Friday, May 30, 2014

WAKANDARASI WA KAMPUNI YA SINOTEC KUTOKA DAR WAONANA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA, TAYARI KWA KUANZA KAZI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI KUPITIA MRADI WA REA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wakandarasi wa kampuni ya Sinotec kutoka Dar es Salaam walipofika ofisini kwake jana kutambulisha rasmi kampuni yao ambayo hivi karibuni itaanza kazi ya kuweka miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupitia mradi wa REA kutoka Mjini Sumbawanga kwenda vijiji mbalimbali Mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa Mkoa amesema zoezi hilo ni katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala CCM na Serikali iliyopo madarakani.
Viongozi wa kampuni ya Sinotec kutoka Dar es Salaam wakitoa maelezo ya mpangokazi wao ambao kwa kuanzia wanaandaa vifaa na kuvipeleka maeneo husika kabla ya shughuli yenyewe rasmi kuanza.
Picha ya pamoja.

Wednesday, May 28, 2014

OFISI MPYA YA EWURA YAANZISHWA MKOANI RUKWA, KUSIKILIZA KERO MBALIMBALI ZA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na mjumbe wa baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA (Nishati na Maji) Ndugu Daniel Mtweve kulia na Mtoa huduma kwa wateja wa shirikia hilo Mkoani Rukwa Bi. Zamda Madaba walipofika katika Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa kujitambulisha mapema jana tarhe 27 Mei, 2014. Kwa mara ya kwanza EWURA imeanzisha ofisi yake Mkoani Rukwa baada ya kuwepo kwa kero nyingi kutoka kwa wananchi wanaotumia huduma za nishati na maji. Ofisi hiyo toka ianzishwe sasa ina muda wa miezi miwili.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisisitiza jambo katika kikao hicho.

MKUU WA KITENGO CHA POLISI JAMII NCHINI NDUGU MICHAEL KAMUHANDA AONANA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kushoto akizungumza na viongozi wa Idara ya Polisi Jamii kutoka Makao Makuu ya jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa kitengo hicho Ndugu Michael Kamuhanda walipofanya ziara ya kikazi Mkoani Rukwa jana tarehe 27 Mei, 2014. Ndugu Kamuhanda alisema kuwa pamoja na mambo mengine wamefika kuangalia kama sera na Ilani ya Chama Tawala CCM inazingatiwa ya kuhakikisha kila makao makuu ya kata kunakuwa na kituo cha Polisi pamoja na askari 15 katika kila kata. Amesema kwa kiwango kikubwa sera hiyo imetekeleza na kwamba jitihada zinaendelea kufanywa ambapo polisi wapya watakaomaliza mafunzo hivi karibuni watapangiwa katika vituo husika.
Ndugu Michael Kamuhanda kushoto akiwa na viongozi wengine kutoka kitengo cha Polisi Jamii makao makuu ya Jeshi la Polisi wakiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ofisini kwake mapema jana.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifurahia jambo na viongozi hao wa jeshi la Polisi kitengo cha Polisi Jamii makao makuu ya jeshi hilo. Wa pili shoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa. Mkuu huyo wa Mkoa amelishukuru jeshi la Polisi nchini kwa kuongeza nguvu katika uslama wa raia kwa kuongeza idadi ya Polisi kufikia 15 katika kila Tarafa sera ambayo ni ya kitaifa, aidha ameliomba jeshi hilo makao makuu kuongeza nguvu kidogo kwa jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa katika ujenzi uanoendelea wa nyumba za makazi za askari wa jeshi hilo.

