoka katikati ya makao makuu ya Mkoa wa Rukwa ambayo ni Manispaa ya Sumbawanga.  

Zipo jitihada kadhaa zilizokwishafanywa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya katika kuhakikisha eneo la maporomoko hayo linaimarishwa na kuwa kivutio kikubwa cha utalii na chanzo cha mapato kwa halmashauri husika na taifa kwa ujumla. 

Jitihada hizo ni pamoja kuwahamasisha wananchi wa kijiji cha Kapozwa na wadau wengine katika kutambua umuhimu wa maporomoko hayo ambapo mpaka hivi sasa wananchi hao wameshashiriki kufyatua matofali kwa ajili ya kujenga kituo cha utalii katika eneo hilo.

 Jitihada zingine ni zile za kupima viwanja na kuandaa michoro katika eneo hilo ambapo ramani imeshaidhinishwa na tathmini ya kuwafidia wananchi maeneo yao imeshafanyika. 

Aidha zimekuwepo jitihada za kutafuta fedha kutoka Serikalini na kwa wahisani mbalimbali katika kusaidia kujenga na kuimarisha utalii katika maporomoko hayo (Kalambo Falls). Wakala wa Misitu Taznania (TFS) wamesaidia upatikanaji wa kiasi cha fedha (Tsh. Mil. 10) ambazo zitasaidia kufungua baadhi ya mitaa katika eneo liliopimwa na shughuli zingine zitakazohitajika katika eneo hilo.  

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya anawaomba wadau wote wa utalii nchini ikiwemo Serikali, Mashirika binafsi, Wawekezaji na Wahisani mbalimbali kuwa na jicho la pamoja katika kuona Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls) yanachukuliwa umuhimu wa pekee wa kuendelezwa na kutangazwa kwa nguvu kwani ni miongoni mwa kivutio kikubwa cha utalii nchini na barani Afrika kwa ujumla. 

Kutokana na maporomoko hayo kuwa mpakani nchi ya Zambia imekuwa ikitumia fursa ya mpaka huo kuendeleza eneo lao la mpakani na kuitangaza Kalambo Falls jambo ambalo likiachwa kwa muda mrefu bila Tanzania kuchukua hatua kama hiyo itapelekea dunia kubaki na picha isiyo sahihi kuwa maporomoko hayo yapo nchini Zambia wakati sehemu kubwa ipo Tanzania na hata muonekano mzuri unapatikana kutokea Tanzania na maji ya mto huo yanatokea Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiangalia ramani ya viwanja vilivyopimwa katika kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii katika kijiji hicho cha mpakani na nchi ya Zambia yalipo maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). Mkuu huyo wa Mkoa alikabidhiwa ramani hiyo na Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya ya Kalambo Ndugu Makwasa Biswalo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Meneja wa Misitu Wilaya ya Sumbwanga na Kalambo Ndugu Martin Hamis wakipanda mti wa kumbukumbu katika eneo lililopimwa la kijiji cha kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii wa maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na wapimaji wa ardhi kutoka chuo cha Ardhi Morogoro walioshiriki na wataalamu wa ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kupima ardhi ya kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii wakiangalia Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls).
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifurahia jambo na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian katika maporomoko ya mto Kalambo. Nyuma yao anaeimarisha usalama ni WP Lucy. 
Sehemu ambayo ni nusu ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiangalia bonde la maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian akiangalia bonde la maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu ya jitihada za wananchi wa kijiji cha Kapozwa ambao wamefyatua matofali kwa ajili kujenga kituo cha utalii kwa ajili ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu ya mchoro kwa ajili ya kujenga kituo na geti la utalii katika maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). Jitihada hizi zimefanywa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya.
Vijana wa nchi jirani ya Zambia wakiwa wanapunga upepo kandokando ya maporomoko ya mto Kalambo. Upande wa nyuma zinaonekana ngazi maalum ambazo ni sehemu ya miundombinu iliyojengwa na Serikali ya Zambia kuwavutia watalii katika eneo hilo. Serikali ya Tanzania ina changamoto kubwa ya kuhakikisha eneo hilo muhimu la utalii linaendelezwa ili kulijengea umiliki halali tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo inaonekana limetelekezwa kwa muda mrefu.
Mara baada ya wanahabari hawa kupata picha za habari ilikua ni fursa mwanana kwao kupata picha za viganjani (simu) kwa ajili ya matumizi ya whatsapp, facebook, twiter n.k. Kama inavyoonekana pichani Bwana Brown Tawa akimpiga picha kwa kutumia simu ya mkononi mwandishi mkongwe nchini ambaye pia hujiita Askofu wa Kanisa la kujitegemea Ndugu Nswima Errrrrrrrnest wa TBC Rukwa. 
Sehemu ya bonde ambalo ni maangukio ya maji ya mto Kalambo yanapotengenezwa maporomoko (Kalambo Falls).

