Sunday, July 27, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AFUTURISHA WAISLAMU MKOANI HUMO

Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa picha hii. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Sheikh Rashid Akililimali akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kushoto muda mfupi baada ya futari iliyoandaliwa na Mkuu huyo wa Mkoa katika viwanja vya ofisi yake Mjini Sumbawanga tarehe 26/07/2014.

Katika salamu zake Sheikh huyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa uamuzi wake wa kuwaunganisha Waislamu wa Mjini Sumbawanga katika futari hiyo ambayo ilihudhuriwa na waumini zaidi ya 70. Aliwaomba wabunge wa Bunge Maalum la Katiba waliosusia bunge hilo kupitia kiongozi huyo wa Mkoa kurudi bungeni kwa ajili ya kuwatengenezea wananchi Katiba wanayoisubiri kwa hamu.

"Toka mmeanza bunge hili la katiba naskia Serikali tatu, Serikali mbili mara moja mara mkataba lakini sjaskia mkijadili mambo ya kiuchumi au ya kijamii ambayo yanamgusa mwananchi moja kwa moja......" Alisema Sheikh Akilimali kumwambia Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.

Aliwaomba wabunge wote wa UKAWA kurejea bungeni kutengeneza katiba ambayo itabadilisha maisha ya watanzania waweze kuondokana na umaskini na kupata maisha bora tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo wamekua wakijadili mivutano ya kisiasa pekee.

Kwa upande mwingine shekhe huyo aliwataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuishi kwa amani, ushirikiano na upendo baina yao katika kuuletea Mkoa maendeleo kwa kuweka pembeni tofauti zao za kiitikadi za kisiasa, dini hata ukabila.

 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya alishukuru kwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa viongozi wa dini Mkoani humo na kuwataka waendelee kuudumisha kwa maslahi ya Mkoa na taifa kwa ujumla.

KUFUATIA MUAMKO HAFIFU WA UCHANGIAJI DAMU MKOANI RUKWA KUTOKANA NA DHANA POTOFU ZILIZOPO, MADAKTARI WAONYESHA MFANO KWA KUCHANGIA DAMU KATIKA HOSPITALI KUU YA MKOA HUO

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia damu katika zoezi lilioendeshwa na Shrika la Red Cross katika kuchangia damu Mkoani Rukwa. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine uhaba ambao unafikia nusu kwa nusu ukilinganisha kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo. Uhaba huo umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wkichangia damu.
Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
Dkt. Marwa akichangia damu.
Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.

Thursday, July 17, 2014

SPECIAL MESSAGE FROM ROSE MLAY; A NATIONAL COORDINATOR OF WHITE RIBBON ALLIANCE FOR SAFE MOTHERHOOD TANZANIA (WRATZ)

Dear all,

Please receive this good news and share.
Because of the White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) members  and partners advocacy campaign with a theme "Be Accountable so that Mothers and Newborns Can Survive Childbirth, high level politicians including Hon Prime Minister of the United Republic of Tanzania were convinced that the only way we could eliminate the tragedy of pregnant mothers and new borns dying due to childbirth complication is to ensure they all access Life Saving Services, technically known as Comprehensive Emergency Obstetric and Newborn Care (CEmONC) and qualified health workers near their homes which are health centres.  In order to achieve this the campaign called for a specific budget line item with funds for CEmONC in the comprehensive council health plans.

The Prime Minister on the White Ribbon Day on March 15, 2014, gave a directive that all councils must ensure CEmoNC was available at health centres. They need to ensure omong others functioning operating theatres, laboratory to test and store safe blood, medicines, supplies, equipment and above all qualified health workers. It is possible. The directive was aired by WRATZ campaign media partner ITV/RO for 4 months. WRATZ and Parliamentarian  for Club for Safe Motherhood involved all members of parliament (MPs)on this campaign and in a one day meeting organized by WRATZ, 96 MPs signed the petition on CEmONC and raised huge debate on the issue during budget sessions

According to Mandella, the issue is in our hands NOW, just the matter of putting funds and actions on our will and words. Thus the councils countrywide heard the directive and this month of June 2014 WRATZ checked the council budget plans and for the first time ever, there is a specific budget line item with funds for CEmONC!