Monday, May 26, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AHUDHURIA IBADA YA KUMWEKA WAKFU ASKOFU CONRAD NGUVUMALI WA KANISA LA MORAVIAN JIMBO LA RUKWA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akimkabidhi zawadi ya picha, Askofu wa Kanisa la Moraviani jimbo la Rukwa, Conrad Ernest katika ibada ya kumwapisha  askofu huyo iliyofanyika  kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga May 25,2014
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Askofu Conrad Ernest Nguvumali baada ya kuwekwa Wakfu kuwa Askofu wa Kanisa la Moravian jimbo la Rukwa katika ibada iliyofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga  May 25, 2014.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MKUTANO WA WADAU WA UHAMASISHAJI WA UBIA BAINA YA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI (PPP) KATIKA SEKTA AFYA MKOANI RUKWA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi mkutano wa wadau wa uhamasishaji wa ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPP - ("Public and Private Partnership") katika Sekta ya Afya uliofanyika leo katika ukumbi wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa. Katika hotuba yake ya ufunguzi amesema ili kufikia lengo kuu la millennia ifikapo mwaka 2015 la kupunguza vifo vya watoto, akina mama wajawazito na kuweza kudhibiti magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza pamoja na kuboresha mazingira na kupata maji salama Serikali peke yake haitaweza bila kushirikiana na Sekta Binafsi ambayo pia imekua na mchango mkubwa katika kujenga afya za watanzani.
Ndugu Paul Michael Nadrie muwezeshaji wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPP - (Public and Private Partnership) katika Sekta ya Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwasilisha moja ya mada katika Mkutano huo. Alieleza kuwa zipo faida nyingi za PPP ikiwemo kuongeza na kusogeza huduma za afya kwa wananchi pamoja na kuongeza ushindani katika kutoa huduma za afya nchini. Akigusia changamoto amesema zipo changamoto nyingi ikiwemo uelewa hafifu wa PPP kwa watekelezaji na jamii kwa ujumla, uwazi katika utekelezaji wa PPP (Public and Private Partnership), upatikanaji wa mikopo ya mda mrefu, uwezo hafifu wa kufanya upembuzi yakinifu na uwezo hafifu wa kiuchumi katika kushiriki kwenye miradi ya PPP (Public and Private Partnership).  
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akitambulisha wajumbe katika kikao hicho kutoka Sekta Binafsi na Sekta ya Umma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.

Sunday, May 25, 2014

MWENGE WA UHURU 2014 WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO, WAMMULIKA MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ALIYEKATWA MKONO MWAKA JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (katikati) akishiriki mbio za Mwenge wa Uhuru (2014) na viongozi wa mbio hizo kitaifa, viongozi na wafanyakazi wa Serikali, vyama vya siasa Mkoani Rukwa na wananchi muda mfupi kabla ya kukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro baada ya Mwenge huo kukamilisha mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe 25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne (4). 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe 25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne (4). 
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru (2014) kitaifa Ndugu Wito Mlemelwa (katikati) kwa niaba ya Kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa (2014) Ndugu Rachel Kassanda akimkabidhi mlemavu wa ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga msaada wa ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) na jembe la kulimia wanyama (Plau) jana tarehe 24-05-2014 vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutokana na mama huyo kukatwa mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina mwishoni mwa mwaka jana. Kushoto anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Methew Sedoyyeka.
Ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai waliotolewa msaada kwa Mama Maria Chambanenge.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru (2014) kitaifa Ndugu Wito Mlemelwa (katikati) kwa niaba ya Kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa (2014) Ndugu Rachel Kassanda akimkabidhi mlemavu wa ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga msaada wa jembe la kulimia wanyama (Plau) na ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) jana tarehe 24-05-2014 vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutokana na mama huyo kukatwa mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina mwishoni mwa mwaka jana. 
Mlemavu wa ngozi Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga ambaye alisababishiwa ulemavu mwingine wa viungo mwaka jana 2013 na watu wasiojulikana baada ya kukatwa mkono wake wa kushoto kwa imani za kishirikina akishika Mwenge wa Uhuru jana tarehe 24-05-2014 ulipotembelea kijijini kwao kuzindua mradi wa maji na kumkabidhi msaada wa ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) na jembe la kulimia wanyama (Plau) vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mama huyo. 

Friday, May 23, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA ALA KIAPO RASMI CHA UHANDISI LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (PE. 1656) akila kiapo rasmi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian Matembele kwa mujibu wa sheria ya usajili wa wahandisi (Engineer's Registration Act (Cap 63), Kanuni na sheria ndogo zote zilizowekwa na zitakazowekwa ikiwemo mwendo wa utendaji kazi pamoja na maadili katika taaluma ya uhandisi. 

