Friday, February 28, 2014

NAKALA YA RASIMU YA PILI YA KANUNI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI MTAMBO MAALUM WA USIMAMIZI NA UHAKIKI WA MAWASILIANO YA SIMU

  Mgeni Rasmi Kuwasili Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete ,  Rais wa Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizindua Rasmi Mtambo Maalum wa Usimamizi na Uhakiki wa mawasiliano ya Simu kwa kukata utepe ambapo sherehe hizo zilifanyika  Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya  Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia niWaziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ProfJohn Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe  kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
 Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete ,  Rais wa Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa akiwa katika 'Laptop' kwa ajili ya kubofya ili kuruhusu Rasmi mtambo huo kuanza kufanya kazi.
 
 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma akitoa Maelezo ya kina kwa Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete ,  Rais wa Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jinsi Mtambo huo unavyofanya kazi
 Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete , Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  akizungumza Jambo wakati wa uzinduzi Rasmi  wa Mtambo huo. (Picha na Father Kidevu Blog)

Thursday, February 27, 2014

MKUU WA WILAYA YA NKASI IDDI HASSAN KIMANTA AONGOZA SIKU YA USAFI NA UPANDAJI MITI WILAYANI HUMO

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akijumuika na watumishi wa idara mbalimbali na wananchi wa Wilaya hiyo katika siku maalum ya usafi na upandaji miti kiwilaya iliyofanyika tarehe 20 Januari 2014 Mjini Namanyere Wilayani Nkasi. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nkasi)

Tuesday, February 25, 2014

TAARIFA YA HABARI YA ITV KUHUSU MILIPUKO MIWILI ILIYOTOKEA ZANZIBAR.........


...........................................................................................................
  Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu cha mripoko katika eneo la mkunazini, na kuleta mtafaruku na tukio hilo la mripuko katika majira ya mchana, Katika mripuko huo hakuna mtu aliyepata majarana na uharibifu wa majengo katika eneo hilo.  
 Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa ni bomu, katika tukio hilo hakuna Mwananchi aliyejeruhiwa
  Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika eneo la tukio na kutowa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa alipofika katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika eneo hilo, wakati wa mripuko huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuagalia na kuchunguza tukio hilo la mripoko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.

Monday, February 24, 2014

HABARI ILIYOTUFIKIA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA RUVUMA....

Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko (kushoto) akikabidhi funguo za gari jipya kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Naftali Saioloyi (kulia).Gari hilo aina ya Landcruiser Station Wagon lenye namba DFPA 160 limetolewa kwa msaada wa shirika la Waltereed Program kusaidia utoaji wa huduma za UKIMWI .Tukio la makabidhiano imefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mapema mwishoni mwa wiki.
Gari hili ndilo lililokabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea likiwa ni msaada kutoka shirika la Waltereed Program kuhudumia shughuli za UKIMWI katika Manispaa hiyo. (Picha na Revocatus Kassimba Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma)

RAIS KIKWETE ASAIDIA KUENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA WODI YA DHARURA YA WATOTO NA VIFAA VYAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

p6Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa baada ya kuwasili katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p23Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo  na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.p24Mkurugenzi wa Radio One Bw. Deo Rweyunga  akitangaza mchango wa mwenyekiti wa  makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi kiasi cha shilingi milioni 100   katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi bilioni moja zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p25Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa UNICEF nchini kwa mchango wa dola za kimarekani 100,000 huku  Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa wakishuhudia katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.p30Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa NSSF Bw. Juma Kintu kwa mchango wa mfuko huo katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.p32Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 toka kwa wawakilishi wa PPF ukiwa   mchango wa mfuko huo katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p37Rais mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa  akimshukuru mwakilishi wa taasisi ya WAMA Bi. Caroline Mthapula  kwa mchango wa taasisi hiyo  katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p48Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bi  Lucy Kimei kwa kuwasilisha shilingi milioni tatu kama mchango wa familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt Charles Kimei   katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.p49Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bw. Lumbila Fyataga, mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Ikulu,  kwa mchango wa kununua kifaa cha kuwapa joto watoto wachanga (Infant radiation warmer)  katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam

Saturday, February 22, 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2013 YATANGAZWA

Kaimu Katibu Mkuu wa baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde akisoma matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2013 Dar es Salaam 

--- 
KUANGALIA MATOKEO YA MITIHANI

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (CSEE) uliofanyika Novemba 2013  yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
  
 
 
 
 

Friday, February 21, 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA JOB MASIMA AKAMILISHA ZIARA YAKE KWA KISHINDO MKOANI RUKWA,