Yesterday Thursday of July 2014, WRATZ spent a day with Religious Leaders of Rukwa who mobilized their congregation to petition for the accessibility for CEmONC by all women as a move for accountability on our side--providing feedback to participants.

The Regional Commissioner, Hon. Enge. Stella Manyanya who officiated this meeting told the religious leaders that they are in a position to ensure none of the women in their churches or mosques die in childbirth due to lack of information. "It is God's commandment that we increase and women were given this task through pregnancy labor and delivery...so her life and that of the newborn must be protected", she said and wanting to know whether there is a difference between a city woman's labor and the village woman's labor. If not, then health centres should have CEmONC and not hospitals which are only in Cities.

The Religious leaders wanted to know how they could be a watchdog to ensure the funds in this budget item is spent for CEmONC? The government officials gave them a very clear approach, and they promised to take up this task.
ar
The Religious Leaders declared that before they start a sermon or  meetings they would start with Wajibika Mama Aishi "Be Accountable so that Mothers and Newborn can Survive Childbirth. They all felt accountable to the needless deaths and they will make others do the same--e.g men must save money for the safety of their pregnant wives, use of family planning...

 Please share and if you can, let us all ensure this budget lite item does not go dry at any one time and that the money is spent for CEmONC. 

Wajibika Mama Aishi, "Be Accountable so that mothers and newborns can survive childbirth.

Thanks.

Rose
 
Rose Mlay
National Coordinator,
White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ)
164C Msasani Beach, Kinondoni
P. O. Box 65543, Dar es Salaam
Email address: rose.mlay@gmail.com
Mobile phone: +255 754 316 369
Skype:rose.mlay
Twitter: WRATanzania

Tuesday, July 15, 2014

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA KATIKA KUHAMASISHA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN) KATIKA SEKTA YA ELIMU MKOANI HUMO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza kwa hisia kubwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Itwelele iliyopo Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 15/07/2014 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kuhamasisha mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa shule za Msingi na Sekondari Mkoani Rukwa. Katika ziara yake hii amepata fursa ya kuonana na wanafunzi na wadau wa elimu zikiwemo kamati za shule mbalimbali katika kata za Manispaa ya Sumbawanga na viongozi katika kujadili na kuweka mkakati wa kufanikisha mpango huo. Katika kuhakikisha BRN inafanikiwa ametoa maagizo kadhaa kwa viongozi husika ikiwemo kila shule ya msingi kuhakikisha kuwa na darasa la awali, kila shule ya sekondari kuwa na maabara ya sayansi, kila shule kutengeneza matofali 150, 000 na kila mzazi au mwananchi wa kata husika kutoa mchango wa Tsh. 10,000/= kusaidia ujenzi wa maabara hizo na madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kushoto) akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Sumbawanga wakati akikagua moja ya maabara iliyokwishajengwa katika shule ya Sekondari Itwelele.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akizungumza na wananchi wa kata ya Pito wakiwa katika zoezi la kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na maabara katika shule za kata hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikagua sehemu ya mahindi yaliyozalishwa katika shamba la shule ya Sekondari Itwelele ikiwa ni matunda ya mpango ulioanzishwa na Serikali ya Mkoa wa Rukwa wa kugawa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa shule zote Mkoani Rukwa ambazo zilitakiwa kulima shamba lisilopungua ekari tano litakalotumika kama shamba darasa na kusaidia upatikanaji wa chakula kwa shule husika. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wadau wa elimu katika kata za Katandala, Izia na Majengo jana tarehe 14/07/2014 katika shule ya Sekondari Mazwi mjini Sumbawanga. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga akifafanua moja ya jambo katika kikao hicho. Alieleza kuwa kero inayowakabili wananchi na wanafunzi wa shule iliyokaribu na Dampo la Jangwani inakaribia kuisha kutokana na ujio wa magari mawili mapya ya kubebea taka yanayotegemewa kuwasili wiki hii mjini Sumbawanga.
Baadhi ya wadau wa elimu kutoka kata za Katandala, Izia na Majengo Mjini Sumbawanga wakiwa katika kikao cha kujadili mkakati wa kufanikisha mpango wa Matokeo Makubwa sasa (Big Result Now) kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (hayuko pichani).

