Tuesday, August 12, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA RAIS UHURU KENYATTA MJINI DUBAI

 Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia  ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama.
  Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
 walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda na Rais Jakaya Kikwete wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia  ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
Balozi wa Tanzania  katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe.Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na balozi wa Kenya katika UAE Mhe Mohamed Gello katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai ambapo mabalozi hawa walifika kuwapokea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta waliosimama kwa muda mjini hapo wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi za Afrika ulioandaliwa na Rais BArack Obama wa Marekani.Picha na IKULU

Wednesday, August 6, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AUFAGILIA MTANDAO (BLOG) WA RUKWA REVIEW

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akipokea maelezo ya jinsi mtanadao (Blog) wa Rukwa Review unavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katika maonyesho ya Nane nane kanda ya nyanda za juu kusini yanayoendelea Jijini Mbeya. Mhe. Waziri Mkuu alifurahishwa kuona Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa inafanya mambo yake kisasa kupitia mtandao huo ambapo alisema "...haya ndiyo mambo tunayoyataka, mnaweka taarifa zenu humo watu duniani kote wanaona na wanapata fursa ya kutoa maoni yao...". Kulia anaefanya mambo ni muendeshaji wa mtandao huo Ndugu Hamza Temba.

UONGOZI WA MKOA WA RUKWA WADHAMIRIA KUFUNGUA UTALII "KALAMBO FALLS"

Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya ya Kalambo Ndugu Makwasa Biswalo (katikati) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya eneo lililopimwa katika kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza Utalii katika Kijiji hicho ambacho kina maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls), maporomoko ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika yakiwa na urefu wa mita 235. 

Uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya umeonyesha jitihada za makusudi kuhakikisha unafungua fursa za utalii katika maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls) ambayo ni maporomoko ya pili kwa urefu barani Afrika yakiwa na urefu wa mita 235.

Maporomoko hayo ambayo yanahitaji kuwekewa mazingira mazuri kuvutia watalii wa nje na wa ndani yapo mpakani mwa Tanzania na Zambia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo na yanafikika katika umbali usiozidi Km 110 kutoka katikati ya makao makuu ya Mkoa wa Rukwa ambayo ni Manispaa ya Sumbawanga.  

Zipo jitihada kadhaa zilizokwishafanywa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya katika kuhakikisha eneo la maporomoko hayo linaimarishwa na kuwa kivutio kikubwa cha utalii na chanzo cha mapato kwa halmashauri husika na taifa kwa ujumla. 

Jitihada hizo ni pamoja kuwahamasisha wananchi wa kijiji cha Kapozwa na wadau wengine katika kutambua umuhimu wa maporomoko hayo ambapo mpaka hivi sasa wananchi hao wameshashiriki kufyatua matofali kwa ajili ya kujenga kituo cha utalii katika eneo hilo.

 Jitihada zingine ni zile za kupima viwanja na kuandaa michoro katika eneo hilo ambapo ramani imeshaidhinishwa na tathmini ya kuwafidia wananchi maeneo yao imeshafanyika. 

Aidha zimekuwepo jitihada za kutafuta fedha kutoka Serikalini na kwa wahisani mbalimbali katika kusaidia kujenga na kuimarisha utalii katika maporomoko hayo (Kalambo Falls). Wakala wa Misitu Taznania (TFS) wamesaidia upatikanaji wa kiasi cha fedha (Tsh. Mil. 10) ambazo zitasaidia kufungua baadhi ya mitaa katika eneo liliopimwa na shughuli zingine zitakazohitajika katika eneo hilo.  

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya anawaomba wadau wote wa utalii nchini ikiwemo Serikali, Mashirika binafsi, Wawekezaji na Wahisani mbalimbali kuwa na jicho la pamoja katika kuona Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls) yanachukuliwa umuhimu wa pekee wa kuendelezwa na kutangazwa kwa nguvu kwani ni miongoni mwa kivutio kikubwa cha utalii nchini na barani Afrika kwa ujumla. 

