Sunday, December 21, 2014

KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA MKOA WA RUKWA...

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati akizungumza katika kikao cha baraza la biashara Mkoa wa Rukwa kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa RDC Mkoani humo.
Mwanasiasa mkongwe nchini na Mbunge wa zamani wa jimbo la kwela Ndugu Chrissant Mzindakaya akichangia mawazo yake katika kikao hicho ambapo alitilia mkazo uwekezaji katika maporomoko ya mto kalambo katika kukuza utalii na uwekezaji Mkoani Rukwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara nchini aliyejulikana kwa jina moja la Bwana Mbilinyi akichangia mawazo yake katika kuinua biashara Mkoani Rukwa.
 Afisa katika Dawati la Uwekezaji Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Ndugu Misasi Marco akiwasilisha moja ya mada katika kikao hicho.

Saturday, December 13, 2014

GARI LA MBUNGE WA JIMBO LA KWELA (CCM) IGNAS MALOCHA LAVAMIWA NA KUVUNJWA VIOO

Hii ni gari ya mbunge wa jimbo la kwela Ignas Malocha ambayo imevunjwa vioo na wafuasi wanaosadikiwa kuwa wa vyama vya upinzani ktk kijiji cha Kapenta jioni ya tarehe 12 /12/2014. Mbunge huyo alikuwa akitokea kijiji cha Kaoze aliposhiriki mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa za CCM, kundi la vijana walitanda barabarani kisha kuanza kutoa lugha chafu kuona hivyo dereva aligeuza gari huku mawe yakirushwa ambayo alivunja vioo hivyo. Kimsingi hakuna aliyejeruhiwa ktk tukio hilo.
Picha na habari hii kwa hisani ya matandao wa Facebook na Mussa Mwangoka Sumbawnga.

Thursday, December 11, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AONGOZA WATUMISHI WA JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA HUO KATIKA USAFI WA MAZINGIRA (SUMBAWANGA NG'ARA)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akishiki kwa vitendo katika usafi wa mazingira kwa kusafisha choo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo ikiwa ni utaratibu wa kawaida uliowekwa kwa wafanyakazi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kushiriki katika usafi wa mazingira  unaobebwa na kaulimbiu ya "Sumbawanga Ng'ara" katika kila Alhamisi ya wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ofisi Bw. David Mlongo juu kuboresha usafi katika mazingira ya vyoo na jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo.
PICHA NA FRANK MATENY WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA.