Monday, January 19, 2015

MKUU WA MKOA WA RUKWA Eng. STELLA MANYANYA AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA KITUO CHA POLISI LAELA NA KUZINDUA JENGO LA KITUO CHA POLISI TUNKO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kushoto akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la kituo cha polisi Laela, Mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na watu wa Marekani.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la kituo cha polisi Laela, aliwataka wananchi na vyombo vya dola Mkoani humo kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kuhakikisha amani inakuepo katika Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda akitoa salam zake za shukrani kwa wafadhili waliosaidia ujenzi wa majengo hayo ya vituo vya polisi ambao ni Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na watu wa Marekani.
Baadhi ya wakuu wa idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa wakishuhudia zoezi hilo la uzinduzi.
Picha ya pamoja.
PICHA NA MDAU FRANK MATENI (DPS)

MKUU WA WILAYA YA NKASI IDDI KIMANTA AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KIMKOA KWA WILAYA YA NKASI


Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia muda mfupi kabla ya zoezi la uzinduzi wa upandaji miti Kimkoa kwa Wilaya ya Nkasi tarehe 19, Januari 2015. Jumla ya miti alfu tatu (3,000) ilipandwa katika uzinduzi huo.

Watumishi wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi wakishiriki katika zoezi hilo la upandaji miti. 
PICHA NA FESTO CHONYA DAS WILAYA YA NKASI.