Monday, July 14, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA MNADANI MKOANI RUKWA LEO NA KUSIKILIZA KERO ZAO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akizungumza na wafanyabiashara wa mnadani Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 14/07/2014 katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Wafanyabiashara hao waliomba kuonana na Mkuu huyo wa Mkoa kumueleza kero zao ikiwemo tukio la hivi karibuni la tarehe 11/07/2014 la kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kupelekea wafanyabiashara tisini (90) kuporwa simu na fedha katika njia ya Muze. Wafanyabishara hao wamemuomba Mkuu huyo wa Mkoa kuwasaidia katika ulinzi kwenye biashara zao kwani mitaji mingi waliyonayo ni fedha za kukopa ambazo zinahitaji marejesho.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya baada ya kupokea kero za wafanyabiashara hao wa mnadani (hawapo pichani) amelitaka jeshi la Polisi Mkoani Rukwa kuandaa utaratibu maalum wa kuwasaidia wafanyabiashara hao ikiwemo kuwapatia mafunzo maalumu ya mgambo ya kujilinda wao na mali zao. Amelitaka jeshi hilo kukaa na uongozi wa wafanyabiashara hao kuona ni jinsi gani watamaliza kero zilizopo ikiwepo tishio la majambazi na usumbufu wa kwenye malori. Pia amewataka wafanyabiashara hao kutojaza mizigo na abiria kupita kiasi kwenye malori jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao. 
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wafanyabiashara wa mnadani Mkoani Rukwa Ndugu E. Mazwile akizungumza katika kikao hicho ambapo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kutenga muda wake na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Mkoa kwa kufika na kukutana na wafanyabiashara hao na kusikiliza kero zao. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa (kushoto) akiwatambulisha viongozi mbalimbali walioambata na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kikao hicho.
Sehemu ya wafanyabiashara hao wa mnadani.

Saturday, July 5, 2014

KANISA LA TAG (TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD) LAKABIDHI MSAADA WA VYANDARUA 1300 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI RUKWA

Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka vyandarua 1300 vya kukinga mbu waenezao Malaria kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tarehe 04/07/2014. Msaada huo ni sehemu ya vyandarua 8550 vitakavyotolea na Kanisa hilo kwa Mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa katika kuadhimisha  Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa hilo nchini. Pamoja na zoezi la ugawaji vyandarua hivyo maadhimisho hayo yataenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu na huduma mbalimbali za kiroho.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akizungumza katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ambapo amelishukuru kanisa hilo kwa mchango walioutoa wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya malaria. Ameziomba taasisi zingine binafsi kuiga mfano huo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo hapa nchini. Katika hatua nyingine amepiga marufuku matumizi mabaya ya vyandarua ikiwemo tabia ya kuzungushia kwenye bustani za mbogamboga ambapo amezitaka mamlaka husika kuwakamata watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua kali kutokomeza tabia hiyo.
Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano Ndugu Methew Sedoyyeka ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewataka viongozi wa Serikali na wananchi kuhamasishana kwenye shughuli za usafi na uhifadhi wa mazingira ili kutokomeza mazalia ya mbu waenezao Malaria na ugonjwa hatari wa Dengue. 
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya kukabidhi vyandarua 1300 kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa tarehe 04/07/2014. Alisema kuwa Kanisa la TAG lilizaliwa Igale Mkoani Mbeya mwaka 1939 na sasa  linaadhimisha Jubilee ya miaka 75 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Mungu anajali roho yako na mwili wako, jenga mahusiano nae"
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Mtika akifanya utambulisho wa wenyeji katika hafla hiyo.
Vyandarua 1300 vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa na Kanisa la TAG, vyandarua hivyo vitagawiwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizoainishwa Mkoani Rukwa. 
Picha ya pamoja.

Thursday, July 3, 2014

SERIKALI YATHIBITISHA KIFO CHA BALOZI WA LIBYA

Mkurugenzi-wa-Idara-ya-Habari-Maelezo-Asa-Mwambene-kulia-akiwa-na-Mkurugenzi-Msaidizi-wa-Idara-hiyo-Vicent-Tiganya-640x360Msemaji wa serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.
Chanzo:TAARIFA NEWS