Kiapo hicho kimeafanyika leo katika ukumbi wa "video comference" uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo tarehe 23-05-2014. Awali kiapo hicho kilikuwa kifanyike Dodoma pamoja na mawaziri na wabunge wengine ambao ni wahandisi lakini kutokana na majukumu yasiyozuilika Eng. Manyanya ameruhusiwa aape akiwa Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian Matembele wakisaini hati ya kiapo hicho mbele ya mashuhuda mbalimbali walioalikwa katika hafla hiyo fupi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa, pamoja na mambo mengine amesema ni marufuku kwa wahandisi ambao hawajasajiliwa kuidhinisha au kupitisha  kazi za miradi mikubwa katika Mkoa wake wa Rukwa. Aliendelea kusema kuwa kwa Mhandisi yeyote ambaye hajasajiliwa hana mamlaka ya kutumia tittle PE. Eng.....kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa sheria, hata hivyo aliwaahidi wahindisi wote ambao hawajasajiliwa katika Mkoa wa Rukwa ushirikiano katika kuwapa miongozo itakayowawezesha kukamilisha taratibu zao za usajili. Kwa upande mwinine aliipongeza bodi ya ERB kwa kuwa madhubuti na kuweka utaratibu unaowezesha uwajibikaji. 
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian akizungumza muda mfupi kabla ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya. Katika salam zake za ufunguzi amesema lengo la kiapo ni kula yamini kwa anayeapishwa kufanya kazi yake kwa kuzingatia uadilifu wa hali ya juu kwa kuzingatia miiko, kanuni na taratibu zilizowekwa bila kuzivunja ili kuleta ustawi unaokubalika katika jamii.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa kushoto akizungumza katika hafla hiyo. Alisema kuwa kwa upande wa wataalamu wa uchumi wanachangia sana katika kuongezeka au kuzorota kwa maendeleo ya nchi lakini hakuna utaratibu rasmi wa kusajiliwa na kuapishwa, Aliongeza kuwa pengine ingekua hivyo wataalamu hao wangekuwa makini zaidi katika kupanga mipango ya nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta kulia akitoa salam zake katika hafla hiyo. Katika salam hizo alitoa pongezi nyingi kwa niaba ya viongozi wote wa Mkoa wa Rukwa na wananchi kwa ujumla kwa Eng. Manyanya kwa kuwa mfano kwa kuapa kama ambavyo matakwa ya sheria ya usajili wa uhandisi inavyomtaka. Hiyo imekua ni chachu kwa wengine wote ambao hawajajisajiliwa na kuapa waone ni muhimu sasa kufanya hivyo. Kiapo hicho kinatoa funzo kwa watumishi wa kada zote kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo wa hali ya juu.  
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (katikati waliokaa) na Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa (nyuma waliosimama). Wengine kushoto waliokaa ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian na Bi. Z. A. Mpangule Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Sumbawanga kulia. 
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na baadhi ya wahandisi waliosajiliwa na ambao hawajasajiliwa kutoka Mkoa wa Rukwa (nyuma waliosimama) muda mfupi baada ya kuapishwa. 
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katikati na baadhi ya wananfunzi waalikwa katika hafla hiyo kutoka Shule ya Sekondari Mazwi ambao wanasomea masomo ya sayansi. Aliwaasa wanafunzi hao kutoogopa masomo ya sayansi, kufanya kazi kwa bidii na kuwa ili kufikia aslimia 50/50 katika ngazi za maamuzi ni muhimu wanawake kusoma masomo ya fani zote ikiwemo uhandisi ili kuongeza ajira zenye tija kwa wanawake na kipato cha familia na sauti za maamuzi kwa ujumla.
Picha ya pamoja.

Thursday, May 22, 2014

ZIARA YA MWENGE WA UHURU WILAYANI KALAMBO MKOANI RUKWA LEO

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Festo Chonya wa pili kulia akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian mara baada ya kumaliza mbio zake wilayani Nkasi mapema leo asubuhi tarehe 22 Mei, 2014.
Mratibu wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu Abuubakar Serungwe kulia akitoa neno la shukurani kwa uongozi wa Wilaya ya Nkasi kwa ushirikiano walioutoa wakati Mwenge huo upo Wilayani humo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bi. Rachel Kassanda akizindua rasmi wodi ya wazazi ya Samazi mwambao wa Ziwa Tanganyika Wilayani Kalambo leo tarehe 22 Mei, 2014. Kulia anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Iddi Hassan Kimanta.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Kimanta akitoa  maelezo mafupi kuhusu kitanda cha kujifunguliza wazazi kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bi. Rachel Kassanda baada kuzindua wodi hiyo ya wazazi ya Samazi mwambao mwa ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa.
Sehemu ya wananchi wengi wa Kijiji cha Samazi mwambao mwa ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa walikusanyika kushuhudia ujio wa Mwenge wa Uhuru kijijini hapo.
Kwa wale waliokosa pa kukaa walilazimika kupanda miti na kuhatarisha maisha yao ili wapate fursa ya kupata taswira iliyo mwanana ya Mwenge wa Uhuru.
Ndugu Enock Nguvumali Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji Nyuki Kijiji cha Kisumba akishika Mwenge wa Uhuru leo tarehe 22 Mei, 2014. Mapema kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Bi. Rachel Kassanda alizindua mradi wa kutundika mizinga ya kisasa ya nyuki katika Kijiji cha hicho.
Wadau wa Mwenge wa Uhuru ambao pia ni wakuu wa idara katika Wilaya Kalambo Ndugu Mirunga (kushoto) na Maholani wakijadili jambo muda mfupi kabla ya kusomwa Risala ya Utii ya Mwenge wa Uhuru kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani Kalambo.