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kukagua gari aina ya Ashok Leyland iliyotolewa na Wizara yake kwa ajili kuimarisha viteule vya kijeshi vilivyopo Mkoani Rukwa. Katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinavikabili vitua hivyo Wizara ya ulinzi kupitia kwa Katibu Mkuu huyo imetoa gari mbili, boti mbili na fedha kwa ajili ya kuboresha makazi na miundombinu katika viteule hivyo. Kwa upande mwingine amesema kuwa baadhi ya vifaa vingine vitatoka makao makuu ya jeshi katika kuboresha viteule hivyo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama ishara ya makabidhiano ya gari mbili pamoja na michango mingine itakayotumika katika viteule vya jeshi vilivyopo Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwasha gari hilo kama ishara ya kupokea misaada hiyo kwa viteule hivyo vilivyopo Mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima wa pili kushoto akitoa majumuisho ya ziara yake kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa leo. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambae ndiye chachu kubwa ya mafanikio haya kwa kumualika Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi kuja kujionea changamoto zilizopo amemshukuru kwa kuitikia wito wake na mchango wa ujumla uliotolewa na Wizara yake katika kuimarisha ulinzi katika ukanda wa ziwa Tanganyika unaopakana na nchi za Burundi, Zambia na DRC. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu  Symthies Pangisa kushoto  akizungumza katika kikao hicho cha majumuisho ambapo amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na msafara wake kwa kazi nzuri waliyoifanya Mkoani Rukwa katika kipindi chote cha ziara yake ya siku tatu.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha majumuisho wakifuatilia kwa makini.

Wednesday, February 19, 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI AWASILI MKOANI RUKWA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU, AAHIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VITEULE VYA JESHI VYA KIRANDO NA KASANGA MKOANI RUKWA

Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima akishuka kwenye ndege aina ya Auric Air katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mapema jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Rukwa kufuatia mwaliko wa Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akimtambulisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga jana.
Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akisalimiana na mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Chrissant Mzindakaya katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na msafara wa Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima ofisini kwake jana. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kukubali mwaliko wake. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameahidi kuboresha miundombinu ya viteule vya jeshi vilivyopo Mkoani Rukwa ukiwepo usafiri, majengo na nishati ya umeme wa jua.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akisalimiana na rafiki yake wa siku nyingi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luten Kanali Sipe mara baada baada ya kuonana na msafara wa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ofisini kwake jana. 
Katibu Tawala wa Mkoa Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiutambulisha msafara wa Katibu Mkuu kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta (hayuko pichani).

Monday, February 17, 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII AKEMEA DAWA ZA KULEVYA, ASEMA WATANZANIA ZAIDI YA 500 WASHIKILIWA NCHI ZA NJE,WENGINE 100 WASUBIRI KUNYONGWA NCHINI CHINA

Katibu Mkuu Anna Maembe akisalimiana na akina mama wanakikundi cha kutunza Mazingira katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa jana. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMA.......................................................................
KATIBU Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Anna Maembe amewataka vijana nchini kuachana kabisa na biashara ya dawa za kulevya kwani inawasababishia matatizo makubwa katika maisha yao badala yake wajiunge na kutengeneza vikundi vya kijasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kujikwamua kimaisha na kufikia ndoto zao.
Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa, zaidi ya vijana 500 wa Kitanzania wako kizuizini katika nchini tofauti duniani walikokamatwa wakisafirisha dawa hizo, huku vijana wengine wapatao 100 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa nchini China.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii wakati wa ziara yake katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa jana, ambapo alisema biashara hiyo inachafua sana jina la Tanzania katika Jumuia ya Kimataifa kutokana na idadi kubwa ya vijana kujihusisha na biashara hiyo.
Akizungumzia sera ya Jinsia inayotekelezwa na wizara yake, Katibu Mkuu huyo alisema haina lengo la kuwafanya wanawake kuwatunishia misuli wanaume katika familia bali ni kuwawezesha wanawake kushiriki katika uzalisha na kukuza kipato cha familia na taifa  kwa ujumla ili kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimepanda sana kwa sasa.
Vilevile alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto ili kujua changamoto zinazowakabili ikiwemo unyanyasaji wa kijinsi na kisaikolojia wanazokumbana nazo na pia kuwapatia haki zao za kimsingi kama elimu, afya na kusikilizwa kama  ambavyo sera ya watoto hapa nchini inavyoelekeza.
Katika kuimarisha vikundi vya wanawake mkoani Rukwa, katibu mkuu Maembe ametoa shilingi milioni 43 kutoka katika wizara yake, ambapo vikundi kutoka katika Halmashauri za wilaya ya Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Vijijini na Manispaa vitanufaika kwa mtindo wa wanachama wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo kwa ajili ya kutekeleza shughuli zao za kiuchumi.
NA RAMADHANI JUMA,
AFISA HABARI OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO

Tuesday, February 4, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJENGO YA BUNGE MJINI DODOMA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi inayokarabati na kufanyia marekebisho ukumbi wa bunge mjini Dodoma tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali za majengo ya Bunge jijini Dodoma alikotembea kukagua inayokarabati na kufanyiwa marekebisho tayari tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua sehemu ya kukalia katika Ukumbi wa Bunge  mjini Dodoma alikotembea kukagua maendeleo ya ukarabati na kufanyiwa marekebisho tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.PICHA NA IKULU