Kutokana na maporomoko hayo kuwa mpakani nchi ya Zambia imekuwa ikitumia fursa ya mpaka huo kuendeleza eneo lao la mpakani na kuitangaza Kalambo Falls jambo ambalo likiachwa kwa muda mrefu bila Tanzania kuchukua hatua kama hiyo itapelekea dunia kubaki na picha isiyo sahihi kuwa maporomoko hayo yapo nchini Zambia wakati sehemu kubwa ipo Tanzania na hata muonekano mzuri unapatikana kutokea Tanzania na maji ya mto huo yanatokea Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiangalia ramani ya viwanja vilivyopimwa katika kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii katika kijiji hicho cha mpakani na nchi ya Zambia yalipo maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). Mkuu huyo wa Mkoa alikabidhiwa ramani hiyo na Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya ya Kalambo Ndugu Makwasa Biswalo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Meneja wa Misitu Wilaya ya Sumbwanga na Kalambo Ndugu Martin Hamis wakipanda mti wa kumbukumbu katika eneo lililopimwa la kijiji cha kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii wa maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na wapimaji wa ardhi kutoka chuo cha Ardhi Morogoro walioshiriki na wataalamu wa ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kupima ardhi ya kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii wakiangalia Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls).
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifurahia jambo na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian katika maporomoko ya mto Kalambo. Nyuma yao anaeimarisha usalama ni WP Lucy. 
Sehemu ambayo ni nusu ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiangalia bonde la maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian akiangalia bonde la maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu ya jitihada za wananchi wa kijiji cha Kapozwa ambao wamefyatua matofali kwa ajili kujenga kituo cha utalii kwa ajili ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu ya mchoro kwa ajili ya kujenga kituo na geti la utalii katika maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). Jitihada hizi zimefanywa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya.
Vijana wa nchi jirani ya Zambia wakiwa wanapunga upepo kandokando ya maporomoko ya mto Kalambo. Upande wa nyuma zinaonekana ngazi maalum ambazo ni sehemu ya miundombinu iliyojengwa na Serikali ya Zambia kuwavutia watalii katika eneo hilo. Serikali ya Tanzania ina changamoto kubwa ya kuhakikisha eneo hilo muhimu la utalii linaendelezwa ili kulijengea umiliki halali tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo inaonekana limetelekezwa kwa muda mrefu.
Mara baada ya wanahabari hawa kupata picha za habari ilikua ni fursa mwanana kwao kupata picha za viganjani (simu) kwa ajili ya matumizi ya whatsapp, facebook, twiter n.k. Kama inavyoonekana pichani Bwana Brown Tawa akimpiga picha kwa kutumia simu ya mkononi mwandishi mkongwe nchini ambaye pia hujiita Askofu wa Kanisa la kujitegemea Ndugu Nswima Errrrrrrrnest wa TBC Rukwa. 
Sehemu ya bonde ambalo ni maangukio ya maji ya mto Kalambo yanapotengenezwa maporomoko (Kalambo Falls).

Monday, August 4, 2014

TUNAKUTAKIA HERI KATIKA SIKU YAKO HII YA KUZALIWA ENG. STELLA MANYANYA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ikiwa leo tarehe 04 Agosti ni siku yako ya kuzaliwa, Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na mtandao wa rukwareview tunakutakia heri na fanaka katika siku yako hii muhimu. Tunakuombea kwa Mwenyezimungu aendelee kukupa afya njema na hekima katika kuuongoza Mkoa wetu wa Rukwa kufikia malengo tuliyojiwekea. "Tupo pamoja nawe bega kwa bega" RUKWA RUKWA NA MAENDELEO. N:B Pichani juu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiwa anapunga upepo kandokando ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls) leo tarehe 04/08/2014 .

Saturday, August 2, 2014

WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA KATIKA MAADHIMISHO YA NANENANE NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA LEO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya hiyo leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya ambapo alipokelewa na viongozi waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya (Pichani Kulia).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda (aliyeshika boga kushoto) akisikiliza maelezo ya kilimo bora cha maboga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Kulia kwake ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Merry Nagu na pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akipokea maelezo kutoka kwa mjasiriamali kuhusu kilimo cha Uyoga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya.  Wa pili kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na Mbunge wa zamani wa jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda wa pili kushoto akiangalia mbegu ya uyoga alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mwanasiasa nguli nchini na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela Dkt. Chrissant Mzindakaya na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.
Kilimo cha uyoga ni rahisi kwani sio lazima uwe na shamba, kama unavyoonekana pichani.
Picha ya pamoja kati ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, viongozi wa serikali mkoani Rukwa na wajasiriamali wadogowadogo mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 02/08/2014 katika maonyesho ya wakulima Nanenane nyanda za juu kusini Jijini Mbeya. 

MAONYESHO YA NANE NANE 2014 NYANDA ZA JUU KUSINI KUZINDULIWA RASMI LEO NA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA, RUKWA YAPIGA HATUA KATIKA VIFUNGASHIO VYA BIDHAA MBALIMBALI

kaulimbiu ya Maonyesho hayo kitaifa.
Banda la Halmashauiri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikagua bustani za mbogamboga za Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika  maonyesho ya Nanenane Nyanda za Juu kusini Jijini Mbeya leo tarehe 02/08/2014. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Symthies Pangisa.
Bidhaa za mazao mbalimbali kutoka Rukwa.
Bidhaa mbalimbali zikiwa katika vifungashio vya kisasa vikiwa na maelezo ya bidhaa husika.
Bidhaa mbalimbali za mazao kutoka Rukwa zikiwa katika vifungashio maalum, bidhaa hizi na nyingine nyingi zinapatikana katika mabanda ya Mkoa wa Rukwa.
Asali za nyuki wanaouma na wasiouma.
Rosela Wine.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikagua moja ya banda la ususi mapema leo tarehe 02/08/2014.
Moja ya shamba la kisasa la mfano la ngano na maharage katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Bustani Gunia kwa ajili ya mbogamboga. Bustani hii ni rahisi kufanyika majumbani kwani hutumia eneo dogo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na msafara wake wakiwa katika zoezi la ukaguzi wa bustani za mboga mbalimbali.
Zana mbalimbali vya uhunzi vya wajasiriamali kutoka Rukwa. Zana hizi hutengenezwa kwa kuyeyusha vyuma vilivyotumika (Reycling) 
Zana za uhunzi.
Ufugaji bora wa mbuzi.
Kilimo cha kisasa.
Ufugaji wa kisasa wa Ng'ombe.

Ufugaji wa kisasa wa kuku wa kienyeji.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na msafara wake wakiwa katika zoezi la ukaguzi wa bustani za mboga mbalimbali katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ambayo ni mara yao ya kwanza kushirikia katika maonyesho haya.