Monday, August 4, 2014

TUNAKUTAKIA HERI KATIKA SIKU YAKO HII YA KUZALIWA ENG. STELLA MANYANYA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ikiwa leo tarehe 04 Agosti ni siku yako ya kuzaliwa, Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na mtandao wa rukwareview tunakutakia heri na fanaka katika siku yako hii muhimu. Tunakuombea kwa Mwenyezimungu aendelee kukupa afya njema na hekima katika kuuongoza Mkoa wetu wa Rukwa kufikia malengo tuliyojiwekea. "Tupo pamoja nawe bega kwa bega" RUKWA RUKWA NA MAENDELEO. N:B Pichani juu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiwa anapunga upepo kandokando ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls) leo tarehe 04/08/2014 .

Saturday, August 2, 2014

WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA KATIKA MAADHIMISHO YA NANENANE NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA LEO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya hiyo leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya ambapo alipokelewa na viongozi waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya (Pichani Kulia).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (aliyeshika boga kushoto) akisikiliza maelezo ya kilimo bora cha maboga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Kulia kwake ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Merry Nagu na pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akipokea maelezo kutoka kwa mjasiriamali kuhusu kilimo cha Uyoga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya.  Wa pili kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na Mbunge wa zamani wa jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda wa pili kushoto akiangalia mbegu ya uyoga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.
Kilimo cha uyoga ni rahisi kwani sio lazima uwe na shamba, kama unavyoonekana pichani.
Picha ya pamoja kati ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, viongozi wa serikali mkoani Rukwa na wajasiriamali wadogowadogo mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. 

MAONYESHO YA NANE NANE 2014 NYANDA ZA JUU KUSINI KUZINDULIWA RASMI LEO NA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA, RUKWA YAPIGA HATUA KATIKA VIFUNGASHIO VYA BIDHAA MBALIMBALI

kaulimbiu ya Maonyesho hayo kitaifa.
Banda la Halmashauiri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikagua bustani za mbogamboga za Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika  maonyesho ya Nanenane Nyanda za Juu kusini Jijini Mbeya leo tarehe 02/08/2014. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Symthies Pangisa.
Bidhaa za mazao mbalimbali kutoka Rukwa.
Bidhaa mbalimbali zikiwa katika vifungashio vya kisasa vikiwa na maelezo ya bidhaa husika.
Bidhaa mbalimbali za mazao kutoka Rukwa zikiwa katika vifungashio maalum, bidhaa hizi na nyingine nyingi zinapatikana katika mabanda ya Mkoa wa Rukwa.
Asali za nyuki wanaouma na wasiouma.
Rosela Wine.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikagua moja ya banda la ususi mapema leo tarehe 02/08/2014.
Moja ya shamba la kisasa la mfano la ngano na maharage katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Bustani Gunia kwa ajili ya mbogamboga. Bustani hii ni rahisi kufanyika majumbani kwani hutumia eneo dogo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na msafara wake wakiwa katika zoezi la ukaguzi wa bustani za mboga mbalimbali.
Zana mbalimbali vya uhunzi vya wajasiriamali kutoka Rukwa. Zana hizi hutengenezwa kwa kuyeyusha vyuma vilivyotumika (Reycling) 
Zana za uhunzi.
Ufugaji bora wa mbuzi.
Kilimo cha kisasa.
Ufugaji wa kisasa wa Ng'ombe.

Ufugaji wa kisasa wa kuku wa kienyeji.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na msafara wake wakiwa katika zoezi la ukaguzi wa bustani za mboga mbalimbali katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ambayo ni mara yao ya kwanza kushirikia katika maonyesho haya.