Wednesday, May 21, 2014

MWENGE WA UHURU WAANZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi (kulia) Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe mapema leo, baadae aliukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta ambapo umeanza mbio zake katika Wilaya hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisoma hotuba ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Mkoani Rukwa ukitokea Mkoa jirani wa Katavi mapema leo. Katika hotuba yake hiyo amesema Mwenge huo utatembelea miradi ya maendeleo 28 na vikundi 27yote ikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh.bilioni nne (4). Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mke wa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akipiga picha na Mwenge wa Uhuru mara baada ya Mwenge huo kuzindua nyumba ya makazi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya hiyo mapema leo. Kushoto ni Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bi Rachel Kassanda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa huo Ndugu Symthies Pangisa wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Rukwa leo ukitokea Katavi.
Ndugu Congores Kipozo Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji wa Kijiji cha Lunyala Wilayani Nkasi akiupigia saluti Mwenge wa Uhuru ulipotembelea Kijijini hapo leo kuzindua mradi wa josho la mifugo.
Miongoni mwa Viongozi wa Mkoa wa Katavi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe watatu kulia mara baada ya kukabidhi mwenge wa Uhuru kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa leo ambapo utakimbizwa katika Wilaya tatu na Halmashauri nne za Mkoa huo kwa muda wa siku nne.

Saturday, May 17, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKAGUA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA, APIGA MARUFUKU UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (Mb) katikati akitoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Mkandarasi anaejenga mradi wa maji wa kijiji cha Malonje ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali za kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Mradi huo wa maji ambao unaelekea kukamilika umefadhiliwa na benki ya dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya Tsh. Milioni 279. Katika maagizo aliyoyatoa ni pamoja na kupiga marufuku shughuli zote za kilimo na ufugaji karibu na vyanzo vya maji kulinda vyanzo hivyo.
Sehemu ya banio la kukingia maji kwenye chanzo cha maji (chemchem) katika kijiji cha Malonje ambalo ni sehemu ya mradi huo, baadhi ya wananchi wameonekana kuendesha shughuli zao za kilimo na ufugaji karibu na chanzo hicho ambapo wamepigwa marufuku kuendeleza shughuli hizo za uharibifu wa chanzo hicho cha maji. 
Bwana Danford Anania Kaimu Injinia wa Maji Manispaa ya Sumbawanga wa pili kulia akitoa maelezo ya tenki la maji lenye ujazo wa lita 45, 000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya. Tenki hilo limejengewa pampu itakayotumia nguvu ya nishati ya jua kusukuma maji katika vijiji vya jirani vya Malonje ikiwa ni sehemu ya mradi wa maji wa Kijiji cha Malonje katika Manispaa ya Sumbawanga.
Banio la kukinga maji kwenye chanzo (chemchem) ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa mradi wa Maji katika kijiji cha Mlanda Manispaa ya Sumbawanga ambapo mradi huu utakaotumia zaidi ya Tsh. Milioni 394 unajengwa na mkandarasi Safari General Traders na unategemewa kuhudumia wanachi wa kijiji cha Mlanda. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alitembelea jumla ya miradi mitano ya Maji katika Manispaa ya Sumbawanga ambayo ni Malonje, Mlanda, Pito, Chilenganya na Kanondo. Aliwataka wakandarasi waharakishe kumaliza kazi walizobakisha ili wanancni waweze kupata huduma hiyo muhimu ya maji. Aidha alikataa kukagua moja ya mradi kwa vile mkandarasi husika amekua akitoa visingizio mbalimbali vya kutokumaliza kazi. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malonje muda mfupi baada ya kukagua mradi wa maji na Zahanati katika kijiji hicho, aliwataka wananchi hao kuwaendeleza watoto wao kielimu na kushirikiana na uongozi wa kijiji katika kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya maji. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawannga Ndugu William Shimwela.

Thursday, May 15, 2014

HABARI ZA MICHEZO: KUELEKEA "WORLD CUP" BRAZIL, FAHAMU MAKUNDI YA TIMU ZOTE NA KLABU ZINAZOONGOZA KUTOA WACHEZAJI WENGI KWENYE MICHUANO HIYO

fifa_world_cup_2014_wallpaper1
Homa ya kombe la dunia inazidi kupanda zikiwa zimebaki takribani wiki zipatazo nne kabla ya michuano hiyo haijaanza kutimua vumbi kwenye viwanja tofauti nchini Brazil. Timu zote 32 tayari zimeshatangaza vikosi vyao kwa ajili ya michuano hiyo.

1613854_710679932328222_4444464783027608059_n