Monday, March 31, 2014

KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHMAN KINANA ATINGA NKASI ,MAMIA WAHUDHURIA MKUTANO WAKE MJI MDOGO WA NAMANYERE

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Jumapili, Machi 30, 2014.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete, akimshukuru Kinana kwa hotuba nzuri katika mkuatano huo wa Namanyere.
 Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia mkutano huo wa Namanyere
 Kijana Elias Yeremia akimuuliza swali Kinana jukwaani, katika mkutano huo wa Namanyere, Nkasi mkoani Rukwa
 Wazee wakimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
 Vijana wa Namanyere wakiwa wamepanda juu ya lori siyo kwa lengo la kusafiri bali kuhakikisha wanamuona Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
 Mamia ya wananchi kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na kinamama wa hamasa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, Jumapili, Machi 30, 2014, katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kizitatua,
 Kikundi cha matarumbeta kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
Mzee Rogas Nkana akimpatia ushahidi wa vielelezo na nyaraka mbalimbali kuhusu mirathi ya binti yake ambayo amefuatilia kwa muda mrefu hadi sasa bila mafanikio. Mzee Nkana alidai mbele ya Kinana kwamba madai hayo kwa ajili ya mirathi ya kifo cha binti yake ambaye alifariki dunia mwaka 2000 akiwa mtumishi wa Wirzara ya Mambo ya Ndani katika Jeshi la Uhamiaji yamekuwa kitendawili licha ya kufuatilia katika ofisi husika. Mzee Nkana alipata fursa hiyo wakati Kinana alipoamua kukutana na waasisi wa Chama na mabalozi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali katika ukumbi wa Community Centre katika mji mdogo wa Namayere wilayani Nkasi. Picha zote na Bashir Nkoromo

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA MKOANI RUKWA

 Baadhi ya Wananchi na wanachama mbalimbali wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa mapema leo asubuhi. 
 Ndege iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwasili katika uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mchana huu. 
 Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa,tayari kwa kuanza ziara yake rasmi mkoni humu,ambapo ziara yake itaanzia Wilaya ya Nkasi,mkoani Rukwa.
 Ndugu Kinana akipokelewa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali mkoa wa Rukwa mara baada ya kuwasili .
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa.
Katikubu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Ndugu Chrisant Mzindakaya,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi na wanachama mbalimbali wa CCM waliofika uwanja ndege mjini Sumbawanga kumpokea. Kinana amewasili mkoani humu  ambapo anatarajia kuanza ziara yake rasmi ya siku 21 Mkoani Rukwa, Katavi na Kigoma.
 Ni Chungu lakini kinatumika kama ngoma kikiwa kimebebwa baada ya kazi yake kuisha wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana mjini Sumbawanga.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akisalimiana na vinaja wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Rukwa katika mapokezi ya Ndugu Kinana.
Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukiondoka uwnaja wa ndege mjini Sumbawanga mapema leo ukielekea wilayani Nkasi kuanza rasmi ziara yake ya siku 21,ambayo itaambata na mikoa mitatau ikiwemo Katavi na Kigoma.

Wednesday, March 26, 2014

MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) WILAYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA

Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo (NHIF) wakiwa katika Mkutano wa kujadili umuhimu wa wa huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na kuangalia namna ya kuzindua rasmi mpango wa kuchangia kabla ya kuugua katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya jana Mjini Matai. Katika salamu zake za ufunguzi alizitaka halmashauri Mkoani Rukwa kuhakikisha kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyake vyote vya maamuzi, Aidha alizitaka Halmashauri ziandae utaratibu wa kuzitambua familia zisizo na uwezo wa kuchangia na zitenge fedha kutoka katika vyanzo vyake ili kuzilipia familia hizo na kuhakikisha kuwa hakuna mkazi wa Halmashauri husika anapoteza maisha kwa kukosa fedha za kuchangia katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Mwanachama wa mfuko huo anatakiwa kuchangia Tsh 10,000/= kwa mwaka ambao ni mchango wa kaya moja isiyozidi watu sita.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu Filbert Ngaponda (Mwana wa Magreth) akiwatambulisha washiriki wa Mkutano huo wakiwepo watendaji wa Serikali na madiwani wa halmashauri hiyo pamoja na wageni mbalimbali waalikwa ambao ni wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (CHF).  
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia washiriki wa mkutano huo.
Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Hamza Temba wa pili kushoto akiwa na baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NHIF) Mkoa wa Rukwa mara baada ya Mkutano huo.
Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Rukwa wakijadili jambo kuhusiana na huduma za mfuko huko. Kulia ni Ramadhan Juma Ofisa Habari Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo, Hamza Temba Ofisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa na Ndugu Mussa Hajj Chewa Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo
Picha ya Pamoja ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, viongozi wa Serikali, Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Watumishi wa ofisi hiyo Mkoa wa Rukwa. 

Tuesday, March 25, 2014

BREAKING NEWS - RC MARA AAGA DUNIA

TAARIFA AMBAZO ZIMENIFIKIA KUTOKA KWA WADAU WA HABARI MKOANI MARA ZIMNASEMA KWAMBA MKUU WA MKOA HUO, AMEFARIKI DUNIA. TAARIFA HIYO IMESEMA KWAMBA MKUU H...UYO WA MKOA ALIKUWA WILAYANI TARIME KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI. NA KABLA YA ZIARA YAKE ALIKUWA OFISINI KWA MKUU WA WILAYA HIYO, JOHN HENJEWELE AKIPOKEA TAARIFA YA WILAYA. NDIPO ALIPOA ANZA KUTOKWA POVU JINGI MDOMONI, NA KISHA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPTALI YA WILAYA, IYOPO KARIBU KABLA YA KUPOTEZA MAISHA. POLENI WANA MARA

Monday, March 24, 2014

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, SAZI SULULA, AKAGUA MIRADI YA HIFADHI YA ZIWA TANGANYIKA MKOANI RUKWA

Safari ya msafara wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Sazi Sulula mwishoni mwa juma katika kukagua miradi inayofadhiliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na wahisani wengine katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa haikuwa rahisi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya barabara kutokana na mvua kubwa kunyesha na hivyo kupelekea magari ya mizigo inayokwenda nchi jirani za Burundi na DRC kupitia bandari ya kasanga kukwama na kuziba njia. Juhudi za ziada kwa kushirikiana na wananchi pamoja na mkandarasi anaejenga barabara hiyo ya Sumbawanga - Kasanga kwa kiwango cha lami zilisaidia katika kuhakikisha magari yote yaliyokwama pamoja na msafara wa katibu Mkuu yanavuka salama.   
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Sazi Sulula (watatu kulia) akiwa na msafara wake wakielekea kagua wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo ikiwa ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na mradi wa hifadhi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi unaoelekea kukamilika wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Katika msafara wake aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia)Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Sazi Sulula akizungumza na mhudumu wa afya katika wadi ya wazazi Samazi juu ya huduma na mahitaji ya kituo hicho kipya ambacho kinategemewa kuanza kazi siku za hivi karibuni.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake wakikagua vitanda kwa ajili ya wanafunzi pamoja na daharia katika shule ya  Sekondari Kasanga  Mkoani Rukwa. Mradi huo wa daharia (bweni) ni kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika Shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Sazi Sulula katika Wilaya yake kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko la samaki la Kirando linalofadhiliwa na mradi wa usimamizi wa Ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuonyesha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Sazi Sulula (wa pili kushoto) sehemu inapojengwa gati kwa ajili ya kushushia samaki na abiria katika soko hilo pamoja na eneo linalojengwa kwa ajili ya kukaushia samaki wabichi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake katika kukagua ujenzi wa miundombinu inayoendelea kujengwa katika soko la samaki la Kirando Wilayani Nkasi Mkaoni Rukwa mwishoni mwa juma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Sazi Sulula akitoa baadhi ya maelekezo kwa mkandarasi wa Soko la Samaki la Kirando ambae pia anajenga Gati linaloonekana kwa ajili ya kuunganisha huduma katika soko hilo na bidhaa za samaki zinazotoka  ziwani (Ziwa Tanganyika).  
Gati linaloendelea kujengwa kwa ajili yakuhudumia soko hilo la samaki la Kirando wilayani Nkasi.

Friday, March 21, 2014

MKUU WA WILAYA YA NKASI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AFUNGUA RASMI KAMPENI YA TOHARA KWA WANAUME MKOANI RUKWA LEO

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Tohara kwa wanaume Mkoani Rukwa iliyofanyika kimkoa katika Tarafa ya Challa Wilayani Nkasi. Akihutubia katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya Mkuu huyo wa Wilaya amesema hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu 2014 Mkoa wa Rukwa unatakiwa uwe umeshafanya tohara za wanaume 22, 000 ikiwa ni agizo la kitaifa ambapo hadi sasa jumla ya wanaume 7,000 wameshafanyiwa tohara.  

Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo Mkoani Rukwa tangu kampeni hiyo ianze tarehe 17 Machi 2014 hadi jana tarehe 20 Machi 2014 jumla ya wanaume 583 wameshafanyiwa tohara ndani ya siku 4 katika kituo kilichopo tarafa ya Challa. Kampeni hiyo inaenda sambamba na zoezi la upimaji wa VVU ambapo kati ya wananchi 699 waliopimwa ni mmoja tu amekutwa na maambukizo ya virusi hivyo katika tarafa hiyo ya Challa.

Akizungumzia faida za tohara kwa wanaume amesema husaidia kupunguza uwezekano wa akinamama kupata kansa ya kizazi  pamoja na kusaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiwasalimia wananchi wa tarafa ya Challa waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akizungumza katika hafla hiyo. Akizungumzia juu ya zoezi hilo la tohara amesema tohara kwa wanaume husaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%. 
Zoezi la Tohara likiwa linaendelea katika zahanati ya Challa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa awasalimu wananchi wa Challa.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha (watatu kulia), Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Albinus Mugonya (wa tano kulia) na watumishi wa Idara ya Afya katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo.

Sunday, March 16, 2014

WAZIRI WA AFYA DKT. SEIF RASHID AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA SIKU YA UTEPE MWEUPE TANZANIA MKOANI RUKWA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiwa katika zoezi la ukaguzi wa mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu na huduma za mama wajawazito na watoto wachanga katika maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe Tanzania yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa katika Tarafa ya Mtowisa. Dkt. Seif Rashid alimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambae awali alikubali kushiriki maadhimisho hayo ambapo amekabiliwa na majukumu mengine ya kitaifa. Kushoto kwa Dkt. Seif Rashid ni Mratibu wa Taifa wa Utepe mweupe Mama Rose Mlay. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni "WAJIBIKA MAMA AISHI"
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akihutubia katika maadhimisho hayo ambapo aliwapongeza wadau wote wanaopigania na kusaidia afya ya mama na watoto na kuahidi kutoa kipaombele katika bajeti kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto nchini. Aidha amezitaka Halmashauri nchini kutoa kipaombele kwa kuongeza bajeti zao katika kuhudumia afya ya mama wajawazito na watoto wachanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa salamu za Mkoa wa Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya katika Maadhimisho hayo ya kitaifa. Katika Salamu hizo alisema zipo changamoto nyingi  katika sekta ya afya zinazohitaji ufumbuzi wa haraka ikiwemo upungufu wa watoa huduma, vifaa tiba, dawa, magari ya kubebea wagonjwa, vituo vya kutolea huduma za afya na vingine kuwa mbali na maeneo ya wananchi kwa baadhi ya maeneo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akifafanua baadhi ya mambo katika sekta ya afya Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akikabidhi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid maoni na maombi ya wakazi wa Wilaya yake katika kuimarisha sekta ya afya katika Wilaya yao na Taifa kwa ujumla.
Maadhimisho hayo yalitawaliwa na hali ya hewa ya mvua ambayo hata hivyo haikuathiri mwenendo mzima wa ratiba iliyopangwa, baadhi ya wananchi walilazimika kutumia miamvuli na wengine kuonyesha uzalendo mkubwa na kuamua kunyeshewa hadi kukamilisha maadhimisho hayo, hata hivyo mvua hiyo ilikatika karibu na kufikia mwishoni mwa maadhimisho hayo.
Bi Adrianne Strong ambae nae ni mdau wa afya ya mama wajawazito na watoto wachanga akitoa salam zake na kujitambulisha. Hivi karibuni Bi Adriane Stong kwa kushirikiana na waumini wenzake wa Kanisa la University United Methodist Church la Washington DC Marekani walitoa msaada wa boti na life jacket kwa ajili ya kusaidia huduma za afya ya mama wajawazito na wagonjwa mwambao wa Ziwa Rukwa.
Balozi wa Utepe Mweupe Tanzania ambae pia ni mwanamuziki Sara Thomas akijumuika na wanawake wengine kuimba wimbo wa kuihimiza Serikali na wananchi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha wanaokoa maisha ya mama wajawazito na watoto wachanga.
Zoezi la uchangiaji wa damu salama lilikua likifanyika katika kila Wilaya za Mkoa wa Rukwa katika wiki ya maadhimisho hayo ya utepe mweupe ambapo chupa za damu zaidi ya alfu moja zilichangiwa na wananchi wa Mkoa wa Rukwa.